Tarehe 2 Mei, 2017

Tarehe 2 Mei, 2017

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Kumi na Tano – Tarehe 2 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae, tunaendelea na Mkutano wetu wa Saba, leo ni Kikao cha Kumi na Tano. Katibu! NDG. NENELWA M. WANKANGA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/2018. NDG. ALMAS A. MAIGE - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE: Taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu Shauri la Kudharau Mamlaka ya Spika 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) linalowahusu Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe na Mheshimiwa Halima James Mdee. Taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu Shauri la Kuingilia Uhuru na Haki za Bunge linalowahusu Ndugu Paul Christian Makonda na Ndugu Alexander Pastory Mnyeti. Taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu Shauri la Kudharau Mamlaka ya Spika linalomhusu Mheshimiwa Ester Amos Bulaya. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati. Naomba Katibu hizo taarifa Waheshimiwa Wabunge wagaiwe mapema. Katibu tuendelee. NDG. NENELWA M. WANKANGA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali la kwanza linaulizwa na Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba, Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Na. 119 Ujenzi wa Barabara ya Mwandiga - Chenkele - Kagunga MHE. PETER J. SERUKAMBA aliuliza:- Mheshimiwa Rais alipokuja kwenye kampeni aliahidi kuanza ujenzi wa barabara ya Mwandiga – Chankele – Kagunga. Je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, barabara ya Mwandiga – Chankele - Kagunga yenye urefu wa kilometa 55.76 ipo katika eneo la mwambao wa Ziwa Tanganyika. Tayari upembuzi yakinifu umefanyika na kubaini kuwa zinahitajika shilingi bilioni saba kuweza kujenga barabara hiyo. Mheshimiwa Spika, kutokana na uwezo mdogo wa Halmashauri, ilikubalika kupitia Kikao cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Kigoma, iweze kuhudumiwa na Wakala wa Barabara Mkoa (TANROADS). Maombi hayo yamewasilishwa kwa Waziri mwenye dhamana na ujenzi kwa ajili ya kupata kibali. SPIKA: Swali la nyongeza, Mheshimiwa Peter Serukamba. MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya nadhani Mheshimiwa Naibu Waziri hakuwasiliana na watu wa ujenzi, kwa hiyo, kinachoendelea ni zaidi ya hiki alichokisema. Kwa hiyo, naomba labda hili swali nilitoe. SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Lubeleje, Mbunge wa Mpwapwa, swali la nyongeza. MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Meneja wa TANROADS wa Mkoa ameshaikagua barabara ya kutoka Gulwe – Berege – Chitemo – Mima – Chazima - Igodi Moja – Igodi Mbili mpaka Seluka; na kinachosubiri sasa hivi ni barabara hii ipandishwe hadhi ili iwe barabara ya Mkoa. Je, Mheshimiwa Waziri anasemaje na kwa ombi hilo Serikali inawaambiaje wananchi wa maeneo hayo? 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Hili lilikuwa ni la watu wa ujenzi wenyewe, lakini Mheshimiwa Naibu Waziri kama una maelezo kidogo, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lubeleje, grader la zamani, makali yale yale kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Lubeleje swali hili alikuwa akiliuliza mara kadhaa na hapa umesema kwamba ni kweli. Kwa sababu naamini wenzetu wa Wizara ya Ujenzi jambo hili walishalisikia na ninakumbuka Naibu Waziri wa Ujenzi siku ile alikuwa analizungumza suala hili kwamba jambo hili linafanyiwa kazi. Imani yangu ni kwamba kwa sababu barabara hii ni ya kimkakati nami nakiri wazi kwamba na wewe barabara hii inakuhusu katika eneo lako. Basi naamini Wizara ya Ujenzi itafanya kila liwezekanavyo barabara hii kuipa kipaumbele katika yale matakwa ya wananchi wa eneo hilo. SPIKA: Ahsante sana. Swali linalofuata ni la Mheshimiwa Saumu Heri Sakala, Mbunge wa Viti Maalum. Na. 120 Mpango wa Kutengeneza Magari ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani MHE. SAUMU H. SAKALA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza magari yaliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa haraka kutokana na uhaba wa magari unaosababishwa na ubovu wa magari? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saumu Heri Sakala, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ina jumla ya magari 15 ambapo kati ya hayo magari 11 yanafanya kazi. Matengenezo ya magari ya Halmashauri yanafanyika kupitia fedha za matumizi mengineyo zinazotengwa kila mwaka. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri hiyo iliidhinishiwa shilingi 52,500,000 kwa ajili ya matengenezo ya magari na katika mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri hiyo imetengewa shilingi milioni 73. Hivyo, Halmashauri inashauriwa kuweka kipaumbele na kuhakikisha fedha zinazotengwa zinatumika kutengeneza magari ili kuimarisha usimamizi wa Halmashauri. SPIKA: Mheshimiwa Saumu, nilikuona, swali la nyongeza. MHE. SAUMU H. SAKALA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ambayo nimepata kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini ningependa kumweleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Pangani ina magari mawili tu kati ya hayo magari 11 ambayo umeyataja, lakini magari yale ni chakavu mno kiasi kwamba yanapoenda service basi yanalazimika kutengeneza kitu zaidi ya kimoja yaani sio service tu ya kawaida, lazima unakuta na vitu vingine vinakuwa vimeharibika pale. Mheshimiwa Spika, Serikali pengine haioni umuhimu wa kununua magari mengine mapya badala ya kuacha magari yale chakavu yaendelee kutumikia Hospitali ya Wilaya ya Pangani? Ahsante. (Makofi) SPIKA: Majibu ya swali hilo la magari chakavu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, ni kweli, na mimi 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) nilivyofika Pangani, Mheshimiwa Mbunge anakumbuka nimefika pale nimeona changamoto hii ya magari. Magari yale ni kweli ni miongoni mwa magari chakavu kama ilivyo katika Halmashauri nyingine. Nikijua wazi kwamba kipaumbele cha kununua magari ya Halmashauri huwa yanafanywa hasa na Halmashauri yenyewe ikianzia katika mchakato wa awali. Hata hivyo, Serikali katika kuimarisha huduma ya afya, tulinunua karibu magari 50 tukapeleka katika maeneo ambayo vipo vifo vingi zaidi. Hata hivyo tuna mkakati mwingine, tukipata gari la ziada tutafanya hivyo. Mheshimiwa Spika, suala la ununuzi wa magari naomba watu wa Halmashauri ya Pangani tuweke kipaumbele, lakini Serikali haitasita kusaidia wananchi wa Pangani tukijua wazi Jimbo lile na eneo lile jiografia yake iko tata sasa; ukitoka pale Hospitali watu wa Mwela huku na watu wa upande mwingine wana changamoto kubwa sana mpaka kwenda eneo lile. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali tunaliangalia hilo, lakini tutashirikiana vyema na wenzetu wa Pangani kuhakikisha mambo yao yanaenda vizuri. (Makofi) SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Saddiq Murad, swali la nyongeza. MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Spika, naomba nami niulize swali moja dogo la nyongeza kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Mheshimiwa Naibu Waziri umetembelea Wilaya ya Mvomero na umejionea mwenyewe hali halisi ya Wilaya; leo gari la afya ambalo linatumika kwa ajili ya chanjo ndilo linatumika kwa ajili ya kukusanya mapato, lakini Idara ya Ujenzi haina gari, magari yote ni chakavu. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kutusaidia sisi watu wa Mvomero ili tuweze kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano? 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, anachosema ni kweli. Siku ya Alhamisi tulikuwa Jimboni kwake pale na tulitembelea mpaka Hospitali ya Wilaya na kubaini changamoto na jiografia ya eneo lile kuanzia Turiani na maeneo mengine. Mheshimiwa Spika, eneo lile ni kweli, hata nilipokutana na wataalam pale, kuna changamoto ya magari. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama nilivyosema pale awali ni kwamba mchakato wa ununuzi wa magari mara nyingi sana unaanza na kipaumbele cha Halmashauri yenyewe, lakini kwa sababu tuko pamoja hapa na Mbunge siku ile tulikubaliana mambo mengine ya msingi. Tutaendelea kushirikiana vya kutosha kuona ni jinsi gani tutaiwezesha Halmashauri ya Mvomero iweze kufanya vizuri. Ndiyo maana Serikali hata katika suala zima la miundombinu, wewe unafahamu jinsi tunavyowekeza pale hata katika ujenzi wa lami. Lengo kubwa ni kwamba wananchi wa Mvomero wapate matunda mazuri ya Mbunge wao. Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itashirikiana naye, pale kwenye mahitaji ya haraka tutafanya kwa ajili ya wananchi wake na watendaji waweze kufanya kazi vizuri katika Jimbo la Mvomero. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Afya, majibu ya nyongeza. WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    378 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us