MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao Cha Thelathini Na Mbili – Tare

MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao Cha Thelathini Na Mbili – Tare

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Thelathini na Mbili – Tarehe 18 Mei, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na kikao chetu cha thelathini na mbili. Katibu! NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, ningependa kutoa Taarifa inayohusiana na kukamilika kwa Mkutano wa Nne wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika hapa kwetu tarehe 8 hadi 27 Aprili, 2018. Waheshimiwa Wabunge, kuanzia tarehe 8 hadi 27 Aprili, 2018 Bunge la Afrika Mashariki (East Africa Legislative Assembly) lilikuwa na Mkutano wake wa Nne ambao kwa mwaka huu ulifanyika hapa Tanzania na kipekee katika Ukumbi wa Msekwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo kuwa mkutano wa kwanza kufanyika kwenye viwanja vyetu vya Bunge hapa Dodoma na wa kwanza kufanyika Tanzania chini ya Serikali ya Awamu ya Tano. (Makofi) 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa Ibara ya 55(1) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mikutano ya Bunge hili hufanyika kwa mzunguko miongoni mwa nchi wanachama kila baada ya miaka miwili na nusu. Lengo la kufanyika mikutano hii kwa mzunguko ni kukuza ushirikiano na mawasiliano baina ya Bunge hilo na Mabunge ya nchi wanachama. Waheshimiwa Wabunge, kufuatia taratibu za uendeshaji wa Bunge hilo wa kutoa fursa maalum kwa Rais wa Nchi mwenyeji kuhutubia kwenye mkutano husika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alihutubia Mkutano wa Bunge hili tarehe 24 Aprili, 2018 ambapo baadhi ya Wabunge, Wajumbe wa Kamati ya Uongozi na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge walihudhuria kwa niaba yetu. Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano huo wa Nne wa Bunge la Afrika Mashariki shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwa ni pamoja:- (i) Shughuli za Kamati za Bunge la Afrika Mashariki zilifanyika; (ii) Kamati Ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Afrika Mashariki ilikutana; (iii) Miswada miwili ya Sheria ilijadiliwa na kuwasilishwa; (iv) Mkutano wa kubadilishana uzoefu baina ya Kamati za Bunge la Afrika Mashariki na Kamati za Kudumu za Bunge letu ilifanyika; (v) Palikuwa na kushiriki kwenye zoezi la upandaji miti 1,000 ambalo lilifanyika katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM); (vi) Wabunge wa Afrika Mashariki waliweza kushiriki kwenye sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) na Zanzibar zilizofanyika tarehe 26 Aprili, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma; na (vii) Pia walishiriki kwenye michezo ya kirafiki ya mpira wa miguu kati ya timu ya Bunge la Afrika Mashariki na timu yetu ya Bunge Sports Club. Waheshimiwa Wabunge, kwa kumalizia, napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Wabunge wote, kumshukuru Katibu wa Bunge na watumishi walioko chini yake wote na wadau wengine wote kwa namna tulivyoweza kushiriki kwa pamoja kwa njia moja au nyingine katika kufanikisha mkutano huu. Aidha, napenda kuwataarifu kwamba Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ameniandikia barua kutoa shukrani za dhati kwa Ofisi ya Bunge kwa maandalizi mazuri yaliyofanyika na ofisi yetu ili kufanikisha mkutano huo. (Makofi) Maandalizi hayo yaliyofanywa na Bunge letu yaliwezesha mkutano huo kufanyika kwa ufanisi na kumalizika kwa mafanikio makubwa. Ahsanteni. (Makofi) Katibu! NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2018/2019. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. Katibu! 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali la kwanza litaulizwa kuelekea Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na litaulizwa na Mheshimiwa Khadija Nassir Ali, Mbunge wa Viti Maalum. Mheshimiwa Khadija tafadhali. Na. 266 Kuwawezesha Wanawake na Vijana Kiuchumi MHE. KHADIJA NASSIR ALI aliuliza:- Miongoni mwa matakwa ya Serikali ni kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi. Je, Serikali inatekelezaje suala hilo? SPIKA: Majibu ya swali hilo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mavunde tafadhali. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Khadija Nassir Ali, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kutokana na kutungwa kwa Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 pamoja na sheria mbalimbali zinazohusu uwezeshaji wananchi kiuchumi, Serikali inatekeleza Mpango wa Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi kama ifuatavyo:- Moja, ni kutambua umuhimu wa mafunzo ili kuwawezesha wanawake na vijana kukuza shughuli zao za kiuchumi na kujikwamua kimaisha. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Pili, ni kuhamasisha vijana na wanawake kujiunga na vikundi vya kiuchumi vya Vyama vya Kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) ili kujipatia kwa urahisi mitaji ya kuanzisha na kuendelez amiradi ya kibiashara. Tatu, ni kuwekeza katika Sekta ya Ufundi stadi ili vijana wanaohitimu waweze kuwa na ujuzi wa kuweza kujiajiri. Nne, kuanzisha miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ni chanzo cha ajira kwa wanawake na vijana. Tano, ni kuanzisha Benki ya Wanawake kwa lengo la kutoa mikopo kwa wajasiriamali wanawake na pia uwepo wa mifuko maalum ya uwezeshaji wa akina mama (WDF) na vijana (YDF). SPIKA: Mheshimiwa Khadija, swali la nyongeza nimekuona. MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba nielezee masikitiko yangu juu ya majibu ya Serikali ambayo amenipatia. Mheshimiwa Spika, majibu ambayo Serikali imeleta yako kisera zaidi, nilitegemea yaje majibu ambayo kidogo yangeleta taswira na mwanga kwa vijana. Mheshimiwa Spika, nashindwa kuelezea malalamiko yangu kwa vile tuko kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani lakini kwa kweli nimesikitishwa sana na majibu. Baada ya kusema hayo nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Spika, kwa vile Serikali imepanua fursa ya elimu kwa kuongeza Vyuo Vikuu vya Elimu ya Juu na Elimu ya Kati. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendana basi na mahitaji yaliyopo? Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kiasi gani Mfuko wa Vijana umeweza kuwagusa walengwa ukizingatia na hali halisi iliyopo? Ahsante. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Majibu ya maswali hayo likianzwa na kutoridhishwa kabisa na Mheshimiwa kwa majibu ya awali. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa na mipango mbalimbali ya kuwawezesha vijana na akina mama na msingi mkubwa wa uwezeshaji huo unatokana na sera. Kwa hiyo, nimuondoe tu hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba majibu haya kwa sababu ya uwezeshaji na sera inatuelekeza hivyo ndiyo maana yalijikita hapo. Mheshimiwa Spika, nikienda katika swali lake la kwanza la kujua kuhusu ongezeko la idadi ya wahitimu wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Ufundi ikilinganishwa na nafasi za ajira. Kama Serikali na kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2014 ya Integrated Labour Force Survey ambayo imeeleza kinaga ubaga juu ya nafasi za ajira zinazotengenezwa kila mwaka lakini na watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa mwaka husika kwamba idadi imekuwa ni kubwa tofauti na nafasi za ajira ambazo zinatengenezwa. Kwa hiyo, sisi kama Serikali tuliona njia nyingine mbadala ni kuanza sasa kuwabadili mitazamo vijana wetu hasa wahitimu wa vyuo vikuu na kuamini kwamba bado wanaweza wakafanya shughuli zingine za kiuchumi ikiwemo kilimo, ufugaji na biashara na sisi kupitia Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuweza kuwawezesha ili kuweza kufikia malengo yao. Mheshimiwa Spika, sisi kwetu tafsiri kwa mujibu wa Sera ya Ajira ya mwaka 2008, ajira ni shughuli yoyote halali inayomuingizia mtu kipato. Kwa hiyo, tumeanza sasa kuwabadili mitazamo vijana wetu waanze kuamini kwamba si wote ambao wanaweza kwenda kukaa ofisini, lakini pia tunaandaa mazingira mazuri waweze kufanya kazi za kujiajiri. Mheshimiwa Spika, la pili ameuliza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana; ni kweli, kwa mujibu wa Sheria ya Fedha, Sheria Na. 21 ya mwaka 1961, kifungu namba 21(1) 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kilianzisha Mfuko wa Maendeleo wa Vijana ambao lengo lake ni kuhakikisha tunawagusa vijana wengi zaidi kwa kuwasaidia kupata mikopo na mitaji na mikopo yenye riba nafuu. Mheshimiwa Spika, mpaka ninavyozungumza hivi sasa, tayari tumeshafikia vikundi vya vijana 397 ambao tumeshatoa kiasi cha shilingi zaidi ya shilingi bilioni nne kwa ajili ya kuwawezesha vijana. (Makofi) SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Khatib, swali tafadhali. MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Mheshimiwa Spika, mwaka 2015, wakati tukienda kwenye uchaguzi mkuu, kila chama kiliuza sera zake kwa Watanzania. Chama cha Mapinduzi kilitangaza sera kuwapatia wananchi wa Tanzania kila kijiji shilingi milioni 50 sera ambayo iliwavutia sana Watanzania. Je, Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoweka kwa Watanzania? Kama haijashindwa, ni lini pesa hizi zitapelekwa kwa vijiji vyote vya Tanzania? Ahsante. SPIKA: Majibu ya swali hilo tafadhali Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, ni kweli katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 tulieleza bayana ya kwamba moja kati ya mkakati mkubwa wa kuwawezesha wananchi kiuchumi ilikuwa pia

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    210 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us