Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi na Sita – Tarehe 23 Mei, 2014 Mkutano Ulizana Saa TAtu Asubuhi D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za “LAPF Pensinon Fund” kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012 (The Annual Report and Audited Accounts of Local Authorities Pension Fund for the Financial Year 2011/2012). NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA UCHUIKUZI: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi, ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaanza na maswali na Ofisi ya Waziri Mkuu. Atakayeuliza swali letu la kwanza kwa leo ni Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa. Na. 110 Tatizo La Maji Kata ya Mwabomba MHE. RICHARD M. NDASSA aliuliza:- Kata ya Mwabomba yenye Vijiji Vitano (5) vya Ngogo, Mwangika, Chamva, Mwabomba na Mhulula, haina hata kisima kimoja cha maji ya kunywa kinachofanya kazi, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa Wananchi hao hasa ukizingatia uwezo wa Halmshauri ya Kwimba kuwa mdogo kutatua tatizo hilo. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Je, Serikali ina wasaidiaje wananchi wa Kata ya Mwabomba ili waondokane na adha hiyo ya ukosefu wa maji? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa, kama ifutavyo:- Mheshimiwa Spika ninakubaliana kabisa na Mheshimiwa Mbunge kuwa hali ya upatikani wa huduma ya Maji Safi na Salama katika Kata ya Mwabomba, siyo ya kuridhisha. Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 24 tu ya Wakazi wa Kata hii, ndiyo wanaopata huduma ya Maji. Kwa kutambua tatizo hilo, Serikali imeanza kuchukua hatua zifuatazo:- Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014. Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa kushirikiana na Taasisi ya Rotary Club ya Uholanzi, wamechimba na kujenga visima viwili vyenye dhamani ya Shilingi milioni 10,000,000/= katika kijijiji cha Mabomba. Aidha, katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, Halmashauri kupitia vyanzo vyake vya ndani, imepanga kutumia shilingi milioni 8,000,000,000/= kwa ajili ya kuchimba visima viwili vifupi katika kijiji cha Ngogo. Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, kwa mwaka wa 2014/2015, imeidhinishiswa shilingi bilioni 2.5 kwa ajii ya utekelezaji wa Miradi ya maji kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa. Azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji karibu zaidi ili kuwaondolea adha ya kufuata huduma hiyo katika umbali mrefu. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo ya Mheshimiwa Waziri, lakini inawezekana Mheshimiwa Waziri hakupata taarifa kamili kwa sababu mnapo sema asilimia 24 (24%) siyo kweli. Sasa ninaomba taarifa muende mzipate vizuri. Mheshimiwa Spika, kwanza ninaomba uniruhusu, niishukuru sana Serikali, kwa kukamilisha ile Miradi mitano ya uchimbaji wa visima katika Jimbo langu la Sumve, ninaipongeza sana Serikali. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa sababu ufumbuzi wa maji katika Wilaya ya Kwimba, hasa Jimbo la Sumve, ni maji kutoka Ziwa Victoria peke yake. Kwa sababu pesa hizi zilizotengwa hizi ni pesa kidogo, Shilingi milioni 8,000,000/=. Shilingi milioni 10,000,000/= ni pesa kidogo sana. Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani sasa wa kuhakikisha kwamba vijii hivyo nilivyovitaja hivyo, vinapata maji ya kutosha kutoka Ziwa Victoria, kwa sababu mpango upo. Ninaomba Serikali itueleze ni mpango upi sasa, na pesa kiasi gani zimetengwa, kwa ajili ya mradi wa maji wa Ziwa Victoria? Mheshimiwa Spika, ahsante sana. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Richard Ndassa, kama hivi ifutavyo. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Ni kweli mpango huo upo, na nia ya Serikali ni kufikisha maji ya kutoka Ziwa Victoria, kupitia Magu mpaka Kwimba, na zimetengwa shilingi 4,000,000,000/= katika mwaka huu wa fedha. MHE. SUSAN A.J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Tanzania nzima tunayo matatizo makubwa sana ya maji. Lakini ninaomba nijielekeze kwenye Mradi wa Maji Dar es Salaam. Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba Serikali imejitahidi kuhakikisha kwamba wananchi wa Dar es Salaam wanapata maji. Lakini katika Mradi ule wa Ruvu Chini, mpaka sasa hivi wamesambaza mabomba kwa muda mrefu sana na wananchi wanasema mabomba yamesambazwa lakini bado hakuna maji hata kidogo. Mheshimiwa Spika, je, ni lini tatizo la maji, katika mkoa wa Dar es Salaam, hususan Wilaya ya Kinondoni, litapatiwa ufumbuzi na Serikali? SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, nafikiri utakubaliana na mimi hilo ni swali jipya kabisa? Mheshimiwa kwa sababu Dar es Salaam ni Dar es Salaam basi. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Susan Lyimo, kama hivi ifuatavyho. Ni kwei liko tatizo la maji. Lakini leo tutatoa taarifa hapa Bunge, kauli ya Waziri, kuhusu gatizo la maji Dar es Saam. Lakini pia ni kwamba ipo mipango ambayo inaendelea na ulazaji wa bomba umefika maeneo ya Tegeta. Kwa hiyo, Mradi ule utakamilika mwezi Juni, 2014. Lakini Miradi mingine ya Ruvu Juu, inaendelea pamoja na kuchimba visima, ili kuondoa tatizo la maji kabisa katika Jiji la Dar es Salaam. SPIKA: Ndiyo iko kauli ya Waziri wa Maji na imepangwa katika Order Paper ya leo. Na. 111 Tatizo la Maji Tarafa ya Wang’ing’ombe MHE. NEEMA HAMID MGAYA aliuliza:- Je, ni lini tatizo la maji kwenye Tarafa ya Wang’ing’ombe litakwisha? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALAZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema Hamid Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama hivi ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Tarafa ya Wang’ing’ombe ina jumla ya vijiji 44 vyenye wakazi wapatao 65,226 kati yake ni wakazi 37,629 wanapata huduma ya Maji safi na salama ikiwa ni sawa na asilimia 57. Wananchi hao wanapata huduma ya maji toka kwenye miradi ya mserereko inayotumia vyanzo viwili vya kutoka Mto unaoitwa Mtego wa Mbukwa na Mtitafu wa Visima virefu vyenye pampu za mikono miwili katika kijiji cha Uhenga. 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) Pia Mradi wa maji ya kusukuma na Mashine ipo mitatu (3) katika vijiji vya Makondo, Idenyimembe na Lyadembwe. Mheshimiwa Spika, kwakutambua tatizo hili, Serikali, imeanza kuchukua hatua zifuatazo. Kwa mwaka wa fedha 2012/2013 jumla ya shilingi 380,000,000/= zilitengwa kwa ajili ya uboeshaji wa miundombinu ya maji, katika mradi wa Wanging’ombe na Masaulwa. Shlingi milioni 100, zilitumika kukarabatai miradi ya Wanging’ombe na shilingi 280,000,000,000/= zilijenga Mradi wa maji wa Masaulwa. Mheshimiwa Spika, Mradi mingine inayoendelea kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 ni ya vijiji vya Isimike, Igenge, Idenyimembe na Wangama yenye thamani ya shilingi 886,593,887.20. Miradi hiii imefikia hatua mbalimbali ya utekelezaji na inatarajiawa kukamilika mwezi Juni, 2014. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 jumla ya shilingi 418,233,000,000/= zimtengwa kwa ajili ya kuendeela kuboresha hudma za maji, katika Tarafa ya Wangiong’omb ambapo vijiji vya Malangali na Isindagosi vyenye jumla ya wakazi 3,309 vitanufaika. Mheshimiwa Spika, maeneo mengine yaliyobaki, yayaendelea kujengewa miundombinu ya maji kwa kadiri rasilimali fedha itakavyokuwa inapatikana. MHE. NEEMA HAMID MGAYA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri. Ninayo maswali mawili ya nyongeza. (i) Wilaya yetu ya Wang’ing’ombe ni Wilaya mpya. Kwa kuwa Wilaya hii ni mpya na matatizo ya Maji yako kwa kipindi kirefu sasa, nilitaka kusikia sauti ya Serikali, kutaka kujua itasaidia vipi, Wang’ing’ombe kutatua tatizo la maji kwa kupitia mradi mkubwa wa kitaifa wa maji na Matokeo ya Haraka Sasa (GRN)? (ii) Kuna Mradi ulioanzishwa mwaka 1976, na UNICEF, Mradi ule haujawahi kukarabatiwa, wala kupanuliwa miundombinu yake. Kwa sababu kadiri siku zinavyozidi kwenda watumiaji wa maji wanaongezeka. Kuna Kata mbili ambazo zina shida sana ya Maji. Kata ya Saja ya Kijombe. Kwa kuboreshwa kwa Mradi huu, tutaweza kuhudumia viiji vingi sana vilivyopo katika Kata hiyo. Kwa sababu shinda ya maji, hasa iko kwenye Tarafa ya Wang’ing’ombe. Mheshimiwa Spika, naomba majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Hamid Mgaya, kama hivi ifutavyo. Mheshimiwa haya majina haya, wewe utakuwa unayafahamu, ni ya kule kwako waliko meguka ndiyo waliokwenda Wanging’ombe, kwa hiyo unayafahamu vizuri. Yananipa tabu hapa kuyatamka, ni majina magumu ya Kihehe. Mheshimiwa Spika, lakini la kwanza ambalo nilitakakusema, ni hii, Mheshimwia Mbunge ana underscore point ya msingi, na asubuhi tumeii-discuss. Mheshimiwa Spika, Wanging’ombe ni Wilaya mpya, imeanza juzi juzi tu. Bajeti yake hii iliyopia hapa walikuwa na shilingi 239,000,000/=. Hivi imepanda imekwenda kwenye milioni 418,000,000/=. 4 Nakala ya Mtandao (Online Document) Lakini kuhusu mipango hii inayozungumzwa hapa wanayo barua na Halmashauri zote nchini, zimeandikiwa barua na Waziri wa Maji. Naibu Waziri yuko hapa anafahamu, zikielekezwa kwamba waende kwenye commitments zao kama walivyokuwa wame-plan, bila kujali kwamba hicho kiasi walicho nacho hawana. Kwa maneno mengine sasa hivi, wanayo commitment ya shilingi 889,000,000/= kwa ajili ya Miradi mbalimbali, ambayo iko katika Halmashauri yao. Kwa hiyo ninamwomba Mheshimiwa Mgaya, afuatilie ile. Nina appreciate, ninakubaliana naye ya kwamba Halmashauri hizi changa unatakiwa uzibebe kama unavyobeba mototo wa mwisho pale nyumbani, mdogo unamwangalia. Ndicho anachokisema Mheshimiwa hapa. Ambaye mimi ninampongeza kwamba analiona hilo yeye na Mheshimiwa Lwenge, wanahangaikia katika hali hii. Sisi tutakwenda kuangalia. Mheshimiwa Spika, ametaja huu mradi mwingine hapa ulioanza mwaka 1976 ninakuomba Mheshimiwa Spika, nitafutilia Mradi huu wa karibu.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages177 Page
-
File Size-