NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 19 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Tunaendelea Waheshimiwa Wabunge na Mkutano wa Kumi na Moja, Kikao cha leo ni cha Kumi na Tatu. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO:- Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2018/2019. MHE. PETER J. SERUKAMBA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII:- Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Utekelezaji wa Bajeti na Majukumu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/2018 pamoja 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Peter Serukamba, maoni ya Kambi ya Upinzani siyaoni, Katibu tunaendelea. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri Mkuu karibu tafadhali. (Makofi) Swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Hussein Nassor Amar (CCM), Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale. MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii adimu ya kuweza kumuuliza swali Mheshimiwa Naibu Waziri. MBUNGE FULANI: Waziri Mkuu. SPIKA: Inabidi uombe radhi bwana. (Kicheko) MHE. HUSSEIN N. AMAR: Naomba radhi, ni Waziri Mkuu. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tumepata bahati kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mvua nyingi zimenyesha nchini kwetu na miundombinu takribani asilimia zaidi ya 75 imeharibika. Je, Serikali imejipanga vipi kuweza kuirejesha miundombinu hii katika hali yake? SPIKA: Ahsante sana kwa swali hilo. Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Amar, Mbunge wa Nyang’hwale, kama ifuatavyo:- 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba katika kipindi hiki tumeendelea kupata mvua nyingi sana karibu nchi yote na mvua hizi zimeleta maafa makubwa pamoja na kwamba kwa upande wa kilimo tunapata faida. Nianze kwa kutoa pole kwa Watanzania wenzetu wote waliopata maafa, wako wenzetu wametangulia mbele za haki kutokana na mvua hizi kuwa nyingi na wako watu wameathirika kwa kuharibika kwa miundombinu yao. Wale wote ambao wametangulia mbele ya haki tuendelee kuwaombea, Mwenyezi Mungu aweze kuweka roho zao mahali pema lakini tuwape pole wale wote ambao wamepata athari ya kuharibika kwa miundombinu hii. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge anataka kujua ni namna gani Serikali imejipanga kurejesha miundombinu iliyoharibika. Kwa kuwa mvua hizi zinaendelea na kila mkoa tunazo Kamati za Maafa na miundombinu hiyo iliyoharibika sehemu kubwa ni barabara na miundombinu mingine ambayo ni ya Serikali na ya watu binafsi. Kamati ya Maafa itafanya tathmini ya kujua ni miundombinu ipi imeharibika kwa kiasi gani na ile ambayo ipo upande wa Serikali kama kutakuwa kuna barabara, shule na maeneo mengine taratibu za kawaida za matengenezo zitafanywa. Yale maeneo ya watu binafsi, Kamati zile za Maafa kadiri zitakavyoweza kutathmini zinaweza kufanya maamuzi ya namna ya kusaidia kurudisha miundombinu hiyo, lakini Kamati zile za Maafa ndiyo zitafanya kazi mikoani na kule wilayani. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka nimhakikishie tu kwamba miundombinu ambayo inazungumzwa sasa kama ambavyo tumeshuhudia barabara zetu nyingi zimeharibika, kwa kuwa mkoani kuna chombo kinachoshughulika barabara kinaitwa TANROADS na Wilayani tuna TARURA, vyombo vyote hivi sasa baada ya tathmini hiyo vinaweza kufanya maamuzi ya kurejesha miundombinu hiyo. Ahsante sana. (Makofi) SPIKA: Ahsante. Tunaendelea na Mheshimiwa Upendo Furaha Pendeza wa Viti Maalum - CHADEMA, swali. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia fursa hii kumuuliza Waziri Mkuu swali. Mheshimiwa Spika, katika tamko la kisera la Sera ya Elimu, Serikali imesema itaondoa vikwazo vyote vinavyozuia wanafunzi kupata elimu. Moja ya sababu inayofanya watoto wa kike wanakosa fursa hii ya kupata elimu ni pamoja na wao kuwa katika kipindi cha hedhi na kukosa taulo za kujihifadhi. Mheshimiwa Spika, tunashukuru Serikali kupitia Naibu Waziri wa TAMISEMI imesema kwamba asilimia kumi ya pesa zinazotolewa kwa ajili ya capitation fund, zile shilingi 10,000 ama shilingi 20,000 zitumike kwa ajili ya kuwanunulia watoto wetu sanitary pads ama taulo za kujihifadhi. Hata hivyo, kiasi hicho ni kidogo ukizingatia kwamba kiasi hicho kimepangwa tangu miaka kumi iliyopita kipindi dola moja ikiwa ni shilingi 1,000 na sasa dola moja ni almost shilingi 2,200. Mheshimiwa Spika, kwa nini sasa Serikali ilsilete pendekezo kupitia Finance Bill ya kuondoa kodi ambazo zipo kwenye sanitary pads ili kuhakikisha kwamba bei ya taulo za kujihifadhi kipindi cha hedhi zinashuka kwa hiyo hata hiyo asilimia kumi itakayotolewa kidogo itaweza kusaidia kwa sababu pedi zitapatikana katika bei rafiki? Ahsante sana. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana, kwa hiyo swali lako specifically ni? MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Spika, swali langu specifically ni kwamba… SPIKA: Straight. MHE. UPENDO F. PENEZA: Namuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa nini sasa Serikali isilete pendekezo katika Finance Bill ya kuondoa kodi zote ambazo zipo kwenye taulo za kujihifadhi kipindi cha hedhi? Ahsante. (Makofi) 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Ahsante. Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri Mkuu. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Peneza, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inao utaratibu wake katika kuondoa kodi kwenye bidhaa zote ambazo zinaleta tija pale ambapo zinatumika na jamii yetu huku ndani ikiwemo na jambo ambalo ametaka kupata ufafanuzi. Kwa kuwa Serikali imeanza na kutenga fedha kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kama ambavyo ameeleza na kama ambavyo Naibu Waziri ameeleza, kama alieleza, basi sasa Naibu Waziri anaweza kuona sasa umuhimu kutokana na ombi lako kuwa Serikali sasa itoe pendekezo la kuweza kuingiza kwenye Finance Bill kuona namna ya kuondoa kodi ili hivi vifaa viweze kupatikana kwa bei nafuu. Kwa kuwa Wizara ya Fedha bado haijawasilisha na kwa kuwa Naibu Waziri naye amesikia, watakaa pamoja kuona umuhimu wa jambo hilo na kukushirikisha ili kuweza kuona namna nzuri ya kupunguza bei ya vifaa hivyo ili viweze kutumiwa na walengwa ambao tumewalenga zaidi. Ahsante. (Makofi) SPIKA: Ahsante. Tunaendelea na Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi, Mbunge wa CCM, Jimbo la Musoma Mjini. MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi kumuuliza swali Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu ni kwamba Serikali iliamua kujitoa kwenye biashara na hivyo ikaacha sekta binafsi waweze kuendesha biashara na hii ni katika kuboresha tija. Hata hivyo, kama tunavyofahamu baadhi ya biashara zilizokuwa zinafanywa na Serikali ilikuwa ni pamoja na viwanda mbalimbali vya nguo kama MUTEX, MWATEX na Sungura. Mheshimiwa Spika, swali langu ni kwamba katika Serikali kuachia yapo mafao ya wale watumishi ambayo 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) hayajalipwa hadi leo. Nikiwa specific, bahati nzuri Mheshimiwa Waziri Mkuu ulibahatika kuja Musoma, uliweza kuona mfano wa watumishi wa Kiwanda cha MUTEX toka wakati huo mpaka leo hawajalipwa hayo mafao yao. Kwa bahati nzuri uliahidi kwamba wangeweza kulipwa kwa wakati muafaka. Sasa nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba hawa watu wanaweza kulipwa mafao yao mara moja ili waweze kuendelea na maisha yao maana wametaabika kwa muda mrefu? SPIKA: Ahsante sana. Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri Mkuu tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mathayo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, upo ukweli kwamba Tanzania tuna viwanda vingi na vingine vilikuwa viwanda vya muda mrefu, vipo viwanda ambavyo kwa sasa havifanyi kazi kabisa. Serikali kwa dhamira ya kujenga uchumi kwenda uchumi wa kati kupitia viwanda, tumeendelea kufanya tathmini ya kutosha kwenye sekta hii. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Viwanda imeunda timu ya kufanya mapitio kwenye viwanda vyote tulivyokuwa tumebinafsisha na viwanda vyote ambavyo Serikali tulikuwa tunavihudumia lakini vyote havifanyi kazi ili kwanza tuweze kuvitambua ni vingapi na tulivibinafsisha kwa ajili ya nini ili tuweze kufanya maamuzi. Maamuzi hayo ni kwamba viwanda vyote ambavyo tumebinafsisha na havifanyi kazi tunataka tuvirudishe Serikalini ili tuweze kutafuta wawekezaji wenye uwezo wa kuviendesha viwanda hivi, vile ambavyo vimebinafsishwa hata hivi pia tulivyonavyo sasa. Mheshimiwa Spika, malengo ya kuwekeza tunataka kwanza tupate mtaji, teknolojia lakini pia tuweze kutoa ajira za kutosha na wakati mwingine pia hata kuhakikisha kwamba uzalishaji wa sekta hiyo unaendelea vizuri. (Makofi) 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, swali la Mheshimiwa anataka kujua hatma ya viwanda vile vilivyokufa vilivyokuwa na watumishi na watumishi wale hawajalipwa mishahara yao. Ni kweli baada ya tathmini hiyo, tutabaini uwepo wa watumishi eneo hilo wangapi na madeni yao yakoje na baada ya kuwa tumepata mwekezaji kwa malengo niliyoyataja, sasa tunaweza tukaanza kulipa pia watumishi ambao wanaidai Serikali kupitia viwanda hivyo. Viwanda ambavyo pia vimekuwa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages320 Page
-
File Size-