NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Sita – Tarehe 9 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2019/2020. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka ulioisha tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual Report and Audited Accounts of Mzumbe University for the year ended 30th June, 2017). MWENYEKITI: Katibu! NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza leo linaelekezwa Ofisi ya Waziri Mkuu na linaulizwa na Mheshimiwa Dkt. Raphael Masunga Chegeni, Mbunge wa Busega. MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nipo hapa kwa niaba. MWENYEKITI: Wewe unatoka Busega? MHE. RASHID A. SHANGAZI: Hapana, ila hili ni la kitaifa. MWENYEKITI: Aaa, sawa, kwa niaba. Na. 43 Kauli Mbiu ya Kuvutia Wawekezaji Nchini MHE. RASHID A. SHANGAZI (K.n.y. MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI) aliuliza:- Kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ni pamoja na kuongeza uwekezaji kwa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kuwa vikwazo vinavyoathiri dhana hiyo vinaondolewa? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Raphael Masunga Chegeni, Mbunge wa Jimbo la Busega, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Dira ya Taifa ya mwaka 2025 ni kuifanya Tanzania kuwa Taifa lenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Ili kutimiza dhamira hiyo tunatekeleza mipango mitatu ya maendeleo ya miaka mitano mitano ambayo imeainisha vipaumbele vya Taifa kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Kwa sasa Serikali inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano kwa kipindi cha 2016/2017 hadi kufikia mwaka 2020/ 2021 ambao kipaumbele chake ni ujenzi wa uchumi wa viwanda. Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha vikwazo vinavyoathiri uwekezaji na biashara nchini vinaondolewa kwa kuweka miundombinu muhimu na mazingira ya kisera, kisheria, kanuni na kiutendaji ambao ni wezeshi kwa ajili ya kuendesha shughuli za kiuchumi. Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na kuimarisha miundombinu wezeshi kama vile ujenzi wa reli, barabara, viwanja vya ndege, bandari, umeme na maji hatua ambayo inapunguza gharama za uendeshaji wa biashara na uwekezaji na kuleta wepesi katika uwekezaji na biashara. Aidha, Serikali imeimarisha upatikanaji wa ardhi ambapo Mamlaka za Upangaji Miji zimeelekezwa kuzingatia utengaji wa asilimia 10 ya kila aneo la Mpango Kabambe wa Mji kwa ajili ya uwekezaji wa biashara na viwanda. Vilevile Serikali inaendelea kuendeleza Maeneo Maalum ya Uwekezaji au Special Economic Zones ili kuwezesha upatikanaji wa maeneo ya uzalishaji yenye miundombinu. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia imeendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira bora ya uwekezaji kwa kutekeleza programu za kuboresha mazingira ya uwekezaji na hii ni pamoja na mpango wa kuboresha mfumo wa 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) udhibiti wa mazingira ya biashara nchini au Blueprint. Serikali inaendelea kuimarisha ushirikiano na majadiliano na Sekta binafsi kupitia Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) pamoja na mikutano ya wadau wa Sekta mbalimbali kwa ngazi za Kitaifa, Mikoa na Wilaya ambapo changamoto zinazobainishwa zinapatiwa ufumbuzi. MWENYEKITI: Ahsante. Nimemwona mwenye swali Mheshimiwa Dkt. Raphael Masunga Chegeni. MHE. DKT. RAPHAEL M. CHGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Napenda kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii ya Uwekezaji kwa majibu mazuri na ya kina. Pamoja na majibu haya nina maswali mawili madogo ya nyongeza. La kwanza; kwa kuwa Watanzania wana hamu kubwa sana ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda kama ambavyo kauli ya Mheshimiwa Rais ambayo siku zote amekuwa akiisema na kwa kuwa Wizara hii iko chini ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, nini kauli ya Serikali ya kuleta mabadiliko ya haraka na ghafla yaani radical change yatakayowezesha kutekeleza mapendekezo ya Blueprint ambayo amezungumza hapa na mikakati mingine ya kuharakisha uwekezaji? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wako baadhi ya wawekezaji wa ndani na nje ambao wamekuwa wakizunguka ofisi baada ya ofisi nyingine wakitafuta vibali mbalimbali vya uwekezaji, kitu ambacho kimekuwa kikichafua sana nchi hii kwa sababu wanaposhindwa kupata vibali hivi kwa muda wanahama kwenda nchi zingine na hii inakuwa haileti dalili njema kwa nchi yetu. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kipindi hiki cha Bunge la Bajeti awaite wawekezaji wote ambao wana kero mbalimbali, akutane nao pamoja na Mawaziri wengine wote ili kuhakikisha kwamba matatizo yao yanatatuliwa mara moja? Ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Angella Kairuki. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Chegeni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kuhusiana na tunatoa kauli gani ya kuleta mabadiliko ya haraka au kama alivyoeleza mwenyewe radical change, nipende kusema kwamba ni kweli ili tuhakikishe kwamba tunapata faida ya uwekezaji na biashara nchini, ni lazima mabadiliko ya kina yaweze kufanyika. Tayari kama nilivyoeleza kwenye majibu ya msingi Serikali imeanza kuchukua hatua kupitia maboresho mbalimbali na kama alivyoeleza mwenyewe mpango mzuri wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, tumeandaa pia mpango jumuishi kwa ajili ya utekelezaji wa mpango kazi huu wa kuboresha mazingira ya biashara. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mpango huu utatekelezwa haraka. Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia mpango kazi huo jumuishi tumeeleza kabisa ni masuala gani ambayo yanatakiwa kufayiwa kazi na Wizara ipi pamoja na taasisi zipi za kisekta na tutaendelea kuwafuatilia pia kwa mujibu wa road map ya utekelezaji wa mpango huo kwa namna tulivyojipangia. Pia tutaleta mpango huo kazi tutakapokuwa tayari ili na Waheshimiwa Wabunge waweze kuuona na kuweza kufuatilia na kuweza kujua ni hatua gani tumefikia katika utekelezaji. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali la pili kama nitakuwa tayari kufanya kikao katika kipindi hiki cha Bunge kuwaita wawekezaji wote wenye kero mbalimbali. Kwanza nipende kusema ni ushauri mzuri, lakini la pili tayari tumeanza, nimejigawia vipaumbele, moja tumeanza na mikoa mbalimbali na tunaendelea kufanya hivyo kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa. Pili, kwa kushirikiana na Mawaziri mbalimbali wa kisekta tutaendelea kufanya vikao mbalimbali vya kisekta kwa wawekezaji na wafanyabiashara ili kuhakikisha kwamba tunatatua kero zao mbalimbali. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Mheshimiwa Mbunge ni shuhuda tulipoenda Rungwe kupitia kampuni ile ya Rungwe Avocado pamoja na bwana Robert Clowes ambaye tulienda kuangalia na kutatua mgogoro ule kwenye sekta ile ya kilimo cha maparachichi. Nimshukuru sana kwa ushirikiano ambao aliutoa kipindi hicho na naamini mgogoro ule sasa utafika sehemu nzuri na utaweza kumalizika. Pia nimhakikishie na niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge wote na naomba pia ushirikiano wao wa dhati, endapo kuna mgogoro maalum kwa mwekezaji ambaye anamfahamu au katika Jimbo lake analoliongoza au mkoa wake, basi wasisite kunipa taarifa kwa sababu nimeteuliwa kwa kazi hiyo maalum na niko tayari kuifanya. Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, pamoja na mikoa, pamoja na sekta mbalimbali, ili kuweza kuhakikisha kwamba taswira yetu kama nchi katika uwekezaji tunaendelea kuikuza, wiki ijayo kuanzia tarehe 17 nitakuwa na kikao na wawekezaji wote wa kichina na tutaendelea kufanya hivyo na wawekezaji wa Uturuki, wa Marekani, Uingereza na nchi zingine kwa mujibu wa viwango vile vya nchi 10 zinazoongoza katika kuvutia mitaji nchini kwetu, lakini tutahakikisha pia na nchi zingine tutazingatia. Kwa hiyo nimshukuru Mheshimiwa Mbunge, lakini nitaomba ushirikiano wa Waheshimiwa Wabunge wa dhati. Ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Muda umekwenda Waheshimiwa, tunaendelea swali linalofuata, Mheshimiwa Justin Joseph Monko. Na. 44 Hitaji la Vituo vya Afya Tarafa ya Mtinko – Singida Kaskazini MHE. JUSTIN J. MONKO aliuliza:- Tarafa ya Mtinko Jimbo la Singida Kaskazini yenye Kata sita haina kituo cha afya cha Serikali:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (a) Je, Serikali ipo tayari kukamilisha jengo la kituo cha afya katika Kata ya Makuro lililojengwa na wananchi ili wananchi waweze kupata huduma za rufaa kutoka katika Zahanati zilizopo? (b) Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha za majengo ya ziada katika kituo cha afya Kata ya Makuro ili kutoa huduma bora kwa wananchi? MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Waitara. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages264 Page
-
File Size-