Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 MAJADILIANO YA BUNGE

Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 MAJADILIANO YA BUNGE

Nakala ya Mtandao (Online Document) MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA ISHIRINI __________ Kikao cha Ishirini na Moja - Tarehe 5 Juni, 2015 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, napenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote kwa msiba uliotupata, msiba ulitokea wakati nikiwa Geneva ambapo tulikuwa na kikao cha Kamati Ndogo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Maspika wote duniani utakaofanyika mwezi wa Nane, sasa kuna Maspika kumi ndiyo tupo kwenye maandalizi ya mkutano huo na kilikuwa ni kikao chetu cha mwisho kabla ya mkutano huo. Kwa hiyo, wakati msiba unatokea nilikuwa huko, nilipewa taarifa na nilisikitika sana. Kwa hiyo, tutatangaza baadaye mchana, ni akina nani watakaokwenda kuzika kesho. Katibu! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. CHARLES M. KITWANGA): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa Fedha, 2015/2016. MHE. DAVID H. MWAKYUSA (k.n.y. MHE. PROF. PETER M. MSOLLA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED (k.n.y. MHE. MAGDALENA H. SAKAYA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MAJI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) MASWALI NA MAJIBU Na. 149 Ahadi ya Maji kwa Wananchi wa Wilaya ya Karagwe MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA (k.n.y. MHE. GOSBERT B. BLANDES) aliuliza:- Mwaka 2013 Mheshimiwa Rais aliahidi kuwapatia maji wananchi wa Wilaya ya Karagwe kutoka Ziwa Rwakajunju lililopo Kata ya Bweranyange:- Je, ni lini mradi huu utaanza na kukamilika? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gosbert Begumisa Blandes, Mbunge wa Karagwe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe inakadiriwa kuwa na asilimia 48 ya wakazi wanaopata huduma ya maji. Kwa kutambua tatizo hilo, Serikali imeanza kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa miradi ya maji kutoka Ziwa Rwakajunju umbali wa takribani kilomita 35 hadi Makao Makuu ya Wilaya ya Karagwe. Mradi huu utahusisha maeneo yote yatakayopitiwa na mradi pamoja na Mji wa Kayanga na Omurushaka. Kazi hii ya Upembuzi imeanza na inafanywa kwa ushirikiano wa Wizara ya maji na Mamlaka ya Maji ya Mji wa Bukoba ambayo imeajiri mtaalam Mshauri M/S Basler Holffman Limited wakishirikiana na M/S RWB na WILALEX kuanzia mwaka wa fedha wa 2013/2014 na inatarajiwa kukamilika mwaka wa fedha 2015/2016. Aidha, rasimu ya taarifa ya upembuzi imetolewa na sasa wanaendelea na usanifu wa kina. Mheshimiwa Spika, mradi huu wa kuchukua maji kutoka Ziwa la Rwakajunju unatajia kunufaisha Mji Mdogo wa Kayanga/Omurushaka katika maeneo ya Ndama, Kayanga, Miti, Kagutu, Bujuruga, Kishao, Bugene, Nyabwegira, Nyakahanga na Ihanda yenye jumla ya wakazi 81,591. Mheshimiwa Spika, aidha, vijiji vinavyotarajiwa kupitiwa na mradi huo na kunufaika ni pamoja na Vijiji vya Rukole, Chonyonyo, Kiruruma, Nyakagoyegoye, Nyamieli, Chabalisa, Ahakishaka, Nyakashenyi, Nyabiyonza, Nyakaiga na Kibondo. Azma ya Serikali ni kuhakikisha kwamba ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatekelezwa mara baada ya kukamilika upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi wa maji kutoka Ziwa Rwakajunju. MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kutaja sehemu nyingi na kuonesha kuwa anajua kinachoendelea, lakini naomba nimuulize swali, utafiti tu umechukua miaka mitatu na sasa hivi mwenye swali alitaka kuuliza, ni lini itaanza hiyo shughuli ya kupatia wananchi maji na akawa anataka kuuliza, huo utaratibu utakamilika lini? Mheshimiwa Spika, swali la nyongeza, hili swali liko sawasawa na wana Misenyi ambao tuliuliza Mto Kagera uko katikati ya Mji wetu Mkuu wa Wilaya ya Misenyi na Misenyi hakuna hata bomba moja la maji, hakuna kabisa, hivyo, tunauliza ni lini mtatuwekea maji na Waziri wa Maji 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) alituambia karibuni wataanza kutupa maji salama. Ni lini sasa wataanza kutupatia maji wana Misenyi ikizingatiwa kuwa tumezungukwa na maji? NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mshama kama ifuatavyo:- Kwanza kabisa nikubaliane na majibu ya Msingi ya Mheshimiwa Naibu Waziri na niseme tu kwamba, hii ni ahadi ya Rais, kwa maana ya pale Karagwe, alitoa Mheshimiwa Rais na tumesema kwamba tutatekeleza lakini mradi wowote wa maji ni lazima upitie hatua zote. Kwa hiyo, kwa sasa tunafanya usanifu wa kina, lakini pia katika bajeti ya mwaka huu kumetengwa fedha bilioni moja kwa ajili ya mradi huu. Kwa hiyo, nimwombe tu Mheshimiwa awe na subira na apitishe bajeti yetu ambayo ni leo ili ahadi hii ya Rais tuanze kuitekeleza. Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusu Misenyi ni kweli na nimekuwa nikiongea naye na ameshamwona Waziri tunatekeleza Mradi wa Vijiji Kumi na wazo alilotoa sisi kama Wizara tunalipokea na tunataka kutumia maeneo mengi ambayo yana vyanzo, maziwa na mito kuona kwamba tunapata maji ya uhakika. Kwa hiyo, azma ya Serikali iko pale pale, tutashirikiana naye kuona kwamba yale aliyoshauri tunayafanyia kazi. MWENYEKITI: Ahsante, Wizara ipo mtayasema vizuri. Sasa tuendelee na Mheshimiwa Joseph Selasini swali linalofuata Mheshimiwa Suzan Lyimo kwa niaba yake, naona watu wamekwenda kutangaza nia hawapo humu ndani. Na. 150 Kupandisha Hadhi Mji wa Rombo kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo MHE. SUZAN A.J. LYIMO (k.n.y. MHE. JOSEPH R. SELASINI) aliuliza:- Mji wa Rombo uko katika Kijiji cha Kelamfua hadi sasa:- (a) Je, Serikali iko tayari kuupandisha hadhi Mji huo ambao una vigezo vyote vinavyotakiwa kama vile Hospitali, Mahakama, soko, idadi ya watu na kituo cha mabasi kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo? (b) Je, Serikali itakuwa tayari kulipa fidia kwa wananchi ambao watalazimika kutoa mashamba yao ili kupanua eneo la Mji huo? SPIKA: Ahsante. Naona watu wamekwenda kutangaza nia, hawamo humu ndani. Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu! (Kicheko) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Selasini, Mbunge wa Rombo, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, nakubaliana kabisa na Mheshimiwa Mbunge kuwa Mji wa Rombo umekidhi vigezo vyote vya kupanda hadhi na kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo. Kupitia Bunge lako naomba kutoa taarifa kuwa, tayari Serikali imekwisharidhia na kupandisha hadhi Mji wa Rombo kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rombo na sasa unatambulika kama Mamlaka ya Mji 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mdogo wa Mkuu Rombo na umekwishatangazwa kwenye tangazo la Serikali (GN) Na. 431 la tarehe 31 Oktoba, 2014. Mheshimiwa Spika, uendelezaji wa makazi nchini unaongozwa na Sera ya Taifa pamoja na Sheria ya Mipango Miji, Sheria Namba 8 ya mwaka 2007. Kwa miongozo hiyo, shughuli zotye za uendeshaji wa makazi zinasimamiwa na Halmashauri ya Miji, Wilaya, Majiji na Manispaa husika. Mheshimiwa Spika, Halmashauri imepanga kuwashirikisha wananchi wa maeneo yaliyo karibu na mji huo ili waridhie kuachia maeneo yao kwa ajili ya upanuzi wa huduma za jamii kama shule, maeneo ya ibada, soko, kituo cha polisi, kituo cha mabasi na huduma zingine muhimu pasipo kuhusisha ulipaji fidia. Endapo itabainika wako wananchi wanaohitaji kulipa fidia, Serikali itafanya uthamini wa maeneo hayo ili waweze kulipwa kulingana na Sheria na miongozo yetu iliyopo. SPIKA: Mheshimiwa Suzan Lyimo, swali la nyongeza! MHE. SUZAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru na vile vile naishukuru sana Serikali kwa kuweza kupandisha hadhi huu Mji wa Rombo. Maswali ya nyongeza; kwa imekuwa ni hulka ya Serikali kutokulipa fidia kwa wakati na kwa bei ya soko, hivyo kufanya wananchi wengi kukataa au kugoma kuhama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo hospitali, shule na vitu vingine. Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba watawalipa wananchi hao fidia kwa gharama ya soko la wakati huo? Mheshimiwa Spika, la pili, imekuwa vile vile ni tabia ya Serikali kupandisha hadhi Mikoa, Miji kwa matangazo, lakini vile vile haitoi kipaumbele cha kibajeti, kwa mfano, tunashuhudia Mikoa kama vile Geita, Katavi na Mkoa wa Njombe ambayo imepandishwa kuwa Mikoa, lakini unaona kabisa kuwa bado bajeti hairuhusu na hivyo masuala mbalimbali ya kijamii, kwa mfano, hospitali na mambo mengine unakuta yako palepale. Sasa naomba kujua ni kwa nini Serikali inapandisha hadhi lakini miundombinu inabaki vile vile na hivyo kufanya wananchi washindwe kupata maendeleo kwa wakati? SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu! NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tunapopandisha Miji hii midogo kupata Mamlaka husika ni lazima kuwe na zoezi la upimaji na ongezeko la huduma mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya kuwa Mji kwenye eneo husika na pale ambapo tunagusa maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa fidia, tathimini hufanyika. Mheshimiwa Spika, mara nyingi

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    151 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us