Tarehe 22 Mei, 2017

Tarehe 22 Mei, 2017

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Moja – Tarehe 22 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae, Katibu! NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MWENYEKITI: Ahsante, Katibu!! 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 244 Malipo ya Wenyeviti wa Mitaa na Madiwani MHE. VEDASTUS M. MANYINYI aliuliza:- Wenyeviti wa Mitaa, Madiwani, Wabunge na Rais huchaguliwa na watu wanaoishi katika eneo la mipaka yake na wote hawa wanafanya kazi ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao. Je, Serikali imeridhika na malipo wanayopata Wenyeviti wa Mitaa pamoja na Madiwani? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi, Mbunge wa Musoma Mjini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Waheshimiwa Madiwani na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji katika kusimamia shughuli za maendeleo. Majukumu yanayotekelezwa na viongozi hao ni utekelezaji wa dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi ambapo mipango yote na usimamizi yanafanywa katika ngazi za msingi za Serikali za Mitaa. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikiboresha maslahi ya Waheshimiwa Madiwani kadri uchumi wa nchi unavyoruhusu. Kwa mfano posho ya Madiwani ilipandishwa mwaka 2015 kutoka shilingi 120,000 hadi shilingi 350,000 kwa mwezi. Kwa vipindi tofauti hususani Ofisi ya Rais, TAMISEMI ilipokutana na Waheshimiwa Madiwani katika mkutano wa 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ALAT hoja hii imekuwa ikijitokeza. Hata hivyo Serikali inalifanyia kazi jambo hili kulingana na mwenendo wa Kifedha wa nchi na jambo hili litakapokamilika utekelezaji wake utafanyika. Mheshimiwa Mwenyekiti, Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa hulipwa posho kutokana na asilimia 20 ya makusanyo ya ndani inayopaswa kurejeshwa kwenye ngazi ya msingi katika kata na vijiji. Kila Halmashauri imetakiwa kuhakikisha fedha hizo zinapalekwa kwenye vijiji kwa ajili ya shughuli za utawala ikiwemo kulipa posho na shughuli za maendeleo. Aidha, Halmashauri zimetakiwa kuimarisha makusanyo ya mapato ya ndani ili kujenga uwezo wa kulipa posho hizo kupitia makusanyo yanayofanyika. MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia Serikali kwa maana ya TAMISEMI wametoa muongozo katika makusanyo yale ya Halmashauri kwa maana ya kwamba asilimia 60 zinapaswa kwenda kwenye maendeleo, asilimia 20 zinapaswa kwenda kwenye kata, asilimia 10 zinapaswa kwenda kwa vijana na wakina mama, kwa hiyo Halmashauri inabakia na asilimia 10 peke yake ambayo ndiyo sasa ilipe mishahara na kuendesha Halmashauri. Je, kutokana na hali hiyo ni kwanini sasa hawa Madiwani pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wasilipwe moja kwa moja kutoka Serikali Kuu? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ukiwaangalia hao Madiwani pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanayo majukumu mengi na makubwa kwa hiyo hata wakati mwingine wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na tabu walizonazo hasa hasa za usafiri. Je, Serikali sasa imejiandaaje kuhakikisha kwamba nao inawawezesha kupata usafiri ili waweze kutekeleza majuku yao ya kila siku? (Makofi) 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI majibu kwa kifupi tu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ni kwamba kwanini sasa hawa Wenyeviti wasilipwe moja kwa moja kutoka Serikali Kuu na msingi umesema kwamba kwa sababu kulikuwa na suala zima la mgawanyo wa zile fedha kwamba asilimia 60 ziende katika maendeleo; Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipowasilisha bajeti yetu mwaka Mheshimiwa Waziri alitoa ufafanuzi hapa kwa kina kwamba hili limeonekana kwa sababu lilikuwa hoja ya msingi ya Waheshimiwa Wabunge, ndiyo maana tumetoa maelekezo. Mheshimiwa Waziri alizungumza wazi hapa kwamba fedha hizi sasa zitagawanyika tofauti, kwamba kwa baadhi ya Halmashauri hasa zile ambazo uwezo wake ni mdogo, sasa asilimia 60 zitakwenda katika matumizi haya mengine na asilimia 40 itakwenda katika maendeleo, huu ndio ufafanuzi kulingana na bajeti ya mwaka huu tuliyoipitisha hapa Bungeni. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hata hivyo, lengo letu kubwa katika dhana ya ugatuaji wa madaraka ni kutafuta jinsi ya kufanya katika kuongeza nguvu za Halmashauri za kuweza kukusanya mapato. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mathayo tutaendelea kulisimamia hilo, lakini kubwa na la msingi ni jinsi ya kufanya katika kukusanya vizuri mapato. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hoja ya pili, kuhusu vyombo vya usafiri; ni kweli, tukiangalia viongozi wetu wana changamoto kubwa ya usafiri, kwa sababu kama Madiwani wanafanya kazi kubwa, lakini hili naomba tulichukue sisi Serikali kwa sababu ni jambo ambalo naona ni la msingi hapo baadaye kwa kupitia Halmashauri zetu ni kwa jinsi gani tutafanya kupitia mifuko mbalimbali ili aangalau kuwezesha Waheshimiwa Madiwani waweze kupata vyombo vya usafiri. Hata hivyo jambo hili tutashirikishana vizuri kupitia katika Serikali zetu za Mitaa. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kama ilivyoulizwa katika swali la msingi, baadhi ya Madiwani wanaruhusiwa kuingia katika vikao vya Halmashauri husika lakini baadhi ya Wakurugenzi imekuwa vigumu kwao kuwaruhusu, na mfano mzuri ni Mheshimiwa Stella Allex Ikupa ambaye anapaswa kuingia katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ilala, lakini mpaka leo hii imekuwa vigumu kuhudhuria vikao hivyo. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri unatoa kauli gani ili aweze kuingia katika Baraza hilo na kuwatendea haki watu wenye ulemavu katika kuhakikisha kwamba masuala yao yanaingizwa katika bajeti husika? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hii nadhani kwamba imeshakwisha, kwa hiyo kama kuna ukakasi wa aina yoyote ofisi yetu italifanyia kazi; lengo kubwa ni kwamba mtu aliyepewa dhamana katika eneo hilo aweze kushiriki vizuri hasa lile kundi analoliwakilisha, kundi la walemavu. MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Maftaha Nachuma. Mheshimiwa.... MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Selasini. MWENYEKITI: Selasini amechangia mara nyingi sana. Mheshimiwa… MHE. JOSHUA S. NASSARI: Nassari. MWENYEKITI: Mheshimiwa Nassari. MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Kicheko) Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna watu ambao wanasaidia kazi za uongozi kwenye nchi hii nafikiri hata kuliko sisi Waheshimiwa Wabunge na wamekuwa msaada mkubwa 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) sana kwetu kwenye kutekeleza majukumu yetu kwenye majimbo na kwenye Halmashauri zetu ni viongozi wa Serikali za Mitaa kwa maana ya Wenyeviti wa Vijiji, lakini ambao wanafanya kazi kubwa zaidi ni Madiwani kwenye Halmashauri zetu. Hata hivyo ukweli ni kwamba unapoangalia maslahi ambayo hawa watu wamekuwa wakiyapata ni madogo sana na mara nyingine Serikali inaamua ku-temper nayo kwa makusudi kabisa hata kuingilia ule utendaji wa ndani wa Halmashauri wa moja kwa moja inapokuja suala la matumizi ya fedha. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kila wakati tumekuwa tukihoji kwenye Bunge hili kwamba ni lini Serikali inakwenda kuboresha maslahi ya Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Madiwani ili nao waweze kuishi kama viongozi na waonekane kwamba kweli kazi wanayoifanya inathaminika kwenye Taifa? Kila siku Serikali inasema… MWENYEKITI: Inatosha, swali limetosha Mheshimiwa. MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwamba, Serikali naomba iji-commit kabisa kwamba ni lini watakwenda kuboresha kabisa haya maslahi ya wenyeviti wa vijiji pamoja na Madiwani na waache kusema tutaliangalia, tutaliangalia……….. MWENYEKITI: Mheshimiwa inatosha. MHE. JOSHUA S. NASSARI: ……ni lini exactly? When? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali tunatambua viongozi hawa wa ngazi za chini, Wenyeviti wa Mitaa, Wenyeviti wa Vijiji na Madiwani wanafanya kazi kubwa sana katika nchi hii, maendeleo yote yanasimamiwa na wao. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ni kweli pia kwamba maslahi ya watumishi mbalimbali wa umma pia watumishi wa kisiasa kila mmoja anasema hayatoshi, tuongeze. Hata 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Wabunge wanasema hivyo, walimu wanasema hivyo na wote wanasema tuongeze. Hili litawezekana endapo uchumi wa nchi utatengemaa. Katika mazingira ya sasa, kinachowezekana na ambacho sisi tunaona kinapaswa kufanywa na Serikali kwa ngazi hizi za chini ni ile asilimia 20 tunayoipeleka kwa ajili ya kuendesha ofisi, lakini pia huwa kuna posho ambayo inapatikana. Asilimia 20 ya kiasi cha shilingi bilioni moja au Halmashauri zingine zinakusanya makusanyo ya ndani mpaka shilingi bilioni 50 si hela kidogo zikigawanywa vizuri Kwa hiyo mimi niseme tu kwamba tunatambua mchango wa viongozi hawa wakati ambapo uchumi utatengemaa tunaweza tukaongeza lakini kwa sasa utaratibu ndiyo huo. Mheshimiwa Mwenyekiti, mgawanyo wake kama tulivyosema, 40% zitakwenda kwenye miradi

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    276 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us