NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Tano – Tarehe 6 Aprili, 2020 (Mkutano Ulianza Saa Nane Mchana) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Mheshimiwa Wabunge, tukae, Katibu NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: (i) Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2019; (ii) Ripoti ya Jumla ya Ukaguzi wa Ufanisi na Ukaguzi Maalum kwa kipindi kinachoishia tarehe 31 Machi, 2020; (iii) Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2019; (iv) Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2019; 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (v) Ripoti ya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kaguzi za Ufanisi yaliyotolewa Mwaka 2016; (vi) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi kuhusu Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Shughuli za Manunuzi ya Umma; (vii) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi kwenye Utekelezaji wa Jitihada za Kitaifa za Kupambana na Utakasishaji wa Fedha nchini; (viii) Majumuisho ya majibu ya Hoja na Mpango wa Kutekeleza Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2019. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): (i) Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2019; (ii) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi kwenye Ubora wa Shughuli za Ujenzi na Ukarabati wa Barabara za Lami Mijini; (iii) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Ukusanyaji Mapato toka vyanzo vya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; (iv) Taarifa ya Majibu ya Serikali na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka ulioshia tarehe 30 Juni, 2019; (v) Taarifa ya Serikali kuhusu Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa Hesabu za Mwaka wa Fedha 2017/ 2018. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Ripoti ya Ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Makusanyo ya Mapato kutoka kwa Kampuni za Simu. WAZIRI WA KILIMO: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Miradi ya Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya Kutunzia Mazao. NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Shughuli za Kinga na Chanjo. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi katika Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Mifugo. WAZIRI WA NISHATI: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Upatikanaji wa Umeme na Uhakika wa Utoaji Huduma za Umeme. NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: (i) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi kuhusu Upatikanaji usioridhisha wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi yenye ubora kwa Watanzania; 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (ii) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa Utoaji Programu za Kuwajengea Uwezo Walimu – Kazini. SPIKA: Ahsante sana. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yaliulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 35 Uhaba wa Watumishi wa Sekta ya Afya MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza:- Sekta ya Afya nchini inakabiliwa na uhaba wa Watumishi:- Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kuziba pengo hili? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuajiri wataalam wa kada mbalimbali za Sekta ya Afya nchini ambapo kuanzia Mei, 2017 hadi Julai, 2019 jumla ya watumishi 8,994 wameajiriwa na kupangwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imepewa kibali cha kuajiri Madaktari 610 ambao watapangwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 36 Kuboresha Zahanati ya Bassotu – Hanang MHE. ROSE K. SUKUM aliuliza:- Kutokana na wingi wa watu na shughuli za kiuchumi zilizopo katika Kata ya Bassotu kama vile uchimbaji madini, uvuvi, kilimo, ufugaji na biashara na hivyo kuwa na hatari ya milipuko ya magonjwa:- Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Watoto, Wanawake, Wanaume na nyumba za watumishi wa Zahanati ya Bassotu? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rose Kamili Sukumu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kutokana na Mwongozo unaosimamia utoaji wa huduma za afya, zahanati hazina Wodi ya Watoto, Wanawake na Wanaume. Hata hivyo, kutokana na umbali uliopo kati ya zahanati hiyo na Hospitali ambao ni kilometa 55, Serikali itafanya tathmini ili kuboresha miundombinu iliyopo na kuifanya Zahanati ya Bassotu kuwa na hadhi ya Kituo cha Afya. Na. 37 Kuboresha Huduma za Afya Tunduru MHE. ENG. RAMO M. MAKANI aliuliza:- (a) Je serikali ina mpango gani wa kuboresha huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru na Katika Vituo vya Afya Nakapanya na Matemanga? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Vituo vya Afya na Zahanati katika Kata na Vijiji ili kuendana na Sera ya Afya na Ilani ya CCM? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Ramo Matala Makani, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na mpango wa uboreshaji wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru ambapo wodi mbili ziko katika hatua ya ukamilishaji kwa gharama ya Shilingi milioni 140. Aidha, Hospitali imewezeshwa kufungua duka la dawa na kupatiwa mashine ya Ultrasound. Serikali imetumia shilingi milioni 500 kukarabati Kituo cha Afya Matemanga na Shilingi milioni 200 kujenga wodi ya mama na mtoto na jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Nakapanya? (b) Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mpango wa ujenzi wa Vituo vya Afya kwa awamu na tayari imekamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya vitatu Wilayani Tunduru kwa gharama ya shilingi biloni 1.3 na inaendelea na ujenzi wa Kituo cha Afya Nakapanya kwa gharama ya shilingi milioni 200. Majengo mengine yaliyobaki yataendelea kupewa kipaumbele ili kufikia azima ya kusogeza huduma karibu na wananchi. MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, je, ni lini Serikali itaifanyia ukarabati miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Tunduru yakiwemo majengo yake (wodi, vyumba vya upasuaji, majengo ya mapokezi na kadhalika kwani miundombinu hiyo ni chakavu kutokana na umri mrefu tangu uhuru? 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, swali la pili, Sera ya Afya inafafanua kuhusu hitaji la uwepo wa Kituo cha Afya kwa kila Kata. Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Nampungu ambayo ni mojawapo ya kata tatu za Tarafa ya Nampungu yenye kata tatu na hakuna Kituo cha Afya hata kimoja? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Engineer Ramo Matala Makani, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwanza, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi kuwa, Serikali inaendelea na mpango wa uboreshaji wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru ambapo wodi mbili ziko katika hatua ya ukamilishaji kwa gharama ya Shilingi milioni 140 na Hospitali imewezeshwa kufungua duka la dawa na kupatiwa mashine ya Ultrasound. Serikali itaendelea kuikarabati, kuipanua na kuiboresha Hospitali ya Halmashauri ya Tunduru kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Aidha katika Hotuba itakayowasilishwa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tutatoa ufafanuzi kuhusu mpango wa ujenzi na ukarabati wa hospitali kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Mheshimiwa Mbunge anaombwa kuvuta subira mpaka wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Mheshimiwa Spika, pili, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya ya msingi nchini kwa kukarabati miundombinu iliyopo, kukamilisha maboma na kujenga miundombinu mipya. Hadi Machi, 2020 vituo vya kutolea huduma za afya 400 ikiwemo Hospitali za Halmashauri mpya 98 zimepokea fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza hili, Serikali imetoa kipaumbele kwa maeneo ambayo yana uhitaji mkubwa wa huduma za afya kwa kuzingatia vigezo vya wingi wa watu, umbali na maeneo ambayo ni magumu kufikika. Serikali inaendelea kutekeleza Sera na Mpango huu kwa awamu kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 38 Barabara ya Kutoka Mbulu - Haydom Kilometa 50 MHE. ZACHARIA P. ISSAY aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mbulu mpaka Haydom kilometa 50 kama ilivyopitishwa kwenye bajeti ya 2019/2020? WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia Paulo Issay, Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mbulu – Haydom kilometa 50 ni sehemu ya barabara ya Karatu, Mbulu, Haydom, Sibiti, Lalago – Maswa kilomita 389 ijulikanayo kama Serengeti Southern Bypass.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages165 Page
-
File Size-