Majadiliano Ya Bunge ______

Majadiliano Ya Bunge ______

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Kumi na Tatu - Tarehe 22 Juni, 2010 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MHE. KIDAWA HAMID SALEHE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI): Taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Kilimo. Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MHE. SALIM HEMED KHAMIS - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Taarifa ya Msemaji wa Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:- Randama za Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. 1 MASWALI NA MAJIBU Na. 86 Kuhusu Soko la Wamachinga Dar es Salaam MHE. MOHAMMED ALI SAID aliuliza:- Soko la Wamachinga lililopo Ilala Jijini Dar es Salaam lilitegemewa liwe limefunguliwa ndani ya mwaka 2009:- Je, ni sababu ipi iliyokwamisha kufunguliwa na kuanza kufanya kazi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Ali Said, Mbunge wa Magogoni, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kukwama kufunguliwa kwa soko la Wamachinga Jijini Dar es Salaam kumetokana na kuchelewa kukamilika kwa ujenzi. Ujenzi wa soko hilo ulikuwa ukamilike na kukabidhiwa tangu Septemba, 2008 sababu ya kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo ni mabadiliko katika ubunifu wa mradi ambapo awali ilikusudiwa jengo liwe na ghorofa tatu. Wakati Mkandarasi akiwa ameanza kazi ya kuchimba msingi, wadau mbalimbali walijenga hoja kwamba kuongezwe ghorofa katika jengo hilo hadi kufikia ghorofa tano. Baada ya kukubaliana kuongeza idadi ya ghorofa ili jengo liwe na uwezo wa kuchukua wafanya biashara wengi zaidi iliazimu kufanya upya usanifu wa jengo na hivyo kuchelewesha kazi ya ujenzi. Mheshimiwa Spika, baada ya Mkandarasi kukamilisha ujenzi hatimaye jengo lilikabidhiwa rasmi kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tarehe 21 Me, 2010 tayari kwa matumizi. Kwa sasa Halmashauri ya Jiji inakamilisha matengenezo ya vizimba na kazi hiyo ikikamilishwa soko litafunguliwa na wafanyabiashara wataanza kazi rasmi katika jengo hilo. Na. 87 Hitaji la Magari Mawili ya Kubebea Wagonjwa –Sengerema 2 MHE. ERNEST G. MABINA (K.n.y. MHE. SAMUEL M. CHITALILO) aliuliza:- Kwa kuwa Wilaya ya Sengerema ina wakazi wengi na Majimbo mawili (Sengerema na Buchosa) lakini kuna gari moja tu la kubebea wagonjwa ambalo halitatoshelezi kuhudumia wakazi wote:- Je, ni lini Serikali itaipatia Wilaya ya Sengerema magari mawili zaidi ya kubebea wagonjwa. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MISTAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Samuel Mchele Chitatilo, Mbunge wa Buchosa, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ina eneo la mraba lipatalo kilomita 8,817 na ina vituo vya tiba 60 ikiwemo Hospitali teule moja inayomilikuwa na Jimbo la Katoliki la Geita. Kati ya vituo hivyo vituo vya avya ni 8 na zahanati 51 na Halmashauri ina wakazi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 600,000. Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema haikuwa na gari maalum la kubebea wagonjwa tokea miaka ya nyuma. Huduma hii imekuwa ikitolewa magari ya kawaida mfano Landcruiser Hard top lililokuwa limetolewa na Shirika la Oxfarm kwa ajili ya huduma ya Mama na Mtoto. Mwaka 2007/2008 Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema katika bajeti yake ilitenga shilingi milioni 84.0 kwa ajili ya kununua gari maalum la kubebea wagonjwa na liliweza kununuliwa mwezi Novemba 2008. Gari hili lilitumika hadi tarehe 12 Juni, 2009 wakati lilipopinduka likifuata mgonjwa na kuharibika kabisa. Kwa kuwa lilikuwa limekatiwa Bima (Comprehensice) kutoka Shirika la Bima la Taifa, mchakato ulianza kwa kuwasiliana na Shirika la Bima na mazungumzo yanaendelea ili kupata gari lingine. Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo Idara ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema inayo magari mawili ambapo kati ya hayo moja linatumika kutoa huduma ya mama na mtoto na vilevile linatumika kabeba wagonjwa (ambulance). Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema iendelee kutoa kipaumbele kwa suala hili la ununuzi wa magari ya wagonjwa na kutenga fedha katika bajeti yake. Hilo ni jukumu la msingi la msingi la Halmashauri husika. MHE. ERNEST G. MABINA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa tatizo lililoko Sengerema ni 3 sawasawa kabisa na tatizo lililoko Geita. je, Serikali inasemaje kuvipa gari la wagonjwa vituo vya afya vya Kasamwa, Nzera, Katoro na Geita kwenyewe? NAIBU SPIKA: Kwa hiyo, atoe magari Sengerema aache Buchosa? Mheshimiwa Waziri majibu. (Kicheko) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA : Mheshimiwa Naibu Spika, katika hotuba yangu nilisema kwamba tutanunua magari ya wagonjwa yapatayo 50 lakini kipaumbele kitakuwa kwa Wilaya mpya, Wilaya ambazo hazina kabisa gari ya kubebewa wagonjwa na Wilaya zile ambazo ziko pembezoni. Kwa hiyo, kipaumbele kitakuwa zaidi ya huko kuliko Mikoa au Wilaya ambazo ziko katika hali ambayo si ya pembezoni. MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Tatizo la Buchosa ni sawasawa na Mwibara na uzuri ni kwamba Mheshimiwa Waziri amesema kwamba atatoa kipaumbele kwa Majimbo yale ya pembezoni na Jimbo la Mwibara liko pembezoni. Je, anatoa ahadi gani kwa ajili ya Jimbo la Mwibara? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kabla ya Bunge lako kwisha nilete ile orodha ya Wilaya ambazo zitagawiwa magari hayo ili tuweze wote kuiona na tujue kwamba ni Halmashauri gani itapata magari hayo. MHE. RAMADHANI A. MANENO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri na mimi nina swali moja la nyongeza. Tatizo la magari ya kubebea wagonjwa ni tatizo lililopo katika nchi nzima kwa ujumla na kwa kuwa amesema ataleta orodha itakayoonesha magari yatakayosambazwa katika Wilaya lakini katika orodha hiyo nataka Mheshimiwa Waziri anihakikishie katika Wilaya ya Bagamoyo ina Majimbo mawili Chalinze na Bagamoyo. Gari ya wagonjwa itakayokuwepo katika Wilaya ya Bagamoyo kwa maana ya Makao Makuu ya Wilaya ni umbali wa kilomita kama 180 kati ya Bagamoyo na Chalinze. Je, wale wagonjwa watakaokuwa wanapata matatizo kwa ajili kusafirishwa Tumbi kuna uwezekano wa kupata gari lingine ambayo itakaa katika Jimbo la Chalinze? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri majibu. Hiyo orodha italeta fitna tu. (Kicheko) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tukishanunua yale magari tunapeleka katika Halamshauri mbalimbali, Halmashauri hizo ndizo zinazopanga kwamba ni kituo gani cha afya kiko pembezoni zaidi na tumefanya hivi kwa miaka yote na baadhi ya Halmashauri imefanya hivyo. Nimeshuhudia kwa Chamwino tuliwapa gari lakini wamepeleka kwenye kituo cha afya ambacho kiko pembezoni kabisa mwa 4 Chamwino. Kwa hiyo, ni Halmashauri yenyewe ndiyo itakayoamua kwamba gari hilo lipelekwe katika kituo gani cha afya. Na. 88 Matukio ya uhalifu kuongezeka – Mbozi Magharibi MHE. DR. LUKA J. SIYAME aliuliza:- Kwa kuwa matukio ya ujambazi, ghasia, mauaji na upotevu wa mali za watu kwenye Kata za Tunduma, Kapele, Nkangamo na Ndalambo zilizopo mpakani mwa nchi ya Zambia katika Jimbo la Mbozi Magharibi yanazidi kuongezeka kila siku, na kwa kuwa kutokana na uchache wa askari Polisi, uhaba wa vitendea kazi na ukosefu wa gari, askari Pollisi huchukua muda mrefu kufika au mara nyingine kutofika kabisa kwenye maeneo ya tukio na kufanya tatizo hilo kuwa kubwa kila siku:- Je, Serikali itachukua hatua gani za dharura ili kupunguza matukio hayo ya uhalifu. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dk. Luka Jelas Siyame, Mbunge wa Mbozi Magharibi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi Wilayani Mbozi zikiwemo uchache wa askari na uhaba wa vitendea kazi, hali ya uhalifu katika Wilaya hiyo si ya kutisha ikilinganishwa na Wilaya nyingine za Mkoa wa Mbeya na Tanzania kwa ujumla. Aidha, takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba kutokana na kuimarika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, matukio ya uhalifu kutoka Wilaya hiyo yamekuwa yakipungua kwa miaka mitatu mfululizo. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikiendelea kutatua tatizo la usafiri katika vituo vya Polisi kadri Bajeti inavyoruhusu. Kwa sasa Kituo cha Tunduma kina gari moja(1) aina la Land Cruiser Pick up pamoja na pikipiki tano. Aidha, kituo cha Kamsamba kina pikipiki moja. 5 Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya vyombo vya usafiri vituo huongezewa nguvu kwa gari la OCD Mbozi pamoja na pikipiki zilizopo Wilayani. Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2010/2011 Wilaya ya Mbozi itaongezwa askari wapya wanaohudhuria mafunzo CCP Moshi pamoja na gari moja kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. MHE. DR. LUKA J. SIYAME: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali moja dogo la nyongeza. Lakini kabla ya hapo naomba tena nichukue fursa hii kuwaelezea wale wananchi wa Jimbo la Mbozi Magharibi ambao hadi jana walikuwa bado wananipigia simu za kuuliza kama kweli wamepata Wilaya. Napenda niwathibitishie kwamba tumepata Wilaya na inaitwa Momba na kwa hali hiyo naomba kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi tushirikiane nao miaka mitano ijayo ili tuweze kuijenga Wilaya mpya ya Momba. NAIBU SPIKA: Sasa mbona unatumia zaidi muda wako? MHE.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    200 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us