MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Arobaini – Tarehe 31 Mei, 2019

MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Arobaini – Tarehe 31 Mei, 2019

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Arobaini – Tarehe 31 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendele na Mkutano wetu wa Kumi na Tano, na leo ni Kikao cha Arobaini. Katibu. NDG. BAKARI KISHOMA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. KEMILEMBE J. LWOTA – MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati hukusu Makadrio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. WILFRED M. LWAKATARE - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kuhusu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. SPIKA: Katibu. NDG. RAMADHAN ABDALLAH ISSA – KATIBU MEZANI: Maswali. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali; swali la kwanza linaanza na Mheshimiwa Esther Michael Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum. Kwa niaba yake, Mheshimiwa Mariam Ditopile. Na. 330 Mkakati wa Kulinda Ajira Zisizo Rasmi kwa Vijana MHE. MARIAM D. MZUZURI (k.n.y. MHE. ESTHER M. MMASI) aliuliza:- Kutokana na kutimizwa kwa masharti na matakwa ya Kisheria ya kutangaza Mkoa wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi ni dhahiri imevutia wadau wengi wa uwekezaji katika nyanja mbalimbali za kiuchumi:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kulinda ajira zisizo rasmi kwa vijana wahitimu Tanzania hasa wa Mkoa wa Dodoma? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Anthony Mavunde, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY PETER MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Michael Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kutangazwa kwa Mkoa wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi, kumevutia uwekezaji katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na za kijamii na hivyo kusababisha ongezeko la ajira rasmi na zisizo rasmi. Katika kulinda ajira za vijana wanaojishughulisha katika sekta isiyo rasmi, ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Serikali inatekeleza mikakati ifuatayo:- Kwanza, ni kuhamasisha vijana wakiwemo wahitimu kuunda makampuni katika Mkoa wa Dodoma, ambapo jumla ya makampuni 12 ya vijana yameundwa. Pili, kuwezesha vijana kupata mikopo yenye masharti nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Vijana pamoja na mapato ya ndani ya Halamshauri, ambapo katika Mkoa wa Dodoma vijana kupitia vikundi na makampuni 978, wamewezeshwa mitaji yenye thamani ya jumla ya shilingi 2,557,090,486/= kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya kuanzisha au kuendeleza biashara zao. Tatu, kurasimisha ajira za vijana wanaojishughulisha katika sekta isiyo rasmi kwa kuwatambua na kuwapatia vitambulisho vya mjasiriamali ili kuwawezesha kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa. Nne, kutoa mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali kwa jumla ya vijana 1,240 wa Mkoa wa Dodoma, kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa katika 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) shughuli za ujenzi na biashara hapa Dodoma kupitia programu mbalimbali. Tano, kurasimisha ujuzi uliopoatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo katika kada za ufundi mbalimbali kwa vijana 245 wa Mkoa wa Dodoma ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa au kuendelea na mafunzo ya ngazi za juu. Sita, kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (greenhouse) kwa vijana 18,800 nchi nzima, ambapo vijana 800 wanatoka Halmashauri nane za Mkoa wa Dodoma. SPIKA: Mheshimiwa Mariam ameridhika. Uliza swali lako Mheshimiwa Mariam Ditopile. MHE. MARIAM D. MZUZURI: Mheshimiwa Spika, napenda kwanza kumpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo yana tija kwa vijana wa Mkoa wa Dodoma; na kwa vile yeye mwenyewe ni mtu sahihi, ni Waziri kijana, ni kijana na ni Mbunge anayetokana na Mkoa wa Dodoma, nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, moja ya mazao ya biashara yaliyoonyesha kuwa na tija kwenye kilimo biashara Mkoa wa Dodoma ni pamoja na zao la zabibu, lakini mara baada ya Dodoma kutangazwa kuwa Makao Makuu ya Nchi, wageni wengi hususan kutoka katika nchi jirani za Afrika Mashariki, wameonekana kuvutiwa na uwekezaji kwenye zao la zabibu kama zao la biashara. Je, Serikali haioni umuhimu wa kutenga ardhi na pembejeo kwa vijana wa Mkoa wa Dodoma ili wawezeshiriki rasmi kwenye Sekta ya Kilimo cha Biashara kwenye zao la zabibu? (Makofi) Swali la pili. Kwa kuwa kuna vijana tayari wamejiajiri kwenye ujasiriamali wa mazao, hususan katika zao la biashara la ufuta, lakini hivi karibuni kumetokea sintofahamu kwa Mkoa wa Dodoma hasa kwenye Wilaya ya Kondoa kuwazuia vijana hawa wasinunue ufuta kutoka kwa 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wakulima kwa kisingizio cha kuwa na stakabadhi ghalani, jambo ambalo halipo katika Mkoa wa Dodoma:- Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu vijana hawa ambao wameamua kujiajiri? Mheshimiwa Spika, nashukuru. (Makofi) SPIKA: Majibu ya maswali hayo mawili, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Anthony Mavunde, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY PETER MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, naomba uniruhusu kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge Mariam Ditopile kwa namna ambavyo anawasimamia vijana wa nchi yetu ya Tanzania na hususan Vijana wa Mkoa wa Dodoma. Mwenyezi Mungu akubariki sana. Mheshimiwa Spika, ni kweli, baada ya tangazo la Makao Makuu na pia baada ya Serikali ya Awamu ya Tano sikivu kufanya marekebisho katika ule mchuzi wa zabibu ili kuwavutia zaidi wakulima wa zabibu kuendelea kuilima zabibu, mwamko umekuwa mkubwa kwa vijana na kama Serikali mkakati wake katika eneo hili ni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, la kwanza, yalitoka maelekezo mwaka 2014 kutoka kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, ya kila Halmashauri nchi nzima kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za vijana kufanya kilimo. Kwa Mkoa wa Dodoma na hasa katika maeneo ambayo yanalima zabibu, tayari maelekezo yalishatoka na katika master plan ya Jiji la Dodoma, ambayo itakwenda kukamilika hivi karibuni, yametengwa maeneo maalumu ya kuhakikisha kwamba zao hili la zabibu halipotei. Mheshimiwa Spika, hivyo, vijana pia watapata fursa ya kuweza kunufaika kupitia maeneo hayo ili nao waweze 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kulima zabibu na kujiongezea fursa ya kuendeleza mitaji yao na biashara zao. Mheshimiwa Spika, kubwa zaidi kuliko yote ni kwamba, Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maeneo yake ambayo wametenga kwa ajili ya shughuli za vijana, wameshapeleka wataalam kwenda SUA kukaa na wataalam wa SUA kwa ajili ya kuja na mpango mzuri endelevu wa kilimo cha zabibu ambacho kitakuwa kimefanyiwa utafiti ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika. Mheshimiwa Spika, siyo zabibu tu, kwa Dodoma hapa, vijana wengi hivi sasa wanafanya biashara za mazao, kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema; na hivi sasa tayari tunavyo viwanda ambavyo vimeanza kufanya kazi. Kwa mfano, Kiwanda cha Mazao Mchanganyiko ambacho kwa mwaka kitahitaji tani 12,000 za mahindi na tani 6,000 za alizeti. Kwa hiyo, tunachukua fursa hii pia kuwaalika vijana kushiriki katika kilimo hicho. Mheshimiwa Spika, swali la pili la Mheshimiwa Mbunge, analijibu Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo ambaye ameandaliwa kwa ajili ya kulijibu swali hilo. Mheshimiwa Spika, nakushukuru. SPIKA: Kwa kifupi, Mheshimiwa Waziri wa Kilimo mwenyewe, kwa kifupi tafadhali. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda nichukue nafasi hii kumpongeza Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo ameyatoa. Ni kweli kabisa kumetokea sintofahamu katika zao la ufuta katika maeneo mengi hapa nchini na hasa katika mikoa ambayo inazalisha kwa kiwango kikubwa sana. Utaratibu ambao tumeweka kama Serikali, ni kwamba tunatumia ule utaratibu wa mwaka 2018 wa kuhakikisha, mtu yeyote anayetaka kununua ufuta, anaruhusiwa kwenda kununua maadam afuate taratibu zinazostahili; na wote wanaruhusiwa na hatujaweka masharti yoyote. (Makofi) 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, sasa hivi kumetokea katika baadhi ya mikoa, wanasema kwamba tunatumia mfumo wa soko la bidhaa yaani TMX na kuna maeneo mengine wanalazimisha kwamba wanaoruhusiwa ni hawa, hatujaweka huo utaratibu. Kila mtu anaruhusiwa kwenda kushiriki na huo utaratibu wa soko la bidhaa utakapokamilika, tutatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kuanza kutumia huo mfumo. Kwa mwaka huu kwa sababu mfumo hatujaukamilisha sawasawa, basi mfumo wa zamani unaendelea kutumika. Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Mtaona swali hili moja limechukua dakika 10 Waheshimiwa Wabunge. Tuendelee na Ofisi ya Mheshimiwa Rais TAMISEMI, swali la Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Maswa Magharibi, kwa niaba yake nimekuona Mheshimiwa Leah Komanya. Na. 331 Walimu wa Kike katika Shule za Msingi na Sekondari MHE. LEAH J. KOMANYA (k.n.y. MHE. MASHIMBA M. NDAKI) aliuliza:-

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    312 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us