NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Saba – Tarehe 10 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU): The follow-up Report on the Implementation of the Controller and Auditor General’s Recommendations for the five performance Audit Reports Issued and tabled to the Parliament on April, 2015. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): (i) Ripoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Taarifa za Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 za Mamlaka za Serikali za Mitaa. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (ii) Performance Audit Report on Monitoring of Building Works in Urban Areas as Performed by the President’s Office – Region Administrations and Local Government. (iii) Taarifa ya Majibu ya Serikali na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2018. (iv) Taarifa ya Majibu ya Serikali kuhusu Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. (v) Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2019/2020 naomba kuwasilisha. MHE. GEORGE M. LUBELEJE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa na Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2019/2020. MHE. DANIEL E. MTUKA – K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Utekelezaji wa Bajeti na Majukumu ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA NA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kuhusu Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/ 2020. NAIBU WAZIRI WA FEDHA: (i) Ripoti ya jumla ya Ukaguzi wa Ufanisi na Ukaguzi Maalum kwa kipindi kinachoishia tarehe 31 Machi, 2019. (ii) Ripoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2018. (iii) Ripoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2018. (iv) Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. (v) The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of Information Systems for the Year ended 30th June, 2018. (vi) The Performance Audit Report on Management of Bulk Procurement of Government of vehicles as performed by the Government Procurement service Agency. (vii) Majumuisho ya majibu ya Hoja na Mpango wa kutekeleza Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2018. NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: (i) The Performance Audit Report on the Management of Water Projects in Rural Areas. (ii) The Performance Audit Report on the Management of Water Supply projects from Borehole Sources in Tanzania as Performed by the Ministry of Water. NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA): (i) Ripoti ya Ukaguzi na Usimamizi wa Shughuli za Ujenzi wa Miradi ya Maji na Umwagiliaji, (The Performance Audit Report on Management of Construction Activities on Irrigation Projects). (ii) Ripoti ya Ukaguzi na Utendaji kuhusu Upatikanaji na uwezo wa kupata Pembejeo Bora za Kilimo, yaani mbegu na mbolea kwa Wakulima yaani The Performance Audit Report on Availability and Accessibility of Good Quality Agricultural Imputs (seeds and fertilizers) to farmers. NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: (i) Ripoti ya Ukaguzi kuhusu Utoaji wa Huduma za Dharura na Rufaa katika Hospitali za Rufaa (The Performance Audit Report on Management of provision of Referral and Emergency Healthcare Services in Higher Level Referral Hospitals as performed by the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children. (ii) Ripoti ya Ukaguzi wa kuhusu utoaji huduma Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (The Performance Audit on Management of Provision of National health Insurance service as Performed by The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children and National Health Insurance Fund. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2018 kuhusu Performance Audit Report on Maintenance of Power Generation Plants. NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:- Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Juni, 2018 kuhusu Ufanisi juu ya Usimamizi wa Elimu kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum (The Performance Audit Report on Management of Education for Pupils with Special Needs. A Report of the Controller and Auditor General March, 2019). NAIBU SPIKA: Ahsante, Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Mendrad Lutengano Kigola, Mbunge wa Mufindi Kusini, swali lake litaulizwa kwa niaba yake na Mheshimiwa Omari Kigua. Na. 53 Hitaji la Hosteli za Wanafunzi – Mufindi Kusini MHE. OMARI M. KIGUA (K.n.y. MHE. MENDRAD L. KIGOLA) aliuliza:- Sekondari za Jimbo la Mufindi Kusini zinakabiliwa na tatizo la hosteli kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga hosteli kwa kila sekondari katika Jimbo la Mufindi Kusini? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mendrad Lutengano Kigola, Mbunge wa Mufindi Kusini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ina shule za sekondari 43 ambapo kati ya hizo shule 21 zina daharia (hostel). Katika mwaka wa fedha 2018/2019, shule nyingine mbili za sekondari za Ihowanza na Mninga zinaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa hosteli ili kufanya idadi ya shule zenye hosteli kufikia 23. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetenga kiasi cha shilingi milioni 60 kupitia mapato ya ndani ili kusaidia ukamilishaji wa daharia zilizopo katika hatua ya ukamilishaji. Vilevile Lyara in Africa wamepanga kusaidia ujenzi wa hosteli katika Shule za Sekondari za Kiyowela na Idunda na CAMFED wamesaidia ujenzi wa hosteil ya Ihowanza. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Omari Kigua, swali la nyongeza. MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri lakini nina maswali mawili, kama ifutavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, changamoto ya hosteli ambayo imejitokeza katika Jimbo la Mufundi Kusini haitofautiani sana na hali iliyopo katika Jimbo la Wilaya ya Kilindi. Ni ukweli usiopingika kwamba suala la hosteli ni kitu muhimu sana kwa sababu linachangia katika ufaulu wa watoto wetu. Je, Serikali iko tayari sasa kuhakikisha kwamba shule zote za vijijini ambazo watoto wanatembea kwa umbali mrefu zinakuwa na hosteli? 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kwamba katika Jimbo la Kilindi ipo Shule ya Kwamkalakala ambayo ni miongoni mwa shule kumi za mwisho ambazo zimefanya vibaya kutokana na kutokuwa na hosteli. Je, Serikali ipo tayari kutoa msaada maalum kuhakikisha kwamba shule ile inajengewa hoteli? Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge wa Kilindi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza anataka kujua kama Serikali iko tayari kujenga hosteli kwenye shule zote za sekondari. Ni ukweli usiopingika kwamba hakuna mtu ambaye anapinga kutokuwa na hosteli katika shule zetu, zimeonesha tija na hasa kusaidia watoto wa kike waweze kupata muda mwingi wa kujisomea na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao ambao pia wamekuwa wakifanya vizuri wale ambao wamebahatika kusoma vizuri. Mheshimiwa Naibu Spika, tunao mpango kupitia EPforR, tumepeleka fedha katika hosteli zetu na Kilindi wamepata hosteli moja ambayo nilienda kuitembelea. Tutaendelea kufanya hivyo kwa mwaka wa fedha huu ambao tumeleta bajeti leo mezani kwenu, Waheshimiwa Wabunge watuunge mkono ikishapita tutaangalia namna ya kuboresha.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages386 Page
-
File Size-