NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Kumi na Nne – Tarehe 22 Aprili, 2020 (Bunge Lilianza Saa Nane Mchana) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Tisa, Kikao cha leo ni cha Kumi na Nne. Waheshimiwa Wabunge msishangae kumuona Spika naye leo amekuja kivingine, majibu yake ni rahisi tu ukishamshaona Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi naye amepiga barakoa maana yake ni kwamba lazima tufuate utaratibu. Leo Mheshimiwa Waziri Mkuu hatutakuwa naye badala yake tunaye Dkt. Hussein Mwinyi yeye ambaye ana kaimu nafasi hiyo ya kuongoza shughuli Bunge. Kwa hiyo, wenye yoyote ya kiserikali tuwasiliane naye. Katibu! NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2020/2021. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021. MHE. DEVOTA M. MINJA - NAIBU MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO): Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2020/ 2021. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na.123 Mradi wa Maji Kutoka Pongwe Kwenda Muheza MHE. YOSEPHER F. KOMBA aliuliza:- Kwa muda mrefu mradi wa maji unaotoka Pongwe kwenda Muheza Mjini umekuwa ukisuasua na upelekaji fedha za mradi usioridhisha:- (a) Je, mradi huo una gharama kiasi gani mpaka ukamilike, na Je, mpaka sasa ni kiasi gani cha fedha kimepelekwa kwa ajili ya mradi huo? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (b) Je, ni lini wananchi wa Wilaya ya Muheza wategemee kukamilika kwa mradi huo ili waondokane na kero ya maji inayowakabili kwa sasa? WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yosepher Ferdinand Komba Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji katika Mji wa Muheza, mwaka 2017 Serikali ilianza kujenga mradi huo kwa kupanua mtandao wa maji kutokea katika mtandao wa maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga. Mradi huo umebuniwa kutekelezwa kwa awamu mbili kwa jumla ya shilingi bilioni 6.11. Hadi kufikia mwezi Machi, 2020, Serikali imeshafanya malipo ya jumla ya Shilingi Bilioni 3.6 kwa Wakandarasi waliokuwa wakidai kutokana na kazi walizotekeleza. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa awamu ya kwanza inayohusisha ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa laki saba (700,000), ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 16.9, ujenzi wa nyumba mitamba na ufungaji wa pampu mbili za maji, utekelezaji wake umefikia asilimia 95 na utekelezaji wake unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili, 2020. Awamu ya pili ya mradi huo inahusisha ujenzi wa bomba la majisafi lenye kipenyo cha milimita 300 na urefu wa kilomieta 8.2 kutoka Mowe hadi Pongwe. Utekelezaji wa awamu hii unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2020. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuwalipa Wakandarasi kwa wakati ili kuwezesha mradi huo kukamilika kama ilivyokusudiwa na kuwapatia wananchi wa Muheza huduma ya Majisafi na salama. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na.124 Tatizo la Mabomba Kutoa Maji Machafu – Manispaa ya Mtwara Mikindani MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza:- Kumekuwa na tatizo la kutoka maji machafu ya bomba katika Manispaa ya Mtwara Mikindani Je, tatizo hilo linasababishwa na nini na litaisha lini? WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tunza Issa Malapo, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, vyanzo vya maji vinavyotumika kuwahudumia wananchi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ni visima vilivyoko kwenye mabonde ya Mtawanya, Mchuchu na Rwelu. Mheshimiwa Spika, ni kweli maji yanayopatikana kwenye visima vinavyotumika katika Manispaa ya Mtwara yana changamoto ya kuwa na rangi ya tope kutokana na chujio lilipo lina uwezo mdogo hivyo linazidiwa na kiasi cha maji kinachozalishwa. Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa chujio hasa uondoshaji wa tope linalosalia kwenye maji (rapid sand filter) kwenye eneo la Mangamba. Aidha, pamoja na jitihada nzuri za Serikali zinazoendelea kufanyika, tatizo hili litakwenda kukoma kabisa kupitia utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Mtu Ruvuma – Magamba. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 125 Kuanzisha Shule Maalum za Vipaji vya Michezo na Sanaa MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kuanzisha Shule Maalum za Vipaji vya Michezo na Sanaa.? WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Cosato David Chumi (Mbunge), Mafinga Mjini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa shule maalum katika kuibua na kukuza vipaji na vipawa mbalimbali hapa nchini. Kwa msingi huo, Serikali inaandaa Mwongozo wa Usajili wa Shule utakaowezesha wadau wa elimu hapa nchini kuanzisha na kusajili shule za kuibua na kukuza vipawa na vipaji katika tasnia mbalimbali ikiwemo Michezo na Sanaa. Mheshimiwa Spika, ili kuwa na wataalam wa Sanaa na Michezo watakaofundisha katika shule zetu, Serikali inaendelea kuandaa walimu kupitia Chuo cha Ualimu Butimba ambacho hutoa Astashahada na Stashahada za Ualimu katika michezo. Aidha, Serikali inaandaa walimu wa Michezo na Sanaa katika ngazi ya Shahada kupitia Vyuo Vikuu. Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hutoa Shahada za Elimu ya Michezo (Physical Education), Sanaa za Ufundi (Fine Arts), Muziki (Music) na Sanaa za Maonesho (Performing Arts). Aidha, Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya na Taasisi ya Sanaa Bagamoyo vilivyo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo vinatoa fursa nyingine ya kuendeleza vipaji vya Sanaa na Michezo nchini. Mheshimiwa Spika, kwa sasa, Serikali imekuwa ikitoa elimu ya Michezo na Sanaa shuleni kupitia vipindi vya masomo darasani, shughuli za nje ya darasa na mashindano 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) mbalimbali ya Michezo na Sanaa kama vile mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) shule za Sekondari (UMISETA) na kwa Vyuo vya Ualimu (UMISAVUTA). Na. 126 Uzalishaji wa Madini ya Niobium Wilaya ya Mbeya MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza:- Je, ni lini uzalishaji wa madini ya Niobium utaanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya? WAZIRI WA MADINI alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Oran Manase Njeza (Mbeya Vijijini), kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mradi wa uchimbaji madini ya Niobium unamilikiwa na Kampuni ya Panda Hill. Kampuni hii ina ubia na kampuni ya Cradle Resources Limited asilimia 50 na Tremont Investments asilimia 50. Kampuni hiyo inamiliki Leseni tatu za Uchimbaji wa Kati wa madini ML 237/2006, ML 238/2006 na ML 239/2006 zilizotolewa tarehe 16 Novemba, 2006 zikiwa na kilomita za eneo la mraba 22.1. Mheshimiwa Spika, mradi utahusisha uchimbaji wa madini ya Niobium ambayo yataongezewa thamani kwa kuchanganywa na madini ya Chuma na kuwa Ferro-Niobium zao ambalo litauzwa kwa wanunuzi mbalimbali waliopo Ulaya, Asia na Amerika ya Kaskazini. Mheshimiwa Spika, mwekezaji ameshafanya Upembuzi Yakinifu (Feasibility Study) uliokamilika mwaka 2016 na kujiridhisha uwepo wa mashapo ya kutosha utakaowezesha uhai wa mgodi kuwa takribani miaka 30. Hata hivyo, kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017, Mwekezaji alilazimika kupitia upya na kurekebisha taarifa ya upembuzi yakinifu ili kuzingatia 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) viwango vipya vya mrabaha, kodi na hisa za Serikali. Hivyo, mwekezaji amewasilisha andiko la mradi la kuomba ufafanuzi wa vipengele mbalimbali vya Sheria na kutoa mapendekezo yake juu ya utekelezaji wa mradi huo, pamoja na suala la fidia ya ardhi kwa Gereza la Mbeya ambalo linatakiwa kuhamishwa ili kupisha Mradi. Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea andiko hilo, hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo majadiliano na mwekezaji ambapo, Wizara inatarajia kutoa mapendekezo yatayowezesha kuanza kwa utekelezaji wa Mradi huo. Na. 127 Ushirikiano Kati ya TFF na ZFF MHE. SAADA MKUYA SALUM aliuliza; Je, ni kwa kiasi gani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweza kushirikiana na Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) katika kukuza Soka la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saada Salum Mkuya, Mbunge wa Welezo kama Ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) yamekuwa yakishirikiana kwa karibu katika kuratibu na kukuza mchezo wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania. Ushirikiano wa mashirikisho haya umejikita katika maeneo mbalimbali muhimu ya maendeleo ya soka hapa nchini ikiwemo haya yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, katika kuendesha Soka la vijana, TFF kwa kushirikiana na ZFF mashindano yote ya Kitaifa ya Vijana (U15 na U17) hushirikisha mikoa yote ya Tanzania
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages227 Page
-
File Size-