MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao Cha Ishirini Na Mbili

MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao Cha Ishirini Na Mbili

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Ishirini na Mbili – Tarehe 4 Mei, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:- Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. MWENYEKITI: Ahsante, Katibu. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Tunaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. David Mathayo. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 177 Ukosefu wa Waganga na Watumishi wa Afya - Same Magharibi MHE. VENANCE M. MWAMOTO (K.n.y. MHE. DKT. DAVID M. DAVID) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka waganga, watumishi wa afya pamoja na vitendea kazi katika zahanati za Same Magharibi zilizojengwa kwa ushirikiano wa wananchi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.David Mathayo, Mbunge wa Same Magharibi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua tatizo la upungufu wa watumishi wa sekta ya afya katika Jimbo la Same Magharibi, ambapo mahitaji ni watumishi 867 lakini waliopo ni 287, upungufu ni watumishi 585. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imepeleka watumishi wapya 10 wa sekta ya afya katika jimbo hilo. Katika mwaka wa fedha 2018/2019, Halmashauri ya Wilaya ya Same imeomba kibali cha kuajiri watumishi wapya 104 wa sekta ya afya ambao watapangwa katika vituo vyenye upungufu mkubwa wa watumishi. MWENYEKITI: Mheshimiwa Balozi Mwamoto. MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Kakunda, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, je, atakuwa tayari kufika katika Wilaya ya Same ili kwenda kuona hali ambayo ipo sasa hivi? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Wilaya ya Kilolo inajenga hospitali kubwa na nzuri, je, ni kiasi gani cha wahudumu au Madaktari wanaweza kuwatengea kwa msimu huu? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kifupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mwamoto na Mheshimiwa Dkt. Mathayo huko aliko kwamba nitafika Same baada tu ya Bunge la bajeti. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mwamoto kwa kufanya ufuatiliaji wa kina na wa karibu, katika kipindi cha miezi minne au mitano ameweza kufanikiwa na Serikali imepeleka pale zaidi ya shilingi bilioni nne kwa ajili ya kujenga hiyo hospitali ya wilaya na Mheshimiwa Rais juzi ameweka jiwe la msingi. Nimhakikishie tu kwamba tutashirikiana na wenzetu wa utumishi kuhakikisha hospitali ile inapata watumishi wa afya kwa mujibu wa kitange na uwezo wa Serikali. MWENYEKITI: Ahsante. Nimshukuru Mheshimiwa Waziri wa Nchi kwa majibu mafupi ya Serikali pamoja na maswali mafupi ya ziada, hongereni sana. Tunataka Bunge liende hivi, maswali mafupi na majibu mafupi. Mheshimiwa Mama Kilango na Mheshimiwa Mbatia. MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi hii. Kwa kweli wananchi wa Wilaya ya Same kwa ujumla wao wanajitahidi sana kujenga zahanati. Ningemwomba Mheshimiwa Waziri aone umuhimu wa Serikali kwenda kuona jitihada zile, naomba atuambie hapa ndani atakwenda lini na atatoa msaada gani kwa sababu hali ya wananchi hasa wa milimani upande wa afya ni mbaya sana? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri ni lini tu utakwenda? 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Anne Kilango Malecela na wananchi wote wa Wilaya ya Same kwamba nitakapokwenda katika Wilaya ya Same sitaishia katika Jimbo la Same Magharibi peke yake bali nitapita mpaka kwenye Jimbo la Same Msahariki. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante, imeshatosha Mheshimiwa Naibu Waziri unakwenda tu basi, Mheshimiwa Mbatia. (Kicheko) MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Nini utaratibu wa Serikali katika kuhakikisha wananchi au mashirika mbalimbali wakishajenga zahanati hizi kwa mfano Jimbo la Vunjo Zahanati ya Kochakindo ina zaidi ya miaka mitano ilijengwa na TASAF haina watumishi wala vifaa kwa ajili ya kutoa tiba. Utaratibu wa Serikali ni upi? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu kwamba swali la Mheshimiwa James Mbatia linaonekana ni maalum kwa eneo maalum. Kwa hiyo, namwomba sana baada ya kikao hiki leo hii tuweze kuonana ili anipe details. MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu. Na. 178 Mishahara kwa Wenyeviti wa Vitongoji, Mitaa na Vijiji MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza:- Serikali inaanzia katika ngazi ya kitongoji, mtaa na kijiji:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni lini viongozi na Wenyeviti wa Vitongoji, Mtaa na Kijiji watalipwa mishahara? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa sifa zinazomwezesha Mtanzania kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kijiji, Kitongoji au Mtaa ni pamoja na kuwa na shughuli halali inayomwingizia kipato. Kwa muktadha huo, utaratibu wa viongozi kwa ngazi hiyo kulipwa mishahara kama ilivyoulizwa katika swali la msingi haujawahi kuwekwa kwenye sheria yoyote. MWENYEKITI: Mheshimiwa Kiswaga. MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa hata sisi viongozi wa Bunge mojawapo ya sifa ni kuwa na kazi halali zinazotuingizia kipato kama hawa Wenyeviti wa Vitongoji ambao sisi tunalipwa, wao hawalipwi. Je, Serikali iko tayari kuleta sheria ili waweze kulipwa mishahara? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa viongozi hawa ndiyo wanaohamasisha maendeleo kama ujenzi wa zahanati, shule za msingi, sensa na kusimamia amani, je, Serikali iko tayari iko tayari kuendelea kuwalipa posho? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la kwanza, napenda nimhakikishie kwamba wakati wowote Serikali inapopata 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) mapendekezo huwa inayafanyia kazi. Kwa hiyo, mara tutakapopata mapendekezo kutoka kwenye vikao halali vinavyohusika tunaweza wakati wowote tukafanya marekebisho ya sheria kutokana na muktadha wa muda utakavyokuwa na mapendekezo yatakavyokuwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kuhusu kulipa posho, Serikali ilishatoa Mwongozo tangu mwaka 2003 kwamba yatumike mapato ya ndani kulipa posho kwa viongozi hawa na posho zile zimeainishwa. Kwa hiyo, ni jukumu la Wakurugenzi wa Halmashauri na Mheshimiwa Mbunge namwomba sana asimamie kwenye jimbo lake na watumie Mwongozo huo kuhakikisha kwamba viongozi wetu hawa wanalipwa posho. MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea na Mheshimiwa Hasna Sudi Katunda, Mbunge wa Kigoma Kusini. Na. 179 Kuligawa Jimbo la Kigoma Kusini MHE. HASNA S. K. MWILIMA aliuliza:- Jimbo la Kigoma Kusini lenye ukubwa wa kilometa za mraba 10,178 lina jiografia mbaya na idadi ya wakazi wake ni kubwa sana:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuligawa jimbo hilo na kuanzisha halmashauri nyingine ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za kijamii kiurahisi? (b) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo katika Tarafa ya Nguruka? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali refu la 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Hasna Sudi Katundu Mwilima, Mbunge wa Kigoma Kusini, lenye vipengele (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kuyagawa majimbo ya uchaguzi kwa kuzingatia vigezo vya idadi ya watu, jiografia, hali ya mawasiliano, ukubwa wa jimbo na uwezo wa ukumbi wa Bunge. Mheshimiwa Mwenyekiti, ili Jimbo lolote ligawanywe, Tume hutoa tangazo kuhusu nia hiyo. Baada ya tangazo, mapendekezo hujadiliwa katika vikao vya Halmashauri, Kamati ya Ushauri ya Wilaya na Mkoa na hatimaye kuwasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo hutangaza jimbo jipya baada ya kupata kibali cha Rais. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, vigezo vinavyozingatiwa katika kuanzisha Mamlaka za Miji Midogo ni pamoja na idadi ya watu wasiopungua elfu hamsini, kata zisizopungua tatu, eneo lisilopungua kilomita za mraba mia moja na hamsini, viwanja vilivyopimwa visipungue asilimia 30 ya eneo lote, uwepo wa mpango kabambe wa uendelezaji wa mji (master plan) na huduma za jamii za kukidhi ukuaji wa mji. Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mapendekezo ya kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo yanapaswa kuanzia kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji, Kamati ya Maendeleo ya Kata, Baraza la Madiwani, Kamati ya Ushauri ya Wilaya na Mkoa kwa kuzingatia vigezo hivyo kwa mujibu

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    288 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us