Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nane – Tarehe 24, Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua SPIKA: Kabla ya kuendelea na shughuli nina matangazo machache tu ya utangulizi. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Mheshimiwa Shukuru Kawambwa, anao wageni ambao wametoka Jimboni kwake kuhudhuria Kikao cha leo cha Bunge wako kumi na nne (14). Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo naomba asimame pale alipo. Katibu wa Vijana, Katibu wa Wazazi, Katibu wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) na Madiwani wote wa Jimbo la Uchaguzi la Bagamoyo wakiongozwa na Mheshimiwa Almasi Masukuzi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, wale pale karibuni sana. Waheshimiwa, tunashukuru sana mmeona ni vema mje muungane nasi kushuhudia shughuli za Bunge letu. (Makofi) Kwa umuhimu huo huo naomba nimtambulishe Mama Kawambwa, mkewe Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na watoto wao watatu, nadhani ni wale pale. Karibuni sana Bungeni.(Makofi) HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo kwa Mwaka wa Fedha 2006/2007. MHE. JOYCE N. MACHIMU – (k.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO NA ARDHI): 1 Maoni ya Kamati ya Kilimo na Ardhi Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara Hiyo kwa Mwaka 2006/2007. SPIKA: Ahsante sana. Sasa ni Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu sekta ya kilimo na ardhi.(Makofi) MHE. MWADINI ABBAS JECHA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI: Maoni ya Kambi ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Waziri hiyo kwa Mwaka 2006/2007. MASWALI NA MAJIBU Na. 260 Vifaa Vya Kinga kwa Wazoa Taka MHE. MWAKA ABDULRAHAMAN RAMADHAN aliuliza:- Kwa kuwa kuna utaratibu wa Afya ya Wafanyakazi Occupational Health, Mfanyakazi anahitaji kujikinga na madhara ya kiafya anapofanya kazi Occupational Hazard anatakiwa avae vitendea kazi vya kinga:- (a) Je, kwanini wazoa takataka katika magari ya taka hasa wa Magomeni Mapipa wanazoa taka bila vitendea kazi vitakavyowalinda kama vile gloves na mask za pua? (b) Je, wafanyakazi hao huwa wanapimwa afya zao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa, Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwaka Abdulrahaman Ramadhan, Mbunge Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kuna utaratibu wa uwekaji Kinga ya Afya na ajali kwa wafanyakazi wanapokuwa kazini. Aidha, wafanyakazi wote kutegemea mazingira ya kazi wanazofanya wanatakiwa kutumia vifaa vya kinga ya afya na ajali. Kwa upande wa wafanyakazi wa wanaozoa taka wanatakiwa wavae vifaa vya kinga ya 2 mdomo (masks), mikono (gloves), sare (reflectors) kofia (headgear) pamoja na viatu imara (kama, gumboots) ili kujikinga na uwezekano wa kupatwa na magonjwa ama kupatwa na ajali yoyote wanapokuwa kazini. Mheshimiwa Spika, ni kweli pia kulikuwa na tatizo la wazoa taka kufanya kazi bila vifaa vya kinga katika magari ya taka ya Magomeni Mapipa na kwingineko katika Manispaa ya Kinondoni. Kwa hivi sasa kazi ya uzoaji taka katika maeneo mbalimbali ya Manispaa imetolewa kwa sekta binafsi. Kutokana na hatua hii tatizo la wafanyakazi kutotumia vifaa vya kinga kidogo limepungua. Hata hivyo ili kuhakikisha kuwa kuna mazingira salama ya wafanyakazi, hatua zifuatazo zimechukuliwa na Halmashauri husika:- (i) Manispaa kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imeanzisha programu ya uhamasishaji inayofanyika katika ngazi zote za Utawala ili kusisitiza matumizi ya vifaa vya kinga ya afya kwa wafanyakazi wanao zoa taka. (ii) Manispaa imeweka taratibu za ufuatiliaji wa karibu kuona kwamba makampuni ya kuzoa taka yanatekeleza suala la vifaa vya kinga kwa wafanyakazi wao. (iii) Manispaa imeendelea kuimarisha mfumo wake wa ukaguzi wa huduma za usafirishaji, msisitizo mkubwa ukiwa kwenye kufuatilia namna bora ya matumizi ya vifaa vya kinga ya afya na ajali kwa wazoa taka. Mheshimiwa Spika, kwa kweli vikundi na Makampuni yanayotoa huduma ya uzoaji taka yameboresha zaidi hali ya matumizi ya vifaa vya kinga kwa wafanyakazi ingawa bado hawajafikia kiwango cha juu cha matumizi hayo. Hata hivyo kuna baadhi ya wafanyakazi wa kuzoa taka wamekuwa wazembe kuvitumia vifaa hivyo na hivyo kuhatarisha afya zao. Aidha ni wazi kuwa matandao wa ufuatiliaji haujafanikiwa kufika katika maeneo yote ya Manispaa, hivyo tunawaomba wadau wote waonapo kasoro kama hizi waiarifu Mamlaka husika ili waajiri wa wazoa taka hao waweze kuchukuliwa hatua zinazostahili mara moja. (b) Mheshimiwa Spika, ni jukumu la kampuni husika kuhakiki kuwa wafanyakazi wao wana afya njema kwa kuwapa vifaa vya kinga ya afya zao na kuwawekea bima ya afya na pia kuwapima afya zao mara kwa mara. Hata hivyo imebainika kuwa wengi wa wazoa taka ni wafanyakazi wa muda yaani vibarua wa siku na hivyo hawapimwi afya zao. Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na sekta binafsi, wanaendelea kuboresha mazingira ya kazi ya uzoaji taka ili kuwavutia wafanyakazi wa ajira ya muda mrefu ambao pia watawekewa Bima na kupimwa afya zao mara kwa mara. MHE. DR. ZAINAB A. GAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa sio tu Dar es Salaam peke yake na maeneo mengi afya ya mfanyakazi na kuvaa vifaa vinavyomtakia ajikinge imeonekana si suala linalochukuliwa umuhimu wake. Unajikuta hata wanaofanya kazi ya vumbi wanapewa maziwa badala ya kuwekewa bima. 3 Je, kuna chombo au sheria inayofuatilia suala hili kuwa watu wasipofuatilia suala hili la Occupational Heath wachukuliwe hatua? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Usalama yaani Occupational Health and Safety ya mwaka 2004 kifungu namba 24.(2) kinasisitiza juu ya umuhimu wa kuvaa vifaa salama ili kujikinga na maradhi. Pia katika kila Halmashauri kuna Sheria ndogo ndogo ambazo pia zinahusu usafi na mazingira. Vilevile Serikali katika Manispaa au Halmashauri mbalimbali kuna wakaguzi wa afya wanapita sehemu mbalimbali ili kuhakikisha kwamba wafanyakazi au hao wazoa taka wanavaa vifaa vya kinga kama vile nilivyovitaja hapo juu, gloves, Helmet na pia gumboots na makoti ili kujikinga na afya zao. Lakini ninachosisitiza ni kwamba naomba wadau mbalimbali tushirikiane kuhakikisha kwamba hao wafanyakazi wanavaa vifaa hivyo, wengi hawapendi kutumia vifaa hivyo. Kwa hiyo, naomba wadau mbalimbali tushirikiane, sheria zipo na Serikali inasisitiza ili kuhakikisha kwamba hao wafanyakazi wanakuwa salama. Na.261 Kilimo cha Umwagiliaji – Bonde la Mto Bubu. MHE. PASCHAL C. DEGERA aliuliza:- Kwa kuwa utafiti uliofanywa mara nyingi umeonyesha kuwa Bonde la Mto Bubu linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji Je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati muafaka wa kutekeleza mradi huo ili kuwapunguzia wananchi wa Mkoa wa Dodoma umaskini iliokithiri? NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA (MHE. HEZEKIAH N. CHIBULUNJE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Paschal Degera, Mbunge wa Kondoa Kusini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua tafiti mbalimbali zilizokwishafanywa katika Bonde la Mto Bubu kuanzia Kondoa hadi Bahi. Mheshimiwa Spika, kaitka miaka ya 1970 baada ya Serikali kuanzisha Mipango wa Maendeleo ya Uwiano ya Mikoa (RIDEPS), na baada ya mji wa Dodoma kutangazwa rasmi kuwa Makao Makuu ya Serikali, tafiti zilianza upya katika Bonde la Mto Bubu kwa kutumia wataalam Wazalendo wa iliyojulikana Water Development and Irrigation Division (WD&ID). 4 Aidha kati ya mwaka 1974 na 1977 wakati wa Serikali inaandaa Dodoma Region Water Master Plan, iliyokuwa Wizara ya Maji, Madini na Nishati ilifanya uchunguzi mwingine katika Bonde la Mto wa Bubu kwa lengo la kupata maji ambayo yangekidhi mahitaji ya maji wa Dodoma na Vijijini vinavyouzunguka mji. Mheshimiwa Spika, kilele cha tafiti za Mto Bubu zilihitimishwa na kampuni ya Ujerumani inayoitwa Agrar-Und Hudrotechnic (GMBH) ambayo mwaka 1984 iliandaa usanifu na makisio ya ujenzi wa mabwawa ya Farkwa na Upendo kwa ajili ya kumwagilia mashamba yenye ukubwa wa hekta 10,000. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa 1984 gharama za mradi mzima zilikadiriwa kuwa USD milioni 75 na shilingi bilioni 3.011 za Tanzania. Kwa wakati huo Serikali haikuwa na uwezo wa kutekeleza mradi huu kutokana na gharama yake kubwa sana kwa kuzingatia vipaumbele vingine vya maendeleo vilivyokuwepo wakati huo. Muda mrefu umepita, baadhi ya malengo, mikakati na gharama za utekelezaji vimebadilika; vitahitajika kuchunguzwa na kuboreshwa upya ili vizingatie mikakati mingine mipya kama vile MKUKUTA, athari kwa mazingira, nishati mbadala na kadhalika. Mheshimiwa Spika , Bonde la Mto Bubu limetambuliwa na kuainishwa na Wizara katika Mpango Kamambe wa Kilimo cha Umwagiliaji Maji. (National Irrigation Master Plan (NIMP) uliokamilika mwaka 2003. Miradi iliyoainishwa chini ya NIMP inaanza kutekelezwa katika programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) ambayo katika utekelezaji wake kwa kipindi cha miaka saba unaanza mwaka huu, 2006/2007. Katika programu hii sekta ndogo ya umwagiliaji itatumia takribani shilingi trilioni 1.4 na mradi ya umwagiliaji itakayoibuliwa katika Bonde la Mto Bubu itaendelezwa chini ya Programu hii. Wazira itaendelea kushirikiana na Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kuchambua miradi ya umwagiliaji
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages163 Page
-
File Size-