![Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)](https://data.docslib.org/img/3a60ab92a6e30910dab9bd827208bcff-1.webp)
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 9 Agosti, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2006/2007. MHE. ZAYNAB MATITU VULU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE): Maoni ya Kamati ya Mambo ya Nchi za Nje Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. MHE. ABUBAKAR KHAMIS BAKARY - (MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI: Maoni ya Kambi ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. MASWALI NA MAJIBU Na. 366 Kuigawa Wilaya ya Geita MHE. JAMES P. MUSALIKA aliuliza:- 1 Kwa kuwa, vigezo vya kugawa Wilaya ni pamoja na ukubwa wa eneo na idadi ya watu na kwa kuwa, Wilaya ya Geita inakidhi vigezo hivyo:- Je, ni lini Serikali itaigawa Wilaya ya Geita? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa James Philipo Musalika, Mbunge wa Nyang’hwale, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, uundaji na ugawaji wa wa maeneo mapya ya kiutawala hapa nchini unatawaliwa na Sheria za Serikali za Mitaa Na. 7 kwa (Mamlaka za Wilaya) na sheria Na. 8 kwa (Mamlaka za Miji) za mwaka 1982 na Sheria za Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Na. 12 ya mwaka 1994. Sambamba na Sheria hizo vigezo muhimu vilivyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kwenye Waraka wa Mwaka 1995 ni pamoja na:- 1. Eneo la Wilaya moja lisilopungue kilomita za mraba 5,000; 2. Idadi ya Tarafa zisizopungua 5; 3. Idadi ya Kata zisizopungua 15; 4. Idadi ya Vijiji visivyopungua 50; 5. Idadi ya wakazi wasiopungua 100,000; na 6. Jiografia ambayo inafanya huduma kwa wananchi kuwa ngumu kwa sabau ya milima, mito, misitu, maziwa, mabonde au visiwa na kadhalika. Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na vigezo hivi wananchi wa eneo husika wanatakiwa kuwa na nia ya kugawa Wilaya yao kuwa zaidi ya moja na waombe rasmi. Maombi yanatakiwa kuambatanishwa na baraka za Vikao husika katika Ngazi za Wilaya na Mikoa na yaeleze bayana sababu za kutaka Mkoa au Wilaya igawanywe. Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Geita, ina vigezo vinavyostahili kuifanya igawanywe kwani ina kilometa za mraba 7,825, Majimbo 3 ya Uchaguzi Kata 33, Vijiji 187, idadi ya watu 782,782 kwa mujibu wa sensa ya 2002. Aidha, kwa kuzingatia vigezo hivyo, zipo Wilaya nyingi sana zinahitaji kugawanywa kwa kuwa ni kubwa kieneo na zina idadi kubwa ya watu kwa mfano Wilaya ya Kasulu ina watu 628,667 na Wilaya ya Mbozi ina watu 515,270. Kwa kutumia vigezo vilivyopo kigezo cha watu pekee kinafanya Wilaya 27 zihitaji kugawanywa na kuzingatia ukubwa wa eneo Wilaya 32 zinahitaji kugawanywa. Mheshimiwa Mwenyekiti, ugawaji wa Wilaya au maeneo mapya huwa muafaka endapo Serikali inalo fungu la kuyajenga Makao Makuu ya Wilaya, gharama za uendeshaji na uwekazi miundombinu muhimu pamoja na watumishi katika Wilaya husika. Ugawaji wa Mkoa au Wilaya huigharimu Serikali takriban shilingi bilioni 1 kwa 2 Wilaya na bilioni 4 hadi 6 kwa Mkoa. Hivyo, Serikali hugawa maeneo kwa awamu kulingana na uwezo. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kwamba Serikali itaendelea kugawa maeneo mapya ya kuitawala ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Geita kadri uwezo wa kifedha utakavyokuwa unaruhusu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa urahisi na kutimiza ahadi ya Serikali ya awamu ya nne ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. (Makofi) MHE. JAMES P. MUSALIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amekiri kwamba Geita inavyo vigezo vya kufanywa igawanya na kwa kuwa iko namba moja kwa zile Wilaya kwa maana idadi ya watu lakini pia hata nataka awe specific. (a) Je, Serikali iko tayari kuigawa Wilaya hiyo kwa mwaka huu wa Fedha kwa kuanzia tuanzie Geita mwaka huu na kama sivyo ni lini? (b) Kwa kuwa wananchi wa Geita kupitia Baraza lao la Madiwani wameshakaa na kupendekezo kuhusu kugawanywa kwa Wilaya je, Serikali iko tayari kuheshimu maamuzi na kuyabariki kwamba Wilaya mpya sasa iitwe Nyang’hwale na na Makao Makuu ya Wilaya hiyo iwe mji mdogo wa Karumwa? (Makofi) (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye swali langu la msingi kwamba Wilaya ya Geita ina vigezo ambavyo vinatakiwa igawanywa na zipo Wilaya nyingi ambazo zina vigezo muhimu ambavyo vinatakiwa vigawanywe. Masuala yote hayo yameshawasilishwa katika ofisi yetu na ofisi yangu inayachambua hayo maeneo ili kubainisha ni lipi lipewe kipaumbele katika kugawa katika mwaka huu wa fedha na mwaka ujao wa fedha. Kuhusu suala la kupitisha kwenye vikao husika ni kweli Wilaya ya Geita imeshapitisha suala la kuigawa hiyo, Wilaya katika vikao vyote vinavyohusika na imeshawasilishwa katika ofisi yetu. Kama nilivyosema kwamba tuko katika mchakato wa kuchambua Wilaya hizo zote kwamba ni Wilaya ipi ambayo tuipe kipaumbele kulingana na uzito na vigezo husika. Pia tunaangalia na uwezo wa kiuchumi kama nilivyosema kwenye suala langu la msingi. MHE. DR. CHRISANT M. MZINDAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amekiri kwamba iko haja ya kuweza kugawa hizi Wilaya na kwa hesabu yake amesema ziko 37. Je, atakubaliana nami kwamba inahitaji watulie ili uamuzi huu ufanyike bila kuchelewa kwa sababu ya kuleta maendeleo ya nchi kwa haraka? (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa niaba ya Waziri Mkuu niseme yafuatayo kuhusiana na eneo hili la ugawaji wa maeneo mapya. 3 Tulishawahi kulieleza jambo hili hapa Bungeni kwako tukatoa idadi ya Wilaya ambazo tunadhani zinastahili kugawanywa. Lakini tukaeleza vile vile Wilaya hizi zitakuwa zinatolewa kidogo kidogo kwa sababu kuna gharama kubwa sana wakati wa kuanzisha Wilaya hizi. (Makofi) Kwa hiyo, bado mimi nafikiri nitoe rai kwa Mheshimiwa Dr. Mzindakaya, pamoja na Waheshimiwa Wabunge, kwa ujumla kwamba jitihada za Serikali zitaendelea lakini itakuwa ni vigumu sana kufikiria kwamba tunaweza tukaanzisha Wilaya Mpya kwa mara moja karibu 30 na zaidi si rahisi mzigo utakuwa mkubwa kuliko tunavyofikiria. Lakini tunatoa ahadi kwamba kila itakavyowezekana tutawasilisha mapendekezo haya kwa viongozi wa kitaifa na yale yatakayoonekana yanabadalika basi tutakuwa tunatoa kidogo kidogo. (Makofi) Na. 367 Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 MHE. DR. HAJI MWITA HAJI (k.n.y. MHE. COSMAS M. MASOLWA) aliuliza:- Kwa kuwa, kumbukumbu zinaonyesha kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji ilishaingia katika mpango wa muda mrefu wa Maendeleo ya Taifa, mpango wa kwanza, mwaka 1964 – 1980, mipango wa pili mwaka 1981 – 2000 na sasa mpango wa tatu unaohusu Tanzania yote ujulikanao kama kama Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 unaohusu Tanzania Bara tu:- (a) Je, ni sababu zipi zilizosababisha kutokuwa na mpango mmoja wa muda mrefu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyokuwa katika mpango wa pili wa taifa wa maendeleo? (b) Je, Serikali haioni vema kuwa na mpango wa pamoja wa maendeleo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuondoa utata kwa wafadhili kuliko ilivyo sasa ambao dira ya Taifa ya Maendeleo Tanzania Zanzibar 2020 inatofautiana na ile ya Tanzania Bara? (c) Je, Serikali imepanga vipi kwenye mipango yake ya maendeleo suala la ahadi za Mheshimiwa Rais, kwenye hotuba yake ya tarehe 30.12.2005 juu ya kuchangia maendeleo ya uchumi wa wananchi wa Tanzania, Zanzibar? NAIBU WAZIRI WA MIPANGO, UCHUMI NA UWEZESHAJI atajibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumjibu Mheshimiwa Cosmas Masolwa, Mbunge wa Bububu, swali lake lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Napenda kulieleza Bunge lako Tukufu kuwa si sahihi kwamba Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, inahusu upande mmoja tu wa Jamhuri ya Muungano, yaani Tanzania 4 Bara. Tukumbuke kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, katika maandalizi yake ilishirikisha wadau mbalimbali Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Miongoni mwa walioshirikishwa ni Wabunge wa Bunge lako Tukufu na Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar. Aidha, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ilijadiliwa na makundi mbalimbali Bara na Visiwani vikiwemo vyama vya siasa, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, Jumuiya za Wanawake na Vijana, Vyama vya Wafanyabiashara na wenye viwanda, wakulima, wasomi watu mashuhuri katika histori ya nchi yetu na wananchi wa kawaida. Hivyo kwa kuzingatia muktadha huu utaona kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inajumuisha Watanzania wote Bara na Visiwani na ni yenye malengo shirikishi. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwapo kwa Dira ya maendeleo 2025 kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020 ni makubaliano ya mwelekeo kiuchumi na kijamii uliopata ridhaa ya wananchi wote. Kinyume na ilivyokuwa katika mpango wa pili wa muda mrefu (1980 – 2000), ambapo kulikuwapo na mipango ya pamoja na maendeleo ya miaka mitano, utekelezaji wa Dira ya Taifa ya maendeleo 2025 unazingatia zaidi mazingira na muundo wa sehemu husika. Kwa upande wa Tanzania Bara, Dira hutekelezwa kupitia Mpango wa muda wa kati (MTP) wa miaka mitatu mitatu. Mikakati na programu mbalimbali zimeandaliwa ili kutekeleza dira kama vile
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages126 Page
-
File Size-