Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Arobaini na Saba – Tarehe 18 Agosti, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009. MHE. WILSON M. MASILINGI - MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA: Taarifa ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009. MHE. SAVELINA S. MWIJAGE (K.n.y. MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM - MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA): 1 Taarifa ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na maoni ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009. MASWALI NA MAJIBU Na. 407 Malipo ya Watendaji Katika Uandikishaji wa Wapiga Kura MHE. SIJAPATA F. NKAYAMBA aliuliza:- Kwa kuwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilianzishwa nchini kote na Walimu pamoja na watendaji ndio waliohusika katika zoezi la uandikishaji na kwa kuwa kazi ilifanyika kwa mwezi mmoja lakini malipo yalitolewa nusu (laki nne tu) na kwa kuwa baadhi ya watendaji waliendelea tena na kazi ya kufanya masahihisho kwa mwezi mmoja lakini hawakulipwa:- (a) Je, fedha iliyobaki italipwa lini? (b) Je, fedha ya malipo ya mwezi mmoja italipwa lini? (c) Kama kazi iliyoongezwa ya mwezi mmoja ilikuwa ni ya kujitolea kwa nini Serikali isiwaambie wahusika? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijajibu swali, naomba kutoa neno la shukrani kwa Wabunge wenzangu hasa baada ya kuondokewa na Mama yangu mpendwa, Mama Lucia Deaisile Mwanri, wakati nilipopata tatizo hili Ofisi yako pamoja na Wabunge wenzangu walisimama imara na walihakikisha kwamba wananifariji katika hali hii ngumu ambayo ilinipata. Kwa niaba ya familia napenda kuchukua nafasi hii kusema ahsante kwako, kwa Spika mwenyewe, kwa Waziri Mkuu, viongozi wote pamoja na Waheshimiwa Wabunge wenzangu. Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. 2 NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sijapata Fadhili Nkayamba, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a), (b) na (c) kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba watumishi Walimu pamoja na watendaji walishiriki katika mchakato wa kuandaa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Katika zoezi hilo Wakurugenzi wa Halmashauri ndiyo waliokuwa wasimamizi katika Halmashauri zao na kila Mtendaji wa Kata alikuwa ndiye msimamizi mkuu katika Kata husika. Baadhi ya Waratibu Kata Elimu pia walishiriki kama wakufunzi. Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha kwamba, zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi kila mdau aliyeshiriki alitakiwa kutekeleza wajibu wake kwa makini. Ilipotokea kasoro mwandikishaji kwenye kituo husika pamoja na Afisa Mtendaji walitakiwa kufanya marekebisho kwa kuzingatia viwango vilivyokubaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili hatimaye walipwe staili zao. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma wahusika wote walilipwa haki zao na kama wapo baadhi ambao hawakulipwa naelekeza kwamba wawasilishe vielelezo vyao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma kwa ajili ya uhakika. Iwapo itabainika kwamba ni kweli hawakulipwa baadhi ya posho zao watalipwa mara moja. Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu waandikishaji ambao waliendelea tena na kazi ya kufanya masahihisho ilipotokea kasoro ya uandikishaji kwenye kituo husika ilikuwa ni wajibu wa mwandikishaji kusahihisha, hivyo walioendelea na kazi kwa kufanya masahihisho walikuwa wanatimiza wajibu wao ili kuboresha palipokuwa na kasoro. MHE. SIJAPATA F. NKAYAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa watumishi hao walifanya kazi yao kwa mujibu wa sheria lakini katika malipo Halmashauri ya Kigoma Vijijini walilipwa laki nne, Kigoma Mjini walilipwa laki nane. Je, kwa kuwa wote walifanya kazi moja wao walilipwa nusu na wengine wakalipwa taslimu. Je, ilikuwakuwaje wao walipwe nusu na wengine walipwe taslimu na ni vigezo gani vilivyotumika? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili… NAIBU SPIKA: Wengine walilipwa cheque wengine taslimu au? (Kicheko) MHE. SIJAPATA F. NKAYAMBA: Wengine walilipwa laki nne na wengine walilipwa laki nane. Hilo la kwanza. Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kwa kuwa watumishi hao walipokuwa wanakwenda kumdai Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Mkoa aliwaambia kuwa 3 wapeleke barua ya mkataba. Je, ina maana Tanzania nzima wale walioandikisha daftari la wapiga kura walikuwa na mkataba? NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama tulivyoeleza hapa, tumewasiliana na wenzetu kule Kigoma na wao records zao zinaonyesha kwamba wale wote ambao walitumika katika zoezi la kuandaa hili daftari walilipwa na kama nilivyojibu hapa kama kuna vielelezo vyovyote vile ambavyo vinathibitisha na kuonyesha kwamba hawa watumishi walitumika lakini hawakulipwa kama ilivyostahili. Tumeagiza hapa kwamba walipwe mara moja na tunachohitaji ni huo ushahidi na wala hakuna haja ya ku-doubt hayo anayosema Mheshimiwa Mbunge. Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la kwamba hawa ambao walikuwa wamedai hiyo nusu iliyobakia kwamba wametakiwa kutoa mkataba, nadhani ni katika ule mchakato tu wa kutaka kupata huo ushahidi na vitu vingine. Hapa kinachotakiwa ni kwamba kama waliingizwa katika orodha ya watu waliofanya zoezi hili na kama kweli walitumika kama inavyozungumzwa watalipwa. Ambao tunasema hawastahili kulipwa ni wale ambao walikuwa wameandikisha hili daftari lakini wakawa wamekosea, sasa kile kipindi cha kusahihisha ndicho tunachosema hawawezi kulipwa. MHE. EMMANUEL J. LUHAHULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa tatizo la mapunjo kwa hawa walioandikisha hili daftari la wapiga kura linaelekea kuwa ni tatizo kubwa ambapo hata mapunjo mengine yanasababisha hata Walimu kutaka kuandamana katika nchi hii. Walimu wanataka kuandamana kwa ajili ya mapunjo yao na kwa nini sasa Serikali isifanye utaratibu wa kuhakiki mapunjo ya Walimu hao pamoja na watumishi wengine haraka ili kuzuia hali hii? NAIBU SPIKA: Mapunjo ya uchaguzi au mapunjo ya nini? MHE. EMMANUEL J. LUHAHULA: Mapunjo ya uchaguzi ni sawasawa tu na malipo ambayo Walimu wanalalamikia. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Luhahula, siyo sawa. Ahsante. Tunaendelea. Na. 408 Uuzaji wa Nyumba za Serikali MHE. SAID A. ARFI (K.n.y. MHE. MHONGA S. RUHWANYA) aliuliza:- Kwa kuwa utaratibu wa uuzaji wa nyumba za Serikali nchini umeliingizia Taifa hasara kubwa na kusababisha matumizi yasiyo ya lazima kwa kuwalipia gharama za malazi watendaji wake wanapohamishiwa katika vituo vipya vya kazi Mikoani:- 4 (a)Je, Serikali inafahamu kuwa Majaji watatu wa Kanda ya Tabora wameishi kwenye Hoteli ya Orion Tabora Hotel kwa kipindi kirefu kutokana na kukosa nyumba za Serikali? (b)Kutokana na hadhi zao umuhimu na unyeti wa kazi zao Majaji hutakiwa kufanya kazi na kuishi mazingira yaliyo tulivu na comfortable hivyo kupelekea Serikali kuwalipia chumba chenye hadhi ya suit ambacho ni shilingi 120,000/= kwa siku. Je, Serikali imetumia kiasi gani kulipa hoteli kwa kipindi chote? (c)Je, ni hasara kiasi gani imesababishwa na uuzaji wa nyumba nchi nzima? NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Miundombinu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a)Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora katika nyakati tofauti kuanzia mwaka 2006 waliwahi kuishi Hoteli ya Orion. Hata hivyo, kwa sasa hakuna Jaji yeyote ambaye bado anaishi hotelini Mkoani Tabora. Mheshimiwa Jaji aliyekuwa amebaki hotelini hapo aliondoka na kuhamia kwenye nyumba ya Serikali mwezi wa Agosti, 2007. (b)Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na hadhi za Waheshimiwa Majaji kutakiwa kupata chumba cha suit jumla ya fedha iliyotumika kulipia malazi ya Waheshimiwa Majaji watatu katika Hoteli ya Orion, kuanzia mwaka 2006 hadi Julai, 2007 ni Sh. 22,063,950/=. Aidha, gharama ya chumba kimoja kilichokodishwa ilikuwa Sh. 42,000/= na siyo Sh. 120,000/= kama ilivyosemwa na Mheshimiwa Mbunge. (c) Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchukua fursa hii kulieleza Bunge lako Tukufu kuwa, hatua ya Serikali kuuza baadhi ya nyumba zake imekuwa na faida na manufaa yafuatayo:- (i) Watumishi wa umma waliouziwa nyumba hizo sasa wanaishi katika nyumba zao, nyumba ambazo ni bora kuliko nyumba walizokuwa wanapanga awali. (ii) Uuzwaji wa nyumba za Serikali umeweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizokuwa zinatumika kugharamia matengenezo ya nyumba hizo ambazo sasa zinalipwa na waliozinunua. (iii) Kutokana na mapato yaliyotokana na kuuzwa nyumba hizo, Wizara yangu kupitia Wakala wa Majengo imeweza kujenga nyumba mpya 967 katika maeneo 5 mbalimbali nchini. Nyumba hizo zimeingizwa kwenye mpango wa kuwauzia na nyingine kuwapangisha watumishi wa umma. MHE. AMOUR S. ARFI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa katika majibu ya swali la msingi Mheshimiwa Naibu Waziri anasema kwamba, imepatikana
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages140 Page
-
File Size-