
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Tano – Tarehe 12 Aprili, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioisha tarehe 30 Juni, 2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Financial Statements of Local Government Authorities for the Financial Year ended 30th June, 2010). NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE.GREGORY G. TEU): Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of the Financial Statement of the Central Government for the Year ended 30th June, 2010). Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Mashirika ya Umma kwa Mwaka 2009/2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Financial Statement of Public Authorities and other Bodies for the Financial Year 2009/2010). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ukaguzi wa Ufanisi na Upembuzi kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Machi, 2011 (The General Report of the Controller and Auditor General on the Performance and Forensic Audit Report for the Period ended 31st March, 2011). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Ufanisi wa ufuatiliaji na Tathmini ya Mgawanyo wa Bajeti kwa Shughuli za Huduma za 1 Kijamii kwa Akina Mama na Watoto Tanzania (The General Report of the Controller and Auditor General on Performance Audit on the Monitoring, Evaluations and Budget All action for Maternal Health care activities in Tanzania). MASWALI NA MAJIBU Na. 61 Wabunge wa Viti Maalum wa Upinzani Kubaguliwa MHE. CHRISTINA L. MUGHWAI aliuliza:- Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa inaeleza kuwa Baraza la Madiwani linaundwa na Madiwani wa Kata, Wabunge wa Majimbo, Wabunge wa Viti Maalum na wale wa Kuteuliwa wanaotoka katika Halmashauri ikiwa ni pamoja na Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango. Aidha, kumekuwepo na Wabunge wa Viti Maalum wa Upinzani kuzuiliwa kuhudhuria Vikao vya Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango katika Halmashauri zao:- (a) Je, ni sheria ipi inayoruhusu ubaguzi kwa Wabunge hao? (b) Je, Wabunge hao watatekeleza vipi wajibu wao kwa Wananchi kwa kuwa wanazuiwa kuhudhuria vikao hivyo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, katika Sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna Sheria yoyote inayoruhusu ubaguzi wa aina yoyote. (b) Mheshimiwa Spika, Kamati za Kudumu zote za Halmashauri, isipokuwa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, zinapaswa kuwa na Wajumbe wasiozidi theluthi moja ya Wajumbe wote wa Baraza. Kwa upande wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Kanuni za Kudumu za Halmashauri zinaelekeza kuwa, Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ni wale tu wanaoingia kwa nyadhifa zao ambao ni Mwenyekiti au Meya; Makamu Mwenyekiti au Naibu Meya; Mbunge wa kuchaguliwa anayewakilisha Jimbo; Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Halmashauri; na Wajumbe wawili miongoni mwa Madiwani wote wanaoteuliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri na kuthibitishwa na Baraza. 2 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kila Jimbo lina Mbunge wa kuchaguliwa, Mbunge huyo ndiye anayewajibika kwa Wananchi wote wa makundi yote yaliyomo kwenye Jimbo hilo na anayepaswa kujua kinachoendelea katika Jimbo husika na endapo Mbunge wa Viti Maalum atakuwa na jambo la kuliwasilisha kwenye Vikao vya Halmashauri, atawasilisha hoja hiyo kwenye Baraza la Madiwani, ambalo linawajumuisha Wajumbe wote au atawasilisha kwa Mbunge wa Jimbo ambaye atawasilisha kwenye Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango. MHE. CHRISTINA L. MUGHWAI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ambayo nayo hayakuniridhisha sana, nina maswali mawili ya nyongeza:- (a) Ikiwa Kanuni za Halmashauri zinaelekeza kuwa Wabunge wa Viti Maalum si Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmshauri ama Manispaa; jambo ambalo linashangaza kwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum wanaruhusiwa kuwa Wajumbe wa Bunge wa Kamati ya Fedha nikimaanisha Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na LAAC; je, Waziri haoni kwamba, Kanuni hizi za Halmashuri zimepitwa na wakati na zinahitaji kubadilishwa ili kuongeza nguvu katika usimamiaji wa fedha za umma tukizingatia kwamba ubadhirifu mkubwa wa fedha hizi unatokea katika Halmashauri zetu? (b) Mheshimiwa Spika, katika Kikao cha Kamati ya Uongozi na Mipango cha Halmashuri ya Wilaya ya Singida kilichofanyika tarehe 10 Februari, 2011, Wabunge wa Viti Maalum tulipata barua za mwaliko kutoka kwa Wakurugenzi kuhudhuria kikao hicho. Cha kushangaza, tulipofika Mkurugenzi huyo baada ya kutukabidhi makabrasha, alitutoa nje tena bila staha kwa kutueleza kuwa, sisi hatukuwa Wajumbe wa Kikao hicho. Je, Waziri anasema nini juu ya udhalilishaji huo uliofanywa na Mkurugenzi mbele ya Watumishi wa Halmshauri na Madiwani? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ninachokizungumza hapa, ninazungumzia Sheria na Kanuni zinazotawala mpango huu. Ninajua kabisa kwamba, jambo hili lina sensitivity yake, Wabunge wote wa Viti Maalum wanajisikia kwamba wamebaguliwa, Sheria aninayoisoma hapa ndivyo inavyotamka na Kanuni zetu ndivyo zinavyosema. Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kwamba, kama Mheshimiwa anafikiri hii Sheria imepitwa na wakati, basi sasa ni wakati wa kufukiria tufanye nini; mimi sikuja hapa kuleta la kwangu, ninaleta kile kilichopo hapa. Kwa hiyo, kama kuna mawazo hapa ya kubadili, mimi sina objection; kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninasema hili tutalijadili na ndiyo maana liko tamko hapa lilitolewa na Mheshimiwa Celina Kombani, linalofafanua jambo hili ninalolizungumza. Ninakubali kwamba, sasa ni wakati muafaka 3 wa kutafakari jambo hili sote kwa pamoja, tuone tufanye nini ili na wao waweze kuingia. Hilo la kwanza. Mheshimiwa Spika, la pili, hili sasa linalozungumzwa la Mkurugenzi anayesemekana kwamba, ameandika barua akawaalika, ina maana wao siyo Wajumbe wa Kamati ile; lakini sasa tunasema kwamba, kuna barua imeandikwa hapa. Mimi nakuomba nikimaliza kujibu maswali, nitapiga simu sasa hivi ninataka aniambie ni kwa nini aliandika barua halafu watu wanafika mlangoni anawaambia tokeni. Kama amewaita, ina maana aliona umuhimu wa wao kukaribishwa kwenye ile Kamati. Sasa hili ni jambo ambalo siwezi kulijibu hapa, lakini ninataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba, nitatoa majibu baadaye kuelezea kilichotokea na barua hizo kama mnazo ninaomba mnipatie ili nishuke naye huyo. (Makofi) MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika Halmashauri za Wilaya siyo mahali pekee ambapo Wabunge wa Viti Maalum wamekuwa wanatengwa; na kwa kuwa katika Bodi za Barabara za Mikoa, Wabunge Wanawake wa Viti Maalum nao wamekuwa wanatengwa na siyo Wajumbe wa Bodi za Barabara za Mikoa; na kwa sababu Mheshimiwa Waziri amesema yuko tayari kusikiliza na kufikiria uwezekano wa kufanya mabadiliko ya msingi katika Sheria ili kutokuwabagua Wanawake katika uwakilishi wao; je, Mheshimiwa Waziri haoni kuwa hili jambo ni vizuri likaingizwa katika mpango huo? SPIKA: Sisi kwetu huwa wanahudhuria; sijui wapi huko? Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Freeman Mbowe, jirani yangu, Mbunge wa Hai na pia Kiongozi wa Upinzani hapa Bungeni, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, unajua katika ulimwengu wa leo, kusimama hapa halafu ukasema kwamba, Wanawake wabaguliwe, utapata mgogoro ambao haujawahi kuuona hapa duniani. (Kicheko) Nikisema ninajibu kwa niaba ya Serikali hapa kwamba, unajua Wanawake wawekeni pembeni msiwachukue na nini nitakuwa sieleweki. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anasifika kwa kuwapa Wanawake nafasi nyingi katika Serikali hii, ndiyo sifa yake kubwa sana na sote tunafahamu. (Makofi) Kwa hiyo, mimi niseme hapa kwamba, kwa kuwa hili ni jambo la kutafakari na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani anasema kubaguliwa, wapo wengine ambao wanawaingiza. Sasa tutakwenda kuangalia hiyo busara ambayo inaruhusu hao wengine waingie kule na wengine wabaguliwe, yote kwa pamoja tutayatafakari kama nilivyosema, tutaangalia kwa pamoja. 4 SPIKA: Ninaona Waziri anataka kuongea, maana hayo matatizo yako chini yake. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanza, ninamshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa majibu mazuri. Bodi za Barabara za Mikoani zinatawaliwa na Sheria Na. 13 ya Mwaka 2007, ambayo ndiyo inazungumzia juu ya Road Act. Wajumbe wote wa Bodi ya Barabara huwa wanateuliwa na Waziri wa Ujenzi. Ninataka kumthibitishia Mheshimiwa Mbunge aliyeuliza swali kwamba, Wajumbe wote wanaoleta majina wakiwemo Wabunge Wanawake, huwa ninawateua kwa ajili ya kuwa Wajumbe wa Bodi ya Barabara. Kwa hiyo, hiyo Sheria haibagui na tutaendelea
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages118 Page
-
File Size-