Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA ISHIRINI __________ Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 25 Mei, 2015 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. MAUA ABEID DAFTARI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2014/15 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. MOSES J. MACHALI (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO): Taarifa ya Msemaji wa Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. AGNESS E. HOKORORO (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. CECILIA D. PARESSO - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA KAZI NA AJIRA: Taarifa ya Msemaji wa Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Waziri Mkuu, amemteua Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu Kukaimu nafasi ya Uwaziri Mkuu. Kwa hiyo, sasa ndiyo atachukua nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Serikali Bungeni. Mambo yanaanza polepole. (Kicheko) Katibu, hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU Na. 78 Uhuishwaji wa Daftari la Wapiga Kura MHE. JOSEPH R. SELASINI aliuliza:- 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeweka muda maalum wa kuhuisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, zoezi ambalo litaendelea wakati walimu na wanafunzi wako vyuoni:- (a) Je, ni kwa nini Tume isiandae utaratibu utakaowezesha Walimu na Wanafunzi kujiandikisha katika maeneo watakayopigia kura? (b) Je, kama Tume haitafanya hivyo haioni kuwa ni sawa na kuwanyima wananchi hao haki ya kuchagua Viongozi wanaowataka? NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA (K.n.y. WAZIRI MKUU) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Roman Selasini, Mbunge wa Rombo, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kifungu cha 15 cha Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina wajibu wa kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Uandikishaji unajumuisha kuhuisha Daftari ili kuwapa nafasi wale waliotimiza sifa za kuandikishwa na kuwaondoa wale waliokosa sifa au kubadili taarifa zao. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikihuisha Daftari la Kudumu la Mpigakura kama sheria inavyoelekeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria za Uchaguzi zinamtaka mpiga kura kujitokeza mwenyewe kituoni kujiandikisha au kurekebisha taarifa zake kila inapotokea mahitaji ya kufanya hivyo. Wakati wa kupiga kura, kila mpiga kura anatakiwa aende kupiga kura katika kituo alichojiandikisha. Hata hivyo, vifungu 17 na 19 vya Sheria ya Uchaguzi, vinatoa fursa na utaratibu kwa wapiga kura kuhamishia taarifa zao katika maeneo watakayoweza kupiga kura. Kwa utekelezaji wa vifungu hivi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina utaratibu wa kutoa kipindi maalum kabla tarehe ya kupiga kura ili wale wanaotaka kuhamisha taarifa wafanye hivyo. Kwa mfano, katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Tume ilitoa muda wa siku 30 kabla ya uchaguzi ili wapiga kura waliohitaji kuhamisha taarifa zao kufanya hivyo. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa msingi nilioueleza katika sehemu (a), walimu, wanafunzi walioko vyuoni na wananchi wengine wenye mahitaji kama hayo, watajiandikisha katika vituo walivyopo sasa na endapo wakati wa kupiga kura watapenda kupiga kura katika vituo tofauti na vile walikojiandikisha, utaratibu uliowekwa na Tume wa kuhamisha taarifa zao utatumika ili kuwapa haki ya Kikatiba wananchi hao kushiriki katika uchaguzi. (Makofi) 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu ya hili swali yanachekesha na niseme kwa mara ya kwanza yanaudhi. Kwa sababu mimi sikuulizia wapigakura kwa ujumla wake, nimeuliza wanafunzi wa vyuo vikuu, wanafunzi wa colleges na wanafunzi wa sekondari, ambao hivi sasa zoezi hili likiendelea wapo mashuleni na wakati uchaguzi utakapokuwa unafanyika watakuwa majumbani. (i) Je, hizo siku 30 zinazosemwa vyuo vyote vitafungwa ili hawa wanafunzi waende wakarekebishe hizo taarifa? (Makofi) (ii) Zoezi hili linaendelea kwa teknolojia ambayo tunaamini ni ya kisasa; ni kwa sababu gani wanafunzi hawa wanapoandikishwa huko vyuoni wasieleze vilevile maeneo wanapotoka ili taarifa zao zikahamishwa kwa mtandao kupelekwa kwenye maeneo ambayo wanategemea kupiga kura au hili linafanywa kwa makusudi mazima ili kuwanyima wanafunzi haki yao ya kupiga kura? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Joseph Roman Selasini, Mbunge wa Rombo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali la msingi Mheshimiwa ameuliza wanafunzi, lakini pia na sisi tumeeleza kwamba, katika muda mwafaka na tukaeleza na mifano iliyotumika huko nyuma kwamba, Tume kawaida kabla ya kwenda kwenye uchaguzi, inatoa siku 30 za mwisho, wawe wanafunzi wa vyuo vikuu, wawe watumishi wa vyuo vikuu, wawe Watanzania wengine wote wa kawaida, wanapewa fursa ya kubadilisha na kueleza nia yao kwamba ni wapi wangependa wapigie kura zao. Hili liko bayana. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba nimweleze Mheshimiwa Selasini kuwa, Serikali inajua kabisa kwamba, vyuo vyetu kwa sasa vina wanafunzi wengi na ambao kwa vyovyote vile, hawawezi kunyimwa fursa ya kwenda kupiga kura katika maeneo ambayo wangependa kwenda kupiga kura. Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, hili tumeliweka bayana kabisa. Swali la pili anasema kwamba, nini wasieleze maeneo ambayo watapigia kura. Haya mambo mengine ni masuala ya kuzungumza, ninaamini Tume wanasikia na sisi kama Serikali tumeendelea kuzungumza na Tume. Kwa kuwa Tume wa utaratibu wao, tumesema wakati mwingi siyo vizuri tukaingilia sana 4 Nakala ya Mtandao (Online Document) utendaji wa kazi wa Tume, maana itaonekana na sisi kama Bunge tunaingilia pia utendaji wa kazi wa vyombo vingine. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi tulilolisema ni kwamba, tutahakikisha wale wote wanapiga kura katika vituo ambavyo wangependa kupiga kura, pamoja na kwamba wanaweza wakajiandikisha katika kituo chochote. Kama Serikali tutahakikisha wanapiga kura bila kukosa na wala hakutakuwa na kisingizio chochote. MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, hebu subiri hapo hapo, kwa namna ya kuliweka sawa katika jibu lako la msingi la Serikali, hebu soma tena majibu yako ya msingi sehemu (b) ili Bunge lielewe msimamo mzuri wa Serikali. NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuelewa. Tumejibu kwa msingi kwamba, swali (b) linasema kama Tume haitafanya hivyo, haioni kuwa ni sawa na kuwanyima wananchi hao haki ya kuchagua Viongozi wao? Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema kwenye majibu ya msingi … MWENYEKITI: No, no, no, mimi ninataka nikusaidie wewe, katika jibu lako la msingi, jibu la Serikali soma kipengele cha (b) ili Mbunge aelewe Serikali imesema nini. Umenielewa? NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa sawa. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa msingi nilioueleza katika sehemu (a), walimu, wanafunzi walioko vyuoni na wananchi wengine wenye mahitaji kama hayo, watajiandikisha katika vituo walivyopo sasa na endapo wakati wa kupiga kura watapenda kupiga kura katika vituo tofauti na vile walivyojiandikisha, utaratibu uliowekwa na Tume wa kuhamisha taarifa zao utatumika ili kuwapa haki ya Kikatiba wananchi hao kushiriki katika uchaguzi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, yeye amesema wanafunzi, wanachuo, tumeshaeleza hayo. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante, umeshajieleza. Mheshimiwa Paresso! MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza swali dogo la nyongeza. Utaratibu wa kuandikisha mpiga kura kwa kutumia Mfumo wa BVR unahitaji mwananchi aweke alama za vidole na maeneo mbalimbali wananchi 5 Nakala ya Mtandao (Online Document) wamekuwa wakilalamika zile mashine zinakuwa hazichukui alama za vidole kwa maana ya finger print. Kuna akina mama wanaenda mara mbili mpaka mara saba alama hiyo ya vidole haiwezi kuchukuliwa:- Je, watu hawa ambao wanaathirika kwa namna moja ama nyingine watakosa haki yao ya kupiga kura na kujiandikisha; nini kauli ya Serikali? NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli lazima tukubali kwamba, hii ni teknolojia ya kisasa ambayo inatumika katika
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages322 Page
-
File Size-