Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Tano - Tarehe 4 Novemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Gaudence Kayombo, kwa niaba yake naona Mheshimiwa Mwambalaswa unaweza kumwulizia! Na. 53 Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga Kuwa Mamlaka Kamili MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuza:- Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga umekamilisha vigezo vyote kuwa Mamlaka kamili ya Mji:- Je, ni lini Serikali itaridhia na kutekeleza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gaudence C. Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki, kama ifuatavyo:- 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI)] Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, mwaka 2010, Mheshimiwa Rais, aliahidi kupandisha hadhi Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga kuwa Halmashauri ya Mji. Ahadi hii ilitokana na ukweli kwamba, Mamlaka hii imeonekana kukua kwa kasi, kwa maana ya ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi na kijamii na hivyo Serikali inaona ipo haja ya kuipandisha hadhi ili kuingiza dhana ya Mpango Miji kwa lengo la kuzuia ukuaji holela, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma za jamii. Mheshimiwa Spika, hata hivyo, mchakato wa kuupandisha hadhi Mji wa Mbinga bado unaendelea na ofisi yangu bado haijapokea maombi kutoka Mkoa wa Ruvuma. Tunamwomba Mheshimiwa Mbunge, ashirikiane na Uongozi wa Mkoa ili kuharakisha mchakato wa kuupandisha hadhi Mji wa Mbinga. (Makofi) MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Pamoja na hayo nina swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga, inafanana kabisa na Mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongorosi Wilayani Chunya, ambayo nayo upo katika mchakato wa kuwa Mji Mdogo kamili, kufuatana na ahadi za Mheshimiwa Rais:- Je, ni lini Serikali itakamilisha kuipa Mamlaka kamili Mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongorosi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Victor Mwambalaswa, kama ifuatavyo:- Mchakato wa kufanya Mji wowote kuwa Halmashauri ya Mji au kugawanywa kwa Wilaya au Kata, kwa kiasi kikubwa kunategemea Mamlaka za Serikali za Mitaa zenyewe, Halmashauri, Mkoa pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa hiyo, kwa sasa hivi sina nafasi ya kuweza 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI)] kusema ni lini, kwa sababu bado mchakato huo katika ngazi ya Mkoa wa Mbeya haujakamilika na kuletwa katika Ofisi yetu. MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza kama ifuatavyo:- Kwa kuwa pia katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo katika Tarafa ya Sasawara, Kata ya Lusewa, tuliomba Mji Mdogo Serikalini. Vigezo vyote tumeshatimiza na maombi hayo yapo katika Ofisi ya TAMISEMI:- Je, Serikali imefikia wapi kutamka rasmi mamlaka ya Mji Mdogo Kata ya Lusewa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vita Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Napenda nimhakikishie kwamba, litakapokuwa tayari suala lake tutalishughulikia, lakini mpaka ninavyozungumza, suala linalohusu Mji wa Lusewa halijafika mezani kwangu. Kwa hiyo sina uhakika kama kweli lilishatoka katika Mkoa wake. Ninachomwomba, tukitoka tuwasiliane ili tuone na tuweze kujua limefikia wapi au limekwama wapi. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tuendelee, kwanza miji inazidi kuongezeka. Sasa twende kwa Mheshimwia Moses Machali, swali linalofuata. MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibiwa kwa swali langu, ningependa niwafahamishe Wananchi pamoja na Waheshimiwa Wabunge, juu ya hali ya Mheshimiwa Dkt. Mvungi; ni kwamba, nimetaarifiwa na Mheshimiwa Mbatia, ambaye yuko Hospitali ya Muhimbili kuwa, anaendelea vizuri na Madaktari wanajitahidi kuweza 3 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. M. J. MACHALI] kupigania afya yake. Kwa hiyo, waondoe wasiwasi, naamini atapona. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya mafupi, naomba swali langu namba 54 lipatiwe majibu. Ahsante. Na. 54 Uhitaji wa Watumishi Katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu MHE. MOSES J. MACHALI aliuliza:- Wastani wa Watumishi wa Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu ni 600 lakini kwa mujibu wa Taarifa ya DMO watumishi waliopo sasa ni 186 ambao ni wachache sana:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza watumishi kwenye Hospitali hiyo? SPIKA: Pamoja na taarifa nzuri, lakini siyo utaratibu. Mheshimiwa Waziri wa Nchi, majibu! WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Moses J. Machali, Mbunge wa Kasulu Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua upungufu wa Watumishi wa Sekta ya Afya Nchini. Hivyo basi, iliona ni vyema kuwa na mkakati maalum wa kuajiri wahitimu wote wanaomaliza Vyuo Vikuu vya Afya. Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kwa sasa ina jumla ya watumishi 359 wa kada mbalimbali za afya, wakiwemo Madaktari na Wauguzi, ambao wanatoa huduma za afya kwenye Wilaya ya Kasulu. Hospitali ya Wilaya ina watumishi 206, Vituo vya Afya vina 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI)] jumla ya watumishi 52 na Zahanati zina jumla ya watumishi 101. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa watumishi wa kada za afya, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/13, Serikali ilitoa kibali cha kuajiri watumishi 41 wa Sekta ya Afya, ambapo hadi mwezi Oktoba, 2013 jumla ya watumishi 28 wa kada za afya wamesharipoti katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu. Mheshimiwa Spika, Serikali inao mkakati wa kuhakikisha kuwa inadahili wanafunzi wengi katika Vyuo vya Afya pamoja na kuwalipia wanafunzi hao kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Aidha, Serikali huwapanga watumishi wote wa Sekta ya Afya moja kwa moja katika Halmashauri kadiri wanavyohitimu mafunzo katika vyuo. Serikali itaendelea kuajiri wataalamu mbalimbali wa kada za afya kadiri watakavyokuwa wakihitimu mafunzo na kufaulu ili kuondokana na upungufu mkubwa wa kada hiyo muhimu. MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza:- (i) Kwa kuwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu inaonekana tuna-shortage kubwa sana ya Madaktari hasa Medical Doctors, walikuwa wawili lakini wengine wamepelekwa kwenye Wilaya Mpya; na kwa kuwa madaktari walioko pale wakati mwingine wanaacha kuomba madaktari wa kutosha kutoka katika Wizara ya Afya kwa lengo la kutaka kulinda nafasi zao. Je, Serikali itakuwa tayari kutupatia Madaktari wa kutosha ikiwa kama ni ombi maalum ili kuweza kuziba pengo lililopo hivi sasa? (ii) Katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu zipo changamoto nyingi kama ukosefu wa madawa wakati mwingine na hii inatokana na uzembe na vitendo vya wizi wakati mwingine; vimetokea na vingine tumeweza kudhihirisha. Wakati wa Bunge la Bajeti, niliomba special 5 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. M. J. MACHALI] audit ya kuja kufanya ukaguzi kwenye Hospitali ya Wilaya, lakini ahadi zilitolewa kwamba, watafanya na hakuna ambacho kimefanyika mpaka leo hii, gharama za matibabu zimepandishwa. Je, Serikali itakuwa tayari kupitia Wizara ya TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya, kuweza kutupatia ile timu ambayo niliomba hapa Bungeni na mkaahidi kwamba mtaleta ili twende tukafanye special audit? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Machali, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, suala la kwanza kwamba, madaktari hawaombi madaktari wenzao kwa kulinda vyeo vyao, sidhani kwa sababu uchache ule unawaongezea wao mzigo mkubwa wa kufanya kazi. Katika hali ya kawaida, sidhani kama kuna daktari ambaye angependa afanye kazi za madaktari sita peke yake; kwa sababu bado atapokea mshahara mmoja na bado marupurupu yake yatabaki vilevile, hawezi kupokea ya madaktari ambao hawapo. Mheshimiwa Spika, hata hivyo, suala la kuomba ikama siyo la madaktari wenyewe ni la Halmashauri. Napenda nikuhahakikishie kwamba, Wizara ya Afya na TAMISEMI, wote tunashiriki katika kuhakikisha kwamba, tunapeleka watumishi katika Halmashauri kwa mujibu wa ikama na kwa jinsi wanavyopatikana katika soko la ajira. Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Special Audit, sasa hivi ipo timu kule Kasulu ambayo inafuatilia masuala mbalimbali ya matumizi ya fedha na matumizi ya madaraka katika Mji wa Kasulu. MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. 6 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. M. S. KAKOSO] Kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda imegawanywa na kutoka Halmashauri ya Wilaya Nsimbo na Halmashauri ya Mji Mpya wa Mlele; na wote hao wamekuwa wakichukua wafanyakazi kutoka Halmashauri Mama ya Wilaya ya Mpanda na kufanya tatizo kuwa kubwa sana la ukosefu wa Madaktari katika Halmashauri ya Wilaya:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuleta watumishi wa kada ya afya kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mpanda sambamba na Vituo vya Afya ambavyo kimsingi katika maeneo yote hata yaliyogawanywa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages263 Page
-
File Size-