NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _______ MAJADILIANO YA BUNGE _______ MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao cha Saba - Tarehe 13 Novemba, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tuketi. Katibu. NDG. YONA KIRUMBI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kuhusu Azimio la Kuridhia Marekebisho ya Kigali chini ya Itifaki ya Montreal kuhusu kupunguza Uzalishaji na Matumizi ya Kemikali Jamii ya Hydrofluocarbons (HFCS) chini ya Itifaki ya Montreal inayohusu Kemikali zinazomomonyoa Tabaka la Ozoni (Kigali Amendment on Phasing Down Hydrofluorocarbons (HFCs) to the Montreal Protocol on Ozone Depleting Substances); na Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya SADC ya Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (The Southern African Development 3 Community SADC – Protocol on Environmental Management for Sustainable Development). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. KANALI (MST) MASOUD ALI KHAMIS - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la Kuridhia Marekebisho ya Kigali chini ya Itifaki ya Montreal kuhusu kupunguza Uzalishaji na Matumizi ya Kemikali Jamii ya Hydrofluocarbons (HFCS) chini ya Itifaki ya Montreal inayohusu Kemikali zinazomomonyoa Tabaka la Ozoni (Kigali Amendment on Phasing Down Hydrofluorocarbons (HFCs) to the Montreal Protocol on Ozone Depleting Substances); na Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya SADC ya Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (The Southern African Development Community SADC – Protocol on Environmental Management for Sustainable Development) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa ratiba ya kikao cha leo Serikali inawajibika kuweka pia mezani Azimio la Kuridhia Itifaki ya Marekebisho ya Mkataba wa Marrakesh ambayo inawasilishwa na Wizara ya Viwanda. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda na Biashara, Injinia Stella Manyanya. NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Maelezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki ya Marekebisho ya Mkataba wa Marrakesh ulioanzisha Shirika la Biashara la Dunia (Protocol Amending the Marrakesh Agreement Establishing the World Trade Organization). 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SULEIMAN A. SADDIQ – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la Bunge kuridhia Itifaki ya Marekebisho ya Mkataba wa Marakesh ulioanzisha Shirika la Biashara la Dunia yaani Protocol Amending the Marakesh Agreement Establishing The World Trade Organization. MHE. JOYCE J. MUKYA (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA): Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Azimio la Kuridhia Marekebisho ya Kigali chini ya Itifaki ya Montreal kuhusu kupunguza Uzalishaji na 4 Matumizi ya Kemikali Jamii ya Hydrofluocarbons (HFCS) chini ya Itifaki ya Montreal inayohusu Kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni (Kigali Amendment on Phasing Down Hydrofluorocarbons (HFCs) to the Montreal Protocol on Ozone Depleting Substances); na Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya SADC ya Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (The Southern African Development Community SADC – Protocol on Environmental Management for Sustainable Development). MHE. CECIL D. MWAMBE (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA): Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Marakesh ulioanzisha Shirika la Biashara la Dunia (Protocol Amending The Marakesh Agreement Establishing The World Trade Organization) MWENYEKITI: Ahsante sana. Katibu! 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. YONA KIRUMBI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 85 Kuongeza Madaktari Hospitali ya Gonja – Same MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Serikali inashirikiana na Hospitali ya Gonja chini ya KKKT na Hospitali hiyo inatoa huduma za upasuaji wagonjwa wengi kuliko Hospitali ya Wilaya ya Same. Aidha, Jimbo la Same Mashariki lenye Kata 14 lina Kituo kimoja tu cha Afya kilichoboreshwa hivyo kusababisha msongamano katika Hospitali ya Gonja:- Je, ni lini Serikali itaongeza madaktari katika Hospitali ya Gonja ili iweze kuhudumia Kata tisa ambazo wagonjwa wake wanapata shida sana kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu Hospitali ya Wilaya ya Same? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Naghenjwa Livingstone Kaboyoka, Mbunge wa Same Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Gonja ina jumla ya watumishi 50, kati ya hao watumishi 10 ni waajiriwa wa Serikali. Ili kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya Same Serikali imepeleka watumishi wa kada mbalimbali za afya 68 katika Halmashauri ya Wilaya ya Same kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Oktoba, 2019. Serikali itaendelea kuajiri na kuwapanga watumishi wa kada mbalimbali za afya nchini kwa kutoa kipaumbele kwenye maeneo na vituo vyenye upungufu mkubwa ikiwemo Hospitali ya Gonja. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kaboyoka. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA Mheshimiwa Mwenyekiti, yeah, nashukuru kwa majibu hayo. Mheshimiwa Mwenyekiti, nipende kumueleza Waziri kwamba hospitali hii inafanya operations nyingi kuliko hata Hospitali ya Wilaya ya Same, na wagonjwa wengi wanapenda kuitumia. Niombe tu kwamba ufanye tathmini kuona kwamba kwa volume ya wagonjwa wanaokwenda hospitali ile, je, madaktari hao wanatosheleza? MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Kandege kwa kifupi tu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, niruhusu kwanza nimpongeze kwa dhati kabisa jinsi ambavyo Mhehsimiwa Mbunge amekuwa akipigania suala zima la afya kwa Wananchi wa jimbo lake na tulipata fursa ya kuteta na akasema aneo ambalo fedha zikipatikana tuongeze kituo cha afya. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ni ukweli usiopingika kwamba Hospitali ya Wilaya ya Same ina idadi kubwa ya Wananchi ambao wanafanyiwa upasuaji ukilinganisha na hiyo ya Gonja; lakini pia ni ukweli usiopingika kwamba tunashukuru kazi kubwa inayofanywa na hospitali hii na kwa kadri nguvu itakavyoongezeka na kupata wataalam wa kutosha hatutasahau kupeleka Hospitali ya Gonja. MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa Aysharose N. Matembe Mbunge wa Viti Maalum, bado linaelekezwa Ofisi ya Rais TAMISEMI. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 86 Zahanati ya Mtisi Kuwa Kituo cha Afya MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:- Kata ya Mtama katika Manispaa ya Singida haina Kituo cha Afya kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wake na Sera ya Serikali inaelekeza kila kata kuwa na kituo cha afya. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kuifanya Zahanati ya Mtisi kuwa kituo cha afya, ambayo ujenzi wake umekuwa wa kusuasua kutokana na Serikali kutopeleka fedha za kutosha NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aysharose Ndogholi Matembe, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali imeidhinisha kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya Mtisi kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida. MWENYEKITI: Ahsante kwa majibu safi kabisa, mafupi, to the point. Mheshimiwa Ndogholi. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii, na namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI. Ninalo swali dogo moja la nyongeza:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwa kuwa kuna umbali mrefu kutoka Kata ya Mtamaa hadi kufika Mjini kwenye hospitali ya mkoa; je, Serikali ina mpoango gani wa hara 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kuhakikisha kwamba sasa Zahanati hii ya Mtisi inakuwa kituo cha afya? Nakushukuru. MWENYEKITI: Ahsante. Jibu kwa swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, niruhusu pia nimpongeze Mheshimiwa Matembe kwa kazi kubwa ambayo anafanya katika kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma iliyobora ya afya. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu langu la msingi nimemhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tumetenga shilingi milioni 200. Shilingi milioni 200 zikipatikana tafsiri yake ni kwamba tunakwenda kuboresha hiyo zahanati, na mwendo ni kuhakikisha kwamba igeuke kutoka zahanati na kuwa kituo cha afya hivyo, namuomba Mheshimiwa Mbunge avute subira, tukiahdi tunatekeleza. MWENYEKITI: Mheshimiwa Getere. MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mheshimiwa Mwenyekiti, Zahanati ya Sanzantsi imejengwa toka Mwaka 2014 na imekuwa na vikwazo vingi ikiwemo kujenga
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages191 Page
-
File Size-