Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Tatu – Tarehe 17 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2006/2007. MWENYEKITI WA KAMATI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA: Maoni ya Kamati ya Uwekezaji na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI: Maoni ya Kambi ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, pamoja na Maoni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. SPIKA: Waheshimiwa kabla sijamwita Katibu kwa hatua inayofuata, inanibidi kutambulisha baadhi ya wageni. Kwanza, ninayo furaha kumtambulisha mke wa Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, Bibi Zainabu akiwa na wanawe pale. Nadhani ni utaratibu mzuri Waheshimiwa Mawaziri wa jinsia zote mbili, wenzi wao wawe wanakuwa hapa siku ya kuwasilisha hoja. (Kicheko) 1 Wageni wetu wale wa Jimbo la Lulindi waliokesha njiani, Madiwani 14, wamekwisha wasili. Mheshimiwa Suleman Kumchaya nadhani ndio wageni wake, nadhani watakuwa mkono wangu wa kulia pale. Wale wanatupungia mkono. Ahsante Wapo wageni ambao ni viongozi wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu (Leo mashine yetu inayowasaidia Walemavu kupanda juu kwenye Public Gallery haifanyi kazi) kwa hiyo niliomba wawe kwenye hii Gallery hii hapa kushoto, sijui kama wameweza kufika. Basi tutambue kuwepo kwao. Wapo pia wageni kutoka Jimbo la Kilindi, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogowadogo wa madini kutoka Wilaya hiyo. Mwisho kabisa wapo wageni kutoka kwa Mheshimiwa Ezekiel M. Maige na Mheshimiwa James D. Lembeli, wako Madiwani 10 kutoka Halmashauri ya Kahama wakiongozwa na Mwenyekiti wao ambaye ni Mama Martina Sazia. Ahsante sana. (Makofi) MASWALI NA MAJIBU Na. 214 Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe MHE. EMMANUEL J. LUHAHULA Aliuliza:- Kwa kuwa Wilaya ya Bukombe ni moja kati ya Wilaya ambazo hazina muda mrefu tangu kuanzishwa na inategemea huduma za afya hasa kwenye Hospitali ya Kahama iliyo umbali wa km 100 x 2 = 200 na hospitali ya Biharamulo na kuwa kuwa Bukombe imejitahidi sana kuanzisha ujenzi wa hospitali ya Wilaya kwa nguvu za wananchi, wadau mbalimbali ikiwemo Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. (a) Je, Serikali inaweza kulieleza Bunge mikakati iliyoandaliwa ya kuhakikisha ukamilishaji wa OPD’s, Wodi na kwamba, sehemu nyingine za ujenzi zitakamilika katika Bajeti ili wananchi waanze kupata huduma kwa karibu zaidi na kuokoa maisha ya wananchi wa maeneo hayo? (b) Kwa kuwa, hospitali hiyo iko mbioni kukamilika kama Serikali ikitenga fungu la kufanya hivyo haraka. Je, Serikali inaweza kutanga fedha za ununuzi wa vifaa hivyo vikiwemo vifaa vya theatre, X-ray, OPD’s, Dental Eye na MCH Departments? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Jumanne Luhahula, Mbunge wa Bukombe lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- 2 (a) Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe ulianza mwaka 2002 na umechangiwa kama ifuatavyo:- (i) Nguvu za wananchi – Shilingi milioni 20.7; na (iii) Serikali Kuu - Shilingi milioni 133.9. Aidha Serikali kupitia Local Government Capital Development Grant, mwaka 2005/2006 imepeleka jumla ya Shilingi milioni 191.0 kwa awamu ya kwanza. Kati ya fedha hizi Shilingi milioni 44.0 zimeelekezwa katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya. Mheshimiwa Spika, hali ya utekelezaji wa ujenzi wa Hospitali ni kama ifuatavyo:- (i) Jengo la huduma za akina mama na watoto limekamilika. (ii) Wodi tatu za wazazi, wanawake na wanaume zimekamilika. (iii) OPD iko katika hatua za mwisho za umaliziaji. (iv) X-ray unit iko hatua za mwisho za umaliziaji. (v) Minor- theatre iko hatua za mwisho za umaliziaji. Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe itapelekewa jumla ya Shilingi milioni 313.1 kama awamu ya pili ya Local Government Capital Development Grant. Asilimia 50 ya fedha hizo zitaelekezwa katika miradi ya ngazi ya Wilaya ikiwa ni pamoja na hospitali ya Wilaya. Ukamilishaji wa ujenzi wa Hospitali utategemea jinsi Halmashauri yenyewe itavyolipatia suala la ujenzi wa Hospitali umuhimu. Ikumbukwe kwamba Halmashauri yenyewe ndiyo inayoweka vipaumbele katika shughuli za maendeleo. (b) Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika swali (a) jukumu la kupanga shughuli za maendeleo ni la Halmashauri yenyewe. Idara mbalimbali zitakapoanza kufanyakazi vitendea kazi kama X-ray na vifaa vingine katika Idara za utalaam wa meno na macho na MCH vitanunuliwa kutoka bohari ya vifaa vya hospitali. Serikali Kuu na Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe zitashirikiana kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinapatikana. 3 MHE. EMMANUEL J. LUHAHULA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri; naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza: Kwa kuwa ukamilishaji wa Hospitali hii ya kisasa uko mbioni na ambapo wakati wowote mwezi huu inaweza ikafunguliwa rasmi ili iweze kuanza kutumika kwa sehemu iliyokamilika:- (a) Je, Serikali iko tayari kutoa vibali vya ajira tutakazozihitaji kwa ajili ya Hospitali hiyo na pamoja na hilo, Wizara itutumie Wataalam wengine kutoka Vyuoni kama ilivyokwisha ahidi? (b) Je, Serikali inaweza kuwahakikishia wananchi wa Bukombe na Bunge hili Tukufu kwamba itawaunga mkono wananchi hawa kwa kuwapatia Ambulance haraka iwezekanavyo kwa juhudi walizozifanya na hapo hapo Waziri atakuwa tayari kupokea orodha ya technical equipment tutakazozihitaji ili nimkabidhi wazinunue? SPIKA: Mheshimiwa, nimegundua baadaye kwamba unaonekana ulikuwa kama unasoma hilo swali. Ila nilichelewa tu kwa sababu nilikuwa napewa karatasi moja hapa. Kwa hiyo, ni bahati tu nimekuachia. WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba Nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyoyatoa na vile vile nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Emmanuel J. Luhahula, kwa pamoja kama ifuatavyo:- Kama alivyosema, hiyo Hospitali imefikia hatua ya kuizindua na nimekuwa na bahati ya kuizindua hiyo Hospitali kwa Niaba ya Serikali siku ya Ijumaa inayofuata. Ningependa kusema kwamba hiyo itanipa fursa ya kwenda kuikagua na kuelekeza na kuangalia mapungufu yako wapi ili tujue Serikali itafanyaje ili kuikamilisha kama Hospitali zingine. MHE. FUYA G. KIMBITA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Swali langu ni kwamba naulizia. Je, Serikali kwa kupitia Serikali za Mitaa labda, ina mpango gani wa kuimarisha Hospitali zilizopo kwenye njia kuu (high way) kutokana na hii hali ya ajali zinazotokea mara kwa mara hata ile ya Wilaya ya Hai ikiwa mojawapo? 4 SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nadhani hilo ni swali jipya. Tunaendelea. Swali linalofuata! 5 Na. 215 Matengenezo ya Barabara Wilayani Sengerema MHE. ERENEST G. MABINA aliuliza:- Kwa kuwa, mkakati wa kitaifa wa kupunguza umaskini na kukuza uchumi (MKUKUTA) unatambua umuhimu wa kuwepo Benki ya Kitaifa ya Maendeleo ya Wanawake, Tanzania kama nyenzo mojawapo ya kupambana na adha ya umaskini na kwa kuwa Serikali imekwishaamua benki hiyo ianzishwe:- (a) Je, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inachukua hatua gani za vitendo kuanzisha benki hiyo? (b) Je, Wizara haioni kwamba, kuendelea kuchelewesha uanzishwaji wa benki hiyo, kunawakatisha tamaa wanawake wa nchi yetu na kupunguza ari na kasi ya maendeleo yao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Naomba kujibu swali la Mbunge kwamba barabara ya Nzera – Sungusira ni barabara ya Mkoa na iko kwenye kiwango cha changarawe. Aidha, barabara ya Sungusira – Idoselo – Misri – Mkolani – Lubanga hadi Busilasoga ni barabara ya Wilaya na ina urefu wa km. 53. Barabara hii imekuwa ikifanyiwa matengenezo mara kwa mara kama ifuatavyo:- xKwa Mwaka wa fedha 2003/2004, barabara ya Sungusira – Idosela yenye urefu wa km. 6 ilifanyiwa matengenezo katika maeneo korofi ya Sungusira hadi Nyakibanga kwa gharama ya shilingi milioni 4.2. xMwaka wa fedha 2004/2005, barabara hiyo kutoka Misri hadi Mkolani, yenye urefu wa km. 8 ilifanyiwa matengenezo kwenye maeneo korofi kwa gharama ya Shilingi milioni 7.8. Na kutoka Sungusira – Idoselo yenye urefu wa km 6 ilifanyiwa matengenezo kwenye maeneo korofi ya Sungusira hadi Nyakibanga kwa gharama ya Shilingi milioni. 4.1. Pia katika mwaka huo huo wa fedha, barabara ya Lubanga – Nyakaduha, yenye urefu wa km. 14 ilifanyiwa matengenezo katika maeneo korofi ya Luganga hadi Nyakaduha kwa gharama ya Shilingi milioni 18.2. xMwaka wa fedha 2005/2006, barabara ya Misri – Mkolani – Lubanga imefanyiwa matengenezo ya muda maalum kwa gharama ya Shilingi milioni 37.6. hasa katika sehemu za Misri – Ibisobageni, Misri – Mkolani hadi Ibisobageni. Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha 2006/2007 Serikali kupitia Halmashauri ya imetenga jumla ya Shilingi milioni 10. kwa ajili ya matengenezo ya kawaida Fedha hizo zitatumika kufanya matengenezo katika sehemu ya Mkoani – Nzela yenye urefu wa km. 3 kwa gharama ya Shilingi milioni1.5 na Kabanwa – Nyakaduha, yenye urefu wa km 12 6 kwa gharama ya Shilingi milioni 9. Kutokana na ufinyu wa bajeti, Serikali itaifanyia matengenezo kwa kiwango cha changarawe katika barabara hiyo wakati hali ya

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    121 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us