24 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 24 Aprili, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAJI: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maji kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. AMINA N. MAKILAGI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI):- Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 24 APRILI, 2013 NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Makilagi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Kinamama wa CCM Tanzania. Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani. Namwona Mheshimiwa Cecilia Paresso. MHE. CECILIA D. PARESO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA MAJI):- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Maji Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MASWALI NA MAJIBU Na. 95 Serikali Kushindwa Kulipa Madai Mbalimbali ya Wafanyakazi MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA (K.n.y. MHE. DAVID E. SILINDE) aliuliza:- Miongoni mwa malalamiko makubwa ya wafanyakazi kwa Serikali ni kushindwa kulipa malimbikizo yao ya mishahara, likizo pamoja na makato mengine. (a) Je, ni lini Serikali itayashughulikia matatizo haya na kuwalipa wafanyakazi stahili zao? (b) Je, kwa nini Serikali imekuwa ikipuuza malalamiko ya wafanyakazi hao na kuyafanya yaonekane sio ya msingi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA aljibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa David E. Silinde, Mbunge wa Mbozi Magharibi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- 2 24 APRILI, 2013 (a) Serikali imekuwa ikilipa madai ya malimbikizo ya mshahara ya watumishi wa Umma kulingana na uwezo wake ambapo katika mwaka wa fedha 2011/2012, Serikali ililipa madai ya malimbikizo ya mshahara kwa watumishi 54,010 yenye jumla ya shilingi 72,351,994,390.92/-. Aidha katika mwaka wa fedha 2012/2013 Serikali imeendelea kulipa madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma hadi kufikia Machi, 2013 jumla ya madai ya watumishi wa umma 11,820 kati ya watumishi 52,039 wamelipwa malimbikizo ya mishahara na kiasi cha shilingi 12,603,190,834/- kimetumika. Malipo ya malimbikizo ya watumishi 27,245 yenye thamani ya shilingi 16,089,986,605/- yalikuwa yameshahakikiwa na yanasubiri kufanyiwa malipo kutegemeana na upatikanaji wa fedha. Madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi 12,974 lenye thamani ya shilingi 12,588,847,207/- yalikuwa kwenye hatua ya uhakiki kabla ya kuingizwa kwenye mfumo. Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuepuka tatizo la malimbikizo ya mshahara vilevile Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali iliyojiwekea kama ifuatavyo:- (i) Serikali imeanza kutumia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mshahara (Human Capital Management Information System (HCMIS) katika kushughulikia mishahara ya watumishi wa umma pale mwajiri alipo ili kuepuka ucheleweshaji. (ii) Kutekelezwa kwa Waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Na.1 wa mwaka 2009 kuhusu udhibiti na ongozeko la madeni ya Serikali kwa watumishi wa Umma, Waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Na.1 wa mwaka 2010 kuhusu uwajibikaji katika kusimamia rasilimali watu Waraka wa Katibu Mkuu Utumishi Na. 1 wa mwaka 2011 kuhusu kuimarisha usimamizi wa rasilimali watu Waraka wa Hazina Na. 2 wa mwaka 2010 kuhusu uwajibikaji na udhibiti katika usimamizi wa malipo ya mishahara. 3 24 APRILI, 2013 (b) Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na hatua hizi nilizozitaja hapo juu sio kweli kwamba Serikali imekuwa ikipuuza malalamiko ya wafanyakazi kwa kuwa kwa nyakati mbalimbali ikipokea, huhakiki na kulipa madai ya malimbikizo ya mshahara na matumizi mengineyo. (Makofi) MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa Serikali imekiri kwamba imeanza kulipa madeni ya wafanyakazi wakiwemo walimu kuanzia mwaka 2011/2012 lakini kutokana na taarifa tulizo nazo ni kweli kwamba kuanzia mwaka 2011 kushuka chini bado kuna watumishi hususan walimu ambao wana malimbikizo ya mishahara yao na stahili zao hususan Chama cha Walimu ambacho kimetoa taarifa kwamba mpaka sasa hivi kinaidai Serikali jumla ya shilingi bilioni 27. Je, ni lini Serikali italipa malimbikizo ya watumishi hawa hususan walimu ili elimu yetu iendelee kuwa endelevu na bora? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika Bajeti ya mwaka jana tulipitisha hapa fedha za kuwalipa walimu ambao watafanya kazi katika mazingira magumu jumla ya shilingi 500,000/-. Lakini mpaka sasa hivi kuna malalamiko makubwa ya walimu hususan ni vijijini wanaofanya kazi katika mazingira hayo magumu kwamba zile fedha hazijalipwa mpaka sasa hivi na kwa taarifa tulizo nazo ni kwamba zile fedha zilitoka kwa wafadhili na Wizara imetumia katika shughuli nyingine. Je, ni utaratibu gani uliotumika kwa Wizara kubadilisha matumizi ya fedha hizo bila kwanza kuleta hapa Bungeni? Ahsante sana. WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA ELIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, moja ni kwamba Julai, 2011 wakati Chama cha Walimu kilipotangaza kwamba kinaidai Serikali shilingi bilioni 29, ilikuwa inajumuisha malimbikizo ya madeni yote mpaka kipindi hicho. 4 24 APRILI, 2013 Lakini Serikali ilifanya hatua ya kukaa nao pamoja baada ya kutangaza hivyo, ikaamua kuhakiki pamoja na CWT na ikagundulika kwamba sio bilioni 29, waliyokuwa wanasema bali ni shilingi bilioni 52. Serikali ikatenga fedha hizo ikaanza kuzilipa awamu kwa awamu lakini kwa njia uharaka kwa sababu ilipangwa mishahara ilipwe na Hazina na fedha zisizokuwa za mishahara italipwa na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu. Mpaka Januari mwaka huu 2013 deni lile la bilioni 52 pesa zote zimekwishalipwa na hakuna pesa ambayo haijalipwa. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, nina hakika kwamba kuanzia pale tulipokubaliana hivyo madeni yaliendelea kujijenga lakini tuko katika mkakati kama alivyosema, alitangulia kujibu swali hili kwamba tuko katika mkakati wa kuhakikisha kwamba tunadhibiti na haturudii tena kurundikana na madeni hayo kwa miaka ijayo ili tuwaondoshee adha walimu katika nchi yetu. Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hili la pili linalohusu shilingi 500,000/- zile za mazingira magumu ambazo tumepewa na wahisani; tulipewa fedha hizo kwa mwaka mmoja na kwa walimu tu. Wakati zinaandaliwa kulipwa ikazuka mgogoro kwamba wale wanaoripoti mwaka juzi ule ndiyo wanalipwa posho zile za kuingia katika mazingira magumu. Lakini Walimu waliokuwepo nao wakadai kwamba sisi je, ambao tupo tayari hapa posho zetu ziko wapi. Lakini katika mazingira tuliyonayo kuna watumishi wengi tu kwenye Wilaya hizo kama waganga na kadhalika ambao wakaja juu nao. Serikali ikalazimika ku-hold na kuzungumza na mhisani ili zitumike zile pesa kwa namna nyingine ya kuwafaa walimu hawa kuliko kuwapa posho ambayo tayari imeshaingia katika mgogoro. (Makofi) 5 24 APRILI, 2013 MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa mujibu wa Katiba kifungu cha 20 (1) na (4) suala la wafanyakazi kuwa wanachama wa chama chochote cha wafanyakazi ni suala la hiari. Sasa hivi karibuni kuna kesi moja pale manispaa ya Kigoma Ujiji ya walimu kuendelea kukatwa asilimia mbili na Chama cha Walimu. Tatizo lililopo ni mwajiri kukataa kuondoa yale makato na kesi ilishaisha Mahakamani. Suala hili halipo Mahakamani kama Mheshimiwa Naibu Waziri alivyoeleza. Je, Waziri yupo tayari kuweza kusimamia suala hili ili kuhakikisha kwamba walimu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambao wameshaomba kujiondoa na shauri lilishakwisha Mahakamani ili makato yao haya ya asilimia mbili yaweze kusimama mara moja ili wizi huu au tatizo hili la Chama cha Walimu kuendelea kuwakata pesa zao ambazo wao hawako hiari iweze kukoma? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Machali, swali la msingi linahusu malimbikizo ya mishahara lakini namwona Mheshimiwa Waziri Kazi na Ajira. WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Chama cha Wafanyakazi ni chama cha hiari na tunaomba wafanyakazi wote wajue hivyo. Kwa hiyo, walimo kama wafanyakazi wengine kuingia CWT lazima waingie kwa hiari kwa kujaza fomu na kwa kujaza fomu nyingine ambayo inaruhusu makato. Lakini tatizo la walimu ni kwamba katika Sheria hiyo wanapokuwa wafanyakazi wanapoingia kwenye chama na ni zaidi ya asilimia 50 kuna kitu kinaitwa Wakala wa kusaidia mazungumzo na mwajiri kwa chama husika. Kwa hiyo, walimu kinachowakumba ni hicho. 6 24 APRILI, 2013 Lakini tumeshaagiza vyama vyote vituletee taarifa ni wafanyakazi wangapi wanaowakata na ni wafanyakazi wangapi wanaokatwa hiyo ada ya uwakala. Chama cha Walimu wametuambia by June, 2013 watakuwa wametuletea hiyo taarifa na tumewaagiza pia watoe elimu kwa wafanyakazi wao kabla hawajawakata hiyo ada ya uwakala. Na. 96 Tatizo la Ulipaji wa Mafao ya Wastaafu MHE. SAID AMOUR ARFI aliuliza:- Kumekuwepo na tatizo sugu la kulipa mafao ya wastaafu na mirathi kwa waliokuwa watumishi wa umma. Je, ni sababu zipi zinazopelekea Serikali isilipe stahiki hizo? NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha napenda kujibu swali la Mheshimiwa Said Amour Arfi, Mbunge wa Mpanda Mjini, kama ifuatavyo:- Mhehsimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa inalipa stahiki za wastaafu na warithi wa mirathi kwa wakati pale nyaraka na kumbukumbu kamilifu zinapofikishwa Hazina. Mheshimiwa Naibu Spika, sababu kubwa inayosababisha malipo tajwa kuchelewa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages242 Page
-
File Size-