Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Nne – Tarehe 2 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mne Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) Pamoja na (Utawala Bora) kwa mwaka wa Fedha 2012/2013. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (UTAWALA BORA) (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, (UHUSIANO NA URATIBU): 1 Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. JOHN P. LWANJI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) Pamoja na (Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. ANDREW J. CHENGE - MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi, Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. KULIKOYELA K. KAHIGI - MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA) PAMOJA NA (UTAWALA BORA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani ya Ofisi ya Rais (Menejimentii ya Utumishi wa Umma) Pamoja na (Utawala Bora) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. 2 Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita Katibu ili atuongoza ratiba yetu ya leo, nasimama kwa mujibu wa Kanuni kuwapatia taarifa ifuatayo:- Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Spika wetu, Mama Anne Makinda, hatakuwa hapa Bungeni kwa siku kadhaa, amepata msiba, amefiwa na Bibi Zena Stephan Semamba. Huyu Bibi Zena Stephan Semamba alikuwa ndiye mtunzaji wa Marehemu Mama yake mzazi katika kipindi kile ambacho Marehemu Mama yake mzazi alipokuwa akiugua lakini katika kipindi chake cha uzee huyu Marehemu Zena Stephan Semamba ndiye alikuwa mtunzaji mkuu wa yule Marehemu Mama yake na Mheshimiwa Spika. Kwa hiyo, huyo mtunzaji naye Mwenyezi Mungu amemwita. Hivyo basi Mheshimiwa Spika, anawajibika kwa kweli kwenda kuhakikisha anamfanyia mazishi huyu Mama yetu Zena Stephan Semamba. Kwa hiyo, hatutakuwa naye hapa kwa siku zile ambazo atakuwa anashiriki kikamilifu kwenye msiba huo. Kwa hiyo, nimesimama kuwapa taarifa hiyo. Basi sisi tutaendelea na shughuli hizi mpaka hapo Mheshimiwa Spika atakaporudi ataungana nasi kuendelea na kazi zilizopo Bungeni. 3 MASWALI NA MAJIBU Na. 108 Gharama za Maonyesho ya Miaka 50 ya Uhuru MHE. SALIM HEMED KHAMIS (K.n.y. MHE. HAMAD RASHID MOHAMED) aliuliza:- Je, hadi sasa Serikali imetumia kiasi gani cha fedha kwa kila Wizara kwa ajili ya maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi wangu wa Jimbo la Siha ninaomba kutoa pole sana kwa Mheshimiwa Spika, kwa msiba huu ambao umetutangazia sasa hivi. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yalifanyika nchi nzima kwa kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 1 Juni, 2011 hadi tarehe 12 Desemba, 2011. 4 Serikali iliadhimisha Kumbukumbu hii muhimu ya taifa letu kwa faida ya Watanzania na hasa kukijengea uzalendo kizazi cha sasa ambacho hakikuwepo wakati tulipopata uhuru. Aidha, kupitia maadhimisho hayo ya kihistoria, nchi yetu imejitangaza nje ya nchi na kujiletea sifa kubwa na pia kuvutia wawekezaji na utalii. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kufanikisha maadhimisho hayo, Serikali ilipanga kutumia shilingi bilioni 30. Hata hivyo katika kubana matumizi Serikali imetumia shilingi bilioni 27.5 (27,540,218,803) ambazo ni matumizi ya Wizara, Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi mbalimbali. MHE. SALIM HEMED KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza mawili madogo ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na sherehe kubwa za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru ambazo zilifanyika nchi nzima Mikoa na Wilayani na ambazo zimegharimu mabilioni ya fedha. (a) Je, nini tathimini ya Serikali kuhusiana na jambo hilo? (b) Kwa kuwa kupanga ni kuchagua na kwa kuwa hivi sasa nchi yetu inakabiliwa na mambo muhimu ya kimsingi kwa mfano upungufu mkubwa wa madawati mashuleni, vitabu vya walimu na wanafunzi, nyumba za walimu, madaktari na wafanyakazi wengine wa Serikali, maabara na kadhalika. 5 Je, isingekuwa jambo la msingi kwamba Serikali ingefanya sherehe moja tu kubwa ya kitaifa ili kuokoa fedha ile ambayo ingetumika kujenga shule, kununua madawati, vitabu na kadhalika? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Salum Hemed Khamis, kama ifuatavyo:- Kwanza kuhusu tathimini sisi wote ni mashahidi Wabunge wote na Tanzania, vizazi hivi vipya vyote vimeona jinsi ambavyo tumeweza kuiweka nchi yetu katika historia yake. Nchi ambayo haina historia imekufa. Kwa hiyo, tulichofanya hapa wako watoto ambao wamezaliwa hawajui kipindi hiki cha uhuru kilikwenda kwendaje. Kwa hiyo, leo wanajua historia yetu. Wanajua tulianza na vyama vilivyoanza, vilivyopigania uhuru Tanzania Bara na Tanzania Visiwani wanajua. Wanajua mifumo mbalimbali, mabadiliko tuliyopata, siasa ya ujamaa na kujitegemea, misukosuko tuliyopita nayo katikati, kuhama hama katika mfumo wa Chama Kimoja kwenda kwenye vyama vingine na ninyi wote mliona Waheshimiwa Wabunge kwa sababu tulishiriki katika jambo haraka haraka ni kwamba kila mtu aliridhika kwamba walau tumeweza kuwafanya Watanzania na wale wengine walioko nje ya nchi kwamba nchi yetu imetimiza miaka yake 50 jambo ambalo kwa maoni yangu ni jambo la kujivunia sana 6 kwamba tumeweza kuonyesha historia yetu. Tumeweza kujua kwamba tumetoka wapi. Je, ni kiasi gani tumeweza kuelimisha watoto wetu, hospitali zilizojengwa, tumeweza kuonyesha barabara, tumeweza kuonyesha viwanda na mambo mengine ya kiuchumi mbalimbali ambayo yametokea katika nchi yetu. Kwa hiyo, kwenye hili hatuhitaji kumwita mtu kutoka nje atufanyie tathimini, mafanikio ni makubwa tulifanya nchi nzima na sisi wote tuliona jambo lile. (Makofi) Sasa linakuja jambo hapa kwamba hizi hela zinazozungumzwa hapa kwa nini msingezipeleka kwenye madawati, vitabu na kadhalika. Hili tukio la miaka 50 ya taifa si jambo dogo hata kidogo. Kwa maana ya kwamba haya yote ni mafanikio ambayo nimesema hapa yasingelikuwepo sasa kwa maana ya kwamba watu wasingejua, wanafunzi unawaona wamekaa pale juu wao hawajui kipindi hicho cha nyuma kilikuwaje, wamefahamu leo. Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed ambaye ameuliza swali hapa leo watoto hao wanajua Hamad Rashid Mohamed aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Leo watoto wa Tanzania wanajua kwamba amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, leo wanaweza kujua kwamba Makamu wa Rais wa Kwanza Zanzibar pale, leo wanajua alitoka wapi mpaka amefika hapo alipofika. Yako mambo mengi tu ambayo unaweza 7 ukayazungumza hapa ambayo tunatakiwa sisi Watanzania tufike mahali tujidai, tufike mahali tuseme kwamba tunajivunia taifa letu kwamba limeweza kufika katika hatua hii lilipo. Kwa hiyo, mimi nasema kusema kwamba tungepeleka katika elimu tunafanya hivyo, lakini jambo hili pia nalo ni muhimu sambamba na yale mambo ambayo nayazungumza hapa. Nashukuru sana. (Makofi) MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, wakati akisimama kwenye swali la nyongeza alisimama mtu mmoja tu mwuliza swali na nilishasema nimemwona mtu mmoja. Na. 109 Uhamisho wa Walimu wa Taaluma na Elimu Maalum MHE. MARTHA J. UMBULLA (K.n.y. MHE. AL– SHAYMAA JOHN KWEGYIR) aliuliza:- Serikali ilitoa agizo la kutowahamisha watumishi wote wakiwemo walimu wanaojiendeleza kitaaluma na wahitimu wa fani mbalimbali ikiwemo elimu maalum:- (a) Je, ni kwa nini walimu wa taaluma na elimu maalum hususan ya watu wenye ulemavu wamekuwa wakihamishwa bila kuzingatia agizo hilo? 8 (b) Je, uhamisho huo unazingatia vigezo gani hadi kushindikana kuwatambua walimu wa elimu maalum? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Al–Shaymaa John Kwegiyir, Mbunge Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b). (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inawatambua na kuwathamini sana wanafunzi wenye mahitaji maalum na wakati wote imekuwa inatoa kipaumbele cha kuhakikisha walimu wenye fani husika wanapatikana ili kuweza kuwapa fursa sawa ya kupata huduma ya elimu. Uhamisho wa watumishi katika mamlaka za Serikali za Mitaa hufanyika kwa kuzingatia mahitaji kiikama na maombi ya watumishi husika. Kutokana na uchache wa walimu wenye taaluma ya elimu maalum, Serikali imekuwa inahakikisha na kuelekeza kuwa wanapohamishwa au kupangwa wapelekwe katika maeneo yenye mahitaji. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi wanapoomba kuhama wana maelezo yanayotofautiana
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages271 Page
-
File Size-