CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, KAPENGURIA CONSTITUENCY MTELO SOCIAL HALL ON Wednesday, 26TH JUNE 2002 CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, KAPENGURIA CONSTITUENCY, HELD AT MTELO MUNICIPAL HALL ON WEDNESDAY 26th JUNE 2002 Present: Com. Idha Salim - Chairing Com. Prof. Wanjiku Kabira Secretariat Staff in Attendance: Irene Marsit - Programme Officer Geoffrey Imende - Assistant Programme Officer Josephine Ndung’u - Verbatim Recorder District Co-ordinator: Ikiwa umejiandikisha tafadhali usiende mbali. Njoo hapa ndani ukaketi, ili uweze kufuatana na wengine. Please do not register and leave. Come, we shall be calling you, according to your registration. Tafadhali ukijiandikisha njoo hapa dani. Tutafuata jinsi mliovyo jiandikisha. Wale ambao wanafika wakati huu tafadhali jiandikishe pale mlangoni. Wale ambao wanawasili muda ungali kuanzia sasa hadi jioni. Nafasi yenu ndiyo hii. Tafadhali fikeni hapa na mjiandikishe pale mlangoni halafu mketi hapa ili tuweze kuwapata. Please register, come and sit here so that we may call you according to your registration. Tafadhali. (Vernacular dialect) Tafadhali fikeni. Na wale ambao wangependa kuja muingie ndani mtasikia maoni ikitolewa. Tafadhali viti viko vingi. Come in please. Kujeni kutoka huko nje makasikize jinsi maoni itatolewa. Interjection: (inaudible) District Co-ordinator: Tafadhali ukijiandikisha ingia ndani. Usiondoke kwa sababu vile mlivyo jiandikishe 2 ndivyo mtakavyo ingia hapa ndani kutoa maoni. Na wale wengine ingieni dani, ili muweze kurahisisha kazi. Kama umejiandikisha ingia ndani. Com. Salim: Habari za asubuhi? Sisi kama mlivyo hisi wenyewe ni wanatume wa tume ya kurebisha Katiba. Tumefika hapa hivi leo, hapa Kapenguria kuanza kupokea maoni ya wenyeji wa hapa. Na tumefurahi sana kuwa tumepata nafasi hii ya kuja kwenu hapa, kuwajua na kuwasikiza na kuelezena na nyinyi jambo hili muhimu sana. Kwanza kabisa, tungeanza sote kwa maombi. Tumuombe Mwenyezi Mungu kwamba kazi yetu hii ya leo hapa itaendelea vizuri; na kazi ya kurekebisha Katiba kwa jumla itaendelea vizuri kisha tuendelee mbele. Kwa hivyo ningeomba Bwana District Co-ordinator wetu amuite mtu wa dini, atuombee. District Co-ordinator: (Prayer) Basi wale ambao mnaingia tafadhali muingie ili tuweze kufungua hiki kikao kwa maombi. Natuiname: Baba Mwenyezi Mungu tunakuja mbele yako asubuhi ya leo, tunasema asante kuwa wewe una upendo. Bwana umependekeza tangu wewe kikao hiki tulianza kufundisha wananchi na kwa wakati huu Baba Mwenyezi Mungu, Baba wanapoketi kupokea maoni, naikabithi mkononi mwako, macommissioners na wote ambao watatoa maoni yao na wale wote wangetaka kuchangia kwa namna hii na ile. Baba Mwenyesi Mungu na wakabithi wale wote ambao wangali wako njiani wanakuja Baba, chukua nafasi hii kati yetu ili tuweze kutoa maoni yetu kwa upendo wako. Ninaomba nikiamini katika jina la Yesu Kristu na Mkombozi wetu. Amen. Com. Salim: Asante sana kwa maombi hayo. Sasa tungependa kuanza pia kwa kujijulisha. Sisi tumetoka kwenye tume ya kurekebisha Katiba. Hapa ninaye mwenzangu, Commissioner Professor Wanjiku Kabira. Mimi mwenyewe pia ni mwanatume au Commissioner ninaitwa Ahmed Idha Salim. Tunao pia mwenzetu, District Co-ordinator ambao nafikiri mwamjua Robert Katina, na pia tuna staff wetu ambao kazi yao ni muhimu sana, kuhakikisha kwamba kila neno linalosemwa hapa litaandikwa kama upeanavyo wanaandikia. Upande huo, sisi wenyewe tutaandika yanayosemwa na maoni yenu. Pia mnaona kuna microphones hapa, microphones zimeshikanishwa na mashini huko. Kwa hivyo, maneno yeny na maoni yenu pia yanapaswa katika mitambo yetu. Pia kuhakikisha kwamba hakuna maoni yeyote ambao yatapotea katika hewa. Na baadaye tukirudni tutasikiza tapes zetu zote na tutaandika kwa mkono kwenye mashini ili maoni yote yatasikizwa na kuchunguliwa na kufikiriwa katika kuandika Katiba. Kwa hivyo hawa wenzetu pia waliotoka kule tume tunaye kule, Josephine ambaye ana record kila neno na hapa kuna Geoffrey, pia anafanya kazi hiyo hiyo. Na pia tuna Programme Officer ambaye kazi yake ni kuunganisha kazi zetu sote, ambaye ni Irene Marsit. Nafikiri mmemuona hapa akiingia na akitoka. Basi hii ndio tume yetu. Tumefurahi sana kama mlivyo kuja hapa. Hii ni kazi muhimu sana kwetu sisi tunaoishi hapa Kenya. Pia, watoto wetu na wajukuu wetu hapo mbeleni. Kwa hivyo, maoni yenu, ni muhimu sana. Kila tukipata maoni mengi ndio bora zaidi. Na ishara tulio ona, ni kwamba, kutakuwa na watu wengi hapa hivi leo. Kwa hivyo, twawakaribisha 3 kuja na tutawasikiza wote ambao wamejiandikisha. Lakini hatujui idadi ya watu ambao watafika. Kwa hivyo, itabidi kuzingatia wakati. Tunasiku moja tu leo. Tutaanza kwa kumpa kila mtu dakika kumi ambao ataka kutoa maoni yake kimdomo. Dakika kumu tu maximum. Hiyo ndiyo kipimo cha juu kabisa. Lakini ukiwa na maoni ambayo haitafikia dakika kumi, si lazima utumie dakika kumi zote. Utumie ile time ambayo unataka, ili kumpisha mwenzako naye apate nafasi kutoa maoni yake. Ikiwa mmoja wenu ameandika maoni yake. Amekuja na mswada au memorandum, tayari maneno yake yameandikwa, huyo tutampa dakika tano tu. Maana tutachukuwa memorandum yake, na kusoma huko mbeleni tukifika. Kwa hivyo, huyo tutampa dakika tano na dakika tano hizo, asizitumie kusoma aliyo andika, la, atatumia dakika tano hizo ili kutueleza pointi ziliomo katika memorandum yake. Kwa hivyo, tafadhalini, mtupe maoni ambayo ni mapendekezo kuliko kuwa ni maelezo. Sote ni Wakenya. Sote tunajua matatizo ya nchi yetu. Sote tunajua mambo yalioko hapa nchini ya kisiasa, ya kiuchumi, ya utibabu, ya health na ya kielimu. Sio? Kwa hivyo ukiwa na maoni juu ya mambo haya, usiyaelezee ile shida ilioko kwa urefu sana. Eleza, jamani kuna shida hii katika hospitali zetu. Hatuna madawa. Mimi ningependekeza hili na hili lifanywe. Kisha uende kwenye pointi ya pili. Katika eneo ya elimu, mimi ningependekeza hii. Endelea pointi ya tatu, na kadhalika. Kwa jia hii itakuwa ni rahisi sisi kufahamu maoni yako badala ya kueleza kwa urefu sana. Maana ukiyaeleza kwa urefu sana shida tuseme ya elimu peke yake, itachukuwa dakika kumi. Sio? Tunasijua sisi shida. Sema wewe ungependa jambo gani lifanywe katika eneo la elimu. Kwa mfano, huku kwingine tumeambiwa sisi elimu wazazi wanataabu ya pesa, ya karo, tungependa karo ipunguzwe, au karo iondolewe kabisa. Kwa hivyo, toa pendekezo lako juu ya elimu vile unavyoona wewe kwamba tatizo hilo litashafishwa. Na hayo kwa ufupi ambayo ningependa kueleza. Pia, kama nilivyosema, dakika tano ukiwa una memorandum, kumi maximum. Ukiwa unataka kutoa maoni yako kimdomo. Pia unaweza tumia lugha yeyote ikiwa unataka kusema Kiingereza, Kiswahili, utasema, lugha ya Kipokot, ukitaka kusema au lugha yeyote ya kienyeji. Tutatafuta mtu ambaye atatutafsiria sisi lugha ambayo itahitajika kutafsiriwa. Na ukija hapa mbele, jambo la kwanza kabisa kufanya ni kusema mimi ni furani, jina langu ni furani. Ili kwamba kisha tukurundi kusikiza zile tapes, tunajua sasa tunamsikiza mtu fulani akitoa maoni yake. Anza kabisa na jina, kisha uanze na maoni na kama nilivyosema, maoni yawe ni points. Point after point. Kwa njia hii, itakuwa wazi kabisa kujua unapendelea jambo gani lifanywe. Kwa hayo, tuseme tuanzeni kwa jina la Mwenyezi Mungu na baraka zake. Huyu ni Bwana District Co-ordinator niliowatajia kwa jina anaitwa Robert Katina. Robert Katina (District Co-ordinator): Professor Idha Salim na Professor Wanjiku Kabira, Commissioners wa tume hii ya kurekebisha Katiba, wageni wetu, Programme Officers kutoka Nairobi, Wazee na Wamama, hamjamboni? Asubuhi ya leo nafurahi sana kuwaona na bila kupoteza wakati ningewaambia mmekaribishwa sana hapa, kama 4 District co-ordinator na waambia hiyo mlango ni wazi, na muwe huru kabisa kutoa maoni yenu. Huu ndiyo wakati tumekuwa tukiungojea kwa muda mrefu sana. Mtu yeyote kutoka tabaka lolote, kabila lolote, area yeyote, ana uhuru wa kutoa maoni yake. Waweza kutoa maoni kwa niaba yako mwenyewe ama kwa niamba ya community yako ama organisation yako, uko uhuru kabisa. Kwa hivyo, jisikie huru na uje mbele na kutoa maoni yako. So ningependa ku-clarify hiyo msiseme labada tumekubalia wale ama kabila lingine ama nini, hapana. Hapa ni open forum na mtu yeyote anakubaliwa. Asante sana. Com. Idha Salim: Asante sana Bwana Katina kwa maelezo hayo muhimu sana. Sasa ningependa kumuita mwenzetu wa kwanza kabisa kutoa maoni yake. Yeye ni Reverend Jack Mila ambaye ni Pastor. Anataka kutoa maoni yake kwa mdomo na pia ana memorandum. Bwana Reverend, tafadhali ukiwa na memorandum tupe mapendekezo yako katika memorandum, na jaribu usisome tafadhali maanake itachukuwa wakati. Baadaye, tutaisoma. Tumekuhakikishia ya kwamba itasomwa kikamilifu. Jack Mila: I will speak in English. I am Reverend Jack Mila from Bethel Christian Centre. I am very happy this morning to be before the commissioners and my fellow citizens. I want to give my views on the freedom of worship especially in this country because I am a pastor; and I believe I am in the right place to talk about the freedom of worship. and also I ill touch on the religion. Just like all of us know that the current Constitution states that there is freedom of worship in Kenya, this freedom of worship in our current Constitution has brought with it very dangerous religions which have cost many Kenyans their lives. The Government has no machinery to eradicate devil worshipping since the current Constitution does not define the freedom of worship it talks about. Since the Constitution of any country should potray the picture of a country or of any nation, I therefore suggest that the next Constitution
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages111 Page
-
File Size-