NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Mbili – Tarehe 19 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na kikao chetu cha Kumi na Mbili, katika Mkutano wetu huu wa Tatu. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana. Katibu. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na TAMISEMI, swali litaulizwa na Mheshimiwa Katani Ahmad Katani, kwa niaba yake Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda atamwulizia swali hilo. Mheshimiwa Maimuna, tafadhali. Na. 94 Kumalizia Vituo Vya Afya – Tandahimba MHE. MAIMUNA S. MTANDA K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaunga mkono juhudi za wananchi wa Kata za Mnyawa, Nanhyanga, Nambahu, Kitama na Nguja ambao wameanza kujenga vituo vya afya kwa nguvu zao wenyewe kwa kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa vituo hivyo? SPIKA: Majibu ya Serikali kwa swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa, Dkt. Festo Dugange, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Katani Ahmad Katani, Mbunge wa Tandahimba, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kupitia mpango wa uboreshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi ulioanza katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba shilingi milioni 400 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa Kituo cha Afya Mahuta, ambapo ujenzi na upanuzi umekamilika na kituo kinatoa huduma ikiwemo ya upasuaji wa dharura. Mheshimiwa Spika, mwezi Machi, 2021 Serikali imeipatia Halmashauri ya Tandahimba shilingi milioni 150 kwa ajili ya kumalizia maboma ya zahanati nne za Miuta, Chikongo, Mnazi Mmoja na Mabamba. Vilevile, katika Mwaka wa Fedha 2021/2022, Serikali imepanga kutumia shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha maboma matatu ya zahanati na shilingi milioni 500 zitatengwa katika mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya cha Kitama. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi kwa kutenga fedha za kukamilisha maboma ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kwa awamu vikiwemo vituo vya afya katika Kata za Nanhyanga, Nambahu, Kitama na Nguja. SPIKA: Mheshimiwa Maimuna, swali la nyongeza. MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Jimbo la Tandahimba pamoja na Newala Vijijini lina changamoto ya upatikanji wa vifaatiba pamoja na vitenganishi hali ambayo wakati mwingine inasababisha akinamama wanaojifungua kwenda kutafuta kadi za kliniki mitaani. Je, upi mpango wa dharura wa Serikali wa kunusuru hali hiyo ya upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na vitendanishi? Mheshimiwa Spika, swali la pili; Jimbo la Newala Vijijini lenye Kata 22 lina vituo vitatu tu vya kutolea huduma za afya hali ambayo inaleta changamoto kubwa ya upatikanaji wa 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) huduma bora za afya kwa wananchi wake. Je, ni lini Serikali itajenga vituo vya afya katika Jimbo la Newala Vijijini ili wananchi wale wapate huduma za afya kama ambavyo inahitajika? Ahsante. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Festo Dugange, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maimuna Mtanda, Mbunge wa Newala Vijijini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya utoaji huduma za afya katika vituo vya afya kwanza kwa kutenga fedha kwa ajili ya kununua vifaatiba, vitendanishi lakini pia ununuzi wa dawa. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha huu tunaoendelea nao Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 26 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba na tayari shilingi bilioni 15 zimekwishanunua vifaatiba na vimekwishapelekwa kwenye vituo vya afya vya awamu ya kwanza na awamu ya pili. Kiasi cha shilingi bilioni 11 kiko katika hatua za manunuzi na mara moja vifaa hivyo vitanunuliwa na kupelekwa kwenye vituo hivyo. Mheshimiwa Spika, kituo cha afya katika Jimbo la Newala ni moja ya vituo vya afya vilivyojengwa katika awamu ya tatu na ya nne na hivyo vituo hivi vitakwenda kutengewa fedha za ununuzi wa vifaatiba katika mwaka wa fedha 2021/ 2022. Kwa hiyo naomba nimhakikishie Mheshimiwa Maimuna Mtanda kwamba vituo vyake hivi vya afya vitawekewa mpango wa kununuliwa vifaatiba ili viendelee kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na idadi ya vitu vya afya katika kata za Jimbo la Newala Vijijini, ni kweli Serikali 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) inatambua kwamba bado kuna uhitaji mkubwa wa vituo vya afya katika kata za Jimbo la Newala Vijijini na nchini kote kwa ujumla na ndiyo maana katika mwaka wa fedha ujao ambapo Mheshimiwa Waziri atawasilisha Bajeti ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tunatarajia kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vituo vya afya katika kata za Jimbo hili la Newala na nchini kote kwa ujumla. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, suala hili litaendelea kufanyiwa kazi. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaona lakini leo ni Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kwa hiyo mjiandikishe kuchangia. Tunaendelea na Mambo ya Ndani ya Nchi, swali la Mheshimiwa Haji Makame Mlenge, Mbunge wa Chwaka. Na. 95 Malipo ya Mafao Ya Ex E.2152 Makame Haji Kheir MHE. HAJI MAKAME MLENGE aliuliza:- Je, ni lini warithi wa askari E.152 (Makame Haji Kheir) aliyefariki tangu Mwaka 2003 akiwa mtumishi wa Jeshi la Polisi Kituo cha Madema watapewa mafao yake? NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sasa naomba kujibu swali la Mheshimiwa Haji Makame Mlenge Lengelenge, Mbunge wa Chwaka, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi Makao Makuu Dodoma na Ofisi ya Polisi Kamisheni ya Polisi Zanzibar hazijapata kumbukumbu za maombi ya mafao wala nyaraka za mirathi kumhusu Askari tajwa hapo juu kutoka kwa msimamizi wa mirathi. Aidha, kwa sasa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar limeshafanya jitihada ya kufanya mawasilinao 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) na msimamizi wa mirathi ndugu Mlenge Haji Kheir ili kupata nyaraka zinazohusiana na maombi ya malipo ya mafao ya mirathi ya askari huyo ili ziweze kushughulikiwa. Ahsante. SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Makame Mlenge, swali la nyongeza nilikuona. MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali ambayo yametolewa, lakini bado nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa sababu ni muda mrefu sasa toka marehemu alipofariki na hadi leo hajapata na alikuwa ni mtendaji wa Jeshi la Polisi. Je, ni lini sasa Serikali itawapatia mafao yao hawa wahusika? Mheshimiwa Spika, swali la pili; naamini changamoto hii haiko kwa hawa tu, iko kwa watu wengi. Sasa je, Serikali inawaahidi nini wananchi wa Tanzania ambao wana matatizo kama haya juu ya kutatua tatizo hili? Ahsante. (Makofi) SPIKA: Majibu ya maswali hayo mawili, Mheshimiwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimia Khamis Hamza Khamis. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, sasa naomba nijibu swali la Mheshimiwa Haji Makame Mlenge, Mbunge wa Jimbo la Chwaka, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, je ni lini warithi wa marehemu watapata urithi wao. Baada ya kukaa na kupekua, kwanza tumegundua kwamba kweli marehemu alikuwa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi, lakini changamoto kubwa ambayo tulifika tukakutana nayo, tulifika wakati tukakosa kujua ni nani anayesimamia mirathi ya marehemu. Sasa hii kwa kweli kwetu ikaja ikawa ni changamoto. Kwa kuwa tayari msimamizi wa mirathi hii tumeshampata, kikubwa tumwahidi tu Mheshimiwa Mbunge, tutashirikiana tuhakikishe kwamba mirathi au mafao 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) haya yanapatikana kwa wale ambao wanasimamia mirathi hii. Mheshimiwa Spika, kikubwa nimwambie binafsi niko tayari kwenda kukutana na huyo msimamizi wa mirathi na wengine wanaohusika na mirathi hii ili tuone namna ambavyo tunahakikisha watu hawa wanapata mafao yao au mirathi yao kwa wakati. Mheshimiwa Spika, lakini je ni nini sasa kauli ya Serikali katika suala hili au tuna mpango gani? Kikubwa ambacho nataka nimwambie Mheshimiwa cha mwanzo linapojitokeza jambo kama hili kwa wananchi wengine basi cha kwanza kabisa wateue au wafanye uchaguzi wa kuteua msimamizi wa mirathi, kwa sababu sisi la mwanzo tukutane na msimamizi. Yeye ndiye atakayesimamia na kutupa taarifa zote zinazohusika. La pili, tuhakikishe kwamba wanawasilisha vielelezo kwa sababu hatutaweza kujua nini shida yake kama hakuna vielelezo vilivyowasilishwa vikiwemo vya taarifa ya kifo, vikiwemo labda kituo ambacho alikuwa akifanyia kazi, mkoa na kadhalika.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages274 Page
-
File Size-