Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA

Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA

Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Ishirini na Mbili – Tarehe 30 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na :- NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. [The Annual Report of Social Security Regulatory Authority (SSRA) for the Financial Year 2012/2013]. MASWALI NA MAJIBU Na. 153 Wahanga wa Mafuriko ya Mto Mkondoa Kilosa 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. SUSAN L. KIWANGA aliuliza:- Serikali imekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wahanga wa maafa mbalimbali kama vile mafuriko, milipuko ya mabomu, njaa na kadhalika, kwa kuwapa nyenzo mbalimbali za kuendeleza maisha yao kama vile Saruji, mabati na kuwajengea makazi mapya. Je, kwa nini Serikali haikuwasaidia vifaa vya ujenzi wananchi wa Kilosa walioathirika na mafuriko ya Mto Mkondoa yaliyotokea mwaka 2009 na kuwafanya wakose makazi na mpaka sasa wanaishi kweye mahema kama wakimbizi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Susan L. Kiwanga, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Morogoro, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kilosa ilikumbwa na mafuriko makubwa kati ua Desemba 2009 na Januari 2010 kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Dodoma na kusababisha kubomoka kwa Bwawa la Kidete na kufurika kwa Mto Mkondoa. Hatua za dharura zilizochukuliwa na Serikali baada ya maafa kutokea zililenga kuokoa maisha ya wananchi na kuwapatia huduma muhimu za binadamu, kama makazi ya muda, mavazi, chakula, maji, madawa ambapo jumla ya shilingi 1,500,000,000/= zilitumika kutoa huduma hizo. Mheshimiwa Spika, katika kurejesha hali ya kawaida, Serikali imesaidia kupatikana kwa maeneo mapya ya kuishi kwa kuandaa michoro na kupima viwanja 1970 kwa gharama ya shilingi 77.9 milioni. Jukumu la kujenga nyumba limebaki kwa wananchi wenyewe. Serikali huwajibika kugharamia ujenzi wa makazi kwa ajili ya waathirika wa maafa pale tu inapotokea kwamba kwa namna moja ama nyingine serikali ilihusika na athari zilizotokea kama ilivyokuwa katika milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imeendelea kufanya jitihada za kuhakikisha kwamba mafuriko hayatokei tena katika eneo hilo kwa kujenga tuta la kuzuia mafuriko kwenye mto Mkondoa pamoja na kukarabati Bwawa la Kidete kwa gharama ya shilingi bilioni 2.3. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Aidha, Serikali imekarabati miundombinu ya barabara, reli, ujenzi wa shule pamoja na kuhakikisha upatakinaji wa maji safi na huduma muhimu ambavyo kwa pamoja vimegharimu jumla ya shilingi 2,000,000,000/=. MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu haya, lakini hali ilivyo hivi sasa mpaka leo kwamba wale wananchi kule karibuni Kaya 1000 kwanza waliokuwa wamepata mafuriko. Sasa hivi zimebaki kaya 500 kati ya hizo 1000. Kaya 500 wamebaki, hao ndiyo maskini kabisa na wanalala kwenye yale majumba ya mabati, ingawa Mkuu wa Wilaya aliyepita alikuwa anaenda kubomoa yale mabati wakati watu bado wako ndani na wamepewa tangazo wahame. Hata hivyo, kutokana na umaskini waliokuwa nao wale watu hawana jinsi ya kufanya. Je, Serikali haioni kwamba kuna haja ya kuwasaidia hao maskini na siyo tu kuwapa viwanja tu, angalau kuwapatia mabati na sementi kama inavyofanya kwingine ili kuwasaidia hawa watu katika maisha yao ya kila siku? Swali la pili, wakati Serikali inasema kwamba ilitoa karibuni msaada wa shilingi bilioni moja na laki tano na mia tano na laki tatu na pointi, lakini hali halisi ni kwamba, wananchi wale hata mkienda kufanya ukaguzi hii misaada mliyoipeleka haikuwafikia kama inavyopasa. Je, Serikali ipo tayari sasa kwenda kuonana na hawa wahanga ili kuhakiki misaada kama kweli iliwafikia wote wanaohusika? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kiwanga, kama ifuatavyo:- 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) Ni kweli maafa haya yaliathiri watu wengi na hata haya yaliyotokea juzi yameathiri watu wengu na mvua zilizoendelea kunyesha mwezi huu hivi sasa zimeathiri maeneo mengi ya Tanzania. Kwa taarifa tu tathimini tuliyoifanya juzi, tunahitaji zaidi ya shilingi bilioni 43 ili kurejesha miundombinu kama vile ya maji, barabara, umeme katika hali ya kawaida kwa Taifa. Kwa hiyo, maafa haya ni makubwa na hayakutokea huko tu na yametokea nchi nzima na uwezo wa Serikali kujenga nyumba kwa watu wote walioathirika na maafa kama haya ya mvua ni mdogo na ni ngumu sana kufanya. Hata hivyo, nachoweza kusema labda tushauriane na wenzetu wa Halmashauri ili tuone wana mikakati gani ya kusaidia walipa kodi wa Wilaya hii husika. Leo siwezi kuahidi kwamba tunaweza kwenda kusaidia kujenga nyumba 500 za watu hawa. Nitachukua jukumu nitatuma watu wangu tukashauriane na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ili tuone namna gani wao wanaweza kufanya, halafu na sisi tunaweza tuka cheap in kwa namna gani. Lakini hiyo, siyo ahadi ya kujenga nyumba, ila tunakwenda ku-assess ili kuona umaskini wao na namna gani kama tunaweza tukapata uwezo wa kusaidia angalau bati moja mbili, lakini jukumu la msingi la kujenga nyumba ni lao wenyewe. Pili, misaada. Utaratibu wetu sisi kama centre Ofisi ya Waziri Mkuu huwa tunahamasisha jamii. Watu wenye nia njema, watu wenye mapenzi mema na wenzao kusaidia na Serikali huwa inatoa hizi fedha na msaada. Hata hivyo, tunategemea kule chini kwa sababu tumeunda Kamati za Maafa kutoka chini kwenye Kata, Wilaya na Mkoa. Hivyo, tunategemea Kamati zile za Maafa kwenye Kata, Wilaya na Mikoa. Kwa hiyo, tunategemea Kamati zile za Maafa kwenye maeneo yale ya maafa watatumia busara na watazingatia ukweli watagawa hivi vitu vizuri. Kamati za Maafa zinasimamiwa na wenyewe kwenye maeneo yale wale waliotuletea sisi taarifa. Kwa hiyo, kwa haraka haraka hivi siwezi kuamini kwamba misaada hii haikuwafikia, ila tunaweza tukaenda tuka assess vilevile ili kuona kwamba kweli ile misaada maana return za karatasi zimeletwa, lakini tunaweza tukaenda tukafanya ukaguzi kujua. 4 Nakala ya Mtandao (Online Document) Je, ile misaada iliwafikia walengwa? Hilo tunaweza tukafanya. Kwa kwaida wanaosimamia ugawaji wa misaada kama hii kwa wathirika ni Kamati ambazo zinaundwa kwa ushirikishwaji na wale wenye maafa wenyewe. MHE. OMARI RASHID NUNDU: Mheshimiwa Spika, kwa sababu haya maafa, Moto, Mafuriko ni vitu ambavyo haviepukiki vitakuwa vinatokea tu. Sasa Serikali imejipangaje, kuhakikisha kuwa kabla havijatokea yakaibuka maswali ya kuwa watu wamesaidiwaje. Imejipangaje kuona kuwa inakuwa na utayari katika ngazi hizo alizoongelea za Wilaya na Vijiji kwa yaliyotokea, basi kwa uchache tayari ziko hatua za kuanza kusaidia kabla ya misaada mikubwa haijaenda. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu kama ifuatavyo. Hayo anayoyasema ndiyo yanayofanyika, maafa kwanza yakitokea wenye jukumu la awali kabisa ni eneo husika la Wilaya na kwa kweli kwa hili nataka niwashukuru sana Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wote nchini ambao wamesimama kidete katika hatua za awali kabisa kuwasaidia wananchi wanaopata maafa katika maeneo yao. Kama nilivyosema wakati ule wa hotuba ya Bajeti ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Sheria ya Maafa inatukwaza kidogo kwa sababu haitupi uwanja mpana wa kufanya mambo haya. Kwa hiyo, tunaleta hapa Bungeni marekebisho ya sheria ili mambo yote haya mnayopendekeza yaweze kuingizwa kwa sababu kwanza hatuna huo mfuko. Fedha za maafa zenyewe hatuna. Kila yanapotokea ndiyo lazima tuombe Hazina, tunafikiri sasa its high time tuwe na mfuko wa Wilaya, mfuko Mkoani na tuwe na mfuko wa Kitaifa ambao una pesa ambazo zimepangwa kabisa na Bajeti ya Bunge kwamba hizi zipo na zinaweza kufanya jambo gani. Pengine hata haya anayosema Mheshimiwa Susan kwamba pengine kwa sheria ya sasa lakini pengine tunaweza tukarebisha sheria ili kuweza ku- accommodate watu mbalimbali wanaopata maafa hata kuwarudishia mali zao au mambo mengine ambayo wanakuwa wameathirika nayo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Nundu ni kwamba ni kweli tunafanya maeneo yale Kamati za Maafa zinafanya zinajitahidi sana na sisi centre tunasaidia. Hata hivyo, ili tuweze kufanya vizuri lazima tupitie upya sheria yetu. (Makofi) 5 Nakala ya Mtandao (Online Document) Na. 154 Kujenga Wodi katika Kituo cha Afya Tandahimba MHE. JUMA A. NJWAYO aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Mchichira kwa kushirikiana na Halmashauri yao ya Tandahimba wamejenga kituo cha afya lakini hakina wodi za kulaza wagonjwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ili kituo hicho kiwe na wodi za kutosha, hivyo kutoa huduma nzuri kwa wananchi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimwia Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo, Mbunge wa Tandahimba, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli miradi ya Ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati huibuliwa na wananchi wenyewe kupitia Mpango wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo yaani O&OD na kutekelezwa kwa

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    347 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us