Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Mbili – Tarehe 25 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MHE. PROF. JUMA A. KAPUYA – (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. JOSHUA S. NASSARI - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU Na. 255 Kibali cha Ajira Katika Ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji MHE. MWIGULU LAMECK MCHEMBA MADELU aliuliza:- Nafasi nyingi katika ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji vimeshikiliwa na watu wanao kaimu hivyo kupunguza ufanisi katika utendaji kutokana na kuchelewa kwa vibali vya kuajiri kutoka Serikalini:- (a) Je, ni lini Serikali itatoa vibali vya kuajiri watumishi katika ngazi hizo? (b) Je, Serikali itakuwa tayari kutoa mwongozo kuwa watumishi wa ngazi hizo wawe wenyeji/wazawa wa Wilaya husika? (c) Je, Serikali itakuwa tayari kutekeleza ukomo wa muda wa Kukaimu Kisheria? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIKOA (TAMISEMI) (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mwigulu Lameck Mchemba Madelu, Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, vibali vya ajira katika utumishi wa umma, hutolewa kwa nafasi za ajira mpya zilizoidhinishwa katika Ikama na kutengewa fedha katika Bajeti ya mwaka husika na kuidhinishwa na Bunge. Kati ya mwezi Julai, 2011 na Mei, 2012 Serikali imetoa vibali vya ajira kwa nafasi mpya 48,333 kuwawezesha waajiri kujaza nafasi katika kada mbalimbali zilizoidhinishwa katika mwaka wa fedha 2011/2012. Katika mwaka wa fedha 2012/2013 jumla ya nafasi 1,239 za kada za msingi zimeombwa na kuidhinishiwa fedha kama ifuatavyo: Afisa Tarafa nafasi 54, Mtendaji Kata nafasi 410, Mtendaji wa Kijiji nafasi 692 na Mtendaji Mitaa nafasi 83. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika kuajiri watumishi wake inazingatia Sheria na taratibu zinazozingatia Umoja wa Kitaifa na zinazotaka nafasi husika kujazwa kwa uwazi (Open Recrutment System). Hivyo si utaratibu wa Serikali kuajiri watumishi kwa misingi ya uwenyeji/uzawa waliokozaliwa kwani kufanya hivyo ni kinyume na ibara ya 22 (1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997, toleo la Mwaka 2008 inayompa fursa kila Mtanzania kufanya kazi yoyote iliyo chini ya mamlaka ya nchi. Aidha, Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma toleo la mwaka 2009 pamoja na Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria na. 18 ya mwaka 2007, zimeeleza kuwa ajira ya Utumishi wa Umma zitajazwa na watu wenye sifa kutoka sehemu yoyote nchini. Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuondoa changamoto za ajira za watendaji wa ngazi za msingi, Serikali imekwishaamua kuweka utaratibu utakaoziwezesha Halmashauri za Wilaya kuajiri zenyewe kada hizo ili kukabiliana na changamoto. Hatua inayofuata sasa ni kurekebisha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 na Kanuni zake ili iweze kuzingatia uamuzi huo. (c) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni D.24 (3) cha Kanuni za Kudumu, Toleo la mwaka 2009, muda wa Kukaimu nafasi ya Uongozi ni miezi sita. Katika kipindi hicho mamlaka za ajira zinatakiwa kuchukua hatua za kujaza nafasi husika. Serikali inakubaliana na rai ya Mheshimiwa Mbunge ya kutekeleza ukomo wa muda wa kukaimu kisheria. Hivyo ninatoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa nafasi husika zinajazwa mapema iwezekanavyo na kwa kuzingatia mwongozo wa makadirio ya ikama na mishahara wa mwaka 2009/2010 kama ulivyoidhinishwa kwa ajili hiyo. MHE. MWIGULU LAMECK MCHEMBA MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mheshimiwa Waziri Mkuu ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mheshimiwa Rais, ndiye Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya CCM. Utakumbuka kwenye Kamati Kuu ya Mwisho ya Mwaka jana tulipitisha uamuzi kwamba ngazi hizi ziachiwe jukumu la kuajiriwa watu hawa kupitia ngazi ya Halmashauri ili kuondoa ukiritimba. Lakini pia na kuzingatia hali halisi ya sasa kwamba watu wenye sifa za aina hii kufuatana na shule za Kata watapatikana kule kule na Wilayani. (a) Je, ni lini uamuzi huu tena umekuja kubadilika na kuja na majibu ya aina hii? (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya Serikali ili iheshimike ni kuajiri na kufukuza tumekuwa tukilia kila wakati kwamba waajiriwa wakikosea sehemu fulani katika Halmashauri wanahamishiwa sehemu nyingine kwa sababu uhamishaji unatokana na mwajiri kuwa wa ngazi ya juu. Je, kwa nini sasa tusiipe mamlaka Baraza la Madiwani la kuajiri hawa watumishi wadogo wadogo ili wanapokosea katika ngazi husika waweze kufukuzwa bila kusubiria kibali kutoka Makao Makuu? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwigulu Lameck Mchemba Madelu, Mbunge wa Iramba Magharibi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua kwamba Mheshimiwa Mwigulu Mchemba Madelu, anayezungumza hapa Mbunge wa Iramba ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, ninatambua hilo. Siwezi ku-doubt kabisa uelewa wake kuhusu jambo hili tunalolizungumza hapa. Kitu kinachosema hapa hizo kada zilizosemwa zote na kama anavyosemwa Mheshimiwa Mchemba ni kweli Serikali imekubali kwamba zote zirudishwe katika Halmashauri. Nakuomba nikutajie hawa ni pamoja na wahudumu wa Ofisi za Afya, Madereva, Maafisa Watendaji wa Mitaa, Maafisa Watendaji wa Kata, Wapishi, Madobi, Walinzi na Makatibu Muhtasi na wasaidizi mbalimbali. Anachosema ni kweli kabisa ambacho tunakisema hapa hawawezi ile Kamati ya ajira inapokutana katika Halmashauri ikimwita dereva inataka ku-recruit inamwuliza wewe ni mzaliwa wa hapa au siyo mzaliwa wa hapa? Ndicho hicho tu tunachosema hapa. Hicho unachokisema Mheshimiwa Mbunge ni sahihi kabisa unavyosema. Hapa nilipoulizwa ni kwamba tutoe mwongozo kuhusu uzawa ndicho kilichosemwa hapa ndicho tunachosema ndio maana nimekwenda nika- quote Katiba inayosema kwamba mtu yeyote katika Tanzania mahali popote pale anaweza akapata ajira. Hili tunayozungumza hapa kwa vile na wewe amekutaja hapa ili kama mtauliza maswali ya nyongeza mwulize vizuri ili niwaeleze kwa sababu hapa nimejiandaa vizuri, hakuna ugomvi kuhusu kuajiri hawa watu katika ngazi ya Halmashauri, hiyo tumesharudisha. Sasa ataniuliza swali kwa nini hamfanyi? Ile sheria iliyowachukua hawa waliotamkwa hapa ikawapeleka kule utumishi kwa maana ya kuwapeleka kule kwenye kamisheni, sheria ile ilibadilishwa. Kwa hiyo, sheria ile sasa inafanyiwa kazi na cabinet imekwishakupitisha jambo hili sasa kinachofanyika hapa sasa hivi ni kuleta sasa mabadiliko haya na AG ataileta hapa hivi karibuni. La pili, mtu amefanya makosa katika Halmashauri moja anahamishwa anapelekwa Halmashauri nyingine, Mheshimiwa Mwigulu Mchemba yuko right na tumesema akifanya makosa mtu pale Magu hatumpeleki Songea tunamwacha pale pale Magu na tutashuka naye pale pale Magu tena jumla jumla. (Makofi) Kwa hiyo, sasa kama ninyi mnayo mifano na hili limepita mpaka kwenye ile Kamati kwenye Baraza ikaonekana kuna makosa yamefanyika pale na hasa hasa kwa yale yaliyoonekana na CAG report amesema hapa Mheshimiwa Hawa Ghasia na wale wengine wote waliohusika wameeleza hapa kwamba utaratibu ni kwamba hahamishwi tena anabaki pale pale. (Makofi) MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nilikuwa naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri je, Serikali inajua umuhimu wa watendaji wa vijiji, umuhimu wa watendaji wa Kata na kama inajua kwa nini inachelewesha kutoa vibali? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Richard Ndassa, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, nalo hili nililieleze vizuri, vibali vilivyotoka ni 1239 nataka nikuambie hapa Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu mimi najua kwamba swali hili litaulizwa hivyo vibali vilivyotolewa ndivyo vilivyoombwa vyote mpaka kule kwako kule Peramiho vyote ndivyo vilivyoombwa. Mtu akitaka akacheki na nimecheki mpaka asubuhi na Mkurugenzi Mhusika nikamwambia una hakika hakuna wengine, sasa inawezekana kabisa kwamba kule anakozungumza Mheshimiwa Mbunge, wako wengine wamefariki, wengine wameondolewa na nini, wengine wamestaafu na nini hii inaweza ikawa ni kitu kingine kipya. Lakini nataka nikuthibitishie katika nyumba
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages411 Page
-
File Size-