Majadiliano Ya Bunge ______

Majadiliano Ya Bunge ______

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Ishirini na Saba - Tarehe 9 Julai, 2010 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anna S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZlLIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha, 2010/2011. MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO - MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya ya Nishati na Madini Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MHE.SAVELINA S. MWIJAGE (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMATI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA NISHATI NA MADINI): Taarifa ya Msemaji wa Mkuu wa Kambi ya Upinzani Kuhusu Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU BAKARI MAHIZA): 1 Randama za Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. OMAR YUSSUF MZEE): Taarifa ya Majumuisho ya Mpango Mkakati wa Kujibu Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Wizara, Idara za Serikali na Mikoa kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009. MASWALI NA MAJIBU Na. 191 Kuhusu Barabara ya Makutupa Bumila Jimbo la Mpwapwa MHE. GEOREGE M. LUBELEJE aliuliza:- Kwa kuwa barabara ya kutoka Kijiji cha Makutupa hadi Kijiji cha Bumila inahitaji matengenezo makubwa ili kuweza kupitika wakati wote na kwa kuwa lipo korongo kubwa kariBu na shule ya msingi Bumila ambalo hufamya wananchi pamoja na wananfunzi kushindwa kwenda shule kutokana na maji kujaa wakati wa mvua. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha barabara hiyo inatengenezwa na kujenga daraja katika korongo hili kuondoa adha kwa wananchi wa Bumila? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa George Malima Lubeleje, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Makutupa-Bumila ina urefu wa kilomita 4, aidha korongo hilo linalotenganisha sehemu kubwa ya Kijiji na shule ya msingi Bumila lina kina cha mita 7 na upana wa mita 10. Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Kijiji hiki kinahitaki barabara ili kurahisisha mawasiliano pamoja na huduma nyingine za kijamii, kisiasa na kiuchumi. Pia ni kweli kwamba korongo hilo ni hatari sana kwa wananfunzi na wananchi wa Bumila. Serikali ya awamu ya nne inatambua umuhimu wa barabara za Vijijini kama kiungo muhimu cha uchumi kwa wananchi, ikiwemo barabara ya Makutupa- Bumila. 2 Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua hilo, Serikali imeendelea kuzifanyia matengenezo barabara za Wialya na za Vijijini kwa kutumia fedha za Mfuko a Barabara (Road Fund). Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa katika Bajeti yake ya mwaka wa fedha 2010/2011 imetenga kiasi cha shilingi milioni 14 ili kuifanya matengenezo barabara. Pia, na pia Halmashauri iteaendelea kutafuta fedha ili kuweza kujenga daraja ambalo linaunganisha Kijiji na shule ambayo ni taasisi muhimu kwa maendeleo ya Kijiji cha Bumila na Taifa kwa ujumla na kuepusha usumbufu kwa wananchi wa eneo hilo. MHE. GEOREGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali ya nyongeza. Kwanza niishukuru sana Serikali kwa kutenga milioni 14 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii ya Makutupa hadi Bumila na daraja na pia niishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka Mima, Mkanana mpaka Chibwegele. Sasa kwa kuwa fedha hizi ambazo zimetengwa hazitoshi. Je, sasa Mheshimiwa Naibu Waziri utakubaliana na mimi kwamba katika Bajeti ijayo tuongeze fedha ili tuweze kutengeneza barabara hizi kwa kiwango cha lami sehemu hiyo ya Mima na Buchibwegele ili kuboresha mawasiliano katika maeneo hayo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba nipokee hizo shukurani ambazo amezitoa na ningemshangaa sana Mheshimiwa Lubeleje kama asingemshukuru Waziri Mkuu kwa sababu Waziri Mkuu ameshakwenda kule kwake mara tatu mfululizo na hivi tunavyozungumza hapa juzi tumetoa tena hela nyingine. Lile daraja la Godegode tumepeleka shilingi milioni 500 na sasa tumemwongezea tena shilingi milioni 225, hii barabara nyingine anayoizungumzia hapa tumepeleka shilingi milioni 30 zimepelekwa pale. Unaweza kuona jinsi ambavyo tumefanya. Lakini nataka nitambue jitihada za Mbunge huyu. Ni mtu mfuatiliaji sijapata kuona. Kila mahali anakubana kona hii na kona hii. Kwa hiyo, nataka nimthibitishie pia hata kwenye Bajeti ijayo atuombee kwa Mwenyezi Mungu kama mambo yataenda vizuri sisi tutakuwa hatuna tatizo kwenye jambo hilo tutafanya hivyo kama anavyoishauri Serikali. (Makofi) Na. 192 Serikali Kusaidia Ujenzi wa Zahanati MHE. WILLIAM H. SHELUKINDO (K.n.y. MHE. BALOZI ABDI H. MSHANGAMA) aliuliza:- 3 Je, Serikali ina utaratibu gani wa kusaidia ujenzi wa zahanati za Vijiji zinazojengwa kwa nguvu za wananchi zikiwemo zahanati za Vijiji vya Miegeo, Ngulwi, Kwemashai, Mazumbai, Mavului, Ungo Mbelei, Mdando, Bombo na Irente Wilayani Lushoto? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Balozi Abdi Hassani Mshagana, Mbunge wa Lushoto, napenda kutoa maelezo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto kwa sasa ina Kata 32, Vijiji 217 na Vitongoji 1,672 ambapo ina hospitali 2, vituo vya afya 7 na zahanati 40. Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza agizo la Serikali la kuwa na zahanati katika kila Kijiji,Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imekuwa ikizingatia Sera hii katika bajeti yake ya kila mwaka. Katiba bajeti ya mwaka 2007/2008 kupitia fedha za ruzuku ya maendeleo,Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ilitenga jumla ya shilingi milioni 247.5 kujenga wodi 1 ya wagonjwa na jengo la huduma ya Mama na Watoto (MCH), zahanati mpya 12, na nyumba 5 za waganga. Pia kwa mwaka wa fedha 2008/2009 Halmashauri ilitenga jumla ya shilingi milioni 108.0 kwa ajili ya kujenga majengo ya OPD kwenye zahanati mpya 3, kukarabati zahanati,kujenga nyumba 2 za waganga na kumalizia nyumba za watumishi. Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo haya naomba kujibu swali la Mheshimiwa Balozi Abdi Hassani Mshagana, Mbunge wa Lushoto napenda kutoa maelezo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2009/2010 Halmashauri ya Wialaya ya Lushoto ilitenga jumla ya shilingi milioni 220.8 ili kumalizia ujenzi waa majengo ya OPD kwenye zahanati mpya 12. Aidha, , Halmashauri kupitia vyanzo vyake imetenga fungu la kumalizia zahanati mpya ikiwemo zahanati ya Irente ambayo imeuliziwa swali. Pia kwa zahanati za Mazumbai na Mbelei zitanufaika kwa fedha za awamu ya kwanza za Mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo zilizokuja kwa Jimbo la Lushoto. Kwa mwaka wa fedha 2010/2011 Halmashauri imetenga jumla ya shilingi milioni 207.0 kwa ajili ya kujenga zahanati mpya 4 ikiwemo zahanati ya Miego,kupanua zahanati 1 kuwa kituo cha Afya,Maabara, vyumba vya kupumzikia wagonjwa na nyumba 5 za watumishi. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali bado inatambua hitaji kubwa la ujenzi wa majengo ya kutolea huduma za afya hivyo inajitahidi kushirikiana na wananchi katika kuendeleza na kuboresha huduma za afya. Kwa kutumia vyanzo mbalimbali awamu kwa 4 awamu Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto itakamilisha zahanati zinazojengwa kwa nguvu za wananchi, hasa baada ta kupata mwamko kwa kuelimisha na kuhamasisha. MHE. WILLIAM H. SHELUKINDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba, kwa kuwa sasa Serikali inajua kwamba katika Jimbo la Lushoto kuna zahanati hizo 10 amabzo zinajengwa , vile vile katika Jimbo la Bumbuli kuna zahanati ya Msamaka, Mahezangulu, Kiviricha, Kwesine na Kisiwani ambazo zinajengwa. Je, Serikali imejiandaaje kuhusu hasa wafanyakazi wa zahanati hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, tumemsikiliza Waziri wa Afya akizungumza hapa na sisi wenyewe TAMISEMI tumekuwa tunazungumza hapa. Moja ya mambo ambayo tumeyafanya sasa hivi ni kuruhusu kwamba hao wanafunzi wanaomaliza katika Vyuo vyetu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya waende moja kwa moja wapelekwe katika Halmashauri zinazohusika. Kwa hiyo, anasema jambo la maana kabisa kweli zahanati zitaongezeka pale nakubaliana na Mheshimiwa Shellukindo kwamba kuna haja ya kushirikiana ili kuhakikisha kwamba hivi vitu vinapata wataalamu wa aina mbalimbali ambao watasaidia. Liko katika mpango na tunakubaliana na mawazo yake. Kwa hiyo, linatunzwa hilo wala asiwe na wasiwasi kuhusu watumishi. MHE. ZAYNAB M. VULU: Mheshimiwa Naibu Spika, asante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa swali la msingi linazungumzia masuala ya majengo na kwa kuwa katika kuboresha huduma za afya, mbali kuwa na majengo, lazima uwe na wahudumu,uwe na vifaa, uwe na Madakitari Bingwa. Je, Serikali inaisaidiaje zahanati iliyokuwepo Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa kuongezewa huduma muhimu kama za Madakitari Bingwa, vifaa vya maabara na vifaa vya wodi ya wazazi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU,

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    224 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us