Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Nne – Tarehe 9 Mei, 2014 (Mkutano Uianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA) PAMOJA NA (UTAWALA BORA): Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) pamoja na (Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU): Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. JAKU HASHIM AYOUB (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Taarifa ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), (Utawala Bora) pamoja na (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na maoni 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA), (UTAWALA BORA) PAMOJA NA (MAHUSIANO NA UTARATIBU):- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), (Utawala Bora) pamoja na (Mahusiano na Uratibu) kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza Maswali na Ofisi ya Waziri Mkuu. Na. 25 Mgogoro wa Ardhi Kijiji cha Katapulo na Ranchi ya Kalambo MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa Kijiji cha Katapulo na Ranchi ya Kalambo ni wa muda mrefu ambapo wananchi wanalalamikia mipaka kutokuwa sahihi na kutokupewa fidia wakati ardhi yao inachukuliwa tofauti na majirani zao wa Vijiji vya Mbuluma na Mao:- (a) Je, Serikali itamaliza lini mgogoro huo? (b) Je, Serikali inasemaje kuhusu matumizi ya ardhi kwa ambaye hatumii eneo hilo kwa shabaha iliyokusudiwa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo, lenye sehemu (a) na (b), kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna mgogoro kati ya wananchi wa Kijiji cha Katapulo na Ranchi ya Kalambo. Ranchi hii ilianzishwa mwaka 1972 kwa ajili ya shughuli za ufugai wa ng‟ombe. Kiini cha malamiko ya wananchi wa Kijiji cha Katapulo dhidi ya ranchi hii ni kutoeleweka kwa mipaka kati ya Kijijii hicho na Ranchi ya Kalambo ambapo wananchi wanaamini kwamba eneo la ardhi ya Kijiji lilichukuliwa na ranchi hiyo. Aidha, sababu ya pili ya mgogoro huu ni 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) malalamiko ya wananchi kwamba ranchi hiyo haitumiki kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuzingatia dhumuni la kuanzishwa kwake. Migogoro ya ardhi kwa kuhusisha matabaka mbalimbali nchini mfano wakulima na wafugaji ama wananchi na wawekezaji ni mingi sana. Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kwa kutambua ukubwa wa tatizo hili, iliwaandikia barua Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara ikiwataka kuunda Tume ya kuchunguza vyanzo vya migogoro na hatua zilizochukuliwa kutatua ama kutoa mapendekezo ya kutatua migogoro hiyo. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI imepokea taarifa za migogoro ya Mikoa yote ukiwemo mgogoro kati ya wananchi wa Kiiji cha Katapulo na Ranchi ya Kalambo katika Mkoa wa Rukwa. Kwa mujibu wa taarifa ya Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, imebainika kuwa kuna tatizo baina ya wananchi wa kijiji cha Katapulo na Ranchi ya Kalambo. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, imefanya mawasiliano na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambaye ameeleza kwamba amekwishatoa maelekezo kwa kampuni ya Ranchi ya Taifa kufanya tathmini kwa ajili ya kuainisha maeneo yote ya Ranchi za Taifa ambayo hayatumiki ipasavyo na kuwasilisha taarifa Wizarani kwake ili Serikali iweze kufanya maamuzi sahihi ya matumizi ya maeneo hayo. Mheshiiwa Spika, ni matumaini yetu kwamba baada ya zoezi hili kukamilika migogoro na matatizo yote yanayofanana kwenye maeneo mbalimbali katika ranchi hizi nchini yatapatiwa ufumbuzi. MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ambayo sina uhakika kama ni mazuri sana, kwa sababu tatizo hili nililibainisha tangu mwaka 2011 na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Mifugo aliahidi kwamba angelimaliza. Sasa kwa bahati mbaya sana limeenda tena Wizara nyingine lakini ninaamini Serikali ni hiyohiyo. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa lalamiko la wananchi ni pamoja na ardhi yao kuchukuliwa bila kupewa fidia yoyote, Serikali iko tayari kuhakikisha kwamba wananchi wale wanapewa fidia ambayo wanalalamikia? Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hata huyo ambaye amepangishiwa hilo eneo ambalo wananchi hawakupewa fidia, halitumii kwa matakwa yaliyokusudiwa. Je, Serikali iko tayari kuwarudishia wananchi eneo hilo ili waweze kulitumia kwa ajili ya kilimo? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, huko Kalambo anakokuzungumza Mheshimiwa Kandege, tumekwenda naye na Marehemu Chan‟ga, anajua 3 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) tumeliona hili tatizo na tumelizungumzia na yeye mwenyewe anafahamu kwamba tumeliona. Ninaelewa kwamba Mheshimiwa Mbunge anazungumza jambo ambalo ni very sensitive, linagusa mioyo ya wananchi wake na ninajua kuna Wabunge wengi sana ambao wanakumbwa na hali hii tunayoizungumza hapa. Mheshimiwa Spika, nime-quote hapa, nikasema kwamba tumewaandikia Wakuu wa Mikoa ambao wako hapa na wanasikia, nchi nzima tukiwataka watueleze status ya matatizo ya aina hii katika Mikoa yao na solution ambayo wameipata. Wiki mbili zilizopita, Mheshimiwa Waziri Mkuu alituagiza, Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Maliasili, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Mifugo, wote tukutane ili tuweze kuzungumzia jambo hili. Haya yote ndiyo tunayojibu hapa na baadaye amesema anataka aitishe kikao cha wadau wote ili tuweze kuzungumzia jambo hili kwa zaidi. Sisi wote tukiangalia kwenye TV tunaona jambo hili linafanyika hapa. Mheshimiwa Spika, nataka nimwambie Mheshimiwa Kandege kwa swali hili analoliuliza hapa, jana tarehe 8 Mei, 2014 yumo humu ndani na Mheshimiwa Kamani ambaye ni Waziri, tumezungumza nao, tumefanya tele-conferencing kuhusu jambo hili. Niko conscious kwamba jambo linalozungumzwa hapa ni sensitive, siyo jambo tu la kusema nijibu tu ninavyofikiri. Mheshimiwa Spika, nataka kusema hivi, hawa wananchi anaowasema kwamba wao wanadai kwamba eneo hili ni la kwao, so far hatujawezi ku- establish kwamba ni kweli eneo lao lilichukuliwa. Kama nilivyoeleza hapa tunataka sasa tujue, je, ni kweli kwamba eneo ni lao au walikuwa wanatumia eneo hili sasa wanaona hawalitumii tena kwa sababu kuna National Reserves ziko pale. Mheshimiwa Spika, tunachoweza kusema hapa kwa kifupi, kuhusu suala la wale wengine anaosema kwamba walifidiwa, nime-check na Mkuu Mkoa, nikamuuliza je, kuna wananchi ambao wamewahi kufidiwa katika maeneo hayo? She was not clear on that. Ninataka niseme zoezi hili linaendelea. Mheshimiwa Kandege na Mheshimiwa Waziri Mkuu ametuagiza wote tutakutana, tutakaa tutazungumzia jambo hili. Suala analolizungumza Mheshimiwa Kandege kama hawa wananchi wanastahili fidia au hawastahili litazungumzwa katika vikao hivi. Mheshimiwa Spika, la mwisho, ni kuhusu maeneo haya ambayo yanaonekana kwamba hayatumiki kama yalivyokusudiwa. A Member of Parliament anazungumza jambo la msingi sana hapa. Kama mtu amepewa ranchi haitumii, imekaa tu, yako mawazo hayo ya kuzichukua lakini wale wanaomiliki hizi ranchi wanamiliki kisheria. Sasa nikisema hapa kuanzia leo watu 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) wote ambao hawatumii ranchi wananchi wachukue maeneo hayo, watu wataniambia umeipata wapi hiyo? Mheshimiwa Spika, ninachojibu hapa ni kwamba kikao kile ambacho Mheshimiwa Waziri Mkuu amekizungumzia tutakapokaa haya yote anayoyazungumza Mheshimiwa Kandege, yatazungumzwa. Ninajibu hivi ili uwazuie wale wengine wanaotaka kuniuliza maswali kuhusu jambo hili wajue kwamba kuna hilo jambo ambalo tunataka tulizungumze. (Kicheko) SPIKA: Ni kweli tunaendelea na Ofisi ya Makmu wa Rais (Mazingira), majibu yalikuwa marefu. Na. 26 Majanga Yatokanayo na Mabaki ya Taka za Sumu MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO aliuliza:- Dunia inakabiliwa na tishio la majanga makubwa yatokanayo na mabaki ya taka za sumu kutoka viwandani: (a) Je, Serikali inajiandaa viipi kukabiliana na tatizo hilo? (b) Je, nchi zinazoendelea zinapewa ushauri gani ili zisigeuzwe dampo la taka? NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kombo Khamis Kombo, Mbunge wa Mgogoni, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali inakabiliana na changamoto ya udhibiti wa taka sumu kwa kutekeleza Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake za Usimamizi wa Taka Ngumu na Usimamizi wa Taka Sumu na Hatarishi za mwaka 2009. Sheria na Kanuni hizi zimeweka taratibu za kudhibiti ukusanyaji, usafirishaji na utupaji salama wa taka za sumu na hatarishi. (b) Mheshimiwa Spika, Tanzania ni mwanachama wa Mkataba wa Basel unaohusu udhibiti wa usafirishaji wa Taka
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages299 Page
-
File Size-