Majadiliano Ya Bunge

Majadiliano Ya Bunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Nane– Tarehe 27 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa TatuAsubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu. NDG. BAKARI KISHOMA – KATIBU WA MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. VICK P. KAMATA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa bajeti na majukumu ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio na Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. MWENYEKITI: Ahsante, Katibu. NDG. BAKARI KISHOMA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Kadutu. Na. 144 Tatizo la Mawasiliano ya Simu Katika Jimbo la Ulyankulu MHE. JOHN P. KADUTU aliuliza:- Jimbo la Ulyankulu linakabiliwa na tatizo la mawasiliano ya simu hasa katika Vijiji vya Ibambo, Mwongozo, Ichemba, Kanoge, Ilege, Busanda, Bulela, Ikonongo, Igombemkulu na maeneo mengine mengi:- Je, ni lini kampuni za simu zitamaliza tatizo la mawasiliano katika Jimbo la Ulyankulu? NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali la Mheshimiwa John Peter Kadutu, Mbunge wa Ulyankulu, kama ifuatavyo:- 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iliingia Makubaliano na Kampuni ya Mawasiliano ya Vietel ya Vietnam (Halotel) kufikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara ikiwa ni pamoja na maeneo ya Vijiji vya Ibambo, Mwongozo, Ilege, Bulela na Ikonongo. Utekelezaji wa kuleta mawasiliano ya simu kwa miradi hiyo umekamilika ambapo minara imejengwa katika Vijiji vya Ibambo, Keza na King’wangoko. Hata hivyo, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote itahakikisha maeneo yote yanapata huduma hiyo muhimu kama inavyotakiwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, Vijiji vya Lihemba, Kanoge, Busanda na Igombemkulu vitaainishwa na kuingizwa katika orodha ya miradi ya kuwapatia mawasiliano inayosimamiwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote itakayotekelezwa siku za usoni kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. MWENYEKITI: Mheshimiwa Kadutu. MHE. JOHN P. KADUTU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kabla sijauliza maswali mawili ya nyongeza, naomba tufanye marekebisho kidogo kwenye majina ya vijiji, kijiji kinaitwa Ichemba na wala siyo Lihemba. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile minara hii inajengwa kwa umbali mrefu karibu kilometa 30 kwenda mnara mwingine, je, Serikali kwa kushirikiana na makampuni haya iko tayari kuongeza minara mingine katikati ili kuongeza upatikanaji wa mawasiliano? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwenye jibu ametaja mchakato wa ujenzi au kutengeneza minara katika Vijiji vya Ichemba, Kanoge, Busanda na Igombemkulu utafanyika siku za usoni. Kwa Kiswahili rahisi ukisema siku za usoni maana yake haijulikani ni hata baada ya miaka 10, 15 ni siku za usoni. Je, Serikali sasa iko tayari kueleza muda maalum badala ya kutuambia habari za siku za usoni? Ahsante. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitoe shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Kadutu kwa sababu pamoja na mambo mengine tumekwishawasiliana kuhusu masuala ya mawasiliano kwenye jimbo lake na nilimweleza vizuri tu hatua mbalimbali ambazo Serikali imeendelea kuzichukua. Kawaida umbali kati ya mnara na mnara katika eneo ambalo halina milima mingi sana ni radiance ya kilometa 80. Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, Serikali imeendelea kuweka umbali wa radiance ya kilometa 60 kwa sababu umbali huo unarahisisha kuweka mnara mwingine umbali wa kilometa hata 60 kama hakuna milima. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Kadutu kwamba umbali wa minara kama yeye anapata kwa kilometa 30 ni kwa sababu maeneo yaliyopo yana milima milima na tutajitahidi kuangalia sehemu zote ambazo hazipati mawasiliano tusogeze minara mingine ili wananchi waweze kupatiwa mawasiliano kwa urahisi. Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni lini miradi kwenye vijiji vilivyotajwa pale itapatiwa mawasiliano. Kwa sasa hivi tunaorodhesha vijiji na kata mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya nchini mwetu kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote. Hivi ninavyoongea tumepanga tufanye ratiba ndefu ya miezi miwili baada ya Bunge la Bajeti kwa ajili ya kupima kwa kutumia GPS na kuweka alama ni wapi tutaweka minara kwa ajili ya kuwezesha wananchi wa Tanzania wote waweze kupata mawasiliano. MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbatia. MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kuna mwingiliano mkubwa wa njia za mawasiliano hasa SafariCom kwenye Jimbo la Vunjo, Rombo na maeneo yanayozunguka mipakani. Serikali ina mkakati 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) gani, labda washauriane ili kuweza kuona mwingiliano huu unaondoka namna gani kwa sababu wewe mtumiaji unalazimika kuingia kwenye roaming bila wewe mwenyewe kutaka na inasababisha gharama kubwa? MWENYEKITI: Naibu Waziri majibu, Mheshimiwa Dkt. Kafumu na Mheshimiwa Shekilindi wajiandae. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli maeneo mengi sana ya nchi yetu hasa yale ya mipakani kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana wa mawasiliano kati ya hizo nchi jirani na Tanzania. Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote na TCRA tumeendelea kuyaainisha maeneo hayo kwa ajili ya kuongeza nguvu minara yetu na kuzuia frequency ambazo ni mtambuka kutoka nchi moja kwenda nyingine kuhakikisha tunazidhibiti ili Watanzania wapate mawasiliano ya Tanzania na nchi jirani ziendelee kupata mawasiliano kutoka nchi hizo. MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Kafumu ajiandae Mheshimiwa Shekilindi. MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Jimbo la Igunga kama lilivyo Jimbo la Ulyankulu, tuna kata kadhaa ambazo bado hazina mawasiliano. Kata hizo ni pamoja na Kiningila, Isakamaliwa, Mwamashiga, Mtunguru na Kata ya Mwashiku Jimbo la Manonga. Ni lini basi Serikali itasaidia ili wananchi hawa waweze kupata mawasiliano? Ahsante. MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi. MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE - NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Dkt. Dalaly kwa sababu mara nyingi sana 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tumekuwa tukikutana ofisini kwa ajili ya kuongelea kata zake hizo alizozitaja ambazo ni kweli hazina mawasiliano. Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru vilevile kwamba ameshatuandikia hata kwa maandishi na hii taarifa yake tayari iko kwa watu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ambao tumekubaliana kwamba mwezi saba mpaka wa tisa tutakuwa na ziara nchi nzima kuhakikisha tunaweka mawasiliano ya eneo hilo. Namhakikishia tu Mheshimiwa Dkt. Kafumu kwamba nitakapokuwa nakwenda maeneo ya Igunga nitamtaarifu ili tuwe wote kutembelea maeneo haya. Ahsante. MWENYEKITI: Mheshimiwa Shekilindi. MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwanza kabisa nimshukuru Naibu Waziri, Mheshimiwa Nditiye kwa kutuma wataalam wake kwenda kubaini maeneo ambayo hayana minara katika Jimbo la Lushoto. Je, ni lini sasa utekelezaji utaanza ili wananchi wa Lushoto waweze kupata mawasiliano? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu, anataka kujua ni lini tu, halafu jiandae Mheshimiwa Joyce. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza kwenye swali la msingi na kama nilivyoeleza kwenye maswali mengine ya nyongeza, Mheshimiwa Shekilindi kuanzia mwezi wa Saba baada ya Bunge la Bajeti nitafanya ziara ndefu sana ya kutembelea maeneo yote yenye changamoto za mawasiliano nikiambatana na timu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote. Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hakika nitafika jimboni kwake na pia nitafika kwa Mheshimiwa Nape naye ambaye najua kabisa anasumbuka sana kuhakikisha tu kwamba mawasiliano kwa nchi yetu yote yanapatikana bila tatizo. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Joyce. MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Tatizo hili linafafana kabisa na tatizo la Kijiji cha Ngarasero katika Jimbo la Ngorongoro, Mkoa wa Arusha. Je, ni lini Serikali itapeleka minara katika eneo hilo ili wananchi waweze kupata mawasiliano katika Kijiji cha Ngarasero? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu, kwa kifupi. MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE - NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Ngorongoro ni moja kati ya maeneo ambayo nayo yana changamoto ya mawasiliano. Kwa baadhi ya sehemu ambazo zina changamoto, tayari tumekwishatuma watu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kwenda kufanya tathmini ya mahali gani panatakiwa kwenda kuwekwa minara kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo. Mheshimiwa Mwenyekiti, pindi watakapotuletea

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    264 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us