NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Saba – Tarehe 30 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu. NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Taarifa ya Mwaka ya Hesabu za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kwa mwaka wa fedha 2015/2016 [The Annual Report and Audited Accounts of Arusha International Conference Centre (AICC) for the Financial Year 2015/2016]. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. MARTHA J. UMBULLA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MHE. DAVID E. SILINDE - NAIBU MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MWENYEKITI: Ahsante sana. Katibu, tuendelee. NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na maswali kama kawaida. Sasa hivi tunaanza na Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora). Tutaanza na Mheshimiwa Fredy Atupele Mwakibete, Mbunge wa Busokelo. Sasa aulize swali lake. Na. 298 Tatizo la Ajira Nchini MHE. FREDY A. MWAKIBETE aliuliza:- Ajira kwa sasa ni tatizo hapa nchini hasa kwa walimu wa sanaa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuajiri katika sekta mbalimbali? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fredy Atupele Mwakibete, Mbunge wa Busokelo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo na ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7,463 katika shule za sekondari. Kutokana na hali hii Serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao (redeployment) kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka ya Serikali za Mitaa ili kila shule iweze kupata Walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi wa umma 9,721 wameshaajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 Serikali inatarajia kuajiri Watumishi 52,436 wa sekta mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na kuimarisha sekta na maeneo yenye upungufu mkubwa wa watumishi. MWENYEKITI: Mheshimiwa Fredy, swali la nyongeza. MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina swali moja tu la nyongeza. Taifa lolote duniani ili lisonge mbele linahitaji watu waliosoma kada mbalimbali, iwe ni sanaa, sayansi au biashara. Je, Serikali ina mpango gani wa ku-balance wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi, pamoja na wanafunzi wanaosoma sanaa ili isitokee kama sasa tuna ziada ya wanafunzi wa sanaa zaidi ya 7,463 na inapelekea kutokuwa 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) na ajira. Serikali ina mpango gani kwa miaka ya hivi karibuni na baadaye? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Elimu, majibu. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Serikali, imekuwa ikiendelea kuweka mazingira mazuri na kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi. Katika mwaka 2015 mpaka 2016 Serikali ilijikita zaidi katika kuhamasisha Shule za Sekondari kujenga maabara. Katika mwaka 2016/2017 tunasambaza vifaa vya maabara. Hizo zote ni jitihada za kuongeza wanafunzi wa masomo ya sayansi. Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kwamba wanafunzi wanayo hiari ya kuchagua masomo. Kwa hiyo, kama Serikali tunatoa mazingira mazuri. Nangependa kuwaomba Waheshimiwa Wabunge tushirikiane kuwahamasisha wanafunzi pia kuona kwamba masomo ya sayansi na teknolojia nayo ni muhimu ili waweze kuyachukua kwa wingi zaidi. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kapufi na Mheshimiwa hapo utafuata. MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Upungufu mkubwa wa Ikama na zoezi la uhakiki wa vyeti limepelekea shida kubwa ya watumishi katika maeneo ya afya, elimu, Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata katika Manispaa yetu ya Katavi, kiasi cha kwamba mtumishi mmoja anafanya kazi zaidi ya moja. Ni lini Serikali itaajiri katika maeneo hayo niliyoyazungumza? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa ufupi. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Tunakiri ni kweli kuna upungufu 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) mkubwa wa watumishi katika baadhi ya maeneo. Niendelee tu kusisitiza kwamba lengo letu kubwa kama Serikali ni kuhakikisha kwamba, tunaenda kwa kuzingatia maeneo yenye vipaumbele. Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tutahakikisha kwamba tunaimarisha maeneo yenye upungufu mkubwa. Nimweleze tu kwamba katika kada alizozitaja zitakuwa ni miongoni mwa kada ambazo pia tutazipa ajira katika mwaka ujao wa fedha. Vilevile labda nimtoe tu hofu kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi; katika mwaka ujao wa fedha tutatoa ajira 52,436 na labda tu niseme kwa mchanganuo ufuatao:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Sekta ya Elimu tutatoa ajira 16,516 kwa upande wa Sekta ya Afya 14,102, Kilimo 1,487, Mifugo 1,171, Uvuvi 320, Polisi 2,566, Magereza nafasi 750, Jeshi la Zimamoto 1,177, Uhamiaji nafasi 1,500, hospitali za mashirika ya kidini na hiari kwa kuwa nazo tunatoa ruzuku, nafasi 174 pamoja na nafasi nyinginezo 12,673 ambazo zitahusu Sekta zote na jumla kuu ni 52,436. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimtoe Mheshimiwa Kapufi hofu, ikama zote na mapendekezo kutoka kwa waajiri tumezipokea na tutaangalia katika kuimarisha maeneo hayo. MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri. Mheshimiwa Gekul. MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mheshimiwa Waziri ulituahidi kwamba unaajiri walimu wa hesabu katika shule zetu, lakini ajira iliyotoka mwezi wa nne kwa upande wa walimu ni walimu wa biology na chemistry, ulituletea katika shule zetu. Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi nimesema katika Bunge hili kwamba, katika shule zangu kumi za Babati Mjini za sekondari hakuna shule yenye mwalimu wa hesabu. Sasa naomba nifahamu ni kwa nini msituambie kwamba 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) walimu wa hesabu ninyi hamna na hamna mpango wa kutuletea badala ya kutuahidi kila siku kwamba mtatuletea walimu? Watoto wetu hawasomi hesabu. Naomba kauli ya Serikali. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Bahati nzuri ninayo orodha ya nafasi 3,081 za walimu wa hesabu na sayansi ambao tumewapangia vituo katika mwezi Aprili. Mheshimiwa Mwenyekiti, Babati Mjini naweza kuangalia kwa haraka haraka, lakini nitoe tu mfano kwa Tarime DC, tumepeleka walimu wa hesabu, Musoma DC tumepeleka walimu wa hesabu. Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tutaliangalia na kama katika Manispaa yake hajapata kabisa, tutaweza kulifanyia kazi ili naye aweze kupata walimu hao. Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda tu kumtoa hofu Mheshimiwa Gekul kwamba tulitoa kibali cha walimu wa sayansi na hesabu 4,129 na hizi ni kwa ajira za mwaka 2015. Tayari ukiangalia tumepata tu Walimu 3,081, bado kuna nafasi zaidi ya 1,000 na zaidi katika kibali hicho ambacho tumekitoa, bado hawajajitokeza. Tunashirikiana na Wizara ya Elimu pamoja na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) tuweze kupokea maombi hayo, tumeanza kuyachambua. Watakaopatikana naamini ikitokea na walimu wa hesabu wako katika kundi hilo, basi kwa hakika kabla ya mwaka wa fedha na wewe utakuwa umepata walimu hao wa hesabu. MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto. Tunamkaribisha Mheshimiwa Faida Mohamed Bakar, Mbunge wa Viti Maalum aulize swali lake. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 299 Sheria Zinazowanyima Haki Watoto na Wanawake Nchini MHE. FAIDA MOHAMED BAKAR aliuliza:- Sheria nyingi nchini hususan zile zinazohusu haki na stahili za wanawake zimepitwa na wakati na hivyo kuwanyima haki wanazostahili makundi hayo. (a) Je, ni sheria zipi zinazowanyima haki wanawake na watoto nchini? (b) Je, ni lini Serikali italeta miswada ili kuboresha au kubadilisha sheria hizo ili ziendane na wakati na kuwapatia haki zao wanawake na watoto? NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Faida Mohammed Bakar, Mbunge wa Viti Maalum, lenye vipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria za Mirathi za Kimila (Customary Declaration Orders, GN. No. 279 na 436 za mwaka 1963 zimekuwa zikiwanyima haki za urithi na umiliki wa ardhi wanawake na watoto. Vilevile Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 katika Kifungu cha 13 na 17 vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo wa miaka 14 au 15 kwa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages289 Page
-
File Size-