NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Nne - Tarehe 6 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe.Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu. NDG.YONA KIRUMBI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Maswali, Waheshimiwa karibuni kwenye Mkutano wetu, kikao chetu cha nne na swali letu la kwanza linaelekezwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI na linaulizwa na Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda. Na. 24 Ujenzi wa Vituo Vya Afya Ikuti na Ipinda MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:- Je, ni lini ujenzi unaoendelea katika Vituo vya Afya Ikuti, Wilayani Rungwe na Ipinda Wilayani Kyela utakamilika ili kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kupata huduma kwa wakati? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Ikuti kimekarabatiwa katika awamu ya kwanza ya ukarabati wa vituo vya afya 44 ulioanza tarehe 10 Oktoba, 2017 na kukamilika tarehe 31 Januari, 2018 kwa gharama ya shilingi milioni 500 ili kuongeza huduma za upasuaji wa dharura kwa mama wajawazito. Aidha, shilingi milioni 220 zimetolewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba vya upasuaji na samani. Kituo hicho kinaendelea kutoa huduma zote za matibabu isipokuwa huduma za upasuaji wa dharura. Ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya Ikuti umekamilika na kinachosubiriwa kwa sasa ni vifaatiba kutoka Bohari ya Dawa (MSD). Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa kituo cha afya cha Ipinda ulianza Oktoba, 2017 katika ujenzi huu jumla ya majengo mapya nane yamejengwa pamoja na ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje, uwekaji wa miundombinu ya maji safi na majitaka, kichomea taka na ujenzi wa njia zinazounganisha majengo (walk way). Jumla ya shilingi 625,899,806 zimetumika mpaka sasa katika mchanganuo ufuatao; Serikali Kuu shilingi 500,000,000, Halmashauri pamoja na wadau shilingi 90,100,975.40 na wananchi 35,798,830.60. Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majengo hayo, Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imepokea vifaatiba kutoka MSD vyenye thamani ya jumla ya shilingi 73,909,900 na vilivyosalia vinatarajiwa kupatikana mnamo mwezi huu wa nne. Vilevile Halmashauri imenunua vitanda 47, magodoro na mashuka vyenye thamani ya shilingi 27,066,500 ambavyo vimefungwa na vinatumika katika majengo hayo. Kituo cha Afya Ipinda kinaendelea na ujenzi wa miundombinu kwa gharama ya shilingi milioni 500 ambao unahusisha kupanua huduma za upasuaji wa dharura na shilingi milioni 220 zimetolewa kwa ajili ya vifaatiba vya upasuaji na samani. (Makofi) 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwakagenda. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na jibu la msingi la Mheshimiwa Waziri bado kuna shida katika ujenzi unaoendelea pale Ipinda, nilikuwa nataka kujua Serikali imefuatilia gharama ya pesa ilizotoa na uhalisia wa majengo yanayojengwa? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ujenzi wa zahanati ni kitu kingine, lakini utendaji wa wafanyakazi ikiwemo madaktari ni shida hasa Zahanati ya Ikuti Rungwe na hapo Ipinda hakuna watendaji wa kazi. Ni lini Serikali itatoa wafanyakazi ikiwemo madaktari na hasa Madaktari Bingwa wa wanawake kusaidia wanawake wa Wilaya ya zahanati ya Ipinda lakini pia Zahanati ya Ikuti Wilaya ya Rungwe? MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge naombeni muwe mnaenda straight kuuliza maswali ya nyongeza Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mwakagenda kama ifuatavyo:- Katika swali lake la kwanza anauliza iwapo Serikali imefuatalia kujua gharama iliyotumika na majengo ambayo yamejengwa. Majengo ambayo yanajengwa ni kwa mujibu wa ramani ambayo imetolewa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI na ni na suala ambalo matarajio yangu makubwa na Mheshimiwa Mbunge akiwa ni sehemu ya wananchi wa Halmashauri ile ni vizuri akatuambia ni sehemu ipi ambayo anadhani kwamba haridhiki, lakini mpaka sasa hivi ninavyoongea hata Mbunge wa Jimbo hajaleta malalamiko yoyote kwamba labda kuna ubadhilifu katika ujenzi huo. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili anaongelea juu ya suala zima la upatikanaji wa wataalam, suala la kujenga majengo jambo moja na suala la wataalam 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) jambo la pili, naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni nia ya Serikali kuhakikisha pale tunapomaliza ujenzi na wataalam wapatikane kwa mujibu wa Ikama na jinsi mahitaji yanavyopatikana. MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Ungando. MHE. ALLY S. UNGANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwanza sina budi kushukuru vyombo vya ulinzi na usalama hasa Kibiti tunalala usingizi. Swali langu la nyongeza Kituo cha afya kibiti hasa kinazidiwa kutoa huduma, je, Serikali ina mpango gani wa kuijengea Kibiti Hospitali ya Wilaya? MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli huko uhitaji mkubwa sana na kituo cha afya kilichopo kimezidiwa, naomba nimuondoe mashaka Mheshimiwa Mbunge na nimuhakikishie miongoni mwa hospitali 67 zinazotarajiwa kujengwa ni pamoja na Wilaya yake, kwa hiyo, wakae mkao wa kula Serikali inatekeleza ili kuondoa shida kwa wananchi. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kiwanga. MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu nilipata ahadi kutoka Wizara hii kwamba kutapelekwa hela za ujenzi kituo kile cha Mchombe katika Jimbo la Mlimba kiliwekwa katika mpango wa Serikali na kilipata zile grade ambazo zinafaa kupewa pesa ili kuboresha Kituo cha Afya cha Mchombe ambapo kinahutubia kata zisizopungua 10. Je, na katika mpango uliopita hakuna hela iliyopelekwa, mimi tu mfuko wa jimbo nilipeleka hela kidogo kwa ajili ya kusaidia… 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Uliza swali Mheshimiwa. MHE. SUSAN L. KIWANGA: Je, ni lini sasa Wizara ya afya itapeleka pesa za kuimarisha Kituo cha Afya cha Mchombe ndani ya Jimbo la Mlimba? MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri, TAMISEMI majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Susan Kiwanga swali lake la nyongeza juu ya ahadi ambayo anasema ilitolewa, sina uhakika juu ya ahadi hiyo, lakini kama ahadi hiyo imetolewa kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba nimuhakikishie hivi karibuni ni kama nilivyojibu swali la nyongeza jana la Mheshimiwa Mipata kuhusiana na kituo chake cha afya Kasu kuna matarajio ndani ya mwezi huu kuna pesa ambazo zitapatikana kwa ajili ya vituo vya afya visivyopungua 25. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sina uhakika kama katika hivyo 25 na yeye ni miongoni mwa hivyo ambavyo vinaenda kupelekewa pesa. MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea Waheshimiwa swali linalofuata linaelekezwa Ofisi ya Rais hapo hapo TAMISEMI na linaulizwa na Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum. Na. 25 Serikali Kusaidia Vikundi vya Wanawake Rukwa MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia vikundi vya wanawake waliopo katika Mkoa wa Rukwa katika suala la mikopo na kuwapatia elimu ya ujasiriamali? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, vikundi vya wanawake vinawezeshwa kupitia mfuko wa wanawake unaotokana na asilimia tano ya mapato ya ndani ya Halmashauri. Sambasamba na hilo Serikali inawahimiza Maafisa Maendeleo ya Jamii kuendelea kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vikundi vya wanawake ili kuwajengea uwezo, kuibua miradi yenye tija itakayosaidia kupata kipato na kurejesha mkopo. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2016/2017 vikundi vya wanawake 55 vyenye wanachama 698 vimepatiwa mikopo ya shilingi milioni 56.87 kati ya shilingi bilioni 6.5 zilizokusanywa kutokana na mapato ya ndani katika Mkoa wa Rukwa. Vilevile katika mwaka wa fedha 2017/2018 vikundi 33 vya wanawake vimepatiwa mikopo yenye jumla ya shilingi milioni 118 kati ya shilingi bilioni 4.2 ya makusanyo ya mapato ya ndani hadi machi, 2017 sawa na asilimia 2.78. Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kutoa maelekezo kwa Halmashauri kuimarisha makusanyo kwa kutumia mifumo ya kielektroniki iliyowekwa katika Halmashauri zote 185 na kuhakikisha kwamba fedha zinapelekwa kwenye mfuko kila zinapokusanywa. MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Mwakang’ata swali la nyongeza kama unalo. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Swali la kwanza kwa kuwa wanawake wengi wamehamasika sana kuanzisha VICOBA na wengine wameanzisha vikundi mbalimbali kwa lengo la kujikwamua kimaisha lakini wamekuwa wakiangaishwa sana kwa kupata hiyo asilimia 10; sasa ni lini Serikali itaweka mazingira mazuri ili hata kama hiyo asilimia 10 ipo lakini wawekewe mazingira mazuri ya kupata mikopo kwenye mabenki? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kwa kuwa asilimia 10 ya wanawake, walemavu na vijana inachelewa sana kuwafikia
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages181 Page
-
File Size-