JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ___________ HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2021/22 Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishiriki katika mazoezi Jijini Dodoma mwezi Novemba, 2020. Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 7 Mei, 2021. Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikata utepe katika MEI, 2021 DODOMA Uzinduzi wa Ajenda ya Kitaifa ya Kuwekeza katika Afya na ___________________________________________________________________________ Maendeleo kwa Vijana Balehe uliofanyika mwezi Aprili, 2021. KIMEPIGWA CHAPA NA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI,DODOMA-TANZANIA Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Aliyekuwa Rais Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Uzinduzi Jinsia, Wazee na Watoto akipata maelezo kuhusu Mradi wa Kilimo kutoka wa Hospitali ya Kanda Chato mwezi Januari, 2021. kwa Mtaalam wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Best Agriculture Practice Kingkong Mosile alipotembelea Shirika hilo Mkoani Arusha mwezi Mei, 2021. Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais na Mkewe Mama Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Mbonimpaye Mpango wakiwaangalia watoto wanaolelewa Jinsia, Wazee na Watoto akikagua mashine ya kisasa ya CT katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Simulator inayotumika kupanga Tiba Mionzi katika Taasisi ya Dodoma walipotembelea Kituo hicho mwezi Aprili, 2021. Saratani Ocean Road mwezi Julai, 2020. HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2021/22 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ndani ya Bunge lako Tukufu, ambayo imechambua Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ninaomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka 2020/21 na Vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2021/22. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida pamoja na Miradi ya Maendeleo ya Wizara kwa mwaka 2021/22. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu na kuwasilisha hotuba yangu siku ya leo. Aidha, kwa 1 masikitiko makubwa, napenda kutumia fursa hii kutoa pole kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge Wote, Chama Cha Mapinduzi pamoja na Watanzania wote kwa kuondokewa na mpendwa wetu, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, napenda kutoa pole kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuondokewa na Viongozi Wakuu, Hayati Benjamin William Mkapa, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Balozi Mhandisi John Herbert Kijazi, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kazi ya Mungu haina makosa, hili ni pigo kwetu sote na inatulazimu kulikubali na kuendelea pale walipoishia. Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. 3. Mheshimiwa Spika, vilevile, naomba kutoa pole kwako, Bunge lako Tukufu, kwa familia na wananchi wa Mkoa wa Manyara kwa kifo cha Mheshimiwa Martha Umbulla, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) aliyefariki tarehe 20 Januari, 2021 katika Hospitali ya HCG Mumbai, nchini India 2 alikokuwa akipatiwa matibabu. Aidha, natoa pole kwako na familia kwa kifo cha Mheshimiwa Atashasta Justus Nditiye aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Muhambwe (CCM) aliyefariki tarehe 12 Februari, 2021. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. 4. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu na kuwa Rais wa Kwanza Mwanamke Shupavu kuiongoza nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, ninampongeza Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kipekee sana, namshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuonesha imani yake kubwa kwangu na kuniteua kuendelea kuiongoza Wizara kwa maslahi mapana ya nchi. 5. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri uliowezesha kuleta tija na ufanisi katika utendaji 3 na kuimarisha huduma zinazotolewa katika Sekta ya Afya na Sekta ya Maendeleo na Ustawi ya Jamii. Aidha, ninampongeza kwa hotuba yake aliyoiwasilisha kwenye Bunge lako Tukufu tarehe 13 Aprili, 2021 ambayo imetoa mwelekeo wa majukumu yatakayotekelezwa na Serikali katika mwaka 2021/22. 6. Mheshimiwa Spika, ninapenda kukupongeza wewe binafsi kwa kuendelea kutekeleza majukumu yako kwa ufanisi mkubwa katika kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, ninampongeza Naibu Spika Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) katika utekelezaji wa majukumu yake. Vilevile, nitumie fursa hii kuwapongeza Wenyeviti wa Bunge kwa kusimamia vyema mijadala ndani ya Bunge. 7. Mheshimiwa Spika, ninapenda kuwashukuru Mawaziri wenzangu kwa ushirikiano walionipatia ambao umeiwezesha Wizara ninayoiongoza kuendelea kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma za Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii. Wizara itaendelea kushirikiana nao na kuhakikisha tunatimiza dhamira ya Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Afya inaratibiwa vyema na 4 watanzania wanakuwa na afya bora ili washiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa viwanda. 8. Mheshimiwa Spika, kipekee ninapenda kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo (Mb), na Makamu wake, Mheshimiwa Aloyce John Kamamba (Mb) kwa ushauri na maelekezo waliyoyatoa wakati wa maandalizi ya Bajeti hii. Aidha, ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikiano mzuri wanaonipatia ikiwemo kutoa ushauri na maoni mbalimbali yenye lengo la kuboresha huduma za Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii. Ninawaahidi kwamba, Wizara ninayoingoza itazingatia ushauri wao na kuendelea kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu na kazi zetu za kuwatumikia wananchi ndani na nje ya Bunge. 9. Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo ya awali, ninapenda sasa kutoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka 2020/21 (Fungu 52 na Fungu 53), Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi pamoja na Maombi ya Fedha ya kutekeleza Vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2021/22 (Fungu 52 na Fungu 53). 5 B. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2020/21 10. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake, Wizara imeendelea kuzingatia Sera, Mpango Mkakati pamoja na Makubaliano ya Kitaifa na Kimataifa yenye lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya, ustawi na maendeleo ya jamii nchini. Sera hizo ni pamoja na Sera ya Maendeleo ya Jamii (1996); Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000); Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (2001); Sera ya Taifa ya Wazee (2003); Sera ya Afya (2007); na Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008). Vilevile, katika kuandaa mpango na bajeti, Wizara imezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo (2025), Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22- 2025/26), Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs 2030). 11. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, Wizara ninayoisimamia kwa kushirikiana na Wizara nyingine, Idara na Taasisi za Serikali, Wakala wa Serikali na Wadau wa Maendeleo ilipanga kutekeleza afua mbalimbali 6 zenye lengo la kuboresha utoaji huduma za afya, ustawi na maendeleo ya Jamii katika maeneo yafuatayo:- (i) Kuendelea kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma za chanjo ili kuwakinga watoto chini ya miaka 5, akina mama wajawazito na kutoa chanjo nyinginezo za kimkakati za kukinga na kudhibiti magonjwa yanayozuilika kama Homa ya Ini, kichaa cha mbwa na mengineyo; (ii) Kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga vinavyotokana na uzazi; (iii) Kuimarisha Huduma za Lishe na Kuboresha Usafi wa Mazingira nchini; (iv) Kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa yanayoambukiza ikiwa ni Malaria, Kifua Kikuu na UKIMWI pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya Moyo, Kisukari na Saratani; (v) Kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini; (vi) Kuimarisha utoaji wa huduma za afya za kibingwa na ubingwa bobezi; (vii) Kuendelea kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma katika Hospitali ya Taifa, Maalum, Rufaa za Kanda na Mikoa; 7 (viii) Kuimarisha mpango wa Taifa wa utayari wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko, ajali na majanga; (ix) Kuimarisha mafunzo na maendeleo ya wataalam katika Sekta ya Afya; (x) Kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo; (xi) Kukuza usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake; (xii) Kuimarisha upatikanaji wa haki na maendeleo ya mtoto; (xiii) Kuimarisha huduma za ustawi wa jamii kwa wazee
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages275 Page
-
File Size-