Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 18 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita muuliza swali la kwanza nina matangazo kuhusu wageni, kwanza wale vijana wanafunzi kutoka shule ya sekondari, naona tangazo halisomeki vizuri, naomba tu wanafunzi na walimu msimame ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuwatambua. Tunafurahi sana walimu na wanafunzi wa shule zetu za hapa nchini Tanzania mnapokuja hapa Bungeni kujionea wenyewe demokrasia ya nchi yetu inavyofanya kazi. Karibuni sana. Wapo Makatibu 26 wa UWT, ambao wamekuja kwenye Semina ya Utetezi na Ushawishi kwa Harakati za Wanawake inayofanyika Dodoma CCT wale pale mkono wangu wakulia karibuni sana kina mama tunawatakia mema katika semina yenu, ili ilete mafanikio na ipige hatua mbele katika kumkomboa mwanamke wa Tanzania, ahsanteni sana. Hawa ni wageni ambao tumetaarifiwa na Mheshimiwa Shamsa Selengia Mwangunga, Naibu Waziri wa Maji. Wageni wengine nitawatamka kadri nitakavyopata taarifa, kwa sababu wamechelewa kuleta taarifa. Na. 223 Barabara Toka KIA – Mererani MHE. DORA H. MUSHI aliuliza:- Kwa kuwa, Mererani ni Controlled Area na ipo kwenye mpango wa Special Economic Zone na kwa kuwa Tanzanite ni madini pekee duniani yanayochimbwa huko Mererani na inajulikana kote ulimwenguni kutokana na madini hayo, lakini barabara inayotoka KIA kwenda Mererani ni mbaya sana na kwa kuwa, Waheshimiwa Marais wa 1 Awamu ya Tatu na Nne waliwaahidi wananchi wa Mererani kuwa barabara ya kutoka KIA kwenda mererani itatengenezwa kwa kiwango cha lami:- (a) Je, Serikali haioni kuwa huu ni wakati muafaka wa kutengeneza barabara hiyo kwa kiwago cha lami ili kurahisisha mawasiliano na usafirishaji? (b) Je, Serikali inasema nini juu ya suala hili? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dora Mushi, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba Tanzanite ni madini pekee duniani yanayochimbwa huko Mererani kama ambavyo taarifa nyingi zimekuwa zikieleza. Aidha ni kweli kuwa Serikali imeingiza eneo la Mererani kwenye mpango wa Specila Economic Zone. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nakubaliana pia na Mheshimiwa Mbunge kuwa iko barabara ya kutoka KIA hadi Mererani yenye urefu wa Km. 18. Barabara hiyo inaunganisha Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Km. 13, na Wilaya Simanjiro Mkoani Manyara km. 5. Sehemu ya barabara hiyo kuanzia KIA hadi machimbo ya madini ya Tanzanite ya Kampuni ya Tanzanite One (Km.13) iko katika Wilaya ya Arumeru na imekuwa ikihudumiwa na kutengenezwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Tanzanite One kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru na hivyo kupitika kwa wakati wote. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/2007 Halmashauri ya Arumeru itatoa kipaumbele kutengeneza barabara hiyo ili ipitike kwa kutumia fedha za ruzuku isiyokuwa na masharti kutoka Serikali Kuu. Suala la kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami hivi sasa halipo kwa sababu ya ufinyu wa Bajeti uliopo. Mheshimiwa Spika, Km 5 katika barabara hii ziko upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro. Barabara hii imekuwa ikifanyiwa matengenezo ya kawaida ili iweze kupitika wakati wote na Kampuni ya Tanzania One. Kwa mwaka 2006/2007 Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya matengenezo ya kawaida. Hata hivyo Kampuni ya Madini ya Tanzanite One imeahidi kuendelea kutengeneza barabara hiyo ili iweze kupitika kwa mwaka mzima. MHE. DORAH H. MUSHI: Mheshimiwa Naibu Waziri, ahsante sana kwa majibu yako mazuri swali langu la nyongeza ni kwamba, tangu Mererani ipewe baraka ya kuwa mji mdogo, sioni ni kwanini Serikali isichukue jukumu la kuweka miundombinu mizuri kwa mafuaa ya wananchi wa Mererani na wachimbaji kwa ujumla? 2 SPIKA: Kabla Mheshimiwa Naibu Waziri hajajibu namkumbusha Mheshimiwa Mbunge kwamba unaongea na Spika, huongei moja kwa moja na Naibu Waziri. Usiseme Mheshimiwa Naibu Waziri, yeye anajibu tu, Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, ni nia ya Serikali kutengeneza mji mdogo wa Simanjiro kwa miundombinu yote na hasa barabara ndiyo maana katika jibu langu la msingi nimesema kwamba barabara hiyo ilikuwa na inaendelea kutengenezwa kwa kiwango cha kupitika kwa mwaka mzima. Ni nia ya Serikali kwamba miundombinu yote ikiwa ni pamoja na maji, barabara zahanati na kadhalika. Hii ni katika azma ya kuidumisha miji hiyo ya Simanjiro na miji mingine ambayo inachimbwa madini. (Makofi) Na. 224 Tume za Kufuatilia Madai ya Watumishi MHE. ANNA R. LUPEMBE (K.n.y. MHE. PAUL P. KIMITI ) aliuliza:- Kwa kuwa kwa miaka mingi kumekuwepo na Kamati ya Tume za kufuatilia madai ya baadhi ya watumishi kama walimu, waganga na kadhalika:- (a) Je, kwa nini Serikali badala ya kila wakati kuunda Kamati kama hizo kwa ajili ya dharura kusiwe na utaratibu wa Kamati ya Kudumu ya Wabunge kufuatilia malalamiko ya aina zote? (b) Je, malalamiko ya watumishi wa Wizara nyeti kama Majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama yanashughulikiwa kwa njia ipi nyepesi kutokana na unyeti wa shughuli zao? (c) Je, madai ya watumishi waliostaafu kuhusiana na kuongezewa pension kwa kila mwezi yamefikia wapi na maombi hayo yanagharimu kiasi gani cha Bajeti ikiwa watapewa angalau kima cha chini cha mshahara wa mtumishi wa Serikali? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Paul Kimiti, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali yetu inaongozwa kwa mujibu wa Katiba inayotambua mgawanyo wa majukumu baina ya nguzo tatu za dola yaani – Bunge, Mahakama na Serikali. Jukumu la Serikali ni kutawala. Kutokana na msingi huo wa Katiba na kwa madhumuni ya kupata ushauri kwa matatizo ya dharura au maalum Serikali imekuwa ikiunda Tume mbalimbali kuishauri kuhusu masuala ya kiutawala na kuhusisha baadhi ya Wabunge wenye taaluma husika pale inapoonekana busara kufanya hivyo. (Makofi) 3 Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo huo wa mgawanyo wa madaraka, Bunge lako Tukufu ambalo ni chombo cha uwakilishi wa wananchi linao utaratibu wake wa kushughulikia matatizo mbalimbali nchini kwa kupitia Kamati zake mbalimbali za kudumu. Bunge pia linao uwezo kwa mujibu wa Kanuni zake, wa kutoa hoja/azimio Bungeni na kuamua kuhusu kuundwa kwa Tume kwa ajili ya kazi maalum. Mheshimiwa Spika, ili kuheshimu mgawanyo huu wa madarka, ni vizuri utaratibu unaotumika sasa ukaendelea. Aidha, ni vyema ikazingatiwa kuwa kuundwa kwa Kamati hizo hutokana na mahitaji maalum ya muda mfupi na haitarajiwi Kamati hizo kuchukua nafasi ya sehemu ya utawala Serikalini. (b) Mheshimiwa Spika, malalamiko ya watumishi wa Wizara nyeti kama Majeshi, hushughulikiwa kwa taratibu zilizowekwa ndani ya Majeshi husika. (c) Mheshimiwa Spika, takwimu za mwezi Mei 2006 zinaonyesha kuwa Serikali ina wastaafu 58,502 wanaolipwa pensheni ya wastani wa shilingi 29,177,490,930.66 kwa mwaka. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa wastaafu wanaolipwa pensheni iliyo chini ya kima cha chini cha mshahara wa mtumishi wa Serikali ni wastaafu 41,629 ambao wanalipwa pensheni ya wastani shilingi 13,728,170,327.20 kwa mwaka. Mheshimiwa Spika, endapo Serikali itaamua kupandisha pensheni za wastaafu sawa sawa na kima cha chini cha mshahara wa mtumishi wa Serikali, italazimka kulipa kiasi cha shilingi 32,470,620,000 ambacho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi 18,742,449,672.80 ambayo ni asilimia 136.5 kwa mwaka kwa kundi hilo. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kufanyia kazi madai yanayohusu kupandisha kima cha chini cha pensheni. Aidha kutokana na gharama kubwa za kupandisha viwango vya pensheni, Serikali pale uchumi unaporuhusu imekuwa ikihuisha kiwango cha chini cha pensheni hatua kwa hatua kwa lengo la hatimaye kulipa pensheni zinazozingatia angalau mshahara wa kiwango cha chini Serikalini. MHE. DR. CHRISANT M. MZINDAKAYA: Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia swali la msingi ningependa kuuliza swali lifuatalo, kwamba ni kweli na ni jambo zuri kila wakati kuweka Tume za kuchunguza, lakini kama watumishi wanaoutaratibu na kwa upande wa watumishi wanao utaratibu; na kwa upande wa watumishi tunafahamu pia kwamba kuna Tume yao inayoshughulikia maslahi yao. Je, isingekuwa jambo la busara kuliko kila wakati kuweka Tume hizi zinazoshughulikia mishahara na maslahi ya watumishi zikawa ndiyo wajibu wao kufanya kazi hizo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA: Mheshimiwa Spika, pensheni ya watumishi wa umma hutolewa kwa mujibu wa sheria zifuatazo:- 4 Kwanza ni Finance Bill, ambayo ipo chini ya Waziri wa Fedha na mara nyingi wao ndiyo wanaopanga kima cha chini cha pensheni, na pia inashughulikiwa na sheria ya hitimisho la kazi kwa watumishi wa umma. Na. 225 Gharama za Baraza la Mawaziri MHE. GRACE S. KIWELU aliuliza:- Kwa kuwa ni kweli kwamba ukumbwa wa Serikali haupimwi kwa gharama bali hupimwa kwa ufanisi, lakini ni vema Watanzania ambao ndio walipa kodi wa nchi hii wakajua gharama halisi ambazo Baraza la Mawaziri linatumia. (a) Je, ni kiasi gani cha fedha kinachotumika katika Baraza la Mawaziri katika mishahara na magari? (b) Je, ni kiasi gani kilichoongezeka ukilinganisha na Baraza lililopita? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA: alijibu:- Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu swali namba 50 la Mheshimiwa Kiwelu tarehe 13/2/2006, ni sahihi kabisa kwamba ukubwa wa Serikali yoyote duniani haupimwi kwa gharama bali hupimwa kwa ufanisi wa utendaji kazi ambayo ndiyo azma ya Serikali ya Awamu ya Nne. Muundo wa Serikali ya awamu ya nne umezingatia agenda na matakwa ya wananchi ya wakati tulionao hivi sasa. Agenda na matakwa ya kipindi hiki yameleta makujumu mapya na pia kuweka umuhimu wa juu katika baadhi ya majukumu yaliyopo ambayo muundo wa siku za nyuma usingeweza kuyatekeleza kwa ufanisi na tija, kama ambavyo imeanza kujionyesha katika hatua za awali za utendaji wa awamu hii.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages159 Page
-
File Size-