NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Thelathini na Tano – Tarehe 24 Mei, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, Asalam alaykum. WABUNGE FULANI: Waalaykumu s-salam SPIKA: Bwana Yesu Asifiwe. WABUNGE FULANI: Ameen. SPIKA: Kama mnavyojua wiki iliyopita tulipata msiba wa kuondokewa na ndugu yetu, rafiki yetu, Mbunge mwenzetu, Mheshimiwa Khatib Said Haji, Mbunge wa Konde. Tulipata nafasi ya kupumzika siku ile ya msiba kama ambavyo Kanuni zetu zinaelekeza lakini pia tulifanya maandalizi ya mazishi na baadhi yenu mliweza kushiriki kule Pemba, tunawashukuru sana. Kwa niaba ya Bunge, napenda kutoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na kwa Watanzania 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kwa msiba huu mkubwa ambao tumeupata wa ndugu yetu. Alikuwa ni Mbunge mahiri sana aliyelichangamsha Bunge na aliyekuwa akiongea hoja zenye mashiko lakini kama ambavyo Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. WABUNGE FULANI: Ameen. SPIKA: Napenda kutoa taarifa kwa Waheshimiwa Wabunge kwamba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mabadiliko kama mnavyofahamu tayari na katika mabadiliko kadhaa mojawapo ambalo amelifanya ni la Katibu wa Bunge. Aliyekuwa Katibu wetu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai sasa ni Mheshimiwa Stephen Kagaigai, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na badala yake ameteuliwa Ndg. Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu mpya wa Bunge. Naomba nimtambulishe mbele yenu sasa Katibu mpya, ahsante sana. (Makofi/Vigelegele) Kama mnavyofahamu Bunge letu lilianza zamani sana. Hivi Makatibu, Bunge lilianza mwaka gani? NDG. NENELWA J. MWIHAMBI, ndc - KATIBU WA BUNGE: Mwaka 1926. SPIKA: Nilikuwa natafuta Bunge halisi lilianza mwaka gani, ni mwaka 1926 (LEGICO). Kwa hiyo, bado miaka mitatu/ minne kutimiza miaka 100 ya Bunge la Tanzania. Katika miaka hiyo 100 ya Bunge la Tanzania ndiyo mwanamke wa kwanza kuwa Katibu wa Bunge. Kwa hiyo, kwa kweli tunampongeza, niwaombe Waheshimiwa Wabunge wote tumpe ushirikiano wa kipekee, tuoneshe kweli kwamba wanawake wanaweza, asanteni sana. (Makofi/Vigelegele) Katibu! 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. NENELWA J. MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE: KIAPO CHA UAMINIFU Waheshimiwa Wabunge wafuatao waliapa Kiapo cha Uaminifu:- 1. Mhe. Dkt. Florence George Samizi 2. Mhe. Kavejuru Eliadory Felix SPIKA: Katibu. NDG. NENELWA J. MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. MHE. KHADIJA HASSAN ABOUD K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana Mjumbe wa Kamati, Mheshimiwa Khadija Aboud, Katibu. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. NENELWA MWIHAMBI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla hatujaanza maswali, nitoe mwongozo tena kwa sababu tunazidi kuwa wazoefu sasa. Kipindi cha maswali kwa wakati huu wa bajeti ni saa moja tu, maswali yote kumi; ni ngumu sana ku-run kwa utaratibu huo lakini tutajitahidi sana kwamba twende kwa muda huo uliopangwa ili ratiba nyingine nazo ziweze kwenda kama zilivyopangwa tusile muda wenu wa uchangiaji na kadhalika. Kwa hiyo, naomba tujielekeze kwenye lengo la Kikanuni la muda huu, nao ni kwamba unatakiwa uulize swali, habari ya kujenga hoja, kuzunguka, kufanya hivi ni kutupotezea muda; tuulize swali. (Makofi) Waheshimiwa Mawaziri mjibu maswali, msizunguke. Ni lini jambo fulani wewe sema lini basi umemaliza, sijui kitu gani kitu gani jibu moja kwa moja. Kinachotakiwa ni jawabu na hata majibu yenu yale ya msingi huna sababu ya kuwa na jibu la ukurasa mzima. Zipo Wizara zinajibu vizuri sana zinakwenda moja kwa moja lakini zipo Wizara ambazo yaani ngonjera nyingi, hatuhitaji, hapa ni maswali na majibu basi, hakuna kitu kingine. (Makofi) Kwa hiyo, naomba sana kuanzia kesho sasa baada ya kutoa mwongozo huu wote tujielekeze hivyo, unayesimama uliza swali kwa sababu vinginevyo tutakukalisha chini, tukikukalisha chini ni aibu kwa wapiga kura wako, haipendezi, ndiyo maana huwa tunavumilia kidogo lakini sasa usituvute mpaka inafika mahali tukukalishe, jipange uliza swali. Walio wengi wanauliza swali lilelile yaani swali lake la nyongeza linakuwa lilelile la msingi, huwa tunanyamaza tu. Kama umeridhika na jibu unatulia sio lazima uulize swali la nyongeza lakini kama lipo la nyongeza basi linapaswa liwe la nyongeza maana lipo tofauti kidogo na swali la msingi lakini bado lipo katika misingi ya swali la msingi. Kwa hiyo, natumaini mwongozo huu utatusaidia. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Tuwe tunaangalia Mabunge ya wenzetu pia kipindi kama hiki cha maswali na majibu yaani ni swali jibu, ndiyo lengo la kipindi hiki. Kwa hiyo, baada ya mwongozo huo sasa tunaendelea na maswali, tunaanza na swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Igunga, karibu sana Mheshimiwa Ngassa. Na. 283 Hitaji la Gari la Wagonjwa - Hospitali ya Wilaya ya Igunga MHE. NICHOLAS G. NGASSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaipatia Hospitali ya Wilaya ya Igunga gari la kubebea wagonjwa kwa kuwa lililopo limechakaa sana? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Naibu Waziri wa TAMISEMI, hili ni moja ya majibu mafupi na mazuri, hongera Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicholas George Ngassa, Mbunge wa Igunga, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, gari la wagonjwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ni chakavu na halifai kuendelea kutumika. Kwa sasa Hospitali ya Halmashauri ya Igunga imepatiwa gari la Kituo cha Afya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kutoka katika Kituo cha Afya cha Choma ambalo linatoa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto za uchakavu wa magari ya kubebea wagonjwa katika Hospitali na Vituo vya Afya nchini. Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kununua magari ya kubebea wagonjwa na itatoa kipaumbele kwa Hospitali na Vituo vya Afya vyenye uhitaji mkubwa wa magari ya kubebea wagonjwa. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia bajeti ya mwaka 2021/2022 imeweka mpango mahsusi wa kununua magari ya kubebea wagonjwa ambayo yatapelekwa kwenye halmashauri… SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, hayo unayoyasema hayapo katika majibu yako ya msingi, ndiyo yale ambayo tunasema mnaongeza muda bila sababu. Lazima twende na jibu lilelile la msingi ambalo umeliweka mezani hapa. Swali la nyongeza Mheshimiwa Ngassa. MHE. NICHOLAS G. NGASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Sasa naomba kuuliza swali la nyongeza kwa Serikali, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Sera ya Afya ya Mwaka 2007, Sura ya 7 imeweka vigezo kwa Hospitali za Kata na Wilaya na moja ya kigezo ni lazima kuwe na gari la wagonjwa. Sasa Serikali imechukua gari la Kituo cha Afya cha Choma imepeleka Igunga na Kituo cha Afya cha Choma tena kimekosa gari. Je, Serikali haioni tunaendelea kukanyanga Sera ambayo tumejitungia sisi wenyewe? Ahsante. (Makofi) SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, magari yame-swap. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nicholas Ngassa, Mbunge wa Igunga, kama ifuatavyo:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, gari la Kituo cha Afya cha Choma limepelekwa katika Hospitali ya Halmashauri ili kuweza kuboresha zaidi huduma za Halmashauri kwa kuwa Hospitali ya Halmashauri ina wagonjwa wengi zaidi kuliko Kituo cha Afya. Hata hivyo, gari hilo linafanya kazi katika vituo vyote viwili kwa maana Kituo cha Afya na Hospitali ya Halmashauri. SPIKA: Ahsante tunaendelea na swali linalofuata la Mheshimiwa Charles Mguta Kajege, Mbunge wa Mwibara. Mheshimiwa Kajege tafadhali, Mheshimiwa Esther Bulaya kwa niaba yake. Na. 284 Kuzihamishia TANROADS Barabara za Mwibara MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kuipunguzia mzigo TARURA kwa kuzihamishia TANROADS barabara za Bulamba – Karukekere – Nakatubai – Igunchi – Mwitende na Busambara - Mugara zilizopo katika Jimbo la Mwibara? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa David Silinde, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Charles Mugeta Kajege, Mbunge wa Jimbo la Mwibara, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya kupandisha hadhi barabara kutoka barabara za Wilaya na kwenda barabara za Mikoa yanatakiwa kuwasilishwa na kujadiliwa kwenye Vikao vya Bodi ya Barabara ya Mkoa. Endapo Bodi 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) itaridhia mapendekezo hayo, yanatakiwa kuwasilishwa kwa Waziri mwenye Dhamana na barabara ambaye ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi. Mheshimiwa Spika, hatua inayofuata ni maombi hayo kupitiwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi chini ya Kamati ya Kitaifa ya Kupandisha Hadhi Barabara ili kuona kama yanakidhi vigezo
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages323 Page
-
File Size-