NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Thelathini – Tarehe 18 Mei, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Nancy H. Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. Kwa niaba yake Mheshimiwa David Kihenzile. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 253 Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi MHE. DAVID M. KIHENZILE K.n.y. MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi na kuanza kutumia Hospitali ya Wilaya ya Mufindi? NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri. Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri. Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu katika Hospitali ya Halmashauri. Hadi Aprili 2021, ujenzi wa majengo saba ambayo ni jengo la utawala, jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje kwa maana ya OPD, jengo la maabara, jengo la mionzi, jengo la wazazi, jengo la kuhifadhia dawa, jengo la kufulia umekamilika na ujenzi wa wodi ya watoto na wodi ya magonjwa mchanganyiko kwa wanaume na wanawake upo katika hatua ya upandishaji wa ukuta. Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Mufindi. Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga shilingi milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti na wodi ya upasuaji kwa wanaume na wanawake. Hospitali ya Wilaya ya Mufindi imeanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje na inatarajiwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2022 hospitali hiyo itaanza kutoa huduma kwa zaidi ya asilimia 90 ya huduma zote zinazotakiwa kutolewa katika ngazi ya Hospitali ya Halmashauri. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa David Kihenzile, swali la nyongeza. MHE. DAVID M. KIHENZILE Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri lakini nataka niulize maswali madogo mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, moja, hospitali hiyo iko mbali na makazi ya watu, ni upi mpango wa Serikali sasa katika kujenga makazi kwa ajili ya watumishi wa hospitali hiyo? (Makofi) Mheshimiwa Spika, pili, ni upi mpango wa Serikali katika kutatua kero kubwa ya wataalam wa sekta ya afya katika zahanati na vituo vya afya vilivyopo katika Jimbo letu la Mufindi Kusini? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali madogo mawili ya Mheshimiwa David Kihenzile, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ameuliza hapa ni lini Serikali itajenga makazi kwa ajili ya watumishi wa afya wa Hospitali ya Halmashauri ya Mufindi. Nimueleze tu kwamba katika jitihada za Serikali, moja ya 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) jitihada kubwa ni kama tulivyoeleza katika jibu letu la msingi tumekuwa tukiongeza fedha kuhakikisha tunaboresha hospitali hiyo na kila mwaka tumekuwa tukitenga fedha. Kwa hiyo, nimueleze tu kwamba tutaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo kuanzia wodi, OPD pamoja na nyumba za watumishi kadri ya upatikanaji wa fedha. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi, Serikali ina nia njema kwenye suala hili na tutalifanyia kazi ombi lake na siyo tu kwa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi bali kwa nchi nzima katika vituo vya afya, zahanati pamoja na hospitali zetu. Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili kuhusiana na kero ya wataalam, Serikali inaendelea na ajira na katika kipindi hiki Serikali itaajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya zaidi ya 2,600. Katika mgawanyo huo, sehemu ya watumishi hao tutawapeleka katika Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi kwa ajili ya kupangwa kwenye vituo vyake vya afya. Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Abbas Tarimba, swali la nyongeza. MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa changamoto zilizoko katika swali la msingi ni sawa na zilizoko katika Jimbo langu la Kinondoni katika Kata ya Makumbusho ambako kuna dispensary ilianza kujengwa tangu mwaka 2019 na ilikuwa imalizike Aprili, 2020, sasa hivi ni mwaka mmoja haijamalizika. Pamoja na juhudi za Manispaa kusimamia ujenzi ule na Mfuko wa Jimbo, je, Serikali haiwezi ikatia mkono sasa kuhakikisha kwamba dispensary ile inamalizika ili wananchi wa Kata ya Makumbusho, Jimbo la Kinondoni waweze kupata huduma? Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza Mheshimiwa Abbas Tarimba, Mbunge wa Kinondoni, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ameiomba Serikali kuweka mkono katika Kata ya Makumbusho kwenye eneo ambalo limejengwa dispensary ambayo ilikuwa imepaswa kumalizika Aprili, 2020. Tunatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Halmashauri ya Kinondoni hususan katika sekta ya afya, tunatambua kazi kubwa anayofanya Mbunge katika Jimbo la Kinondoni na tunatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali kuboresha sekta ya afya nchini. Kwa hiyo, tumelipokea ombi lake lakini tutaendelea kusisitiza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni sisi pamoja na wao kwa pamoja tuimalize dispensary hii ili wananchi waanze kupata huduma za afya. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. Na. 254 Barabara ya Kiloba-Njugilo MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:- Je, ni lini barabara ya Kiloba – Njugilo yenye urefu wa kilometa 7 itajengwa ili kurahisisha mawasiliano ya wananchi na wanafunzi wanaokwenda Kata ya Masukulu – Rungwe? NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda, Mbunge Viti Maalum, kama Ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Kiloba-Njugilo ni barabara inayounganisha Kata mbili za Bujela na Masukulu. Kwa kutambua umuhimu wake, barabara ya Kiloba-Njugilo ipo kwenye hatua za uhakiki ili iweze kuingizwa kwenye Mfumo wa Barabara za Wilaya kwa maana ya DROMAS ili iweze kupatiwa fedha za Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo na ujenzi. Utaratibu wa kuingizwa kwenye mfumo wa barabara za Wilaya ukikamilika barabara hiyo itatengewa fedha kupitia fedha za Mfuko wa Barabara kwa maana ya Road Fund ili iweze kujengwa walau kwa kiwango cha changarawe na kuiwezesha kupitika katika majira yote ya mwaka. Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali imejenga Daraja la Kigange linalounganisha Vijiji vya Kiloba na Mwalisi kwa gharama ya shilingi milioni 46.8. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, swali la nyongeza. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza niishukuru sana Serikali kwa kukubali kuitengeneza barabara hiyo ya Bujela – Masukulu - Matwebe. Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, ni lini Serikali itaisaidia Sekondari ya Lake Ngozi iliyopo Kata ya Swaya ambapo ni ngumu kufikika majira ya mvua? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Serikali inajipangaje kuhusiana na barabara zote na madaraja ambayo yanaunganisha kati ya barabara na shule ambapo imewafanya wasichana wengi washindwe kwenda shuleni 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kutokana na mvua nyingi zinazonyesha zaidi ya miezi nane katika Wilaya ya Rungwe? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ametaka kufahamu ni lini Serikali tutasaidia kujenga barabara inayoelekea Sekondari ya Lake Ngozi kuhakikisha inapitika ili kusaidia wanafunzi ambao wanatumia barabara hiyo ili iweze kupitika kwa kipindi chote. Mheshimiwa Naibu Spika, nimuahidi kwamba Serikali tunaendelea kutenga fedha kuhakikisha barabara hizo zinapitika kwa wakati wote na tunazingatia maombi maalum kama haya ambayo Mheshimiwa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages204 Page
-
File Size-