MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA TATU Kikao Cha

MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA TATU Kikao Cha

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Thelathini na Tatu – Tarehe 31 Mei, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! (Hapa Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni Walitoka nje) NDG. JOHN N. JOEL - KATIBU MEZANI: Kiapo cha Uaminifu. KIAPO CHA UAMINIFU Mheshimiwa Mbunge afuataye aliapa kiapo cha uaminifu: Mhe. Jaku Hashim Ayoub NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. JOHN N. JOEL - KATIBU MEZANI: Hati za kuwasilisha mezani. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na: NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Mfuko wa Bunge na Mfuko wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017. 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MHE. JULIANA D. SHONZA – (K. n. y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama juu ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika kwa mwaka wa fedha 2015/2016, pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MHE. MCH. PETER S. MSIGWA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha... NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa, huwa hakuna ndugu humu ndani. Mheshimiwa Msingwa, Kanuni tafadhali! Hamna ndugu humu ndani, hamna mtu anayekuwa addressed kama ndugu, endelea. MHE. MCH. PETER S. MSIGWA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Nilitegemea wewe ni ndugu… NAIBU SPIKA: Kanuni unazijua. MHE. MCH. PETER S. MSIGWA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha mezani hotuba ya Mambo ya Nje. Naomba kuwasilisha. NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI: Maswali. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Tutaanza na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa Susan Anselim Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum, swali lake litaulizwa kwa niaba yake na Mheshimiwa Amina Mollel. Na. 266 Idadi ya Shule za Awali Nchi MHE. AMINA S. MOLLEL (K. n. y. MHE. SUSAN A. J. LYIMO) aliuliza:- Elimu bora ni uti wa mgongo wa maendeleo ya jamii yoyote ile na ni msingi bora wa elimu kwa watoto unaoanzia toka shule za awali na za msingi:- (a) Je, kuna shule ngapi za awali kati ya mahitaji halisi? (b) Je, ni nini mipango ya haraka kuhakikisha shule za awali zinakuwepo katika shule zote za msingi za Serikali nchini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Susan Anselim Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, mahitaji halisi ya madarasa ya awali ni 16,014 ambayo ni sawa na idadi ya shule za msingi zilizopo nchini kwa sasa. Shule zenye madarasa ya awali ni 14,946 ambazo ni sawa na asilimia 93.33 ya mahitaji. Hivyo, shule za msingi 1,068 hazina madarasa ya awali. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa vyumba vya madarasa ya awali unafanywa na Halmashauri kwa kushirikisha na nguvu za wananchi kupitia Mpango wa Fursa na Vikwazo yaani O and OD (Opportunity and Obstacle to Development). Azma ya Serikali ni kuhakikisha inajenga na kukamilisha vyumba vya madarasa vya awali kwa shule zote 1,068 zenye upungufu huo. Hivyo nitoe wito kwa Halmashauri zenye mapungufu haya kuangalia upya vipaumbele vyake na kutenga bajeti ya kuwezesha ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Amina Mollel, swali la nyongeza. 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kutokana na mwamko ambao umejitokeza hivi sasa kwa watoto wengi kuhudhuria shule kutokana na elimu bure, lakini vilevile kumekuwepo na changamoto mbalimbali yakiwemo pia malalamiko kutoka kwa wananchi. Je, Serikali inajipanga vipi kuhakikisha kwamba changamato hizi inaziondoa ili watoto wote waweze kupata elimu? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, watoto wenye mahitaji maalum bado wao wanakabiliwa na changamoto nyingi; je, Serikali ili kuendana na kasi hii, inajipangaje kuhakikisha watoto wenye ulemavu ambao jamii imekuwa ikiwaficha na wao pia wanapata nafasi ya kupata elimu bure na kuifurahia nchi yao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika sehemu ya kwanza ni changamoto zinazozikabili shule zetu. Ni kweli mara baada ya mchakato wa Serikali yetu ya Awamu ya Tano, ilipojielekeza kwamba elimu kuanzia shule ya awali mpaka form four kuwa ya bure, tumegundua kuna mambo mengi sana yamejitokeza. Jambo la kwanza ni kitendo cha watoto wengi waliokuwa wakibaki mitaani kwa kukosa fursa ya kujiunga na shule, hivi sasa wanaende shule. Baada ya hilo kilichotokea ni kwamba tumekuwa na tatizo kubwa la upungufu wa madawati na mambo mbalimbali. Katika hili ndiyo maana Waziri wangu wa Nchi sambamba na Waziri Mkuu walitoa maelekezo kwamba ikifika 30 Juni, madawati yote yawe yameweza kupatikana maeneo ili kuondoa changamoto ya watoto wanaokaa chini. Hata hivyo, Serikali imejielekeza kuhakikisha kwamba tunajitahidi katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo madarasa lengo likiwa watoto wote wanaofika shuleni waweze kupata elimu. Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo kuna swali la pili linalohusu watoto wenye ulemavu. Ni kweli mimi mwenyewe nikiri kwamba nimetembelea shule kadhaa za watoto wenye ulemavu, kule Mufindi hali kadhalika pale Dar es Salaam, maeneo hayo nilioyatembelea ni kweli watoto hao wana changamoto mbalimbali, lakini nimeweza kutoa maelekezo mbalimbali kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, wahakikishe kwanza watoto hao wenye ulemavu wanapewa kipaumbele. Ndiyo maana katika bajeti yetu ya TAMISEMI mwaka huu tumejielekeza wazi jinsi gani tumejipanga katika suala zima la watu wenye ulemavu ili kwamba watoto wote wanaoenda shuleni kutokana na hali zao wote waweze kupata elimu. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Amina Mollel, najua kwamba wewe ni mwakilishi halisi na makini sana wa walemavu, tutahakikisha ombi lako hili linafanyiwa kazi katika Serikali hii ya Awamu ya Tano kwa nguvu zote. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwalongo, swali la nyongeza. MHE. EDWARD F. MWALONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumuuliza Mheshimiwa Waziri, ni kwa nini sasa katika yale madarasa ya awali ukiangalia fungu lile la elimu bure wanapotoa ile fedha, wale watoto wa madarasa ya awali hawapati ile fedha na inawafanya wazazi waendelee kuchangia yale madarasa ya awali. Je, ni lini Serikali itaanza kutoa fedha kwa ajili ya madarasa ya awali? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimesema katika majibu yangu ya msingi, ukija kuangalia maeneo mbalimbali ambapo watoto wale wa awali waliokuwa wakienda shuleni, mara nyingi sana walimu waliokuwa wanafundisha utakukuta ni walimu waliokuwa wanachukuliwa mtaani, waliomaliza form four, darasa la saba ambaye anaweza akafundisha. Katika maelekezo ya utaratibu wetu wa elimu, wale watu wote wanaomaliza grade „A‟ wanakuwa na component ya elimu ya awali. Kwa hiyo, utakuja kuona kwamba, wakati mwingine watoto walikuwa wakienda shule wanalazimishwa walipie fedha kwa ajili ya mwalimu wa awali, jambo lile tumesema kwamba, walimu wote sasa hivi wanaomaliza grade „A‟ walimu wale wanaopelekwa mashuleni, kuna mwalimu anayefundisha darasa la awali. Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo yetu kama Ofisi ya Rais – TAMISEMI, ni kuhakikisha Wakurugenzi, wanahakikisha katika allocation ya wale walimu katika shule mbalimbali, wawapeleke walimu ili kusaidia kuondoa ule utaratibu wa wazazi kuwa wanachanga kwa ajili ya kumchukua mtu mtaani kuja kufundisha. Mheshimiwa Naibu Spika, hili tumeenda mbali zaidi, ndiyo maana watu walioshudia mwaka jana hapa katika Chuo chetu cha UDOM, tulipeleke takribani walimu wapatao 17,000 katika somo la KKK. Lengo ni kuwawezesha watoto wanapoingia shuleni kuanzia awali na watoto wa darasa la kwanza waweze kujua kusoma na kuandika. 5 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge ni kweli Serikali tunajua changamoto ni nyingi kutokana na suala la elimu bure, lakini Serikali inaangalia jinsi gani tutatatua matatizo mbalimbali. Mara baada ya kufanya jambo hili tumegundua jambo changamoto nyingi zimeweza kujitokeza, changamoto hizi ni kutokana na hii fursa sasa, Serikali ya Awamu ya Tano iliweza kufungua sasa na kupitia hizi changamoto, ndiyo tunaenda kuhakikisha kwamba tunalijenga Taifa la kupata elimu bora. Changamoto hizi, tutakuwa tunazitatua awamu kwa awamu. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zacharia Issaay swali fupi la nyongeza. Mheshimiwa Dkt. Ishengoma, naona Mheshimiwa Issaay yuko busy! MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA:

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    278 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us