NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Kwanza – Tarehe 6 Novemba, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA (Hapa Wimbo wa Taifa Uliimbwa) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Tukae. Karibuni sana. Waheshimiwa tusikilizane. Brass Band tunawashukuru sana, mnafanya kazi nzuri sana, karibuni sana Bungeni. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: Kiapo cha uaminifu. KIAPO CHA UAMINIFU Wabunge wafuatao waliapa Kiapo cha Uaminifu:- 1. Mhe. Julius Kalanga Laizer; 2. Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara; 3. Mhe. Timotheo Paul Mnzava; na 4. Mhe. Zuberi Mohamed Kuchauka. SPIKA: Katibu 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge, Bunge lilipitisha Miswada mitano ya Sheria ya Serikali ifuatayo:- Kwanza, Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Mkuu ya Nchi ya Mwaka 2018 (The Dodoma Capital City (Declaration) Bill, 2018). Pili, Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania wa Mwaka 2018 (The Tanzania Teachers’ Professional Board Bill, 2018). Tatu, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 02 wa Mwaka 2018 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2) Bill, 2018). Nne, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa Mwaka 2018 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill, 2018). Tano; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018 (The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2018). Kwa taarifa hii napenda kuliarifu Bunge hili Tukufu kwamba tayari miswada hiyo mitano imepata kibali cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa sheria za nchi zinazoitwa:- Kwanza, Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma Kuwa Makao Makuu ya Nchi Na. 5 ya Mwaka 2018 (The Dodoma Capital City (Declaration) Act No. 5 of 2018); Pili, Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania Na. 6 ya Mwaka 2018 (The Tanzania Teachers’ Professional Board Act No. 6 of 2018); 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Tatu, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 ya Mwaka 2018 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2) Act of 2018); Nne, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) Na. 8 ya Mwaka 2018 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Act No. 8 of 2018); na; Tano, Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Na. 9 ya Mwaka 2018 (The Public Private Partnership (Amendment) Act No. 9 of 2018. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijawaita wawasilisha hati, nitambue uwepo Bungeni wa Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii. (Makofi/ Vigelegele) Karibu sana Mheshimiwa Waziri; pole sana kwa yote. Tulikuombea na Mwenyezi Mungu amekubali maombi yetu sasa uko pamoja nasi, karibu tena, karibu sana. (Makofi) Hati za kuwasilisha Mezani, sasa nimuite Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango; Mheshimiwa Naibu Waziri, Dkt. Ashatu Kijaji tafadhali. Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. MARIA N. KANGOYE (K.n.y. MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM (K.n.y. MHE. HALIMA J. MDEE - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana, Katibu! NDG.STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali la kwanza linaelekezwa kwenye Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na litaulizwa na Mheshimiwa Esther Michael Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum. Na. 1 Kulinda Ajira za Vijana Nchini MHE. ESTHER M. MMASI aliuliza:- Ukosefu wa ajira bado ni changamoto kubwa hasa tunapoangalia takwimu za kidunia na hata katika nchi yetu:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (a) Je, Serikali imejipangaje katika kulinda ajira za Vijana kupitia Sera ya Ajira? (b) Kwenye kada ya TEHAMA nchi yetu imekuwa ikipokea nafasi nyingi za ajira kwa Vijana kwenye Taasisi za kifedha kwa kazi nyingi kupelekwa nje ya nchi ikiwemo nchi jirani. Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA NA AJIRA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Michael Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Sera ya Taifa ya Ajira imeweka mikakati ifuatayo katika kulinda ajira za vijana:-. (i) Kuhamasisha mazingira bora ya uwekezaji katika sekta zenye uwezo mkubwa wa kuzalisha ajira hususani kilimo, ujenzi, viwanda na biashara; (ii) Kuwajengea vijana ujuzi wa fani mbalimbali kupitia programu za ukuzaji ujuzi ili vijana wengi zaidi wapate ujuzi stahiki utakaowawezesha kuwa na sifa za kuajirika, kujiajiri na kuwaajiri wengine; (iii) Kusimamia sheria na kanuni za kuwawezesha vijana wazawa wengi zaidi kushiriki katika miradi mikubwa ya maendeleo kama sehemu ya nguvu kazi na watoa huduma; na (iv) Utekelezaji wa Sheria ya Uratibu wa Ajira kwa Wageni Na.1 ya Mwaka 2015 ili kulinda nafasi za kazi kwa Watanzania, kwa kuhakikisha Watanzania wanafanya kazi ambazo vinginevyo zingefanywa na wageni. Mheshimiwa Spika, kada ya TEHAMA ni moja ya Kada ambazo zimewezesha ajira nyingi hapa nchini hivyo Serikali 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) imefanya juhudi kubwa kuhakikisha kunakuwepo naa Wataalam wa kutosha wa sekta hii na kulinda ajira zao kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, moja ni kutoa Wataalam wengi wa fani ya TEHAMA kupitia Vyuo Vikuu na Vyuo vya elimu ya Juu kwa kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kusomea fani za sayansi ikiwemo suala la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, pili ni kuendesha programu za ukuzaji ujuzi ili kuwajengea uwezo Watanzania katika fani ya TEHAMA kupitia mpango wa kitaifa wa kukuza ujuzi na tatu ni kutoa mikopo ya asilimia 100 kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kwa Kada ya TEHAMA. SPIKA: Mheshimiwa muuliza swali, swali la nyongeza. MHE. ESTHER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Swali langu kwa Serikali; Vijana wanaohitimu nchini Tanzania ni takribani laki sita mpaka laki nane kwa mwaka lakini vijana wanaoingia kwenye ajira rasmi na zisizo rasmi ni takribani ni asilimia kumi mpaka 25. Mheshimiwa Spika, nini kauli ya Serikali kutokana na masuala mazima ya retrenchment yanayoendelea nchini Tanzania. Kwa sasa tunayo taarifa ya kwamba kampuni ya TTCL ina mpango wa down size wafanyakazi zaidi ya 500; lakini pia ukienda kwa taasisi zisizo za Kiserikali mfano TBL tumeshuhudia hapa miezi michache iliyopita kwamba wali- retrench zaidi asilimia 80 na wakati huo huo wakihamishia sehemu kubwa ya operations mfano payroll function, lakini pia siyo hivyo tu finance Department ilipelekwa Mauritius; swali langu la kwanza; nini kauli ya Serikali haswa ukiangalia hali halisi ya ombwe kubwa la vijana wanaohitimu pasipo kuwa na ajira? Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kumekuwa na utamaduni mbaya sana unaoendelea kwenye taasisi za kifedha ambapo taasisi hizi zinakuwa zinajisajili Tanzania lakini sehemu kubwa sana ya majukumu ya IT yanakuwa 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) yanafanyika nje ya nchi. Mathalani benki ya Stanchart (Standard Chartered), Baclays, lakini Citi Bank pamoja na Stanbic bank, wamekuwa na utamaduni wa sehemu kubwa ya IT zinakuwa zinafanyika nje ya nchi. Ukiangalia NBC, supply of payment inafanyika South Afrika; ukiangalia Stanchart account opening na pia transaction process zote zinafanyika nchini Kenya. Ukiangalia Baclays function management zinafanyika nchini India, swali langu kwa Serikali. Nini kauli ya Serikali hasa ukiangalia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi hawa wanaohitimu shule ya TEHAMA? Naomba kupatiwa majibu stahiki na Mheshimiwa Naibu Waziri, ahsante. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana kwa swali zuri lenye mifano halisi, majibu ya swali hilo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Anthony Mavunde tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, nikianza na swali la kwanza la kuhusiana na retrenchment. Ni dhahiri kwamba sisi kama nchi katika Sera ya Ajira tunaendelea kulinda ajira za vijana katika nchi yetu kwa kuhakikisha kwamba vijana wengi zaidi wanapata fursa ya kuweza kuajiriwa. Mheshimiwa Spika, alichokisema Mheshimiwa Mbunge, kwa mujibu wa Sheria Na. 6 ya Mwaka 2004 imeweka vigezo ni katika hatua gani mwajiri anaweza akafanya retrenchment. Sheria ile pia imetoa nafasi kwa vyama vya wafanyakazi kushiriki moja kwa moja katika majadiliano kabla jambo hili halijafanyika. Mheshimiwa Spika, rai yangu kwa waajiri wote ni kwamba waendelee kufuata sheria inavyozungumza ya namna ya kuweza kuwaondoa wafanyakaza kazini kwa kuwa jambo hili lipo kisheria.Kazi yetu kama Wizara ni kuhakikisha kwamba taratibu
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages294 Page
-
File Size-