NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Nane – Tarehe 12 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba niwape taarifa. Kama mlivyoona leo tumeingia hapa Bungeni kwa utaratibu mpya tofauti na ilivyozoeleka. Kanuni ya 20(1)(c) ya Kanuni za Bunge inaeleza kwamba Spika ataingia na kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge akiongozana na mpambe wa Bunge lakini haitoi maelezo ya mlango gani utumike wakati wa kuingia au kutoka Bungeni. (Makofi/Kicheko) Katika Mabunge mengi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth) na nchi nyingine, utamaduni uliozoeleka ni kwa Spika wa Bunge kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge akitokea chumba maalum cha Spika (Speaker’s Lounge). Baadhi ya nchi zenye utamaduni huo ambazo mimi na misafara yangu mbalimbali tumewahi kushuhudia ni India na Uingereza, wana utaratibu kama huu tuliotumia leo. Kwa kuwa tumekuwa tukiboresha taratibu zetu kwa kuiga mifano bora ya wenzetu, kuanzia leo tutaanza kutumia utaratibu huu mpya tulioutumia asubuhi ya leo kwa misafara 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kuingia na kutoka Bungeni kwa kutumia mlango wa kuelekea Speakers Lounge, ni kuingia na kutoka kwa utaratibu huu hapa. Waheshimiwa Wabunge, mlango mkuu wa mbele utaendelea kutumiwa na Waheshimiwa Wabunge kama kawaida yenu na Spika na msafara wake watautumia mlango huu mkuu wakati wa matukio maalum ya Kibunge kama vile wakati wa kufunga au kufungua Bunge au tunapokuwa na ugeni wa Kitaifa kama Mheshimiwa Rais akitutembelea tutaingia kwa lango lile kuu, katika siku za kawaida zote tutafuata utaratibu huu mliouona hapa mbele. Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, hii ndiyo taarifa ambayo nataka kuitoa na ina faida nyingi. Wakati mwingine mnaweza mkawa na hasira tunapopita hapa mkaturukia hapo katikati ikawa tabu. Kwa hiyo, hata kiusalama hapa ni bora zaidi. (Makofi/Kicheko) Katibu. NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali, swali la kwanza ni kwa Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mheshimiwa Rhoda Edward Kunchela, Mbunge wa Viti Maalum, kwa niaba yake Mheshimiwa Mbunge wa Rombo. Na. 63 Mgogoro kati ya Wafanyabiashara na Manispaa ya Mpanda MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y RHODA E. KUNCHELA) aliuliza:- Kuna mgogoro kati ya Manispaa na wafanyabiashara wanaomiliki vibanda katika masoko ya Buzogwe Soko Kuu 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) na Mpanda Hoteli ambapo Manispaa inawaongezea kodi wafanyabiashara hao bila makubaliano ya pande zote mbili:- Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kumaliza mgogoro huo maana ni muda mrefu sasa na wafanyabiashara wamefunga vibanda vyao wakisubiri muafaka na hivyo Serikali kushindwa kukusanya kodi? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rhoda Edward Kunchela, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashari ya Manispaa ya Mpanda imejenga vibanda vya biashara katika masoko kwa ubia baina ya Halmashauri na wafanyabiashara (wamiliki/ wajenzi). Masoko ambayo yaliongezewa ushuru wa pango ni masoko yanayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ambayo ni soko kuu la Buzogwe na Azimio. Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda iliamua kufanya mabadiliko ya ushuru baada ya kubaini kuwa wamiliki/wajenzi walikuwa wakinijufaisha wenyewe kwa kuwapangisha wafanyabiashara na kuwatoza kodi kati ya Sh.100,000 hadi Sh.150,000 na kuwasilisha kodi ya Sh.15,000 tu kwa mwezi kwa Halmashauri. Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya kodi yaliyofanyika kwa wamiliki/wajenzi ni kutoka Sh.15,000 hadi Sh.40,000 kwa mwezi. Wadau wote walishirikishwa na makubaliano yaliridhiwa katika vikao vya kisheria vya Halmashauri. Aidha, hakuna maduka yaliyofungwa, huduma zinaendelea kama kawaida na Halmashauri imeendelea kukusanya mapato. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, Halmashauri zinaweza kufanya marekebisho ya kodi wakati wowote. Utaratibu unaotumika katika kuibua na kuongeza kodi/tozo huanzishwa, huchakatwa na kuamuliwa na kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmashauri husika. SPIKA: Mheshimiwa Selasini, swali la nyongeza. MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Wafanyabiashara kote nchini hivi sasa wanalalamika biashara zao kuyumba na ukweli uliopo ni kwamba tatizo hili bado linaendelea katika Manispaa hii ya Mpanda. Je, Serikali iko tayari kuiagiza Halmashauri kwa spirit ya utawala bora kukaa tena na wafanyabiashara hawa ili kuweza kwa pamoja kujadili kiwango ambacho Halmashauri na wafanyabiashara watanufaika ili sasa pande zote mbili ziweze kufanya kazi bila manung’uniko? Mheshimiwa Spika, swali la pili, katika utendaji bora na ushirikiano na Halmashauri ni kwamba maeneo mengi utendaji unaonekana kukwama kwa sababu wakati mwingine mabavu yanatumika katika kuweka hivi viwango vya kodi na kadhalika. Ni lini Serikali itatoa maagizo ya hakika kabisa ili Halmashauri zisigombane na wateja wao ambao ni hawa wafanyabiashara na sasa hivi tunavyohimiza Halmashauri ziweze kuongeza vyanzo vipya vya mapato ili mapato ya Serikali kokote katika nchi yetu yasipotee tu kwa sababu ya uhusiano mbaya kati ya Halmashauri pamoja na wafanyabiashara? (Makofi) SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaibana Serikali kwa jambo ambalo ni letu wenyewe. Madiwani ndiyo mnaongeza hizo bei halafu mnaitaka Serikali iingilie kati wakati ninyi wenyewe ndiyo Madiwani mnaoongeza bei. Mheshimiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa Josephat Kandege, ufafanuzi tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Spika, nafarijika swali kama hili kutoka kwa Mheshimiwa Selasini na bahati nzuri yeye ni Mjumbe wa Kamati ya Utawala na TAMISEMI. Katika nafasi niliyopata kushiriki katika vikao vyake amekuwa akihimiza Halmashauri zihakikishe kwamba zinakusanya mapato yake ili ziweze kujiendesha. Mheshimiwa Spika, umenisaidia. Sisi Waheshimiwa Wabunge ni Madiwani tukiwa kwenye halmashauri zetu. Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ilishirikisha wafanyabiashara, zimeundwa Tume zisizopungua tatu na katika jibu langu la msingi nimeeleza hawa ambao wamekuwa wanapangishiwa wamekuwa wakilipa Sh.100,000 mpaka Sh.150,000. Mheshimiwa Spika, sasa halmashauri katika kuona katika vyanzo vyao ambavyo ni vizuri wakavisimamia iko katika kupandisha kutoka Sh.15,000 ambayo imekuwa ikitozwa zaidi ya miaka 30 na kwenda mpaka Sh.40,000 which is very fair. Mheshimiwa Spika, ameelezea juu ya suala zima la kutokuwa na migongano baina ya wafanyabiashara na halmashauri. Kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi, ushirikishwaji umekuwepo na hata ninavyoongea leo hakuna hata kibanda kimoja ambacho kimefungwa katika Manispaa ya Mpanda kwa sababu ushirikishwaji umekuwepo. Zimekuwepo Tume zaidi ya tatu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maridhiano yanakuwepo na halmashauri inapata chanzo chake cha pesa na kinatumika sahihi. SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Dkt. Mollel. MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Siha inafanana na wilaya iliyotajwa hapo lakini kwa tofauti kidogo, Halmashauri ya Siha ina magulio, haina masoko. Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano alishatoa maelekezo kwamba akinamama wanaotandaza bidhaa chini na wale ambao ni wa chini kabisa wasidaiwe ushuru. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, cha kusikitisha kabisa jana katika Wilaya ya Siha wananchi kwenye soko la Sanya Juu wameenda kulazimishwa kulipa ushuru kwa kutumia polisi na wananchi waliposema Rais alishasema sisi tunaotandika chini tusilipe waliambiwa Rais huyo huyo ndiye anasema tukusanye kodi na bado yeye anatuvuruga kwenye kukusanya kodi, lipeni ushuru na polisi wakapelekwa sokoni na wananchi walipata taharuki sana. Mheshimiwa Spika, sasa naomba nielezwe kwamba tunawezaje kuwasaidia hawa akinamama ambao ni vipenzi vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari alishatoa maelekezo na yamekuwa yakipuuzwa na Halmashauri zetu. (Makofi) SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu, Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, maelekezo aliyotoa Mheshimiwa Rais kwamba wale akina mama ambao wanapanga bidhaa zao ikiwa ni pamoja na wale ambao wanauza ndizi wasibugudhiwe ni msimamo ambao uko thabiti, hauyumbi hata mara moja. Kama kuna Mkurugenzi yeyote ambaye hataki kutekeleza kauli na maelekezo ya Mheshimiwa Rais tafsiri yake ni kwamba Mkurugenzi huyo hajitaki. (Makofi) Mheshimiwa Spika, naomba nikuhakikishie, leo wakati naingia nilimwambia Mheshimiwa Mollel katika maeneo ambayo nina wajibu wa kwenda kutembelea ni pamoja na Jimbo lake hii ni pamoja na kwenda kutazama eneo la ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya. (Makofi) SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tuendelee na swali linalofuata la Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke, Viti Maalum Kigoma. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 64 Uhitaji wa Watumishi wa Afya Katika Zahanati za Mkoa wa Kigoma MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Zahanati nyingi za Vijiji vya Mkoa wa Kigoma katika wilaya zote zina upungufu mkubwa sana wa watumishi wa afya na baadhi ya zahanati hazina Waganga hivyo huduma
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages187 Page
-
File Size-