Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 17 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne. S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO: Hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. MARY P. CHATANDA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEOYA JAMII, JINSIA NA WATOTO): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. JUMA SURURU JUMA – (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE.SALUM K. BARWANY - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. CECILIA D. PARESSO (K. n. y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. SPIKA: Ahsante sana. Naona hapa kunaanzishwa ka-precedence Manaibu Waziri wawili hapa wamekuja wanawasilisha kwa niaba ya Waziri wao wakamtaja na jina, hapana. Ni kwamba unawasilisha kwa niaba ya Serikali na ni Waziri anaweza akawa Waziri mwingine katika Wizara hiyo hiyo akateuliwa Waziri mwingine akasoma sasa atakuwa sio Mheshimiwa Kawambwa wala sio Mheshimiwa Sophia Simba. Kwa hiyo mnawasilisha kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Sio kumtaja Waziri fulani, hapana anaweza kuteuliwa mwingine hapa Waziri akasoma kwa niaba ya Waziri. Kwa hiyo naomba hii msiiweke mnatugeuzia maneno hapa. HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Mwaka 2014/2015 Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu baada ya kuzingatia Taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, sasa lijadili na Kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka 2014/2015. Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia kuwa na afya njema na hivyo kuweza kushiriki Mkutano huu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Spika, tafadhali niruhusu nitumie fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais na Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda, Waziri Mkuu na Mbunge wa Katavi, kwa uongozi wao mahiri ambao umewezesha kushamiri kwa usawa wa jinsia na uzingatiaji wa haki za mtoto katika jamii ya Watanzania. Mwenyezi Mungu awajalie afya njema ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa uendeshaji bora wa shughuli za Bunge. Tunaendelea kumwomba Mwenyezi Mungu awajalie afya njema ili muweze kusimamia na kuratibu shughuli za Bunge kwa ufanisi. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia muda nilionao kuwasilisha hoja yangu naomba hotuba yote kama ilivyo katika kitabu cha hotuba iingie kwenye Hansard. Mapitio ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa kipindi cha Januari, 2011 hadi Machi, 2014. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Januari 2011 hadi Machi, 2014 Wizara yangu ilitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010 kupitia maeneo makuu manne. Maeneo hayo ni pamoja na ajira na uwezeshaji wa wananchi, elimu ya juu, uendeshaji wa makundi mbalimbali na demokrasia na madaraka ya umma. Katika kipindi husika utekelezaji wa maeneo hayo umekuwa na mafanikio kama inavyoelezwa kwa kirefu kwenye kitabu cha hotuba yangu ukurasa wa 3 hadi 11. Hali halisi ya Maendeleo ya Jamii na changamoto zilizopo. Mheshimiwa Spika, sekta ya Maendeleo hapa nchini imeendelea kukua na kutambulika kwa wadau mbalimbali kutokana namchango wake katika maendeleo ya Taifa letu. Naomba kuchukua fursa hii kueleza kwa kifupi hali halisi ya sekta hii katika maeneo ya ushiriki wa wananchi katika maendeleo ya kiuchumi, maendeleo ya jinsia, maendeleo ya watoto na ushiriki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo nchini Tanzania. Mheshimiwa Spika, wataalamu wa Maendeleo ya Jamii ni muhimu katika kuongeza ushiriki wa wananchi katika maendeleo. Kwa sasa kuna wataalamu wa Maendeleo ya Jamii 2,675 katika ngazi ya Halmashauri na 21 katika Sekretarieti za mikoa. 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) Kwa takwimu hizo kuna upungufu asilimia 61 ya wataalamu hao katika ngazi ya Halmashauri na asilimia 16 katika ngazi ya Sekretarieti za mikoa. Aidha, wananchi wameendelea kunufaika na mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi yanayotolewa na vyuo 55 vya Maendeleo ya Wananchi vilivyo chini ya Wizara yangu. Mafunzo haya yanawawezesha kujiajiri na kuajiriwa. Mheshimiwa Spika, hali ya usawa wa kijinsia katika nyanja mbalimbali hapa nchini imeendelea kuimarika. Ukweli huu unadhihirishwa na ushahidi wa kitakwimu na taarifa zilizopo katika maeneo ya ushiriki wa wanawake katika siasa na ngazi za maamuzi, uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, elimu, mafunzo na ajira. Kuongezeka kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati na upatikanaji wa haki za wanawake kisheria. Mheshimiwa Spika, watoto ni sehemu muhimu ya jamii na ndio tegemeo la taifa lolote. Watoto wanahitaji kukua na kuwa raia wema hivyo wanatakiwa kupewa haki na mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na kuishi, kupewa malezi stahiki, kulindwa, kuendelezwa kiakili kwa kutambua na kukuza vipaji vyao kutobaguliwa na kushirikishwa. Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Idadi ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 idadi ya watoto chini ya miaka 18 Tanzania Bara ni 21,866,258 sawa na asilimia 50.1 ya idadi ya watu wote. Kati ya hao wasichana ni 10,943,846 na wavulana ni 10,922,412 kwa kuzingatia umuhimu wa watoto Wizara kwa kushirikiana na wadau inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili watoto wote hapa nchini wapate huduma stahiki na haki zao za msingi kwa maendeleo ya sasa na ya baadaye ya Taifa letu. Mheshimiwa Spika, idadi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali chini ya Sheria ya NGO Na. 24 ya mwaka 2002 iliyorekebishwa mwaka 2005 imeendelea kukua mwaka hadi mwaka ambapo kufikia tarehe 17 Machi, 2014 idadi ya Mashirika hayo ilifikia 6,427 kutoka Mashirika 3,000 yaliyokadiriwa kuwepo mwaka 2001 wakati Sera ya Taifa ya NGO ilipokuwa inaandaliwa sawa na ongezeko la asilimia 100. Mashirika haya yanajishughulisha na kazi mbalimbali ikiwemo elimu, mazingira na mabadiliko ya tabianchi, afya maendeleo shirikishi, haki za binadamu, maendeleo ya jinsia, ushawishi na utetezi, kinga ya jamii, haki za watoto, kilimo, maji na ustawi wa jamii. Kuongezeka kwa idadi na shughuli za NGO’s katika nchi yetu ni matokeo ya mazingira wezeshi yanayoendelea kuboreka mwaka hadi mwaka. Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina ya hali halisi ya sekta ya maendeleo ya jamii, mafanikio yaliyofikiwa na changamoto zilizopo yapo kwenye ukurasa wa 11 hadi 23 wa kitabu cha hotuba. Mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa mwaka 2013/2014 na malengo ya mwaka 2014/2015. 4 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014 Wizara yangu iliendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu yake kulingana na malengo yaliyopangwa. Katika Bajeti mwaka 2013/2014 Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto iliidhinishiwa jumla ya shilingi 25,964,170,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo. Kati ya fedha za Matumizi ya Kawaida shilingi 5,397,496,000 zilikuwa ni kwa ajili ya Matumizi Mengineo na shilingi 8,656,200,000 kwa ajili ya malipo ya mshahara na shilingi 11,910,672,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2014 Wizara ilikuwa imetumia jumla ya shilingi 10,305,162,100 sawa na asilimia mia ya fedha za matumizi ya kawaida zilizopokelewa na shilingi 2,923,620,590 sawa na asilimia mia ya fedha za Maendeleo zilizotolewa. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha utekelezaji wa Mpango wa mwaka 2013/2014 na malengo ya mwaka 2014/2015 kwa kuzingatia maeneo yafuatayo. Maendeleo ya Jamii. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 Wizara yangu ilidahili na kutoa mafunzo kwa wanachuo 2,869 kupitia vyuo 6 vya Maendeleo ya Jamii. Wanachuo 2,036 walidahiliwa katika ngazi ya cheti, 591 katika ngazi ya Stashahada, 234 ngazi ya Shahada na 8 katika ngazi ya Stashahada ya Udhamili. Aidha, Wizara yangu ilikarabati majengo na miundombinu katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale, Misungwi na Mabugai. Katika mwaka 2014/2015 Wizara yangu itaendelea kukamilisha jengo la Maktaba ya Chuo cha Tengeru na Maabara ya Kompyuta katika Chuo cha Mabugai kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014 Wizara yangu ililipa shilingi 84,114,523 zikiwa ni gharama za ukarabati katika Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vya Mputa na Muhukuru mkoani Ruvuma.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    261 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us