Majadiliano Ya Bunge ______

Majadiliano Ya Bunge ______

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA TISA Kikao cha Tatu – Tarehe 1 Novemba, 2012 (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae! Katibu tuanze! MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Kwa bahati nzuri Kiongozi wa Kambi ya Upinzani yupo, tulimsikia huko kwao Hai, lakini kumbe amerudi. Mheshimiwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani! MHE. FREEMAN A. MBOWE – KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kwanza ya kumwuliza Waziri Mkuu swali. 1 Mheshimiwa Waziri Mkuu, tangu wakati wa Bunge la bajeti ilitolewa taarifa rasmi ndani ya Bunge ya kuwepo kwa mabilioni ya fedha za kigeni ambazo zimehifadhiwa katika akaunti za viongozi waandamizi wastaafu na wasio wastaafu katika mabenki ya Uswisi, na Serikali ilitoa kauli kwamba italifanyia kazi jambo hili ambalo ni sensitive sana na hadi hatua ya sasa hatujasikia tamko lolote la Serikali au mkakati wowote wa Serikali wa kujua ukweli wa taarifa hizo, pili, ku-disclose majina ya wahusika na tatu kuchukua hatua za recovery kwa sababu ya faida ya uchumi wa nchi yetu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, una kauli gani ya kuliambia Bunge na kuwaambia Watanzania kuhusu Serikali unayoiongoza ina mkakati gani? SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu! WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mbowe kwa swali lake na ninaomba nirudie niliyoyasema. Niliahidi kwamba hili jambo kwa sababu ya uzito wake na ukubwa wake na involvement ya mambo yaliyokuwa yamejitokeza kwenye vyombo tukasema tutahitaji na sisi kulifanyia uchunguzi wa kina ili tuweze kubaini ukweli na ni hatua stahiki za namna gani zinaweza kuchukuliwa. Sisi hiyo kazi tumekwishaanza kuifanya kwa hiyo tutakapokuwa tumemaliza basi tutatoa kauli kama ilivyo kawaida yetu. SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Mbowe! Labda wewe una majina tayari. (Kicheko) 2 MHE. FREEMAN A. MBOWE – KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Waziri Mkuu, fedha zilizotoroshwa nchini na kuhifadhiwa katika benki za nje hazipo Uswisi peke yake, kuna mabilioni ya dola yamehifadhiwa katika akaunti za nchi za nje katika visiwa mbalimbali ambavyo havitozi ushuru wanaita ni tax havens, kwa mfano Luxernburg, Mauritius, Dubai, British Virgin Ireland, Jews kule Chaim Ireland pamoja na vingine vingi kama Grenada, Mauritius na kadhalika. Mheshimiwa Waziri Mkuu, na hizi fedha ni fedha nyingi za Watanzania ambazo zimepelekwa na wafanyabiashara na vilevile zimepelekwa na viongozi wastaafu na viongozi waliopo Serikali leo na mashirika yake, katika pamoja na mambo mengine dhamira ya kukwepa kodi kwa sababu katika visiwa hivi kodi hazitozwi. Waziri Mkuu, Benki ya Dunia ina kitengo kinachoitwa Assets Recovery Unit ambacho kinasaidia mataifa mbalimbali kujua ukweli kuhusu fedha za nchi ambazo zimehifadhiwa katika mataifa ya nje. Ni kwa nini mpaka leo Serikali yako haijatumia kitengo hiki? Ni kwa nini basi kwa sababu kitengo hiki kipo na kwa sababu uchunguzi umesema hili ni jambo zito, tuwaachie basi World Bank kitengo hiki Serikali iombe kibali cha kusaidia ku-recover fedha hizi na kujua wahusika badala ya kuwaachia vyombo vya ndani ambavyo pengine vinaonekana vinashiriki katika kuhifadhi wale wahalifu? (Makofi) SPIKA: Ahsante! Mheshimiwa Waziri Mkuu! 3 WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbowe anaweza akalirudia swali hili mara mbili au tatu na mimi bado nitakujibu hivyohivyo, kwamba jitihada zinafanyika na zitakapokamilika tutatoa maelezo. Sasa haiwezekani mambo makubwa haya au allegations nyingi kiasi hiki ukategemea kwamba ndani ya wiki moja au mbili au tatu itakuwa imekamilika, hata kidogo! Yes! Kwa hiyo, tukishakamilisha tutalirejesha. SPIKA: Ahsante, sasa kama wanajua wawe wanasaidia pia. Sasa tunaendelea na swali lingine, Mheshimiwa Godfrey W. Zambi! MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika, naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri Mkuu swali lifuatalo. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwenye Bunge la Bajeti la mwaka huu wa fedha mwezi wa nane, nikichangia hotuba ya ofisi yako nilihoji namna ambavyo Bodi ya Kahawa imeundwa bila kuzingatia sheria lakini pia na kanuni zake kutungwa bila kushirikisha wadau. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wewe mwenyewe katika maelezo yako na baadaye Waziri wa Kilimo akitoa maelezo ya nyongeza mlieleza kabisa kwamba ni kweli mmebaini kwamba sheria ya Kahawa ya mwaka 2001 Namba 23 imekiukwa na kwa maana hiyo mtaivunja au kurekebisha ile Bodi. Leo ni miezi mitatu tangu nimezungumza hapa Bungeni hakuna hatua iliyochukuliwa. 4 Je, unawaeleza nini Watanzania na wadau wa zao la Kahawa kuhusiana na jambo hili? SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu! WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kwenye Bunge lililopita suala hili lilijitokeza na kusema kweli baada ya pale tumefanya kazi kubwa ya kuchunguza kwa sababu kulikuwa na madai mengi lakini moja ilikuwa ni suala hili la mgongano wa kimaslahi ambalo lilidaiwa kwamba limekuwa likijitokeza dhidi ya Mwenyekiti wa Bodi lakini kulikuwa na madai vilevile ya baadhi ya wajumbe wa Bodi ile kuwa wameingia au wameteuliwa bila kuzingatia misingi ya kikanuni na kisheria lakini vilevile kulikuwa na madai mengine ya jumla jinsi ambavyo Bodi ilikuwa inaendesha shughuli za Kahawa. Kwa hiyo, tumelifanyia kazi. Naweza nikasema ni kama tumemaliza kwa maana ya kupata maelezo kutoka pande zote zinazohusika lakini tulichofanya tumelazimika sasa kumshauri mwenye mamlaka ambaye ndiye anafanya uteuzi wa Mwenyekiti ili yale mengine yaweze ku-flow bila matatizo makubwa. Kwa hiyo, tunaamini akishatupatia maelekezo yake basi zoezi litakamilika. SPIKA: Ahante, Mheshimiwa Zambi, swali la nyongeza! MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika, swali la nyongeza ni kwamba nilipokuwa nauliza swali la msingi nilizungumza masuala mawil ya msingi na la kwanza umelijibu vizuri nashukuru kwa hatua za Serikali ambazo zinaelekea kuchukuliwa. 5 Lakini sehemu ya pili inahusiana na kanuni za mwaka mwaka 2012 ambazo zimeruhusu ununuzi wa Kahawa mbichi au Cherry na bila kuzingatia maamuzi ya wadau wa zao la Kahawa lenyewe na tunakwenda karibu kwenye msimu mwingine wa zao la Kahawa kwa maana ya mwaka 2012/2013. Waziri Mkuu, unawahakikishia nini wadau wa zao la Kahawa kwamba mpaka msimu unaofuata wa Kahawa kanuni hizo zitakuwa zimesharekebishwa tayari? SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu! WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli lakini hilo niseme tu nilipitiwa kulieleza vilevile. Tulichofanya baada ya mjadala Bungeni sisi tulikaa Serikali na tumepitia kanuni zote zinazodaiwa za miaka ya tangu 2009 mpaka 2012, tumejaribu kutazama vilevile namna wadau wakubwa walivyoshirikishwa katika zoezi lile na kubaini maeneo ambayo tunafikiri yawekwe kwa namna ambayo itaweza kweli kusaidia kujibu maslahi ya Watanzania. Kwa hiyo, nataka nikuhakikishie Mheshimiwa Zambi kwamba tunakwenda na mazoezi yote mawili kwa wakati mmoja, imani yangu ni kwamba kabla ya msimu ujao hili zoezi juu ya kanuni na hili la Bodi pamoja na wajumbe wengine wa Bodi tutakuwa vilevile tumeyakamilisha. 6 SPIKAl: Ahsante, tunaendelea na Mheshimiwa Mohamed Habibu Juma Mnyaa! MHE. ENG. MOHAMED HABIB JUMA MNYAA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa masikitiko ni kwamba nchi yetu hivi karibuni imeingia katika ….. SPIKA: Sauti, halafu muwe brief, naomba muwe brief! MHE. ENG. MOHAMED HABIB JUMA MNYAA: Nchi yetu imeingia katika machafuko ambayo kumetokea uvunjifu wa haki za binadamu. Kwa mwezi mmoja tu uliopita wa Oktoba tumeshuhudia kwa kesi ya kuuawa kwa RPC Barlow Mwanza, kijana Koplo Said Abdulrahman kule Bububu Zanzibar, kijana Salum Hassan Mhaju Amani wa Feshi Zanzibar na hivi juzi siku ya Eid el Haji itakuwa tarehe 26 akakamatwa kijana Hamadi Ally Kaini, Nyerere Zanzibar na Polisi pamoja na vikosi vingine wasiopungua 20. Baba yake mzazi kwenda kuuliza akafukuzwa na Polisi. Lakini kijana yule baadaye siku ya pili baada ya Baba yake kufukuzwa kwenye vituo vyote vya kesho yake akaambiwa mtoto wake amefariki nenda Mochwari katika hospitali ya Mnazi mmoja na akaonekana na madonda makubwa, kafariki mikononi mwa Polisi. Je, ni kwa nini Jeshi la Polisi linashiriki katika uvunjifu wa haki za binadamu mkubwa nchini na mauaji makubwa, na nini hatua za Serikali itakazochukua kukomesha mambo hayo? SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu! 7 WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijaribu kutoa maelezo kidogo tu kuhusiana na swali zito la Ndugu yangu Mheshimiwa Mnyaa. Mauaji yoyote yanapotokea ni mauaji, na kwa hiyo taratibu za kisheria ni lazima zizingatiwe na kama kutatokea kama upo ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba mauaji yale ni ya makusudi wote tunajua kwamba sheria zinataka kitu gani kichukuliwe dhidi ya mhalifu huyo. Kama itatokea kwamba ni mauaji ambayo yataelezwa kwamba hayakuwa ya kukusudia vilevile hatua za kisheria ambazo ni lazima zichukuliwe na mtu apate adhabu stahiki. Sasa kwa kila tukio la mauaji linalotokea kubwa ni uchunguzi unaofuatia baada ya hapo. Umetaja RPC Mwanza na yako mengine mengi ambayo vilevile hukuyataja lakini yametokea, na kila hilo lina maelezo yake na hatua ambazo zimechukuliwa kwa kila moja. Sasa bahati mbaya hili la Zanzibar ambalo umelieleza la juzi sikuwa na taarifa nazo mimi. Lakini tunachoweza kuahidi tu ni kwamba kama limetokea uchunguzi stahiki utachukuliwa na kama wapo ambao wamehusika na jambo hilo ni dhahidi kabisa hatua zinazostahili zitachukuliwa. SPIKA: Mheshimiwa Mnyaa kwa kifupi swali la nyongeza! MHE. ENG. MOHAMED HABIB JUMA MNYAA: Mheshimiwa Spika, nashukuru! Mheshimiwa Waziri Mkuu, uchunguzi wa kisayansi ulifanyika na watu wakakamatwa katika kesi ya Mwanza, 8 na Zanzibar kuna watu wakakamatwa katika kesi ya

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    243 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us