Bajeti 19 Ikulu 1

Bajeti 19 Ikulu 1

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHESHIMIWA ISSA HAJI USSI GAVU KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 MEI, 2019 YALIYOMO YALIYOMO ii ORODHA YA VIAMBATISHO iii VIFUPISHO VYA MANENO iv 1. UTANGULIZI 1 2. UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI KWA KIPINDI CHA JULAI – MACHI 2018/2019 6 2.1 UPATIKANAJI WA FEDHA ZA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA OFISI 7 2.2 MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI KWA KIPINDI CHA JULAI – MACHI 2018/2019 7 3. MWELEKEO WA BAJETI YA OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 53 4. PROGRAMU KUBWA NA NDOGO NA MAKISIO YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 56 5. MAOMBI YA FEDHA KWA KAZI ZILIZOPANGWA KUTEKELEZWA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 66 5.1 MATUMIZI YA KAWAIDA NA MIRADI YA MAENDELEO 66 5.2 MAOMBI YA FEDHA 2019/2020 67 6. HITIMISHO 67 ii OR-MBLM ORODHA YA VIAMBATISHO Kiambatisho Nam. 1: Mapitio ya Upatikanaji wa Fedha kwa Kazi za Kawaida 2018/2019 71 Kiambatisho Nam. 2: Orodha ya Shehia zilizooneshwa Sinema 76 Kiambatisho Nam. 3: Orodha ya Vipindi Vilivyorushwa Hewani na Idara ya Mawasiliano na Habari Ikulu – Zanzibar Kupitia Kituo cha ZBC Radio (A) 77 Kiambatisho Nam. 4: Idadi ya Wafanyakazi Waliopatiwa Mafunzo 82 Kiambatisho Nam. 5: Idadi ya Watumishi Waliokwenda likizo 85 Kiambatisho Nam. 6: Idadi ya Wafanyakazi waliofanyiwa upekuzi na Taasisi walizotoka 86 Kiambatisho Nam. 7: Orodha ya Taasisi Zilizofanyiwa Ukaguzi wa Kiusalama 90 Kiambatisho Nam. 8: Idadi ya Watumishi Waliopewa Mafunzo ya Udhibiti wa Siri na Utunzaji wa Nyaraka za Serikali 91 Kiambatisho Nam. 9: Orodha ya Nyaraka za Sera na Sheria Zilizojadiliwa na Baraza la Mapinduzi 92 Kiambatisho Nam. 10 : Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti 2019/2020 94 Kiambatisho Nam. 11 : Orodha ya Wageni Waliofika Ikulu na Kuonana na Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Kuanzia Mwezi wa Julai, 2018 Hadi Mwezi wa Aprili, 2019 99 iii OR-MBLM VIFUPISHO VYA MANENO ACP African Carribean Pacific Group of States (Mashirikiano ya Nchi za Afrika, Carribean na Pasifiki) APRM African Peer Review Mechanism (Mpango wa Nchi za Afrika Kujitathmini Kiuchumi, Kidemokrasia na Utawala Bora) CCM Chama Cha Mapinduzi COMESA Common Market for Eastern and Southern Africa (Soko la Pamoja la Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika) COSTECH Tanzania Commission for Science and Technology (Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania) EAC East African Community (Jumuiya ya Afrika Mashariki) EPA Economic Partnership Agrements (Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi) GSO Government Security Office (Ofisi ya Usalama wa Serikali) IORA Indian Ocean Rim Association (Jumuiya ya Nchi zilizopakana na Bahari ya Hindi) IPA Institute of Public Administration (Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar) KIST Karume Institute of Science and Technology (Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume) MKUZA Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar MOU Memorundum Of Understanding (Mkataba wa Makubaliano) ORMBLM Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi iv OR-MBLM SADC Southern Africa Development Community (Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika) SMZ Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SUZA State University of Zanzibar (Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar) TEHAMA Teknolojioa ya Habari na Mawasilino TZS Tanzania Shillings (Shilingi ya Tanzania) UAE United Arab Emirates (Umoja wa Falme za Kiarabu) ZACADIA Zanzibar Canada Diaspora Association (Jumuiya ya Wanadiaspora wa Zanzibar wanaoishi Canada) ZBC Zanzibar Broadcasting Company (Shirika la Utangazaji Zanzibar) ZIPA Zanzibar Investment Promotion Authority (Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar) ZPDC Zanzibar Petroleum Development Corporation (Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta Zanzibar) ZU Zanzibar University (Chuo Kikuu cha Zanzibar) v OR-MBLM 1. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako tukufu, likae kama Kamati kwa ajili ya kupokea, kujadili, kuzingatia na hatimae kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 2. Mheshimiwa Spika, kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu mwingi wa rehema na utukufu. Tunamshukuru Yeye kwa kutujaalia kukutana hapa tukiwa wazima na wenye afya njema. Vile vile namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nguvu na uwezo wa kuwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwenye Baraza lako hili tukufu. Namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kutuzidishia siha njema, amani na utulivu katika nchi yetu. 3. Mheshimiwa Spika, kwa heshima naomba kuchukua fursa hii adhimu kumpongeza Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uongozi wake uliojaa hekima na busara. Juhudi, umakini na umahiri wake umeiwezesha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa zaidi ya asilimia 90. Utekelezaji huo unakwenda 1 OR-MBLM sambamba na malengo ya Dira ya Maendeleo ya 2020 pamoja na Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar Awamu ya Tatu (MKUZA III). Namuomba Mwenyezi Mungu amzidishie afya njema yeye na familia yake, ili aendelee kuwatumikia wananchi wa Zanzibar na kuwaletea maendeleo ya haraka zaidi. 4. Mheshimiwa Spika, nampongeza kwa dhati Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kwa namna anavyomsaidia na kumshauri Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na Ofisi yetu kiujumla katika kutekeleza majukumu yatu. Pamoja na kuwa anakabiliwa na majukumu mengi ya Kitaifa, pia amekuwa mstari wa mbele katika kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kitope. Ni imani yetu kuwa wananchi wa Jimbo hilo wataendelea kumpatia ushirikiano, ili aendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi. 5. Mheshimiwa Spika, pongezi maalum nazileta kwako Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa namna unavyoliongoza na kulisimamia Baraza lako Tukufu. Kadhalika, nampongeza Naibu Spika Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma pamoja na Mheshimiwa Mwanaasha Khamis Juma na Mheshimiwa Shehe Hamad Mattar Wenyeviti wa Baraza hili kwa namna wanavyokusaidia katika kazi zako za Baraza. 2 OR-MBLM 6. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee nampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa, Mheshimiwa Panya Ali Abdalla kwanza kwa kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Kamati hii na pili kwa uwezo wake wa hali ya juu katika kusimamia dhamana aliyokabidhiwa. Vile vile, nampongeza Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Ali Suleiman Ali (Shihata) pamoja na Waheshimiwa wajumbe wote wa Kamati hii. Ni imani yangu tutaendelea kushirikiana nao katika kutekeleza ipasavyo majukumu yetu tuliyokabidhiwa. 7. Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa natoa pongezi kwa Waheshimiwa Wenyeviti wa Kamati ya Bajeti Mheshimiwa Mohammed Said Mohammed (Dimwa) na Kamati ya Kudhibiti na Kuchuguza Hesabu za Serikali Mheshimiwa Miraji Khamis Mussa (Kwaza) na Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati hizi kwa ushirikiano mzuri wa kikazi na ORMBLM. Mwisho naomba kumalizia pongezi zangu kwa Waheshimiwa Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi kwa michango, pongezi, ushauri na maelekezo mazuri ambayo kwa namna moja au nyengine yamekuwa yakijenga na kutusaidia katika kutekeleza na kutimiza majukumu yetu ipasavyo. 3 OR-MBLM 8. Mheshimiwa Spika, nitakuwa sijatenda haki bila ya kuwapongeza wananchi wa Zanzibar kwa imani na upendo wao wa dhati katika kumuunga mkono Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa juhudi zake za kuiletea maendeleo Zanzibar. Wito wangu kwa wananchi wote wa Zanzibar waendelee kumuunga mkono na kushirikiana nae kikamilifu kwa maslahi ya kila mmoja wetu. 9. Mheshimiwa Spika, tarehe 30 Aprili, 2019 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepata msiba kufuatia kifo cha Ndugu Juma Ali Juma, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi imepokea kwa mshtuko na huzuni taarifa ya kifo hicho. Marehemu Juma Ali Juma atakumbukwa kwa juhudi, uadilifu na mchango wake mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yake. ORMBLM inaungana na wanafamilia katika kuomboleza msiba huu katika kipindi hiki kigumu. Namuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema Peponi. Amin. 10. Mheshimiwa Spika, msimu wa mvua tayari umenza katika visiwa vyetu. Katika miongo ya hivi karibuni, tumeshuhudia mvua kuwa kubwa zikinyesha katika maeneo yetu ambazo husababisha athari mbali mbali kwa wananchi. 4 OR-MBLM Aidha, wataalamu wa hali ya hewa wametabiri kuwa katika msimu huu wa mvua kutakuwa na mvua kubwa ambazo zitakuwa za wastani au juu ya wastani kwa baadhi ya maeneo. Hivyo, naomba kutoa wito kwa wananchi wote kuchukua tahadhari zinazostahiki, ili kujiepusha na athari zinazoweza kujitokeza. Kwa upande mwengine, nawaomba wananchi wazitumie vizuri mvua hizi kwa kupanda miti na mazao mengine ya chakula. 11. Mheshimiwa Spika, huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislamu wa hapa Zanzibar wanajumuika na waislamu wenzao kote duniani kufunga mwezi huu mtukufu. Mwezi huu huambatana na ibada na kufanyiana mambo mema kwa jamii yetu. Namuomba Mwenyezi Mungu atujaalie funga njema na baraka tele, ili

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    114 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us