NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 16 Aprili, 2019 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae. Katibu. NDG. ATHUMAN B. HUSSEIN – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA (MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wa Rais (Muungano) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA (MHE. KANALI (MST) MASOUD ALI KHAMIS): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. LATHIFAH H. CHANDE (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA - MHE. ALLY SALEH ALLY): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MWENYEKITI: Ahsante. Katibu. NDG. ATHUMAN B. HUSSEIN – KATIBU MEZANI: Maswali. MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa, tutaanza na Ofisi, ya Waziri Mkuu swali la Mheshimiwa Paschal Yohana Haonga. Na. 88 Madai ya Wastaafu Waliokuwa Wanachama wa PSPF MHE. PASCHAL Y. HAONGA aliuliza:- Kuna watumishi katika Halmashauri nyingi za Wilaya nchini walikuwa wanachama wa PSPF wamestaafu zaidi ya 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) mwaka mmoja na hawajalipwa fedha zao za kiiunua mgongo (pension) na kwa sasa wanaishi maisha ya taabu na mateso makali:- (a) Je, ni lini sasa Serikali itawalipa wastaafu hawa? (b) Inasemekana kwamba Serikali imetumia vibaya fedha za PSPF ikiwa ni pamoja na kukopesha baadhi ya watu na taasisi: Je, Serikali haioni kwamba hii inaweza kuwa sababu mojawapo ya kucheleweshwa mafao kwa wastaafu? (c) Fedha za kiinua mgongo ni mali ya Mtumishi anayestaafu: Je, kwa nini Mifuko ya Pensheni isiwakopeshe wastaafu watarajiwa angalau 40% ya fedha hizo bila riba pale inapobaki miaka 10 kabla ya kustaafu? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Paschal Yohana Haonga, Mbunge wa Mbozi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka kufikia tarehe 28 Februari, 2019 Mfuko mpya wa PSSF ulikuwa umekamilisha kulipa malimbikizo ya deni la wastaafu lilorithiwa kutoka Mfuko wa PSPF ambapo jumla ya wastaafu 9,971 wamelipwa stahiki zao zilizofikia kiasi cha shilingi bilioni 888.39. Aidha, Mfuko umekamilisha mfumo wa ulipaji mafao utakaowezesha kufanya malipo katika ngazi ya mkoa na hivyo kuwezesha mfuko kulipa mafao ndani ya muda uliowekwa kisheria wa siku 60 tangu mwanachama anapowasilisha madai. Mheshimiwa Mwenyekiti, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge iliyoanzisha mfuko husika. Sheria hiyo pamoja na mambo mengine inasimamia muundo wa utawala na mfumo wa maamuzi na usimamizi wa uwekaji wa fedha za mifuko. Aidha, sheria 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) inaipa Bodi ya Wadhamini ya mfuko jukumu la kusimamia uwekezaji wa fedha za mfuko kwa uhuru. Hivyo basi, siyo kweli kwamba Serikali inaweza kuingilia uendeshaji wa mifuko au kufanya maamuzi ya uwekezaji ikiwemo kukopesha taasisi au watu binafsi. Mheshimiwa Mwenyekiti, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, imekuwa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanachama wake kupitia vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS) katika maeneo ya kazi. Kwa mujibu wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za mfuko. Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii zinaruhusu wanachama kutumia sehemu ya mafao yao kama dhamana kwa ajili ya kujipatia mkopo wa nyumba kutoka katika mabenki na taasisi za fedha nchini ili kuwawezesha kuboresha makazi wakati wa kipindi cha utumishi wao. Aidha, Kanuni Na. 24 na 25 ya kanuni mpya za Mafao ya Hifadhi ya Jamii za mwaka 2018 zimetoa wigo mpana zaidi kwa wanachama waliochangia kwa miaka isiyopungua 10 kuweza kupata huduma hii tofauti na hapo awali ambapo ni wanachama waliokuwa wametimiza umri kuanzia miaka 55 ndio waliweza kupatiwa mikopo ya kujenga vyumba. MWENYEKITI: Mheshimiwa Haonga. MHE. PASCHAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa mtumishi anapokuwa anaajiriwa, mara ya kwanza na kwenye salary slip yake inaonesha muda atakaostaafu, hivyo inakuwa siyo suala ambalo ni la ghafla, lakini Serikali imekuwa ikichelewa sana kuwalipa watumishi hawa: Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka inapokuwa wamesababisha ucheleweshwaji wa mafao kwa watumishi wa Umma inataikiwa walipe kwa riba? (Makofi) 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Halmashauri ya Mbozi kuna watumishi 35 wamestaafu toka Septemba, 2018, hadi sasa hawajalipwa fedha zao na wanaidai Serikali na wanaishi maisha magumu sana: Je, ni lini sasa Serikali itaacha kuwatesa watumishi hawa wanaoishi maisha ya taabu sana kwa sababu ya ucheleweshaji wa fedha zao? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza Mheshimiwa Haonga amezungumza kuhusu ucheleweshwaji wa ulipaji wa mafao. Kwa mujibu wa sheria ambayo tumeipitisha hapa ndani Bungeni hivi sasa, inautaka mfuko kulipa mafao ya mstaafu ndani ya siku 60. Mheshimiwa Mwenyekiti, zilikuwepo changamoto nyingi hapo awali, nyingi sio kwambwa zinasababishwa na mfuko husika lakini pia wale wastaafu katika namna moja ama nyingine katika uandaaji wa nyaraka na kufuatilia taarifa zao imekuwa pia ikileta changamoto. Baada ya kuunganisha mifuko hii na kwa kutumia sheria mpya, hivi sasa PSSF wameweka utaratibu na motto wao ni kwamba wanalipa mafao tangu jana. Mheshimimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi sasa zoezi la ulipaji wa mafao kwa wastaafu linafanyika kwa kiwango kikubwa sana na kwa idadi ambayo nimesema tayari imeshalipwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu watumishi katika Jimbo lake la Mbozi, kwa sababu hii inakwenda case by case, nisilisemee kwa ujumla, lakini nichukue tu fursa hii kumwambia Mheshimiwa Haonga kwamba ofisi yetu iko wazi, kama kuna madai ya watumishi ambao mpaka hivi sasa bado hawajalipwa mafao yao, basi anaweza kuyasilisha ili sisi Ofisi ya Waziri Mkuu tuweze kufuatilia mkoa husika tujue 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) changamoto ni nini na baada ya hapo tuweze kutatua changamoto yao. Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali kulipa mafao yao kwa wakati kabisa ili kuwafanya watumishi hawa waishi katika maisha ya amani. MWENYEKITI: Ahsante Waheshimiwa, tunaendelea na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Mheshimiwa Bonnah Kamoli. Na. 89 Hitaji la Masoko la Segerea MHE. BONNAH M. KALUWA aliuliza:- Wananchi wa Kata za Kinyerezi, Bonyokwa, Segerea Liwiti, Kipawa, Kimanga, Kisukulu na Tabata wamekuwa wakitumia fedha na muda mwingi kwenda kutafuta bidhaa na huduma katika masoko ya Buguruni na Kariakoo kutokana na kukosa huduma hizo katika maeneo yao:- (a) Je, kwa nini Serikali isijenge soko kubwa katika eneo mbadala lililo katikati na linaloweza kufikiwa na wananchi hao kwa wakati? (b) Je, kwa nini Soko la Kinyerezi lililozinduliwa na Mwenge mwaka 2017 lisifunguliwe ili kutoa huduma kwa wananchi wanaozunguka soko hilo na maeneo ya karibu? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bonnah Kamoli, Mbunge wa Segerea, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala iliweka kipaumbele cha kutekeleza mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Soko la Kisutu utakaogharimu takribani shilingi bilioni 12.17. Mpaka sasa mradi huo umepatiwa jumla ya shilingi bilioni 3.92 na ujenzi unaendelea. Aidha, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetenga shilingi milioni 200 kwa ajili ya kujenga masoko mengine ndani ya Manispaa ya Ilala. Halmashauri inashauriwa kutumia fursa ya miradi ya kimkakati na kuandaa andiko la mradi wa kujenga masoko katika Kata ya Kinyerezi, Bonyokwa, Segerea, Liwiti Kipawa, Kimanga, Kisukulu na Tabata ili kupata fedha za utekelezaji. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Soko la Kinyerezi lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 limepangwa kuanza kutumika Mei, 2019 baada ya matengenezo ya choo ambacho kilikuwa hakijakamilika kwa wakati huo. MWENYEKITI: Mheshimiwa Kamoli. MHE. BONNAH M. KALUWA: Mheshimiwa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages325 Page
-
File Size-