Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA WA KUMI NA MBILI Kikao cha Thelathini na Tisa - Tarehe 5 Agosti, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009 MHE. AL– SHYMAA JOHN KWEGYIR (K.n.y. MHE. JENISTA J. MHAGAMA - MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII): Taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu makadirio ya matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2008/2009. MHE. MGENI J. KADIKA - MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO: Taarifa ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa mwaka wa fedha uliopita, pamoja na maoni ya Upinzani kuhusu Makadirio ya matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2008/2009. MASWALI NA MAJIBU 1 Na. 337 Hitaji la Kuzigawa Kata za Kipanga na Tutuo MHE. MGANA I. MSINDAI (K.n.y. MHE. SAID JUMA NKUMBA) aliuliza:- Kwa kuwa kupitia vikao husika, Kata za Kipanga na Tutuo Wilayani Sikonge ziliombewa ili zigawanywe kutokana na ukubwa wa maeneo ya kata hizo na kwa kuwa ni muda mrefu sasa maombi hayo yako TAMISEMI:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saidi Juma Nkumba, Mbunge wa Sikonge, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumfahamisha Mheshimiwa Mbunge kuwa Halmashauri zote kupitia Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa nchini mwaka mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa Februari, 2003 zilielekezwa kuwasilisha TAMISEMI taarifa za idadi za majina ya vitongoji, vijiji mitaa na Kata. Mwisho wa utekelezaji wa agizo hilo lilikuwa ni mwezi Machi, 2004. Baadhi ya Halmashauri ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge hazikuweza kutumia vema muda huo kuyashughulikia mahitaji yake ya kuanzisha kata upya. Kwa mujibu wa kumbukumbu za Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ni kweli Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge iliwasilisha maombi ya kuzigawa kata za Kipanga na Tutuo na kuanzisha kata nyingine mbili mpya yaani Kata ya Usunga na Kata ya Ibunda. Taarifa ya maombi hayo iliwasilishwa ofisini kwangu tarehe 20 Desemba, 2004, muda ambao tayari ofisi yangu ilikuwa imekamilisha maandalizi ya upatikanaji wa taarifa muhimu kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao nao ulikuwa umekwishafanyika mwezi Oktoba, 2004. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa uchaguzi wa mwaka 2009 ofisi yangu inayashughulikia kikamilifu maombi ya Halmashauri mbalimbali nchini yakiwemo ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ya kuanzisha maeneo mapya ya utawala na uratibu wa zoezi hili karibu unakamilika. Napenda kutoa wito kwa mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi za Halmashauri za Wilaya na Miji, kwamba katika mchakato mzima wa kuandaa na kutekeleza mapendekezo ya kuanzisha maeneo hayo mapya ni muhimu na lazima kushirikisha wananchi wa maeneo husika kupitia vikao vyao vya kisheria na mamlaka zao ambazo husimamia na kutekeleza maamuzi mbalimbali kwa Maendeleo yao. Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini kote utakaofanyika mwaka 2009 ofisi yangu inatarajia kuzifahamisha Halmashauri zote 2 juu ya uamuzi wa Serikali kuhusu maombi ya kuanzisha vijiji, Vitongoji, Mitaa na Kata katika maeneo yao husika. Namshauri Mheshimiwa Nkumba kuvuta subira ili tuweze kukamilisha zoezi hili kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na hatimaye kufanya maamuzi juu ya maombi hayo. MHE. MGANA I. MSINDAI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge Said Nkumba na wananchi wa Kipanga na Tutuo na Sikonge nzima wameridhika na majibu ya Waziri. (a)Je, Waziri tayari kupokea ahsante kutoka kwao? (b)Kwa sababu wananchi wa Iramba nao wameomba kugawanya Kata za Mwanga na Irunda na masharti yote aliyoyasema Waziri wametimiza. Je, nao watafikiriwa ili waweze kupatKata mpya? (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA : Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nishukuru kwa ahsante sana yake lakini naomba nitoe angalizo kwamba ili kuanzisha Kata au vijiji kuna vigezo maalum. Kwa hiyo, kwa Kata moja imetimiza vigezo vinavyotakiwa lakini kwa kata nyingine tumewarudishia kwamba ili waweze kupata Kata inabidi wagawe tena vijiji vingine kwa hiyo, tumewarushia wafanye kazi hiyo haraka ili tuweze kuunganisha katika uchaguzi wa mwaka 2009. Kuhusu Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ni kweli wameleta mapendekezo yao mbalimbali ofisini kwetu na yamo katika mapendekezo ya kuanzishwa Kata ya Mwanga pamoja na Irunda. Lakini kwa Halmashauri nyingine zote nchini nitoe wito kwamba tunaomba wafikishe maombi hayo kabla ya mwezi Desemba ili tuweze kuyashughulikia kikamilifu. Baada ya mwezi Desemba haitakuwa rahisi kushughulikia maombi mbalimbali kwa sababu tutakuwa tumeshaingia kwenye mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri huyu mzoefu kwenye sekta hiyo ya Local Authority na mimi nilikuwa naomba tu kupata uhakika tatizo la Kata ya Magagula ambayo imekidhi vigezo vyote na taarifa zake zilishapelekwa kwenye Wizara yake kwa muda mrefu pamoja na Kata nyingine za Halmashauri ya Wilaya ya Songea. Je, taarifa hizo anazo na mgao huo wa Kata ya Magagula utazingatiwa katika awamu hii anayoifanyia kazi sasa hivi? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI mbona hata mimi nimeleta? (Kicheko) 3 WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Jenista Mhagama alinipa nakala ya ugawaji wa Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea. Kata ya Magagula ni kati ya Kata ambazo ni kubwa sana katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea. Kwa hiyo, maombi yake tumeyapokea tumeyafanyia kazi na Kata ya Magagula imo katika mgawanyo. Na. 338 Taarifa ya Kutuma Fedha Mikoani MHE. BUJIKU P. SAKILA aliuliza:- Kwa kuwa siku za nyuma Serikali ilikuwa na utaratibu wa kuwapa Wabunge taarifa kila ilipotuma fedha mikoani, ili Wabunge wa maeneo husika waweze kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha hizo na kwa kuwa taarifa hizo zilikuwa zikibainisha wazi kiasi cha fedha na aina ya miradi iliyokuwa imekusudiwa jambo lililowarahisishia Wabunge kuafuatilia fedha hizo na matumizi yake. (a)Je, kwa nini Serikali ilisitisha utaratibu huo mzuri? (b) Je, Serikali haioni kuwa kwa kutoziweka fedha hizo wazi kwa Wabunge kunatoa mwanya kwa baadhi ya watendaji wakuu wa idara wasio waadilifu watumie fedha hizo kinyume na malengo yaliyokusudiwa bila kugundulika mapema? (c) Je, Serikali iko tayari sasa kuzielekeza Wizara zote zianzishe na kuendeleza tena utaratibu huo? NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. OMAR YUSSUF MZEE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Uchumi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Bujiku Philip Sakila, Mbunge wa Jimbo la Kwimba, lenye sehemu (a) (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa kuwapatia taarifa za mgao wa fedha Waheshimiwa Wabunge, Viongozi mbalimbali na wananchi mara zinapotumwa kwenye Halmashauri, kwa lengo la kufahamu na kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha hizo hupitia kwa Afisa Masuuli haujasitishwa. Afisa Masuuli anapaswa kuziandikia Halmashauri zake juu ya upatikanaji wa mgao wa fedha na kuzitaka zitangaze upokeaji wa fedha hizo kupitia kwenye vikao vya Madiwani ambamo Waheshimiwa Wabunge ni wajumbe. Aidha, Halmashauri hutakiwa kuwajulisha wananchi kwa kutoa taarifa kupitia kwenye ubao wao wa matangazo. Na kama kuna Halmashauri hazitoi taarifa, nawaomba watoe taarifa hizo mapema iwezekanavyo. 4 (b)Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kuwa utaratibu haujasitishwa, Serikali inaweka wazi fedha zote kwa Waheshimiwa Wabunge, kulingana na utaratibu uliopo. Ni muhimu kwa Serikali kushirikiana kwa karibu zaidi na Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwa ujumla, kufanya hivyo kutasaidia kutotoa mwanya wa ubadhirifu na udanganyika wa mali za umma kwa mtumishi wa Serikali. (c)Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa utaratibu huu ni mzuri, Wizara na Idara za Serikali zinatakiwa kuzingatia kwa ukamilifu utaratibu wa kutoa taarifa za matumizi ya fedha, kutoa taarifa za fedha ni hatua muhimu ya kuendeleza na kukuza utawala bora pamoja na kuleta uwajibikaji mzuri katika matumizi ya fedha za umma. (Makofi) MHE. BUJIKU P. SAKILA: Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba Mheshimiwa Naibu Waziri akubali kupokea shukrani zangu kwa Serikali kwa kutoa maelekezo mazuri sana kwa Halmashauri na sehemu zinazohusika kuhakikisha kwamba Wabunge na Madiwani pamoja na wananchi wanapata taarifa hizi muhimu. (a)Je, Serikali inao utaratibu mahususi wa kufuatilia utekelezaji wa maelekezo hayo mazuri kuhakikisha kwamba Madiwani na Wananchi katika kata zao wanapata hizi taarifa muhimu? (b)Kabla ya kumalizika mkutano huu je, Serikali itakuwa tayari kutupatia taarifa za fedha hizi zilizotumwa katika mwaka wa fedha uliopita pamoja na fedha zilizotumwa kwa ajili ya matumizi ya ofisi za Waheshimiwa Wabunge katika ofisi zao? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. OMAR YUSSUF MZEE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napokea shukrani zake kwa dhati kabisa. Pili, Serikali inao utaratibu wa kufuatilia juu ya utoaji wa taarifa hizi na kama mahali au kuna eneo au kuna Halmashauri hazitoi
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages174 Page
-
File Size-