Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Mbili - Tarehe 12 Juni, 2014 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NA URATIBU: Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. MWIGULU L. M. MCHEMBA): Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha kwa Mwaka 2014/2015 [The Monetary Policy Statement for the Financial Year 2014/2015]. MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, leo ni siku ya Alhamisi tunaanza na Maswali kwa Waziri Mkuu, lakini leo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani hayupo, hivyo naanza kumwita Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah. MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni miongoni mwa nchi nyingi ambazo zimekabiliwa na tatizo kubwa la ajira kwa Vijana. Kila mwaka vijana wanamaliza mafunzo yao lakini ni wachache sana wanaopata ajira na kwa maana hiyo kundi kubwa kubakia halina ajira. Je, Waziri Mkuu una mpango gani, mkakati gani au mazingira gani ya kuwatumia vijana hawa mara tu baada ya kumaliza mafunzo yao. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu majibu, swali limekuwa precise. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah swali lake, mimi nafikiri zuri sana kwa sababu Watanzania wote ndiyo jambo ambalo tunalizungumza sana. (Makofi) Kwanza, nilitaka nianze kwa kusema kwamba tatizo la ajira siyo jambo la Tanzania tu ni tatizo kubwa kwa kweli Afrika na Duniani kote. Lakini kila nchi inajitahidi kuona ni namna gani wanaweza kupunguza hilo tatizo. Kwa nchi changa zenye uchumi mdogo kama zetu nadhani changamoto hiyo inakuwa ni kubwa zaidi, matumaini yangu ni kwamba kwa juhudi ninazoziona zinafanywa na Serikali chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) nina hakika kabisa tatizo hili baada ya muda si mrefu tutakuwa tumelikabili vizuri. Mheshimiwa Spika, kwa sasa, mategemeo yetu makubwa kwenye ajira kwanza ni sekta ya umma yenyewe kwa maana ya Serikali, Mashirika yake, na vyombo vyake vingine ndiyo maana unaona kila mwaka walimu kadhaa tunawachukua, watalaam kadhaa. Kwa hiyo, kuna element hiyo ya sekta ya umma ambayo ndiyo eneo la kwanza tunalolitegemea, lakini siyo kubwa la kuweza kuchukua watoto wote wanaomaliza Vyuo na Elimu ya Juu kwa ujumla. (Makofi) Mheshimiwa Spika, eneo la pili ambalo ndilo tegemeo letu ni sekta binafsi. Ninaposema sekta binafsi hapa ina sura mbili. Sekta binafsi kwa maana kwamba yeye mwenyewe mtu mmoja mmoja kujiajiri kutegemea na fursa anazoziona. Lakini sekta binafsi kwa maana ya kuajiriwa katika vile vyombo au makampuni ambayo tayari yanahitaji ajira. Hivyo, vyote viwili tunajaribu kuvipa msukumo mkubwa sana. Kwa hivyo, kwa upande wa Tanzania ndiyo maana unaona tumekuja na sera za namna mbalimbali za kutuwezesha kuongeza idadi ya Viwanda. Tume-open up sana suala la uwekezaji hapa nchini, tunajitahidi sana kwenye maeneo maalum kama EPZ pamoja na ZES zote hizi ni katika jitihada za kujaribu kuona namna ya kukabiliana na jambo hili. Lakini nilazima nikubaliane na wewe, ni jambo kubwa, ni jambo linatukera lakini nadhani hatua kwa hatua tunaweza tukaendelea kulikabili wote kwa pamoja. (Makofi) MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu yake mazuri, nina swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Waziri Mkuu, Tanzania inatumia fedha nyingi sana kuwafundisha vijana wetu ndani na nje ya nchi. Lakini matokeo ya mafunzo haya na matumizi ya fedha hizi vijana hawa wanaondoka na kwenda kutumikia nchi nyingine jambo ambalo ni hasara kubwa sana kwa Taifa. Je, kama Waziri Mkuu unasemaje kuhusu suala hili, ni hatua gani utazichukua ili watalaam hawa waweze kubakia ndani ya nchi na kuweza kutumia Taifa hili. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, kwanza nataka niseme tu kwamba si dhambi kwa Mtanzania kwenda kufanya kazi nje kama fursa hiyo ipo. Ni jambo ambalo tunapaswa tuwatie moyo,ni namna tu ya watu kutumia muda na fursa walizonazo kuona namna wanavyoweza kujiendeleza. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Kwa hiyo mimi nadhani tusione kama ni jambo baya sana, Hapana! Mimi nadhani tuwatie moyo, waende popote na nchi nyingi ndivyo walivyofanya. Wamewa-encourage vijana wao kwenda popote pale kufanya kazi lakini kwa matarajio kwamba baada ya muda siyo mrefu watarudi, watakuwa wamepanua uelewa wanaweza vilevile wakatuhudumia. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nadhani jambo la msingi ni kwamba hizi sera ambazo tunakwenda nazo, polepole zitapunguza hata hiyo kasi ya watu kutaka kwenda kufanyakazi nje. Kubwa kwani hapa brother ni nini? Kubwa hapa ni je, kuna mahali nitapata vihela hivi niweze kuishi? Kama tutaendelea na sera ya kuongeza mishahara yetu wakati uchumi unapanuka, wengi hawa tunaweza kabisa kuwa-retain kwa sababu watakuwa hawana sababu ya kwenda sehemu nyingine. Mheshimiwa Spika, lakini nakubaliana bado na swali la msingi lipo pale pale ni lazima juhudi za kuendelea kutafuta mbinu mbalimbali za kuongeza uwezekano wa kuwa na ajira pana liwe ndiyo hasa lengo kubwa la kila mmoja wetu. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana, tuendelee na Mheshimiwa Haji Khatib Kai. MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Spika, Taifa lolote Duniani linategemea wasomi na kwa kuwa kuna taarifa za wanafunzi wa UDOM wapatao 500 watazuiliwa kufanya mitihani yao kwa kushindwa kulipa ada za mitihani hiyo. Mheshimiwa Waziri Mkuu, nini kauli yako juu ya Wanafunzi hawa, watoto wa maskini? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, imani yangu mimi kwanza ni kwamba sidhani kama tutaweza kuruhusu wasifanye mitihani, sidhani. Pengine mimi nikushukuru tu kwa sababu umeliuliza, kwa sababu mimi nilikuwa sina taarifa hizo. Nina vijana wangu wa UDOM mara nyingi ni wepesi sana kunifuata wanapokuwa na jambo lolote linalowakabili. Mheshimiwa Spika, hivyo, ninachoweza kuahidi ni kwamba tutalifuatilia kwa karibu sana na tutahakikisha wote wanafanya mtihani, kwa sababu tumewasomesha, tumewapeleka pale, suala la kwamba hana ada leo au nusu ada amelipa haliwezi kuwa ndiyo sababu ya kumfanya mtu ambaye amekaa miaka mitatu, minne asitumie nafasi yake ya mwisho kuweza kufanya mitihani. Hapana! Hilo tutahakikisha wanafanya. (Makofi) MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Spika, nimeridhika na majibu ya Waziri Mkuu. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana, afadhali umetumia busara. Mheshimiwa Suleiman Said Bungara, hawa wote ni CUF leo walijipanga. MHE. SELEMANI S. BUNGARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika Mkoa wa Lindi na Mtwara kwa muda mrefu sasa hivi imezuiliwa mikutano ya hadhara ya kisiasa na ya kidini. Je, ni sababu zipi ambazo zimesababisha mikutano hiyo izuiliwe. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Serikali ilichukua hatua ya kusitisha mikutano ambayo inaweka watu wengi kwa pamoja tangu zilipotokea vurugu pale Mtwara miaka miwili hivi nafikiri na zaidi kidogo iliyopita. Kazi ya Serikali imekuwa ni kuendelea kuhakikisha tunarejesha ile hali ya utulivu kwa Mkoa ule lakini Lindi kutokana na ujirani wake na Mtwara nao walikumbwa na uamuzi huo. Nataka nikuhakikishie tu kwamba jambo hili tunaendelea kulifanyia tathmini na hata juzi nilikuwa nazungumza na Wakuu wa Mikoa yote miwili ili tuweze kufika mahali na kuruhusu tena shughuli fulani ziweze kuendelea kama ambavyo tulikuwa tunafanya kabla. Mheshimiwa Spika, rai yangu tu kwa wana Lindi na Mtwara kutambua tu kwamba sisi kama Serikali tunao wajibu wa kuendelea kuhakikisha watu wanaishi kwa amani, kwa utulivu bila vurugu na kadiri tutakavyopata ushirikiano wa karibu kutoka kwao hatuna sababu yeyote ya kuendelea kushikilia uamuzi huo kwa sababu ulifanywa kwa maksudi maalum, sababu ile ikishatoka hatuna haja ya kuendelea nalo. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Selemani bado una swali la nyongeza? MHE. SULEMANI S. BUNGARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa, sasa hivi kuna utulivu wa hali ya juu, huoni sasa utoe kauli rasmi kwamba mikutano hiyo iruhusiwe, hususani ukizingatia kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaanza hivi karibuni? SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Waziri Mkuu. WAZIRI MKUU:Mheshimiwa Spika, ni vigumu kwangu Mheshimiwa Bungara kusema hivyo hapa, kwa sababu kwa sehemu kubwa ndiyo maana mimi nafuatilia muda wowote. Ile tathmini inayotoka kwenye Mikoa inayohusika ndiyo inaweza kunipa mimi nafasi ya kutoa kauli. Lakini nataka nikuahidi tu kwamba hili jambo halitachukua muda mrefu sana kwa sababu kwa upande wa Lindi kwa mfano nilikuwa karibu tayari nikubali kwamba tufanye hivyo, lakini baadaye wakaniletea tatizo dogo hivi nikaona basi walimalize kwanza halafu tuone kama tunaweza tukawapa muendelee na shughuli kama kawaida. Usione hivi hata sisi kinatuuma, maana na sisi vilevile ni wadau na tungependa na sisi tufanye mikutano hiyo kwa sababu mwaka kesho siyo mbali. Sisi tungependa tuanze 4 Nakala ya Mtandao (Online Document) kuonekana pale kwa nguvu kama ambavyo na ninyi mnavyopenda, lakini nina uhakika tutalimaliza mapema sana kabla hatujafika karibu sana na chaguzi hizo. SPIKA: Ahsante sana. Nimwite Mheshimiwa Assumpter Mshama. MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi nimwulize swali Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninatambua kabisa kwamba ardhi ni mali ya umma na pia mwenye mamlaka nayo ya juu ni Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages111 Page
-
File Size-