1 Bunge La Tanzania Majadiliano Ya

1 Bunge La Tanzania Majadiliano Ya

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Ishirini na Sita - Tarehe 8 Julai, 2010 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO PAMOJA NA NAIBU WAZIRI WA KAZI, AJIRA NA MAENDELEO YA VIJANA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Pamoja na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kwa Mwaka wa Fedha, 2010/2011. MHE. FATMA ABDULLA TAMIM (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII): Taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Jamii Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Pamoja na Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 pamoja na maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hizo kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MHE. NURU AWADH BAFADHILI (K.n.y. WASEMAJI WAKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO PAMOJA NA WIZARA YA KAZI, AJIRA NA MAENDELEO YA VIJANA): Taarifa ya Wasemaji Wakuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezopamoja na Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MHE. JOEL N. BENDERA (K.n.y. WAZIRI WA NISHATI NA MADINI): 1 Randama ya Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa muujibu wa Kanuni ya 38 (5) inapotokea kwamba Waziri Mkuu kwa udhuru maalum hayupo basi hayapo maswali kwa Waziri Mkuu. Hiyo ndiyo hali iliyojitokeza leo. Kwa hiyo, tunaendelea. Tuna maswali tu ya kawaida ambayo tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, swali linaulizwa na Mheshimiwa Nuru Awadh Bafadhili. MASWALI NA MAJIBU Na. 186 Askari wa Usalama Kuhesabu Kura wakati wa Uchaguzi MHE. NURU AWADHI BAFADHILI aliuliza:- Kwa kuwa, kazi ya askari wa usalama n katika kipindi cha Uchaguzi ni kusimamia upigaji kura na sehemu ya kupigia kura, na kwa kuwa, Askari hao hawapaswi kujihusisha na kuhesabu kura:- Je, Serikali inasema nini juu ya Askari ambao huhesabu kura kwenye Uchaguzi mbali mbali? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nuru Awadhi Bafadhili, Mbunge, Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa hakika swali hili limekuja wakati muafaka kwa sababu tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu hivyo napenda kusema kwamba kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 sura ya 343 na sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1979 sura ya 292. Askari wa Usalama waliopangwa kazini kuhakikisha taratibu za Uchaguzi zinazingatiwa, wanawajibu wa kulinda usalama katika vituo vya kupigia kura, vituo vya kuhesabia kura na pia vituo vya kujumlishia kura. Wakati wa kutekeleza kazi hiyo askari wa usalama wanatakiwa kuwa nje ya vyumba au umbali wa kuweza kushuhudia vile vituo vya kupigia,kuhesabia na kujumlishia kura. Endapo itatokea vurugu kwenye kituo,Askari hao wa Usalama baada ya kupata maelekezo kutoka kwa msimamizi wa kituo au msimamizi wa uchaguzi au msimamizi msaidizi wa uchaguzi anaweza kuingia ndani ya chumba cha kura au kwenye kituo na kushughulikia vurugu hizo. 2 Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi, msimamizi wa kituo akisaidiwa na msimamizi msaidizi wa kituo ndiye mwenye jukumu la kuhesabu kura zilizopigwa na wapiga kura kwa kituo hicho na kazi hii hufanyika mbele ya Mawakala wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi husika na watu wengine waliotajwa kwenye sheria za Uchaguzi. Aidha, Serikali haijawahi kupokea malalamiko yoyote kuhusu Askari wa Usalama waliopangwa kulinda vituo vya kupigia kura kuhusika katika zoezi la kuhesabu kura. Hata hivyo, ikitokea Askari anaiingilia mchakato wa kuhesabu kura,atakuwa amevunja sheria za uchaguzi kama mtu mwingine yeyote, hivyo Askari huyo atawajibishwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi kama mtu mwingine yeyote. (Makofi) MHE. NURU AWADHI BAFADHILI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza:- (a)Kwa kuwa Askari hawa wa Usalama wanajua Mijini watu wameelimika kuhusu zoezi zima la kupiga kura na kuhesabu. Kwa hiyo, mambo haya zaidi wanayafanya Vijijini ambako wananchi wanawaogopa Askari. Je, Serikali inatuambia nini kuhusu elimu kwa wananchi wetu wa Vijijini kuhusu hatua mbalimbali la kutoka zoezi la kupiga kura mpaka la kuhesabu kura na kumwondoa Askari ambaye hahusiki? (b)Kwa kuwa, tunaambiwa kwamba Askari atakapokutwa anahesabu kura atawajibishwa. Je, watu hawa watakaomkuta Askari wapeleke wapi malalamiko yao wakati wananchi wetu hususani wa Vijijini wanaogopa Askari? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwanza sio kweli hata kidogo kwamba Watanzania Mijini na Vijinini wanaogopa Askari Polisi, Askari Polisi wanalinda usalama wa Raia na ni kimbilio la Raia muda wote, amjasikia habari hizo na sio kweli hata kidogo kwamba Watanzania wanaogopa Askari polisi. Pili Msimamizi Mkuu wa kituo ndiyo mtu mwenye mamlaka yote wakati huo. Kwa hiyo, matukio yeyote ya uvunjaji wa sheria za uchaguzi ikiwa ni pamoja na yale ambayo pengine yatatendwa na Askari Polisi, basi yapelekwe kwa Msimamizi wa Kituo au Msimamizi Msaidizi au Msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya au Jimbo. MHE. DR. WILLIBROD P. SLAA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza:- Kwa kuwa sasa tumeshuhudia kwa macho yetu, nimeshuhudia mwenyewe Kiteto, nimeshuhudia Busanda, nimeshuhudia Biharamulo wananchi wanapojitokeza wakakutana na Askari kabeba bunduki, wanarudi kule walikotokea. Haya tumeyaona kwa macho anaebisha abishe, nimeyaona Tarime wananchi wanakimbia hata mikutano hawahudhurii kwa sababu hawakuzoea kuona Vijijini 3 Maaskari wenye silaha, Waziri analieleza nini Taifa kwamba elimu kutolewa kwa Askari ni jambo muhimu ili wananchi wasiwaogope hawa Maaskari? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, Askari wanaolinda usala wa raia nchini kwetu wamekuwa wakitenda shughuli zao kwa muda mrefu sana. Tumeogopa wale wa kikoloni lakini sasa ni zaidi ya miaka 50 toka tuwe na Askari wetu wenyewe. Hivyo, basi iwapo kuna raia anamwogopa Askari basi anajidhania kwamba pengine ana makosa. Raia mwema ana sababu gani kumwogopa askari? Lakini la msingi hapa ni kwamba katika swali la msingi tuliulizwa kama tuna taarifa. Sisi taarifa tulizonazo ni kwamba wananchi wanaelewa vyema kabisa wajibu wa Askari kuwa ni kulinda usalama wao. (Makofi) MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: Mheshimiwa Spika, na mimi nakushukuru pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri. Mimi nina swali moja tu la kumwuliza. Katika majibu yake ametaja askari wa Usalama, sasa Askari wa Usalama katika mazingira ya Uchaguzi maana yake ni nini, ni Askari Polisi au ni Askari wa Usalama wa Taifa pamoja na polisi au hata Jeshi anaekuja pale pia ni Askari wa Usalama? (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa maana ya sheria ya Uchaguzi, askari wa Usalama ni Askari mwenye sare. (Makofi) Na. 187 Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu - CDA MHE. EPHRAIM N. MADEJE aliuliza:- Kwa kuwa, Serikali bado inayo dhamira ya kuufanya Mji wa Dodoma uwe Makao Makuu ya Serikali;lakini bado inaendelea kuimarisha miundombinu na kujenga majengo mbalimbali Mkoani Dar es Salaam. (a) Je, Serikali haioni kwamba haitimizi dhamira yake na kwamba hali hiyo inaweza kuwafanya wananchi wakose imani na Serikali yao? (b) Kama dhamira ipo. Je, Serikali inashindwaje kuweka bayana mikakati thabiti ya kujenga miundombinu muhimu kwa ajili ya kuhamisha Makao Makuu kuja Dodoma? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA URATIBU NA BUNGE alijibu:- 4 Mheshimiwa Spika, kabla sijajibu swali la Mheshimiwa Ephraim Nehemia Madeje, Mbunge wa Dodoma Mjini, lenye sehemu (a) na (b) napenda nitoe maelezo mafupi kama ifuatavyo:- Serikali ilianzisha Programu ya Ustawishaji Makao Makuu ambayo ilikuwa inalenga kukamilisha uhamishaji wa Mako Makuu yake kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 1973. Katika kipindi hicho,Serikali ilikuwa imejiwekea mkakati wa kuwezesha utekelezaji wa programu kwa kutenga shilingi za wakati ule milioni 370 kila mwaka kwa miaka 10 kuanzia mwaka 1973. Kwa bahati mbaya sana lengo hili halikuweza kufikiwa kutokana na uhaba wa Bajeti ya Serikali iliyosababishwa pamoja na mambo mengine Vita vya Kagera, kupanda kwa bei ya mafuta miaka ile ya 1980 na pia changamoto nyingine mbali mbali. Hii iliathiri sana uharakishaji wa ukuaji wa Makao Makuu ya Serikali Mjini Dodoma kwa vile huduma muhimu na miundombinu mbalimbali ambayo ingewezesha uhamishaji wa Makao Makuu katika Mji wa Dodoma hazikuweza kujengwa. Kutokana na changamoto hizi, Wizara nyingi zimelazimika kuendelea kubakia Dar es Salaam. Sasa baada ya maelezo haya napenda kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, sasa nijibu swali la Mheshimiwa Ephraim Madeje, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Dhamira ya Serikali ya kuhamia Mji wa Dodoma bado iko pale pale na itaonekana wazi wazi kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo itazinduliwa hivi karibuni. Kwa sasa Serikali inaweka juhudi kubwa kuiwezesha CDA pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi iweze kuchangia katika ujenzi wa Makao Makuu kwa kuweka huduma na miundombinu mbalimbali ili kuiwezesha Serikali kuhamia Dodoma. Aidha,Seriakli imelazimika kuendelea kuweka miundombinu na majengo Jijini Dar es Salaam ili kukidhi mahitaji yake kwa sasa wakati ikisubiri kuhamia

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    185 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us