MKUTANO WA PILI Kikao Cha Tano – Tarehe 8 Februari, 2021 (Bunge

MKUTANO WA PILI Kikao Cha Tano – Tarehe 8 Februari, 2021 (Bunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Tano – Tarehe 8 Februari, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: KIAPO CHA UAMINIFU Mheshimiwa Mbunge afuataye aliapa Kiapo cha Uaminifu:- Mheshimiwa Yustina Arcadius Rahhi SPIKA: Katibu shunguli inayofuata. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO:- Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2021/22 pamoja na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/2022. MHE. OMARI M. KIGUA – MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kuhusu Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/2017 – 2020/2021) na Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) pamoja na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali la kwanza linakwenda Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na litaulizwa na Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, kwa niaba yake Mheshimiwa Cecilia Pareso. Na. 58 Ubovu wa Eneo la Katokoro MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatengeneza eneo la Katokoro linalounganisha Kata za Katoro na Kyamulaile katika Jimbo la Bukoba Vijijini ili kuondoa adha ya usafiri inayowakabili wananchi wa maeneo hayo? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Festo John Dugange, tafadhali. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, eneo korofi la Katokoro ambalo limejaa maji lina urefu wa kilomita 5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Katoro – Kyamulaile – Kashaba yenye jumla yakilomita 15.7 inayounganisha Kata za Katoro, Kyamulaile na Ruhunga. Aidha, barabara hiyo pia inaunganisha maeneo mbalimbali ya Halmashauriya Wilaya ya Bukoba na Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imefanya usanifu kwa ajili ya kuboresha eneo hilo korofi ambapo kiasi cha fedha shilingi milioni 572 kinahitajika kunyanyua tuta la barabara na kujenga makalvati. Mheshimiwa Spika, ili kupata ufumbuzi kwa sasa katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali ilitenga fedha kiasi cha shilingi milioni 87 kwa ajili ya kurekebisha eneo korofi katika barabara hiyo. Hata hivyo, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkandarasi aliyekuwa anafanya kazi hiyo alisimamishwa kutokana na eneo hilo kujaa maji. Mheshimiwa Spika, wakati jitihada za kutafuta fedha kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa kudumu wa barabara hiyo zikiendelea, mara maji yatakapopungua, mara moja Serikali itamrejesha kazini mkandarasi huyo ili kurejesha mawasiliano katika eneo hilo. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Mheshimiwa Paresso, nimekuona nimekuona. MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana lakini kwenye tablets zetu hatuna Order Paper. Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi, naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza, kumekuwa na utamaduni wa fedha nyingi zilizopangwa kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya barabara kucheleweshwa hivyo ufanisi wa kile kinachokusudiwa hakifikiwi. Je, Serikali sasa mko tayari kuhakikisha kama fedha zinatengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara yoyote zinatoka kwa wakati ili barabara hizo zitengenezwe? Mheshimiwa Spika, swali la pili, barabara ya Karatu inatoka Njia Panda – Mang’ola - Lalago ni barabara ambayo inaunganisha Mkoa wa Arusha na Mkoa wa Simiyu. Barabara hii imekuwa ikiahidiwa kujengwa kwa kiwango cha lami hasa kipindi cha uchaguzi ahadi inakuwa ni tamu kweli masikioni mwa wananchi lakini baada ya hapo barabara hiyo haijengwi kiwango cha lami. Serikali mtuambie ni lini kwa hakika barabara hiyo itajengwa kwa sababu Sera ya Wizara ya Ujenzi inasema kuunganisha barabara za Mikoa na Mikoa kwa kiwango cha Lami na barabara ile inaunganisha Mkoa wa Arusha na Mkoa wa Simiyu? SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Dkt. Dugange, majibu tafadhali. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kuhusu fedha za miradi mbalimbali ya barabara kuchelewa kupelekwa katika miradi hiyo, utaratibu wa fedha kupelekwa katika miradi mbalimbali unazingatia upatikanaji wa fedha ambazo zimetengwa kwenye bajeti husika. Hivyo, kutokana na kutegemea mapato 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya ndani kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo, mara nyingi kumekuwa na ucheleweshwaji na miradi hiyo kwa sababu ya upatikanaji wa fedha. Hata hivyo, Serikali imeendelea kuongeza jitihada kuhakikisha kwamba mapato yanakusanywa kwa wakati na fedha za miradi hiyo zinawasilishwa kwenye miradi husika kwa wakati. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mwaka huu wa fedha mpaka sasa takribani asilimia 48 ya fedha ya miradi ya barabara tayari imekwishawasilishwa katika mamlaka ya Serikali za Mitaa na kazi za utekelezaji wa miradi hiyo zinaendelea. Suala hili litaendelea kufanyiwa kazi kwa karibu zaidi. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na barabara ya Arusha Simiyu inayotokea Karatu, ni kweli hii ni barabara muhimu sana na inaunganisha mikoa hii miwili. Serikali ina dhamira ya dhati kuhakikisha kwamba barabara hizi kuu ambazo zinaunganisha mikoa zinajengwa kwa kiwango cha lami ili kurahisisha shughuli za kiuchumi na za kijamii. Mheshimiwa Spika, kama alivyouliza kwamba Serikali imekuwa ikitoa ahadi, ni kweli na ahadi ya Serikali hakika itatekelezwa. Nimhakikishie tu kwamba mara fedha zikipatikana barabara hiyo itajengwa ili wananchi waweze kupata huduma zilizokusudiwa. SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Neema Lugangira, swali la nyongeza. MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Kwanza kabisa, napenda kuipongeza Serikali kwa jitihada kubwa za kuboresha miundombinu ya barabara. Mheshimiwa Spika, napenda kumfahamisha Mheshimiwa Conchesta kwamba tayari kazi ya kuboresha barabara ile inaendelea ili iweze kupitika ambapo sasa hivi wanafanya kazi za kuchepua maji, kuweka mawe na changarawe. Vilevile napenda kumfahamisha Conchesta kwamba mimi pamoja na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) la Bukoba Vijijini tumeshawasiliana na Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI na barabara hii itafanyiwa kazi kwa kuzingatia mpango kazi uliowasilishwa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, aidha, kwa kuwa umuhimu wa kipande hicho cha barabara unafanana na barabara ya Kanazi - Kyaka kupitia Katoro, ni lini barabara hiyo nayo itatengewa fedha na kujengwa kwa kiwango cha lami? SPIKA: Majibu ya swali hilo la Kanyazi, Mheshimiwa Naibu Waziri, TAMISEMI, tafadhali. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema Lugangira, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ni kuboresha miundombinu ya barabara ikiwepo barabara hii ya Kanazi, Kyaka kupitia Katoro. Kimsingi tathmini na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kujenga barabara hizi unaendelea. Mpango umeandaliwa kwa ajili ya kufanya tathmini lakini kuhakikisha kwamba barabara hizi zinatafutiwa fedha ili ziweze kujengwa. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kutekeleza mipango yake hii ya kufanya tathmini lakini pia kutafuta fedha ili barabara hizi ziwezwe kujengwa na kusogeza huduma kwa wananchi. SPIKA: Tunaendelea na swali linalofuata la Mheshimiwa Yahaya Omar Masare, Mbunge wa Manyoni Magharibi, siku hizi sijui unakaa upande gani, uliza swali lako Mheshimiwa Masare. Yaani CCM wote, haya tunaendelea na Wizara ya Maliasili na Utalii, swali litaulizwa na Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Watu wa IT, hebu wekeni maswali haya haraka kwenye tablets. Na. 60 Ongezeko la Wanyamapori katika Hifadhi ya Selous MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na ongezeko la wanyamapori katika Hifadhi ya Mbuga ya Selous na sasa tembo na nyati wanavamia mashamba pamoja na makazi ya wanavijiji na kuleta taharuki:- Je, Serikali inaweza kuwarudisha wanyama hao porini mbali zaidi na wananchi? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri Mary Francis Masanja, tafadhali. NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mali asili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa na inatekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Utatuzi wa Migongano baina ya binadamu na wanyamapori. Aidha, Wizara inaendelea kukamilisha utaratibu wa kuweka alama katika shoroba na mapito ya wanyamapori ili kuimarisha uhifadhi

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    229 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us