MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Pili

MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Pili

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Pili – Tarehe 1 Aprili, 2020 (Bunge Lilianza Saa Nane Mchana) Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alikalia Kiti D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaanza Mkutano wetu wa Kumi na Tisa kikiwa ni Kikao cha Pili katika utaratibu mpya kama nilivyokuwa nimeelekeza jana. Kama nilivyoahidi kwamba tutakuwa tunaendelea kuboresha hapa na pale kwa kadri ambavyo tunaendelea kupata ushauri kutoka kwenu Waheshimiwa Wabunge wa mahali gani na namna gani tuendelee kuboresha. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI SPIKA: Hati za Kuwasilisha Mezani, Waheshimiwa Mawaziri mtaziwasilisha hapo hapo kwenye microphone zenu. Tuanze na Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Mheshimiwa Jenista Mhagama. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ya Makadirio ya Bajeti ya mwaka 2020/2021 na Mapitio ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/2020. SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Nchi. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, hapo hapo ulipo. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 SPIKA: Ahsante sana. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti. MHE. MASHIMBA M. NDAKI - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2020/2021. MHE. OSCAR R. MUKASA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Tume ya Uratibu na Udhibiti wa UKIMWI) kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa Mukasa. Sasa namuita Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu. MHE. HALIMA J. MDEE - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA OFISI YA WAZIRI MKUU: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. SPIKA: Ahsante. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yaliulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 10 Barabara ya Msambiazi- Lutindi-Kwabuluu MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Barabara ya Msambiazi - Lutindi – Kwabuluu ni muhimu kwa uchumi na maisha ya watu wa Korogwe hususan Kata za Tarafa ya Bungu, lakini barabara hii ni mbovu na korofi sana. (a) Je, ni lini Serikali itajenga barabara hii kwa kiwango cha lami? (b) Je, ni lini barabara hii itapandishwa kuwa ya mkoa hasa ikizingatiwa kuwa inakwenda kuunganisha Bumbuli na Lushoto? 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI WA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Timotheo Paul Mnzava, Mbunge wa Korogwe Vijijini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, barabara ya Msambiazi – Lutindi – Kwabuluu ni barabara ya Mkusanyo (Collector road) yenye urefu wa kilometa 17.5. Kuanzia Mwaka wa Fedha 2017/2018 hadi 2019/2020 Serikali imeifanyia matengenezo kwa gharama ya shilingi milioni 43. Katika Mwaka wa fedha 2020/2021 Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Korogwe umeomba kutengewa shilingi milioni 50 kwa ajili ya matengenezo ya barabara hii. TARURA Wilaya ya Korogwe inaendelea kufanya upembuzi wa kina wa mtandao wa barabara zake utakaobaini vipaumbele vya ujenzi wa mtandao wa barabara Wilayani Korogwe kwa viwango vya lami, changarawe na vumbi. (b) Mheshimiwa Spika, kabla ya kuanzishwa kwa TARURA, barabara hii iliombewa kuingizwa kwenye orodha ya barabara zinazohudumiwa na TANROADS kupitia Baraza la Madiwani ambapo baada ya kuanzishwa kwa TARURA imepewa jukumu la kuendelea kuihudumia barabara hiyo. Aidha, Serikali imeshatoa maelekezo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuhusu utaratibu wa Bodi za Barabara za Mikoa, Wabunge au Kikundi cha watu kutuma maombi ya kupandishwa hadhi barabara. Utaratibu huu umetolewa na Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara katika Hadhi Stahiki (National Roads Classification Committee- NRCC). Na. 11 Hitaji la Gari la Wagonjwa – Manyoni MHE. AISHAROSE N. MATEMBE aliuliza:- Ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa Wilaya ya Manyoni umekuwa na madhara makubwa ikiwemo 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kusababisha vifo vya akinamama na watoto pindi wanapotakiwa kukimbizwa kwenye hospitali za Rufani. Je, Serikali ina mpango gani wa kuipatia Manyoni gari la Wagonjwa? WAZIRI WA NCHI, OFISI WA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aisharose Ndogholi Matembe, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ina magari mawili ya wagonjwa, gari moja lipo kwenye Kituo cha Afya cha Nkonko na jingine katika Kituo cha Afya cha Kintinku. Hospitali ya Wilaya inatumia pickup na gari aina ya land cruiser hardtop. Serikali itatoa kipaumbele kwa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni pindi itakapopata magari ya wagonjwa kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Na. 12 Barabara Inayoelekea Kalambo Falls MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza Serikali inatambua vivutio kadhaa vya utalii ikiwemo Kalambo Falls Mkoani Rukwa. Hata hivyo, barabara ya kuelekea maporomoko hayo kutokea Kijiji cha Kawala hairidhishi. (i) Je, Serikali ina mpango gani wa kuiboresha barabara hiyo itakayokuwa ikitumika na watalii? (ii) Je, kwa nini kipande hiki chenye urefu wa kilometa 12 kuanzia barabara ya Kijiji cha Kawala kisiwekewe lami? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI WA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Silafu Jumbe Maufi, Mbunge Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya matengenezo ya kilometa 6.5 za barabara ya Kalambo Falls kwa kiwango cha changarawe na kujenga makalvati kwa gharama ya shilingi milioni 160.8 ili kuhakikisha barabara hiyo inapitika katika kipindi chote cha mwaka. (b) Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/ 2021 Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umepanga kufanya usanifu wa kina wa kipande cha barabara ya kutoka Kijiji cha Kawala hadi Kalambo Falls chenye urefu wa kilometa 12 ili kubaini gharama halisi zinazohitajika kwa ajili ya kujenga kipande hicho cha barabara kwa kiwango cha lami. Na. 13 Mamlaka ya Uhamisho Kubaki kwa Katibu Mkuu Kiongozi MHE. MUSSA B. MBAROUK aliuliza: Tarehe 12 Septemba, 2019 katika Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge yamepitishwa Marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma ili kumpa Katibu Mkuu Kiongozi Mamlaka ya mwisho ya uhamisho wa watumishi wa umma. Je, kwa kumpa Mamlaka ya Mwisho Katibu Mkuu Kiongozi hakutasababisha ukiritimba katika uhamisho wa Watumishi wa Umma? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk, Mbunge wa Tanga Mjini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298, imefanyiwa marekebisho katika Kifungu cha 4(3) kupitia Kifungu cha 69 cha Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 13 ya Mwaka 2019 kwa kumpa Katibu Mkuu Kiongozi Mamlaka ya Mwisho ya Uhamisho wa Watumishi wa Umma kwa kuzingatia Mamlaka yake kama Mkuu wa Utumishi wa Umma kwa mujibu wa Kifungu cha 4(2) cha Sheria hii. Mheshimiwa Spika, pamoja na Mamlaka hayo, Kifungu cha 8(2) cha Sheria hiyo kinampa Katibu Mkuu (Utumishi) Mamlaka ya kuwa Msaidizi Mkuu wa Katibu Mkuu Kiongozi. Hivyo, katika kutekeleza majukumu ya Katibu Mkuu Kiongozi, Kifungu cha 8(3)(h) cha Sheria husika kinampa Katibu Mkuu (Utumishi) Mamlaka ya kuhamisha Watumishi wa Umma kutoka Taasisi moja kwenda nyingine Tanzania Bara. Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, Katibu Mkuu (Utumishi) amekasimu Mamlaka yake kwa Katibu Mkuu (TAMISEMI) ili aweze kuhamisha Watumishi wa Umma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Vilevile, Katibu Mkuu (Utumishi) amekasimu Mamlaka yake kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ili waweze kuhamisha Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mikoa yao. Pamoja na kukasimisha Mamlaka yake, Katibu Mkuu (Utumishi) anaweza kuhamisha Watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yeye mwenyewe pale inapobidi. Mheshimiwa Spika, Ninapenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa marekebisho yaliyofanyika katika Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298, yamempa Katibu Mkuu Kiongozi Mamlaka ya mwisho ya uhamisho wa Watumishi wa Umma ili kuwezesha uhamisho unaofanywa naye kutopingwa au kutotenguliwa na Mamlaka nyingine. Hata hivyo, Mamlaka hayo yatatumika kwa kuzingatia masilahi mapana katika 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Utumishi wa Umma au pale ambapo Katibu Mkuu Kiongozi hakuridhika na uhamisho

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    238 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us