Bunge La Tanzania ______

Bunge La Tanzania ______

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Tisa – Tarehe 25 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. MUSTAFA HAIDI MKULO): Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mwaka 2004/2005 [The Annual Report and Accounts of Tanzania Revenue Authority for the year 2004/2005] NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI (MHE. BERNARD KAMILLIUS MEMBE: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2006/2007. MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA: (MHE. WILLIAM J. KUSILA): Maoni ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI: (MHE. MUHONGA S. RUHWANYA): Maoni ya Kambi ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge kabla ya maswali, kwa kuwa leo ni hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, naomba kwa kweli kwa heshima tutatumbue wageni wa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, 1 Mheshimiwa Kapten Chiligati, lakini wageni hao wamekuja pia kwa niaba ya Mheshimiwa John Lwanji, hao wote ni Wabunge wanaotoka kwenye Halmashauri moja. Kwa hiyo, Madiwani hao ni wageni wa Wabunge hao wote wawili. Wageni hao ni Madiwani 15, nafikiri wako hapa ndani na wanaongozwa na Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Ndugu Mheshimwa Diwani Moses Matonya. Vilevile naomba tutambue wageni wa Wizara hiyo ambao ni Askari wa Jeshi la Magereza 50, nafikiri nao wako humu ndani, ama watakuwepo pamoja nasi baadaye, kama wapo naomba wasimame. Ahsante sana, lakini wameambatana na maafisa uhamiaji 15. Lakini naomba pia nimtambue mke wa Mheshimiwa Chiligati, Mwalimu Glena Chiligati, ahsante sana. (Makofi) Na. 270 Posho ya Walimu MHE. OMAR S. KWAANGW’ aliuliza:- Kwa kuwa, wapo Walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu kutokana na jiografia ya nchi yetu; na kwa kuwa, walimu wanafanya kazi kwa muda mrefu na nyakati zingine hufanya kazi kwa kujitolea:- Je, Serikali ina mpango wa kuwapa walimu posho mbalimbali ya kufanya kazi kwenye mazingira magumu, kufundisha kwa muda wa ziada, kufundisha kwa awamu mbili, ili kufanya kazi yao kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Omar Kwaangw’, Mbunge wa Babati Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba Walimu ndilo kundi kubwa la Watumishi wa Umma lililosambaa na kufanya kazi katika kila kona ya Nchi na baadhi yao katika mazingira magumu kutokana na jiografia ya Nchi na Miundombinu iliyopo. Aidha, walimu pia wamekuwa wakijitolea kufundisha kwa muda wa ziada na katika baadhi ya shule kufundisha kwa awamu mbili double shift. Ni kwa kuzingatia umuhimu wa taaluma ya kazi hiyo, Serikali katika kipindi cha nyuma iliongeza posho ya ufundishaji katika mishahara ya walimu wote Nchini ili iwe motisha kwa kazi ngumu wanayoifanya. Katika mabadiliko ya mishahara yaliyofanywa baadaye na Serikali, posho ya ufundishaji kwa walimu na posho nyingine za Watumishi ziliunganishwa katika mishahara yao. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo Serikali inatambua umuhimu wa kuboresha mishahara ya walimu na Watumishi wengine pamoja na kutoa motisha ya posho 2 mbalimbali. Ni imani yangu kwamba maboresho ya maslahi ya walimu na watumishi wengine yatazingatiwa katika Tume ya Rais ya kuboresha mishahara iliyoundwa mwezi Mei, mwaka 2006. Hivyo, namshauri Mbunge na watumishi wote wakiwemo walimu kuwa na subira wakati Kamati inatekeleza jukumu walilokabidhiwa MHE. OMAR S. KWAANGW’: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa watumishi wengine wanalipwa masaa ya ziada wakati wanafanya kazi ya ziada. Je, ni kwanini jambo hilo haliwezekani kwa walimu, ambao wanafundisha double session kwenye maeneo mbalimbli? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kutambua hilo ndio maana sasa hivi liko katika mchakato wa kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyakazi wote, na sio walimu peke yao. Natambua wazi kwamba wafanyakazi wengine wanalipwa extra duty allowance, na sio overtime kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, lakini kwa walimu mpaka sasa hivi hawajalipwa hiyo extra duty allowance, kwa kutambua hilo ndio maana Serikali sasa hivi inafanya kila jitihada na imeunda kikundi kuangalia posho ya walimu na watumishi wengine ambao wako katika mazingira magumu. MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ningeomba kuuliza swali moja la nyongeza. Amesema kwamba walimu wasubiri ripoti ya Tume iliyoundwa na Mheshimia Rais inayoongozwa na Mheshimiwa Ntukamazima ya kuboresha maslahi ya walimu na wafanyakazi wengine nchini. Mtakumbuka kwamba hapo nyuma, majibu ya Serikali yalikuwa ni kwamba walimu wasubiri matokeo ya Tume ya Omar Kwaangw’ ambayo na wewe Mheshimiwa Mwenyekiti ulikuwa mjumbe wa Tume hiyo, na ripoti tayari, sasa swali langu ni kwamba walimu watasubiri matokeo ya Tume hadi lini? Wakati tume nyingine ya Omar Kwangw’ ripoti yake iko mezani? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu kabisa kulikuwa na Tume ambayo iliongozwa na Mheshimiwa Omar Kwaangw, lakini Tume hiyo ilikuwa inaangalia zaidi malimbikizo ya misharaha. Sasa Serikali imeshaiangalia hiyo taarifa na malimbikizo ya mishahara kama mlivyoona kwa miaka kadhaa, imelipwa kwa walimu na mingine bado inalipwa. Kuhusu shombo mbalimbali ilikuwa haikuzingatiwa zaidi, zaidi zaidi ilikuwa inaangaliwa zaidi malimbikizo ya mishahara ambayo yalikuwa yamekaa kwa muda mrefu. (Makofi) Na. 271 3 Mpango wa Kuboresha Barabara Jijini Dar es Salaam MHE. CHARLES N. KEENJA aliuliza:- Kwa kuwa, kumekuwepo mipango ya kuboresha mtandao wa barabara jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu sasa; na kwa kuwa, mipango hiyo haijatekelezwa:- (a) Je, mpango wa kujenga ring road utaanza lini, na barabara hiyo itapita wapi? (b) Je, Serikali ina mpango kuhusu ujenzi wa barabara za lami kutoka Wazo Hill – Mbezi Luisi na Mbezi Beach – Mbezi Luis kupitia Goba? (c) Kama hakuna mpango wa kujenga barabara hizo siku za karibuni, Je, Serikali haioni kuwa ni vyema kupima barabara hizo mapema kabla wananchi hawajajenga kwenye maeneo zitakapopita barabara hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA): alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Charles N. Keenja, Mbunge wa Ubungo, lenye sehemu (a), (b) na ( c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba kumekuwepo na mipango ya kuboresha mtandao wa barabara Jijini Dar es Salaam ambalo linaendelea kukua kwa kasi kubwa kiasi cha kusababisha sekta ya Miundombinu kama barabara kushindwa kukidhi mahitaji ya watumiaji. Serikali kwa kulitambua tatizo hili ilianzisha mikakati mbalimbali itakayopelekea kuboresha mtandao wa barabara katika Jiji la Dar es Salaam. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mikakati hiyo kipindi cha mwaka wa fedha 2006/2007 Serikali itakarabati na kuimarisha barabara mbadala zikiwemo pia barabara za pembezoni mwa Jiji zinazounganisha barabara Kuu (Ring road). Barabara zitakazoimarishwa katika mkakati huu ni pamoja na barabara ya Mbezi Goba – Tangi Bovu, Mbezi Kifulu – Kinyerezi Banana, Jet Conner – Vituka – Mtongani (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2006/2007 Serikali itafanya upembuzi yakinifu pamoja na usanifu katika barabara ya Tangi Bovu (Mbezi Beach) – Goba – Mbezi Luis – Kifulu – Kinyerezi – Majumba sita, yenye urefu wa kilomita 34 itayounganisha barabara kuu za Bagamoyo eneo la kati ya Tangi Bovu na Bunju, Morogoro eneo la Mbezi na Nyerere eneo la Banana ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami. Gharama ya itakayotumika ni shilingi milioni 160. (c) Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuhakikisha kwamba wnanchi hawajengi katika maeneo zitakapopita barabara hizo Serikali hivi sasa inakamilisha mpango wa kumiliki kisheria hifadhi ya barabara zote zitakazoingia kwenye mpango huu ili ziweze kupimwa. 4 Kwa kuwa maeneo hayo yatawekwa alama haitakuwa rahisi wananchi kujenga katika maeneo husika kwa sababu wataelimishwa. Na. 272 Kituo cha Kulelea Watoto Yatima Msimbazi - Dar es Salaam MHE. MOHAMED ALI SAID aliuliza:- Kwa kuwa, kituo cha kulelea watoto yatima na waliotekelezwa na wazazi wao kilichoko Msimbazi – Dar es Slaam kina uwezo wa kuchukua watoto 45 tu; na kwa kuwa idadi hiyo ni ndogo sana ikilinganishwa na idadi kubwa ya watoto wa aina hiyo; na kwa kuwa, Serikali haikupanga kasma yoyote kuhusu kituo hicho: (a) Je, isingekuwa vyema sasa Serikali ikakitengea fedha ili kukiboresha kituo hicho ili kiweze kuchukua watoto wengi zaidi kuliko ilivyo sasa? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza vituo vingine Dar es Salaam na katika Mikoa yote ya Tanzania ili kukidhi haja hiyo. WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:-

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    165 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us