Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Kumi na Tisa - Tarehe 29 Juni, 2010 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge katika mkutano huu wa ishirini unaoendelea, Bunge lilipitisha Muswada mmoja wa sheria ya Serikali uitwao The Finance Bill, 2010. Mara baada ya kupitishwa na Bunge na baadaye kupitia katika hatua zake zote za Uchapishaji, Muswada huo ulipelekwa kwa Mheshimiwa Rais wetu ili upate kibali chake kwa mujibu wa Katiba. Kwa taarifa hii nawafahamisha kwamba Mheshimiwa Rais ameshatoa kibali chake na sasa Muswada huo ni sheria ya nchi na inaitwa The Finance Act, 2010 Na. 15 ya mwaka 2010. Nadhani hii ni faraja kubwa kwa wenzetu wanaokusanya kodi na ushuru na mapato ya Serikali kwamba kesho kutwa unapoanza mwezi mpya au mwaka mpya wa fedha wanayo sheria nyuma yao, Ahsante sana. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa hatua ya haraka kuweza kutekeleza hilo. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu kwa Mwaka wa Fedha, 2010/2011. MHE. MASOLWA C. MASOLWA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU): 1 Taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Miundombinu kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 pamoja na maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2010/2011. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Cosmas Masolwa, nadhani hii ni mara yako ya kwanza kusimama hapo. Kwa hiyo, nakupongeza sana. Sasa namwita Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Kabwe Zitto, hukuwapo kwa muda wa kama siku kumi na nne hivi. (Makofi /Kicheko) MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nilikuwa Jimboni.(Kicheko) MHE. KABWE Z. ZITTO, MSEMAJI MKUU WA KAMATI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Msemaji wa Mkuu wa Kambi ya Upinzani Kuhusu Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Randama za Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Sayansi, Teknolojia, kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge swali la kwanza nilaelekezwa Ofisi ya Waziri Mkuu na linaulizwa na Mheshimiwa Luhahula wa Bukombe. Hayupo, kwa niaba yake Mheshimiwa Masunga. MHE. JOYCE M. MASUNGA: Mheshimiwa Spika. SPIKA: Dah, jamani vilemba hivi, ndio sio rahisi wanabadili kila siku hawa. Mheshimiwa Joyce Masunga. (Kicheko) Na. 131 Kuwajengea Uwezo Wenyeviti Wa Kitongoji na Serikali za Vijiji MHE. JOYCE M. MASUNGA (K.n.y. MHE. EMMANUEL LUHAHULA) aliuliza:- Kwa kuwa, kuwajengea uwezo viongozi wa Serikali katika ngazi zote ni jambo zuri katika kuleta utawala bora:- 2 (a) Je, nani anawajibika kutoa elimu na semina kwa wenyeviti wa vitongoji na Serikali za vijiji katika maeneo husika? (b) Je, katika Wilaya ya Bukombe semina za wenyeviti wa vitongoji na vijiji zimefanyika tarehe ngapi tangu waingie madarakani mwaka 2004? SPIKA: Majibu Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na wewe pia karibu Bungeni nadhani pia ulikuwa Jimboni. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kuchukua nafasi hii kusema kwamba alinituma Kigoma kule kwa ajili ya sherehe hizi za Serikali za Mitaa. Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kuwapongeza wananchi wa Kigoma pamoja Uongozi kwa kazi nzuri sana inayofanyika katika Mkoa wa Kigoma na ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imetekelezwa kikwelikweli. Wana umeme, wana barabara nzuri na kipekee tunawapongeza kwamba wametufundisha kwamba tuwe tunasherekea sherehe hizi kwa kufanya kazi, tumefyatua matofali na barabara. Kwa hiyo, tunawapongeza sana Mkoa wa Kigoma. Baada ya salamu hizo kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Luhahula, Mbunge wa Bukombe, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, wajibu wa kutoa elimu, semina na mafunzo kwa Wenyeviti wa Vitongoji na Serikali za Vijiji ni Halmashauri yenyewe kwa kuzingatia mahitaji mahususi katika eneo lake. Fedha zinazotumika ni vyanzo vya Halmashauri (Mapato ya ndani na ruzuku inayotolewa kwa ajili ya kujenga uwezo). Aidha, Viongozi hao wanapatiwa mafunzo kuhusu utawala bora, uwakilishi wa wananchi katika vikao vyenye kufanya maamuzi pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo. (b) Mheshimiwa Spika, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe semina kwa Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji zilifanyika kuanzia tarehe 4/6/2007 hadi tarehe 3 21/6/2007. Kufuatia semina hiyo, jumla ya Wenyeviti wa Vitongoji 488 na wajumbe 608 wa Halmashauri za Serikali za Vijiji walihudhuria na kushiriki kikamilifu katika semina hiyo. Mada zilizotolewa ni kama zifuatazo:- (i) Misingi ya Utawala Bora. (ii) Wajibu na majukumu ya Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji. (iii) Utaratibu katika kuendesha vikao na mikutano kwenye ngazi za Vitongoji,Vijiji na Kata. (iv) Aina ya vikao, mikutano inayopaswa kufanyika kwenye maeneo yao. (v) Upangaji wa mipango shirikishi jamii. (vi) Usimamizi wa fedha. Mheshimiwa Spika, mafunzo yaliyotajwa yaligharamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kupitia fedha za kujenga uwezo (CBG) zilizotelewa na Serikali katika mwaka wa fedha 2006/2007 ambapo jumla ya shilingi 7,800,000 zilitumika katika kuendesha mafunzo hayo. MHE. MOHAMED R. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa ardhi ndio rasilimali ya wananchi Vijijini na kuna sheria namba 5 ya mwaka 1999 ndio inayowaweka sawa wananchi hao ili waweze kutumia vizuri rasilima hiyo, lakini elimu ya sheria hiyo katika Vijiji vyetu na Viongozi wake haipo kabisa. Je, Mheshimiwa Waziri, Wizara ya TAMISEMI ina mikakati gani ya maksudi kuwapa semina ya kutosha Viongozi wetu wa Serikali za Vijiji ili waielewe vizuri sheria hii, ili kupunguza matatizo na kutenda haki kwa wananchi walioko Vijijini. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Rished, Mbunge wa Pangani kama ifutavyo:- Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Rished kwamba ardhi ni rasimali muhimu sana katika Kijiji na kama ambavyo tumekuwa tunajibu hapa ndani, ardhi ya kijiji ukutaka kuitumia ni lazima upate ridhaa ya Kijiji chenyewe na mkutano mkuu lazima ukubali kwamba ardhi ile itumike. Sasa ni kweli kama anavyosema maeneo mengine sheria hii haijafahamika vizuri na kueleweka vizuri na kuna haja ya kuendelea kutoa elimu, tunatoa mafunzo ya aina mbalimbali na katika reform program ile kwanza nah ii ya pili pia hayo yamekuwa yanazingatiwa na kama tulivyojibu hapa semina mbalimbali zimekuwa zikitolewa kwa 4 ajili ya Wenyeviti wetu wa Vijiji pamoja na Wenyeviti wa Vitongiji pamoja na watendaji wetu katika Vijiji. Kwa hiyo, nakubaliana naye kabisa kwamba elimu hii tutaendelea kutoa kufuatana na mahitaji, lakini the bottom line is Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ai Halmashauri nyingine yeyote kuna tatizo na kuona kwamba kuna haja ya kufanya hivyo na pale tutakapotakiwa kufanya hivyo kama Serikali, hatutaacha kwenda kwa ajili ya kutoa elimu hiyo. MHE. DR. WILLIBROD P. SLAA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza:- Mheshimiwa Spika, kwa kuwa katika ngazi ya Taifa, Mkoa wa Wilaya, Serikali imeandaa wataalamu maalum kwa ajili ya usimamizi wa fedha na kwa kuwa sasa hivi takribani asilimia 25 ya bajeti nzima inapelekwa Wilayani kwa lengo la kwenda Vijijini kutekeleza miradi na huku hakuna wataalamu walioandaliwa, je Wizara sasa iko tayari kutoa mwongozo rasmi kwamba hawa Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji pale uchaguzi unapofanyika lazima wafanye semina kadhaa za kuwawezesha kusimamia hizi fedha, mabilioni ambayo yanapelekwa Vijijini ili hela hizi zisipotee bila kupata matunda? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwanza mimi nikiri kabisa kwamba ili tatizo ambalo yeye kila wakati tunaposema hapa ni Mwenyekiti wa Local Authorities Accounts Committee kwa hiyo, yuko conversant na eneo hilo. Nikiri kwamba katika eneo hili lote analozungumzia kwenye procurement tuna matatizo, katika maeneo ya fehda nako tuna matatizo na hili tunaliona na tumekuwa tunashirikiana na Wizara ya Fedha na Uchumi, tumekuwa tunashirikiana pia katika Ofisi ya Rais, Utumishi ili kuona kwamba hilo eneo tunawapata watu wengi ambao watatusaidia kwa ajili ya kufanya kazi hii anayozungumza Dkt. Willbrod Slaa na nikiri kabisa kwamba wanapokuwa wamechaguliwa Wenyeviti wetu wapya, mwingine anaweza kwenda pale amechaguliwa ndio, lakini majukumu yanayomuhusu kama Mwenyekiti wa Kijiji hayajui. Kwa hiyo, cha kwanza kabisa tunachokifanya ni kuhakikisha kwamba wanapata, lakini la pili ni kuhusu watendaji wetu wa Vijiji, kwa sasa hivi tumesema kwamba mtendaji wowote wa Vijiji lazima katika programu hii ya miaka mitatu ahakikishe kwamba amesoma walau mpaka kidato cha nne, amefaulu, hakufauli we don’t care lakini at least afike form four. Hii yote ni katika kujenga huwo uwezo na kuhakikisha kwamba tunakuwa na watu ambao ni competent ili Serikali zinazoenda katika eneo lile zisije zikapotea. Tunakubaliana na wewe kwamba tutafanya kazi ya kutoa elimu katika eneo hilo. MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona. Kwa kuwa mara nyingi Serikali inapojibu maswali hasa yanyowahusu Wenyeviti wa Vitongoji ambao mimi najua
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages234 Page
-
File Size-